Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 21,593
- 46,759
Msomi hawezi kuuza genge??Huu mwandiko sio wa muuza genge,wewe ni msomi na una kazi nzuri tu,kuwa wazi hatukurogi
Wauza genge pia wanapata maokotoHuu mwandiko sio wa muuza genge,wewe ni msomi na una kazi nzuri tu,kuwa wazi hatukurogi
Yupo na addiction ya mikopo yaani hapo hana tofauti na mcheza kamali..Wanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.
Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.
Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.
Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.
Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.
Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.
Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.
Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.
Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.
NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Huyu ana kazi nzuri tu usimsikilizeMsomi hawezi kuuza genge??
Liko wapi hilo andiko mkuu kama hutajali?Duu pole sana hili tatizo siyo la mama yk peke Yako ni janga la kitaifa la akina mama wengi wa kitanzania wameathirika na mikopo, hii mikopo ipo milangoni mwao , wakisikia mikopo wanajifunga vibwebwe mbio kwenye mikopo
Kwanini mikopo Iko milangoni kwasababu wakopeshaji ni matapeli wamegundua watu wengi hawajishughulishi wanao kopesha wanafurahia zaidi kuwakopesha wanawake
Mikopo kausha damu:
Hii mikopo inageuka mikopo kausha damu endapo maingizo yako ya Kila siku ama kwa mwezi hayawezi kuresha mikopo kwa muda husika
Mimi nimelifuatilia hili la mikopo kwa kina na Nina andiko lake nilidhani ni fursa y kuelimisha jamii elimu ya ujasiriamali, hiyo fursa haipo mifumo hairuhusu matapeli na wajuaji ni wengi
Una point.Mchukue uishi naye boss
Wanawake jinsi wanavyokua uwezo wao wa kufikiri hupungua kwa kasi
Inawezekana kuna mwamba amemteka mama anamtuma akope
Ndio boss mwanamke anahitaji mtu wa kumuongozaUna point.
Huyu ni mtu kama sio wapili ni watatu nasikia analalamika mama yake kuzidiwa na mikopo. Kuna jamaa mmoja nafahamiana nae alinieleza kesi karibu kama hii hii kuhusu mama ake anakopa sana na anachofanya hakijulikani. Sema huyo jamaa yeye ana ka uwezo kwahiyo hua anamlipia lakini inachosha sana.
Kuna mwingine alinisimulia mama mkwe wake amekamatika kwa wauza madawa haya ya kienyeji kila siku anapigiwa simu atume hela akiuliza za nini anaambiwa za deni la dawa. Akidadisi zaidi mama anakua mkali inabidi atume tuu.
Ni changamoto hawa wamama.
Shida roho inaniuma sana naona kama atapata presha atafariki nachanganyikiwa mmYupo na addiction ya mikopo yaani hapo hana tofauti na mcheza kamali..
Hapo kazi unayo ni kumuomba Mungu tu.. ila ata wakiuza nyumba bado ataendelea kukopa hukohuko kijijini anapokimbilia..
Mimi nakushauri fanya maisha yako hesabu una hasara kwa mzazi basi..
Ninalo cha ajabu fursa za mikopo zinakuja wakati uchaguzi unakaribia baada ya uchaguzi unaachwa uteseke hata hivyo hiyo mikopo imekaa kimitego mitego tu ni wachache tu wanaofaidika, wanaishi kwa matumaini Hadi uchaguzi unapitaLiko wapi hilo andiko mkuu kama hutajali?
Yeye sindoatakufa maan nyumbn kakimbia anaishi mashambani uko anakula nn sasa anaish vip kupata magonjwa ya moyo
Ata uyu mama alikuwa uku mjini pi alikopa ndo kakimbilia kijijin naiyo nyumba utaishi vip bila kuhangaika kutafuta rizikiVijana wengine sijui mmerogwa?? Baba yako ashafariki, nyumba, mashamba n.k vipo. Mama yako yupo mwenyewe na hana chochote cha maana anachofanya. Hakuna ndugu yeyote wa kukaa nyumbani na kulinda mali za familia. Wewe badala ya kurudi ukakaa nyumbani uongoze na kusimamia familia na vitega uchumi vilivyopo unakimbilia mjini kuuza genge, kupanga nyumba na kuishi kwa tabu. Tatizo ni wewe na si mama yako. Rudi kijijini simamia mji. Unatakiwa kujua wazazi wakikua wanahitaji kusimamiwa na sisi watoto wao.