Mama yako na Mke wako nani anastahili kukaa siti ya mbele ya Gari yako mnapotoka wote kwa pamoja?

Mama yako na Mke wako nani anastahili kukaa siti ya mbele ya Gari yako mnapotoka wote kwa pamoja?

Wote ni wanawake, wakae nyuma wapigiane stori za jikoni!
 
Siti ya mbele nitakaa peke yangu wao nyuma na stori zao
 
Hakuna yeyote anayestahili kukaa hapo maana gari sio la kwao ni langu.

Yeyote atakaye penda kukaa atakaa.

Yeyote atakaye wahi kukaa, ataendelea kukaa.
 
Mwanamke wangu kwa ninavyomjua na usanii wake ,atajifanya mwache tu mama akae mbele.
 
Kimamlaka

1. Mungu kwanza

2. Wazazi.

3. Watoto( mke na mume)

Pia seat ya mbele kiutaratibu unatakiwa kubaki wazi,

Ila ikiwa seat unapewa Heshima, ngazi hapo juu zifuatwe.
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Kwani wakikaa nyuma au mbele hawafiki pamoja? Mbona kwenye ndege huwa hatujalishi unakaa mbele au nyuma?
 
MKE.....atakaa mbele...Kuna Dada mmoja nilikuwa nae kimapenzi akapata shida nikawahi kufika kwake nikawa namhudumia poa..chumba na sebulenakaja mama ake nkamuuliza atalala wapi ..akasema khe mi nalala na mama angu nenda kule kwenyumba ya baba mwenye nyumba Kuna chumba nimekuandalia...nkamjibu naenda lodge ...na alfajiri naondoka nshakuaga...sijui mamake alisikia akamwambia lala na mwenzako mi ntaenda kule...Na NI moja ya sababu ya kuachiana nae...nilimpa NAFASI yakipekee kwangu yeye akanipa option...kwa namna yoyote mama atakaa nyuma mbele atakaa MKE..
 
IMG-20241007-WA0000.jpg
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Acheni ku complicate maisha nyie watu!na hio nayo ni kuwaza!!?

Mama mwenye hekima anajiongeza tu anakaa nyuma bila kuambiwa!!!
 
Kwanza seat ya nyumba ndio executive seat kuliko hizo za mbele ambazo watu wengi hukimbilia, ushawahi kuona Rais kakaa seat ya mbele?. Hata hivyo binti (mke) alielelewa vizuri kwao hawezi kukaa kulalamika kwamba nani akae seat ya mbele, mama aachwe achague kokote atakapoona akikaa atakua confortable then mke afuate hiyo ndio heshima ya binti wa kitanzania sababu hata akae mbele au nyuma ukweli ni kwamba haiwezi kuondoa title yake kwamba yeye ni mke na yule atabaki kuwa mama!
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Wote watakaa nyuma....mbele wanatafuta Nini ?
 
Back
Top Bottom