Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

Msalato, Huruma & Nkuhungu secondory kwa pale Dodoma ni viwanda vya uzinzi.. ABC UPPER CLASS
 
CHAPTER 3

Mtoto akaletewa juice ya miwa. Tuko watatu pale story nyingi sana mimi na mwanangu. Ila yule mtoto kapoa sana yaani hajachangamka kabisa. Mara kuna mademu yamekuja pale kununua si yakamuita jina "Nasraaa" yeye mwenyewe kashtuka kinoma kuona anaitwa jina lake.


Mimi mwenyewe nilishtuka kinoma,jamaa yangu kashtuka sana. Nasra yeye mwenyewe kashtuka sana hatari yaani acha tu.

INAENDELEAAAA.....


wale mademu walikuwa wapo kama watano hivi. Ila kati yao mmoja ndio anaonekana kumfahamu. wengine ni kwamba wapo charming tu. Yule demu kaja pale kwa Nasra kamkumbatia nini lakini Nasra bado kapoa tu. Yule demu akawa anamuuliza habari za school kina mwalimu Fulani,kina nani.

anamuuliza demu mbona wewe upo huku school vipi. Na maswali mengine,maongezi yao yule demu alikuwa anasoma na Nasra Mkoa X ila yeye alikuwa class la mbele na ameshamaliza. So,anamuuliza issue sana za skuli. Nasra akampiga kamba pale kwamba amekuja huku anaumwa kuna vipimo...

kuna vipimo kaja kucheki. Hapo Mimi na mwanangu tunawasikilizia tu,ila yule manzi akampa pole sana na mambo mengine. Akamuomba contact,Nasra simu hana😂

jamaa yangu faster akawahi akamwambia yule demu chukua namba yangu. Ukitaka kuwasiliana na Nasra utamcheki hapa sababu tupo nae home. Nasra kabariki jamaa wakabadirishana namba na yule demu. Mimi hapo Nina vicheko vimenikaba kinoma noma yaani natamani nicheki ila naogopa😂

sijakaa sawa Bi mkubwa akanipigia simu swali lake la kwanza " upo wapi ?"

nikamjibu " aaah nishafika dar es salaam ila sijafika kwa dada moja kwa moja nimefikia huku kwa rafiki zangu ninapojisomeaga "

bi mkubwa akafoka foka sana ila msala ukaisha kiupande fulani.


Mda uo Nasra bado alikuwa anaongea na yule demu. basi demu kaaga vizuri kaondoka,huyo demu anaitwa Anit*a kwa sasa ni askari wa jeshi la polisi kitengo cha cyber. Huwezi amini kwa sasa ndio mke wa huyo jamaa yangu tuliyekuwa naye pale. From that day walianzisha mahusiano yakakuwa wakafunga ndoa 2019 December na mpaka leo wako pamoja ni mke na mume kabisa na ndoa ya kanisani. Yaani huwa tunakaa na huyo mwana tunapiga story tunacheka sana😂. Turudi kwa Naa sasa,baada ya huyo Anit*a kuondoka pale nikamuuliza vipi kuhusu huyo manzi. Akaniambia alikuwa headgirl wetu school kamaliza mwaka jana.

So ananifahamu ndio,ok likawa limeisha hilo. Ikabidi nivae sura ya userious kidogo nikaanza kumuuliza "Naa hebu niambie ukweli umefuata nini Dar es salaam na umekuja kwa nani, don't tell me again kuwa umefuata ada kwa baba yako ,sababu unanidanganya. Niambie kama unashida naweza kukusaidia

yes,I remember nilimuuliza nikiwa niko serious na nikiwa nataka majibu serious sababu mpaka pale sikuwa naelewa kitu zaidi ya kujiongeza ongeza mimi mwenyewe. Nikambana na kumwambia "niambie ukweli wote,you never know naweza nikakupa msaada ina case una matatizo fulani.

labda naweza kukusaidia kama utaweza. Kumbuka pale tumekaa ni kwenye kile kigenge cha chapati,hapo wateja hakuna tena wenyewe wapo wanamalizia kazi wafunge.Yule jamaa yangu yuko busy kuchati... Nikimuangalia Naa namuona kweli kuna vitu anataka kuniambia ila ana ogopa yaani.

Nikamwambia twende ndani ukaniambie akasema poa. Basi tukaagana na jamaa yangu yeye akaenda maghetoni mimi na Naa tukashika njia ya kwenda kivulini kumbuka tuna chumba tumelipia kule.

tukaingia ndani. Naa akaanza kuniambia kuwa ni kweli alinidanganya haji kwa baba yake anakuja kwa mwanaume anayetaka kumuoa na pale alipo ametoroka home na shule pia yaani kaacha shule anakuja kuolewa na yule mwana wa Mbezi😳.

nikamuuliza sababu ya kutoroka nyumbani na kuacha shule ni nini hasa akaniambia ni maisha magumu anayoishi Mkoa X na mama yake.

akanipa kwa ufupi kuwa baba yake alimtelekeza yeye na mama yake yeye akiwa mdogo kabisa. Na baba yake akaja Dar es salaam kutafuta maisha mengine from that day hajawahi kumuona baba yake ila huwa anasikia yupo dar alisha oa mwanamke mwingine ila hajawahi kuonana nae.

baada ya baba kusepa alibaki na mama ambaye by that time aliniambia mama yake ana maisha magumu sana. Na shule anayosoma Naa ni shule tu hizi za kata ile alivyoniambia kuwa anasoma shule ya ma sister ni kamba tu alinipiga. Kwa hiyo akaniambia na ana kama mwezi hayuko school...

amekosa ada ile 20,000/=. Amemsubiri sana mama yake apate hiyo 20,000/= ili arudi shule kashindwa. Yaani full machangamoto mzee,yaani life no gumu sana wazee...

huyu mwanaume wa mbezi ambaye sasa alikuwa anakuja kwake kuwa ni mpenzi wake wa siku nyingi ambaye huwa anafanya biashara so anakwenda sana mkoa X ndio walikutana na Naa wakashauriana demu asepe amfuate mchizi Dar es salaam amuoe kabisa. Kwa kifupi jamaa alikuwa anatorosha dent akamuweke

Unyumba. Nikamuuliza kwa hiyo home hawajui uko wapi akasema "hawajui".
Na shule pia wanajua yuko home anatafuta ada😳

Nikamuuliza ikitokea ukapata ada uko tayari kurudi shule akasema "hayupo tayari" hataki kusoma tena anataka kuolewa.

Kwa nini unataka kuolewa wakati wewe ni mtoto mdogo? Akaniambia yaani pale mkoa X.

Mimi na mama tunakaa chumba kimoja mama ana mpenzi wake,siku mpenzi wake na mama akija mama ananiombea nikalale kwa rafiki yake. Yale maisha yamenichosha sana,kama ni kurudi shule labda nirudi hostel.

Lakini sitaki kurudi mkoa X kabisa.

Hapo kumbuka nilipewa mwanzo pesa ya ada almost laki 5 hivi kutoka mkoa X anaoishi mama yangu me.
Laki 4 na nusu kwa ajili ya ada na elfu 50 balance ya matumizi kwenye safari.

Pesa zote nilizokuwa natumia pamoja na Naa nilikuwa natumia ile pesa ya ada. Vyakula usafiri plus na guest per day 24hours ilicost kwa siku moja elfu 15000 na mpaka mda uo teyal tushakaa guest kama siku 2 hivi.

Na jumatatu natakiwa nilireport shuleni lakini pia niende kwa dada japo anione tu.

Na huku Naa anasema hataki kurudi mkoa X anapotokea yeye kama jamaa yake atapatikana basi ataenda kwa jamaa kuolewa.

Hapo teyal nishaila kama laki 2 hivi na sent sent kwenye jiwe 5.

Gusa hapa kupata muendelezo 👇👇👇👇👇👇
Post in thread 'Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike' Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike
 
Msalato, Huruma & Nkuhungu secondory kwa pale Dodoma ni viwanda vya uzinzi.. ABC UPPER CLASS
😁😁😁 Dodoma tena imekuja kuja vipi mkuu wakati nimesema mkoa X sio dodoma 😁😁😁
 
Back
Top Bottom