Mama yangu alifariki huku akijua simpendi

Mama yangu alifariki huku akijua simpendi

Halafu Mwanaume ukioa mwanamke mchawi basi ujue upo wanted wakati wowote kupotezwa mazima!

Sijui huwa ni Kwanini wanawake wachawi wengi huwa ni wajane!

Sijajua kwa wachawi wanaume je nao wanatabia ya kuua wenza wao?!
 
Kama Kuna jambo baya alifanya hadi ikasababisha wewe kumchukia basi chuki yako ndo kitu sahihi kilikua kinamstahili huna cha kujutia
 
Hua lazima inakuja kubounce back hata kizazi chako cha 3..itatokea kuna mtotto nayr hatampenda mamake had anakufa...itakua hivyo hivyo had mwisho wa dunia..so sad
 
IJUMAAAA IJUMAAAA

KUNA MAOMBI YA KUONDOA NUKSI BALAA LAANA MIKOSI KWA KUHANI MUSA RICHARD MWACHA
NENDA UKAMWGIWE MAFUTA UONDOE HIO LAANA KIINGILIO BURE

....SO SAD SIKUHURUMII WEWE NAHURUMIA WANAO KAMA UMEBAHATIKA KUPATA
"Kumwagiwa wese"![emoji848]
 
Habarini za asubuhi wana MMU poleni na majukumu ya kujenga taifa na familia kiujumla.

Kijana wenu nimekuja hapa mbele yenu sijui nahitajI ushauri ama nahitaj nini ila ntafurahi kama ntarejesha amani ya moyo na akili yangu.

Ni hivi mama yangu mzazi alikufa huku akitambua kua mimi mwanae simpendi na kweli sijawahi kumpenda. Kinachoniuma nilishindwa kulificha hili nilimuonesha moja kwa moja so hadi anakata roho alijua fika simpendi.

Kuna muda nikikaa huwa naona nilikosea sana kumuonesha chuki yangu na hili kosa huwa nalijutia sana. Kila siku nawaza namna ya kujisawazisha ila nakosa majibu.

Naombeni ushauri au maelekezo yoyote yanaweza rejesha amani ya moyo wangu.

Natanguliza shukrani.
Ulipanda mbegu ya chuki matokeo yake ni majuto yasiyo na kikomo, Nakushauri utubu ili Mungu akuondolee huo mzigo wa majuto, hapo amani ya moyo itarejea na utakuwa free.
 
Maskini Mama! hakika alifariki kifo cha mateso sana, kama mzazi kujua mtoto uliyemuweka tumboni miezi 9 na kumtoa kwa uchungu wa kuliona kaburi anakuchukia!!! dooh! aliishi kwa mateso sana, [emoji26]

Nijuacho mzazi siku zote hawezi kuweka kinyongo kwa mwanae, alikusamehe kabla hajafa ni muda wa wewe kujisamehe na kuishi maisha yaliyo bora bila kuweka vinyongo vinavyounda roho chafu.

Ila usisahau kitu kinachoitwa KARMA

DAH KUMCHUKIA MAMA NI HASARA HAPA DUNIANI

Niliwahi shuhudia jamaa yangu wa karibu anakuja kwa huku analia. Nilipomuuliza why? Akasema tabia za mama sizipendi kabsaa.
Nikamwambia atulie. Mama ni mama tu hata akiwa mchawi. Nikamshauri amuheshimu lkn ajipe muda wa kufanya mambo yake kuliko kufuatilia mambo ya kifamilia.
 
Binadamu sio mkamilifu,kuna muda anakosea

Mzazi hakosei kivipi?ama mzazi tunamtoa kwenye kundi la binadamu?

Wazazi wanazinguaga kinyama tu,wewe sema hatutakiwi kuwa na chuki kama ya mleta mada
Dah! Ni kweli aisee
 
Jisamehe mwenyew kwanza then usirudie Hilo Kosa wamama maranyingi hawajuagi kama hatuwapendi Bali wanatuchukuliaga kama watoto watukutu na wasumbufu tu ndo maana tunafanya makosa mengi na still Bado wanatubeba na kutuhesabu kama watoto wao
Omba Mungu akusamehe na muombee mama Yako Mungu amrehemu
Wazazi nao huwa wanatukosea, ww kama mzazi ifikie hatua umemuona mtoto kakosea muite kistaarabu umkanye atakuelewa sio kumuoneshea chuki hadi ajue unamchukia.
 
Yani kuna wazazi wanatakaga kuabudiwa kama miungu!

Yani inazidi heshima! [emoji848][emoji848]

Bahati nzuri Neno la Mungu limekwisha kuonya kuwa :

“ Enyi wazazi msiwachokoze watoto wenu”

Mungu alijua kutakuwa na wazazi wachokozi kwa watoto wao!

Na laana isiyo na sababu haimpati mtu!

Imeandikwa!
We acha tu, mi sina baba wala mama ila nimelekewa na babu, yaani japo amenilea tangu mdogo alikuwa ananichukia na kila nikifanya kitu kumridhisha naonekana mbaya anataka anyenyekewe, yaani mara ajiite ye ni Mungu wangu. Nikipata likizo unaenda kwa babu unamnunulia kila kitu ndani unamuacha hata na 50000 lakini bdo analeta makasiriko yaani kunawazazi hovyo sana mara kunakipindi nimeajiriwa anataka tugawane mshahara [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
only God can fix what make you suffer.

you know how..?
 
We acha tu, mi sina baba wala mama ila nimelekewa na babu, yaani japo amenilea tangu mdogo alikuwa ananichukia na kila nikifanya kitu kumridhisha naonekana mbaya anataka anyenyekewe, yaani mara ajiite ye ni Mungu wangu. Nikipata likizo unaenda kwa babu unamnunulia kila kitu ndani unamuacha hata na 50000 lakini bdo analeta makasiriko yaani kunawazazi hovyo sana mara kunakipindi nimeajiriwa anataka tugawane mshahara [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]


Pole mwaya stahamili maana yana mwisho na kwako utakuwa mwisho mzuri, InshaAllah!

Isipokuwa wakati mwingine uwe unaongea nae kumueleza ukweli.

Usimuogope mtu awaye yoyote.

Wakuogopwa ni Mwenyezi Mungu pekee ,

Wanadamu tunaheshimiana.

Amekuona muoga sasa anakutawala!

Tafuta muda kaa nae Penye utulivu mpe ukweli muhimu usimtukane maana ni kosa na ni jinai.

Mpe misimamo yako,

Mwambie wewe bado unapambana huna kikubwa sana muhimu akuombee upate kingi.

Mwambie wewe ni wewe na una maisha yako binafsi na unahitaji kujikimu na future.

Nakwambia atakuheshimu na kukuogopa na atakuomba hela kwa adabu na itakuwa hiyari yako kumpa Au kutompa.
 
watu wote wajue ukiona mzazi anafanya vitu siyo kwako basi yakubidi umchukulie kawaida inawezekana ni suala la psycholojia
trust me kuna mda anajuta jinsi anavyokutreat ila baadae anasahau na kurudia yaleyale
 
Kama baba angu mkubwa vile alikua hapatani na mama ake mpaka anaumwa akalazwa hadi umauti ulipomfika

Hadi kwenye mazishi ya mama yake akawa analeta makwazo na makasiriko yake

Maisha yake kwa sasa hana amani ,mtu wa kufoka ovyo ovyo na mahasira ya ajabu ajabu

Mke alikufa ,mtoto yupo shule ,watu wa Karibu alokua anaishi nao wameondoka hapo nyumbani yani yupo mwenyewe nyumba nzima amekua mpweke mno

Uchumi umeyumba si kama mwanzo

Akilala usiku anapiga kelele kelele tu ukimuuliza shida nini anasema ni ndoto za ajabu ajabu anaota

Kwa ufupi hana amani ya maiaha

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
binamu yangu alitaka kudanganywa na wapambe baada ya kupata visenti,akaanza visa na mama yake yaliyomkuta hatisahau alirudi sifuriii yaani ile sifurii.
na sasa mama yake huyohuyo ndo alikuja kumsaidia
 
mpaka kufikia kujiita hivi ubongo umeshakiri kwamba niko hivo yaani mikosi hainiishi
Mkuu inaonekana una matatizo mengi yanayokusibu na kukuumiza moyo lakini unayaficha hiyo itakufanya uwe mtu wa huzuni maisha yako yote.
Hakuna tatizo jipya chini ya jua,tatizo lolote linalokusibu fahamu ya kwamba kuna watu walishapitia na wana uzoefu wa kutosha humu ndani ya jukwaa.
Weka wazi usaidike ndugu.
 
Ni mambo ya kifamilia mkuu
sasa kama ni mambo ya kifamilia, nahisi familia ingekuwa nzr zaidi kukushauri

hapa hutaki kusema na inakuwa ngumu sisi kukushauri

maana huenda alistahili hilo ulilomfanyia au hakustahili tutujuaje sasa

nawaza kwa sauti
 
Back
Top Bottom