Pole mwaya stahamili maana yana mwisho na kwako utakuwa mwisho mzuri, InshaAllah!
Isipokuwa wakati mwingine uwe unaongea nae kumueleza ukweli.
Usimuogope mtu awaye yoyote.
Wakuogopwa ni Mwenyezi Mungu pekee ,
Wanadamu tunaheshimiana.
Amekuona muoga sasa anakutawala!
Tafuta muda kaa nae Penye utulivu mpe ukweli muhimu usimtukane maana ni kosa na ni jinai.
Mpe misimamo yako,
Mwambie wewe bado unapambana huna kikubwa sana muhimu akuombee upate kingi.
Mwambie wewe ni wewe na una maisha yako binafsi na unahitaji kujikimu na future.
Nakwambia atakuheshimu na kukuogopa na atakuomba hela kwa adabu na itakuwa hiyari yako kumpa Au kutompa.