Mama yangu alifariki huku akijua simpendi

Mama yangu alifariki huku akijua simpendi

Habarini za asubuhi wana MMU poleni na majukumu ya kujenga taifa na familia kiujumla.

Kijana wenu nimekuja hapa mbele yenu sijui nahitajI ushauri ama nahitaj nini ila ntafurahi kama ntarejesha amani ya moyo na akili yangu.

Ni hivi mama yangu mzazi alikufa huku akitambua kua mimi mwanae simpendi na kweli sijawahi kumpenda. Kinachoniuma nilishindwa kulificha hili nilimuonesha moja kwa moja so hadi anakata roho alijua fika simpendi.

Kuna muda nikikaa huwa naona nilikosea sana kumuonesha chuki yangu na hili kosa huwa nalijutia sana. Kila siku nawaza namna ya kujisawazisha ila nakosa majibu.

Naombeni ushauri au maelekezo yoyote yanaweza rejesha amani ya moyo wangu.

Natanguliza shukrani.
Imeanzia katikati story yako wewe sio chizi weka bayana mlolongo wote
 
Kinachokusumbua si kwa vile alifariki ukiwa na chuki bali ni kwamba unasumbuka bado na yale aliyokukwaza nayo na aliondoka akiwa bado hajatafuta namna ya kushusha uchungu wako.

Kwa vile hayupo amua tu kumsamehe na ujisamehe wewe pia kwa kujiumiza, yes kuruhusu mtu mwingine atawale hisia zako ni wewe umeruhusu hizo hisia zikutese.
Sema nakusamehe mama kwa kuniumiza na mimi najisamehe pia, mara nyingi kadri utakavyokumbuka kila jambo lililokujeruhi nafsi.UTAPONA USIJALI.
 
Kama baba angu mkubwa vile alikua hapatani na mama ake mpaka anaumwa akalazwa hadi umauti ulipomfika

Hadi kwenye mazishi ya mama yake akawa analeta makwazo na makasiriko yake

Maisha yake kwa sasa hana amani ,mtu wa kufoka ovyo ovyo na mahasira ya ajabu ajabu

Mke alikufa ,mtoto yupo shule ,watu wa Karibu alokua anaishi nao wameondoka hapo nyumbani yani yupo mwenyewe nyumba nzima amekua mpweke mno

Uchumi umeyumba si kama mwanzo

Akilala usiku anapiga kelele kelele tu ukimuuliza shida nini anasema ni ndoto za ajabu ajabu anaota

Kwa ufupi hana amani ya maiaha

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Kinachokusumbua si kwa vile alifariki ukiwa na chuki bali ni kwamba unasumbuka bado na yale aliuokukwaza nayo na aliondoka akiwa bado hajatafuta namna ya kushusha uchungu wako.

Kwa vile hayupo amua tu kumsamehe na ujisamehe wewe pia kwa kujiumiza, yes kuruhusu mtu mwingine atawale hisia zako ni wewe umeruhusu hizo hisia zikutese.
Sema nakusamehe mama kwa kuniumiza na mimi najisamehe pia, mara nyingi kadri utakavyokumbuka kila jambo lililokujeruhi nafsi.UTAPONA USIJALI.
amina
 
Habarini za asubuhi wana MMU poleni na majukumu ya kujenga taifa na familia kiujumla.

Kijana wenu nimekuja hapa mbele yenu sijui nahitajI ushauri ama nahitaj nini ila ntafurahi kama ntarejesha amani ya moyo na akili yangu.

Ni hivi mama yangu mzazi alikufa huku akitambua kua mimi mwanae simpendi na kweli sijawahi kumpenda. Kinachoniuma nilishindwa kulificha hili nilimuonesha moja kwa moja so hadi anakata roho alijua fika simpendi.

Kuna muda nikikaa huwa naona nilikosea sana kumuonesha chuki yangu na hili kosa huwa nalijutia sana. Kila siku nawaza namna ya kujisawazisha ila nakosa majibu.

Naombeni ushauri au maelekezo yoyote yanaweza rejesha amani ya moyo wangu.

Natanguliza shukrani.

How do you do that kwa mwanamke aliyekubeba tumboni miezi tisa …..ni laana kabisa , na huwa inabebwa utajikuta na wewe unakuwa na watoto hawakupendi ….lazima uvunje laana .

Maama ni mama hata kama dunia nzima inamuona mbaya
 
Maskini Mama! hakika alifariki kifo cha mateso sana, kama mzazi kujua mtoto uliyemuweka tumboni miezi 9 na kumtoa kwa uchungu wa kuliona kaburi anakuchukia!!! dooh! aliishi kwa mateso sana, [emoji26]

Nijuacho mzazi siku zote hawezi kuweka kinyongo kwa mwanae, alikusamehe kabla hajafa ni muda wa wewe kujisamehe na kuishi maisha yaliyo bora bila kuweka vinyongo vinavyounda roho chafu.

Ila usisahau kitu kinachoitwa KARMA.

Kuna mtu kama huyo mama yake aliteseka sana kumtunza kwa kufanya vibarua , anavaa kanga upande etc akafanikiwa kumsomesha ….akapata kazi nzuri sana na pesa zikaanza kuingia ….hakuwahi kumsaidia mama yake alimuacha akaendelea kufanya vibarua vya aibu …na nyumba inaanguka ..akahamia kwa jirani kulikuwa hakuna mtu akawa anaishi kama mlinzi wanamlipa ….
Siku anafariki mtoto wake akatuma pesa kuandaa msiba wa kifahari akaondoka na magari na marafiki zake kwenda kuzika …wakiwa njiani BMW yake ilipata ajali mbaya mke na watoto wakapona wakaenda kuzika yeye akaishia hospotali akapooza huu mwaka wa kumi yupo tu ….mke wake kaingiza mwanamume ndani ….na watoto wake wala hawana muda naye ..yeye ndio anaishi na wheel chair kwenye nyumba mbovu ya mama yake ambayo aliifanyia ukarabati wa voda fasta msiba ulipotokea na kaburi mbele yake …..nayeye anaishi kwa sadaka za “wahitaji” kanisani ….wale wale waliokuwa wanamsaidia mama yake chakula ndio wanampelekea mabaki ya chakula nyumbani ….akiwa na ukiwa na majuto …

Haya mambo sio ya mchezo
 
Nimehisi uchungu sana kusoma hiki kisa,
Nikawaza ninavyompenda Mama yangu eti nimuache aje adhalilike na mimi nipo hai HAPANA,

Juzi tu kuna Kaka amemzika Mama ake kwa Kansa ya Damu lakini yule Kaka alijua kupambana kumuuguza Mama ake wallah, nakumbuka alisema "natamani nipewe dakika 5 zaidi za kuendelea kumuona Mama angu..." Ilikua huzuni sana japo Mama alikua kwenye mateso makali lakini Mtoto alitamani bado aendelee kubaki na Mama ake, [emoji22]

Ngoja nimpigie Mama sasa hivi nimwambie Nampenda sana japo anajua hilo [emoji847]
 
Kwa Kweli Kuna wazazi wengine ni mtihani!

Dunia ina mengi sana!

Wengine unaweza kuta mtoto haelewani na mama yake mzazi sababu mama mzazi anataka kumuua mume wa binti yake na binti anagoma hataki kuwa mjane!

Au wote wachawi mama na mwana halafu walikosana kwenye zamu za kulipa kula mojawapo ya watoto wao.

Yule mtoto tegemeo wa familia au mzuri ndiye anaetakiwa kuuliwa!
 
Ndio maana nchi zilizo endelea wazazi wwnashitakiwa na watoto wao wakiona wamezidi kuzingua.
 
Mtoto wa kizungu anamwambia Hakimu Hawa Au Huyu mzazi ananisumbua kila uchao mara vile mara hivi!

Anasema kwanza mimi sikumuomba anizae [emoji848][emoji848]
Anasema muulize Je nilimuomba anizae?

[emoji3][emoji3][emoji28][emoji23]

Kwanini ananisumbua?
 
Yani kuna wazazi wanatakaga kuabudiwa kama miungu!

Yani inazidi heshima! [emoji848][emoji848]

Bahati nzuri Neno la Mungu limekwisha kuonya kuwa :

“ Enyi wazazi msiwachokoze watoto wenu”

Mungu alijua kutakuwa na wazazi wachokozi kwa watoto wao!

Na laana isiyo na sababu haimpati mtu!

Imeandikwa!
 
Sasa unadhani hiyo ni akili timamu?? Ni sifa hiyo? Hao ni wehu tu. Sio watu wa kuigwa kabisa.
 
Yani kuna wazazi wanatakaga kuabudiwa kama miungu!

Yani inazidi heshima! [emoji848][emoji848]

Bahati nzuri Neno la Mungu limekwisha kuonya kuwa :

“ Enyi wazazi msiwachokoze watoto wenu”

Mungu alijua kutakuwa na wazazi wachokozi kwa watoto wao!

Na laana isiyo na sababu haimpati mtu!

Imeandikwa!
Sisi tumefundishwa haya hapa;

17_23.gif

23. Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.23

17_24.gif

24. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.24

(Qur'aan 17:23-24)
 
Inawezekana labda ni sababu za kishirikina,uliaminishwa na mganga/waganga wa kienyeji kuwa mama yako ndio cuanzo Cha tatizo au tukio fulani baya lililowahi kukutokea.

Au ndiye aliyesababisha ndoa au mahusiano na baba yako kuvunjika/hakuwa mwaminifu. Na wewe ulishuhudia hayo mambo! Ukaishi ukikumbuka. Maisha ya utoto ukalelewa na bibi au mlezi. Na yeye akaendelea na maisha yake bila kujali.

Au alikuwa katili na asiyejali.

Cha msingi sahau na usamehe. Na uombe pia naye asamehe huko alipo. Kubali kuwa sie binadamu hatujambwa wakamilifu. Naye ni binadamu
 
Habarini za asubuhi wana MMU poleni na majukumu ya kujenga taifa na familia kiujumla.

Kijana wenu nimekuja hapa mbele yenu sijui nahitajI ushauri ama nahitaj nini ila ntafurahi kama ntarejesha amani ya moyo na akili yangu.

Ni hivi mama yangu mzazi alikufa huku akitambua kua mimi mwanae simpendi na kweli sijawahi kumpenda. Kinachoniuma nilishindwa kulificha hili nilimuonesha moja kwa moja so hadi anakata roho alijua fika simpendi.

Kuna muda nikikaa huwa naona nilikosea sana kumuonesha chuki yangu na hili kosa huwa nalijutia sana. Kila siku nawaza namna ya kujisawazisha ila nakosa majibu.

Naombeni ushauri au maelekezo yoyote yanaweza rejesha amani ya moyo wangu.

Natanguliza shukrani.
kuna sababu ya kutompenda ila umefanya kosa kumwonyesha wazi,na kama na yy alikufa kwa knyongo hakika laana itakutafuna mpaka unaingia kaburn
 
Daah mkuu poleee[emoji28]

Wanasema katika wakati wowote ule mahusiano yako na mtu yeyeto yule jiulize hivi huyu ikitokea tumeamka asubuh kafa hivi ntakuwa najiskiaje?

Mkuu binafsi naelewa Kuna wazazi wanazingua sana, anakuwa napigo hazieleweki kisa tu kakuzaa na vitisho kibao mpaka mzazi anamtakia mwanae "nisije kukuona kwenye mazishi yangu" kwahyo Kuna vitu vingine huwezi kuzuia Kwa mfano huwezi mkuzuia mtu kukuchukia na hujamkosea

Kama wewe ndio ulizngua tubu bro kama yeye alizungua msamehe na ujisamehe mwenyew

Utasahahu tu baada ya mda, tumeumbwa kusahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikumbukwe kuwa hata wa wachawi wanazaa kama kawaida,

Kwa hiyo mtu kuambiwa mama yako baba yako mchawi usikatae maana inawezekana kabisa!
 
Back
Top Bottom