Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Huyo mama atakuwa mchaga?
 

chabkufanya kama nyumba ipo dar taja location watu tujekuona ila kama mkoani kwa mm sina ofa chukua mawazo yawatu uzeni nyumba kila mtu apasuke kivyake
 
Amenitafuta nimenweleza kasema atalipa anafanya vibarua apate ela alipe ayupo tayar nyumba kuuzwa nikamwambia mm sina chakusema pambana na mm sina ela unajua hsli yangu
Yaah ulifanya vyema mkuu, ni kheri kua muwazi maana bila hivyo nyote mtaishia hivyo na wewe utakopa huku ulipe kule.
 
Wazazi walio wengi wanakopa coz wanajua hata nikishindwa kulipa watoto watalipa
 
Watu mnajua kuendekeza watu haijalish ni nani akivuka mipaka kaa mbali nae kabisa
 
NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Hachezi dubwi kweli huyu?
 
Watu mnajua kuendekeza watu haijalish ni nani akivuka mipaka kaa mbali nae kabisa
Ndugu yangu kakopa mikopo 7 na waliomkopesha wanamuogopa maana akili zake wamekuja kugundua ni 2 kwaa hio tumeanza kusakwa ndugu, mikopo 7 na haijulikani pesa kafanyia nini mamillion kayachezea tu
 
Pole sana, mtu akifikia hatua hiyo inahitajika nguvu ya ziada kwanza atambue shimo alilomo na jinsi ya kuzuia asizidi kuzama humo. Kama ana ndugu zake kaka ama dada zake washirikishe ila wewe mwenyewe hutaweza, ila atazidi kukuumiza kwa kukukamua hela kwa visingizio mbalimbali na usipotuma roho itakusuta na ukituma unajua baki kabisa hiyo pesa siyo kwa alichoombea
 
Fanya ibada ya kumpiga makofi huyo mama yako uenda ukamwokoa kwa hayo.makofi utakayo mchapa ..maana hata ungekuwa doctor na mama yako angekuwa na kansa ya mkono ungeukata huo mkono kuokoa maisha ya mama yako ....tena imeandikwa ni bora kupoteza mkono au jicho au mguu kuliko kuingia hatiani mbele za mungu hivyo chapa makofi huyo mama yako makofi makali haswa hadi ache upumbavu.
 
Ndugu yangu kakopa mikopo 7 na waliomkopesha wanamuogopa maana akili zake wamekuja kugundua ni 2 kwaa hio tumeanza kusakwa ndugu, mikopo 7 na haijulikani pesa kafanyia nini mamillion kayachezea tu
Asa ndugu mmehusikaje??si wamdai wao akope mwingine walipe wengine
 
Acha kujishughulisha na mikopo yake hapo ndipo anapata kiburi fanya mambo yako Wacha afisa mikopo wafanye wanachotaka kufanya utazeeka Kwa ajili ya kusaidia matatizo ya wengine kisa et ni mama mzaz
 
achana naye ili akili imkae sawa,huwezi pata tatizo la afya ya akili kisa mtu mmoja
 
Hii hali ndiyo anayopitia mama mkwe wangu
Ila Mimi Huwa sihangaiki kabisa nilishajisema kama ni nyumba iuzwe tu
Jinsi ulivyoeleza ndivyo na mama mkwe wangu anapitia mpaka na kampuni ni hizohizo
 
Huyo mama yako atakuwa anahonga ndio maana huoni anachofanyia pesa za mikopo.(Ukweli mchungu)

Badili namba ya simu kwa hata mwaka mmoja tu asikupate hewani na kukueleza sound zake,baada ya hapo resume mawasiliano naye mwambie ulikuwa nje ya nchi kiutafutaji otherwise wewe na mama yako mnaenda kufa masikini.

Mwisho endelea kuomba Mungu kwa Imani yako kama ni mkisto nenda kanisani kamlilie Yesu na kumweleza shida zako halikadhalika kama ni mwislamu nenda msikitini kamweleze Allah.

Na endapo huna Imani pole sana..kaza mkanda wa suruali vyema kabisa.
 
Mzee mleta Mada ni binti
 
Acha nyumba iuzwe na yeye atafute pa kuishi maana hata ukipambana ukilipa bado atakopea tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…