Icho chakuuza kufika milioni ndo sina namimi binti najitafuta mamilioni kuyalipa siwezi labda Namimi niingie kwenye mikopoDah inasikitisha sana sometime wazazi wanakera badala ya kuwa mfano mzuri kwa watoto wanakuwa mwiba mchungu!
Njia nzuri ya kukabili tatizo ni kulitatua fanya namna ulipe madeni yote hata kama ni kwa kuuza vitu au rehani. Madeni yaishe akirudia acha apambane mwenyewe.
Ndio hivyo kaka maarifa muhimu mambo kama haya yanatokea hapa tunajifunza kuyatatua.Nipo kaka tupo hum kupata maarifa
Hii njia itamsaidiakama utaweza acha kujihusisha na mikopo yake au kumuuliza chochote kuhusiana na anakopeleka fedha anazokopa, ukiweza usimpe fedha kuliko kipato chako.
Dunia inaenda kasi sana tunahitaji maarifa kila siku changamoto kama hizi ningum sana hasa linapomhusisha mzaziNdio hivyo kaka maarifa muhimu mambo kama haya yanatokea hapa tunajifunza kuyatatua.
anha kumbe we binti, Pole sana dadaetu kiukweli ni changamoto, chakufanya mhimize mama aache hio tabia hata kama ukimwambia ananuna inabidi umwambie.Icho chakuuza kufika milioni ndo sina namimi binti najitafuta mamilioni kuyalipa siwezi labda Namimi niingie kwenye mikopo
Pole sana mkuu. Kama mtu hajapitia hii hali, hawezi kukuelewa.Wanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.
Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.
Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.
Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.
Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.
Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.
Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.
Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.
Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.
NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
ni kweliAsimuendekeze. Muache nyumba iuzwe. Jamaa abadili line na kuachana na huo upumbavu. Wajinga waliozeeka sio wa kuwaendekeza.
Na wewe hebu ondoa ujinga wako... Babaako aliuza ng'ombe kisha akakupeleka ng'ombe wewe shuleMsijikute smart sana, watu wako kwenye matatizo unataka waanze kutafuta italic na times new roman? Pumbaf
Duu pole sana hili tatizo siyo la mama yk peke Yako ni janga la kitaifa la akina mama wengi wa kitanzania wameathirika na mikopo, hii mikopo ipo milangoni mwao , wakisikia mikopo wanajifunga vibwebwe mbio kwenye mikopoWanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.
Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.
Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.
Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.
Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.
Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.
Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.
Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.
Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.
NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Inahuzunisha sana mama angu sijui anashida gani ananiweka kundi gani binti yake roho inaniuma saanaUmenikumbusha nilimwambia mama wakati huo mimi sitaweza kumsaidia ngoja nijaribu kupambana ili mbele yasafari akikosa nguvu zakujipambania nimsaidie bahati mbaya mpaka leo bado sijatoboa mkuu achana nae ukiendelea huyo mama mwisho utakata tamaa yakuishi
Hajamtupa mama yake ila mama kajitupa mwenyewe. Siku zote wema ukizidi uwezo huwa unakuwa ujinga.Pole sana. Unayopitia ni makubwa. Endelea kutafuta ushauri huku na huko. Maana mama huwezi mtupa.
ShukraniPole kwa chnagmoto unayopitia.
Nimepangialia andiko lako, ili kuwarahisishia wadau wengine:
---
Hali Yangu ya Sasa na Uchungu Moyoni
Wanajamii, sijui hata nianze vipi, natamani kulia na kupiga ukunga ili wote mjue jinsi ninavyoumia ndani kwa ndani. Uchungu nilionao ni mkubwa na ninatamani kupata mtu wa kumueleza, lakini nahofia kuchekwa. Sina kaka, dada, wala mdogo; nimezaliwa peke yangu. Hii hali imeninyima amani kabisa, nina maumivu makali moyoni na nahisi aibu kubwa hata kuwaeleza marafiki. Kama kungekuwa mahali pa kulilia, ningekwenda ili huu uchungu uishe.
Tatizo Sugu la Mikopo ya Mama
Kiini cha haya yote ni mama yangu kuwa na tabia ya kukopa kupita kiasi. Hali hii ilizidi baada ya baba kufariki, ingawa hata awali aliwahi kufilisiwa na baba akalazimika kulipa madeni yake. Alipoelemewa na madeni Dar es Salaam, alikimbilia kijijini, lakini kumbe na huko aliendelea na tabia hiyo ya kukopa bila hata kunijulisha. Mara nyingi huniambia anaumwa ili nimtumie pesa, nami kama ninayo huwa natuma.
Mkopo Mpya na Tishio la Kupoteza Nyumba
Kilichonisukuma kuwaandikia leo ni kuhusu mikopo mipya aliyoichukua Desemba kutoka kampuni mbili tofauti: moja ya Shilingi milioni 1.4 na nyingine ya Shilingi milioni 1, ambazo anatakiwa kurejesha kila wiki. Pesa hizi sijui hata alizifanyia nini maana nyumbani kijijini hakuna chochote cha maana zaidi ya kitanda na godoro. Watu wa mikopo walifika nyumbani wakitaka kuiuza nyumba aliyoiweka rehani. Kutokana na hilo, mama amekimbia (leo ni siku ya tatu) na hapatikani kwenye simu yake; inasemekana amekimbilia mashambani. Jana alifanikiwa kunipigia kwa namba ngeni akidai anaumwa sana miguu hawezi kutembea, nikamtumia Shilingi 20,000 kwa ajili ya matibabu, kumbe ilikuwa ni njia yake ya kunipiga kizinga tu.
Changamoto Zangu Binafsi za Kimaisha na Kipato
Mimi mwenyewe hali yangu si nzuri. Nilijitahidi kulipa baadhi ya madeni yake nikiwa chuo kwa kutumia pesa ya 'boom' na faida ya vibiashara vidogo nilivyokuwa nafanya, lakini mtaji uliisha. Kwa sasa sina kazi rasmi, nina kigenge kidogo tu ambacho napambana nacho lakini hakikui; hali yangu ni ileile kila mwaka, hata kunywa soda ni anasa. Ninaishi peke yangu katika chumba cha kupanga, napambana na ugumu wa maisha ya mjini lakini sioni maendeleo. Uwezo wa kulipa haya madeni mapya sina kabisa.
Changamoto ya Mawasiliano na Mama Kuhusu Madeni
Pia, kuna changamoto kubwa ya mawasiliano. Nikijaribu kumuuliza kuhusu mikopo yake, huwa mkali sana, tunaishia kugombana na anaweza kukata mawasiliano kabisa kwa kutokupiga simu.
Ombi la Ushauri: Nifanye Nini?
Wanajamii wapendwa, nimefika mwisho wa akili. Naomba sana msaada wenu wa mawazo: Nifanye nini ili kumsaidia mama aache hii tabia ya mikopo? Na nitawezaje kukabiliana na haya madeni mapya wakati uwezo wangu ni mdogo? Nimekuwa nikimuombea sana abadilike, lakini hali bado ni ileile. Nimechanganyikiwa na sijui nini cha kufanya. Tafadhali nishaurini.
Yah ni kweli kabisa usemacho,kuna wa baba wengi wamekubwa na mfadhaiko wa akili sababu ya madeni ya wake zao yasiyoisha.Duu pole sana hili tatizo siyo la mama yk peke Yako ni janga la kitaifa la akina mama wengi wa kitanzania wameathirika na mikopo, hii mikopo ipo milangoni mwao
Kwanini mikopo Iko milangoni kwasababu wakopeshaji ni matapeli wamegundua watu wengi yajishughulishi wanao kopesha wanafurahia zaidi kuwakopesha wanawake