Kuna maisha ambayo sometimes uchoyo ni lazima ,mfano watoto wa majirani wanakesha kwako kila siku kwenye tv, wa kwako haendi kuzunguka huko.
We unapambana unarudi na 5,000 . Unanunua unga ,mafuta mboga na ndizi 4 ya mtoto hela imeishia hapo . Sasa bajeti ya mtoto wako ufanye ndogo ale kwa shida wakati hao watoto pia wana wazazi wao?
Hivo hivo mtu anakupiga sound ya kukopa we unamhurumia unajinyima mwisho wa siku halipi anakupiga chenga.
Kuna wakati nilikuwa chuo nakaa na jamaa ,yeye hela zake hapiki , kuchanga hataki ,umeme halipi hata matunda mawili ya kuzugia kwamba leo mle pamoja ,we mwenye hitaji utaweka yeye akirudi anajimegea,hela zake zinaishia kwa malaya na pombe ,mwisho wa siku unamlisha mtu mzima ,friji ya kwako umeme unalipa wewe kama siyo upuuzi ni nini?
Mtu mwenye shida anasaidiwa na unajua huyu anastahili na amekwama lakini siyo wapuuzi ambao wanatumia advantage ya udhaifu wako.