DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Hii ni tathmini yangu ya mambo 10 tuliyoyashuhudia katika matamasha ya Simba Day na Yanga Day.
1. Ni wazi mauzo ya jezi mpya za Yanga siyo mazuri. Jezi za Simba zimeuzika saana. Kuna tukio la Yanga la ugawaji jezi mpya bure kwa waliojitolea kutoa damu halafu anayesimamia ugawaji wa hizo jezi yeye mwenyewe amevaa jezi ya zamani.
2. Kitendo cha Simba kususia siasa katika mpira kitaigharimu. Simba ijiandae kupigwa shoti katika ligi ya ndani na hata kimataifa pamoja na ukweli kwamba hata mashabiki wa Yanga hawakuonyesha kuunga mkono siasa ila Azam TV walidhibitiwa ili hilo lisionekane.
3. Tamasha la Simba lilikuwa bora sana. Mpangilio, sauti, nidhamu ya muda, machaguo ya watumbuizaji, nk. Tamasha lilikuwa na class fulani hivi ya juu.
4. Tamasha la Yanga ni ama wanafanya maksudi, kutojali au hujma ili liwe baaaya. Sauti mbaya, kutojali muda, kejeli zilizopitiliza, watu wanapayukapayuka tu bila kuwa na mwongozo, machaguo yasiyo sahihi ya watumbuizaji, nk. Ni kama watu waliambiwa masaa manne kabla kuwa kuna tamasha, wakajiamua wafanye nini. Wachezaji wa Yanga walitokea uwanjani kabla hawajatambulishwa. Kuna wakati Zuchu ana perform, kule nyuma mafataki yanalipuka, wakati huo huo wachezaji wanafanya mazoezi, Zuchu anaamuru taa zizimwe (sijajua usalama wa wachezaji ulikuwaje wakati wanakimbia kwenye giza) ikafika wakati hawakusikilizi kwa hiyo inaonyesha haikufanyika rehearsal. Mechi nayo ilianza 8:48 pm, haya ni maajabu. Sina uhakika kama kwenye ndondo cup hili linafanyika.
5. Kutokana na kilichotokea katika Simba Day, Simba itaenda kupoteza mchezo wa ngao ya jamii. Picha litaanza Kayoko ndiye atatangazwa kuwa mwamuzi wa kati.
6. Simba iwaangalia kwa jicho la tatu wachezaji wafuatao....Kibu, Hamza, Chasambi na Sowah. Kama hujma itafanyika, itapitia hapa.
7. Simba itaendelea kuwa na makandokando hadi pale itakapomfukuza Mangungu
8. Manara ana wasiwasi na kikosi cha Yanga cha msimu huu ndiyo maana tofauti na kawaida yake aliweka akiba ya maneno
9. Yanga itatawala ligi ya ndani ila Azam naona anaweza kuwasumbua. Kimataifa nasita kutabiri ila sioni mwanga sana. Chikola anaenda kung'ara sana na unaweza kwenda kuwa usajili bora wa Yanga msimu huu.
10. Azam TV inaihujumu Simba, kuanzia kwenye mechi zake (matumizi ya camera, watangazaji, nk) hadi katika matamasha au shughuli za nje ya uwanja. Kwenye uzinduzi wa jezi nadhani walienda na camera 2 wakatupigia li wide moja karibia tukio zima. Juzi kwenye tamasha matukio mengi hayakuonyeshwa, kuanzia show ya mataa walienda kwenye drone ya mbali pekee na hawakutuonyesha kwa ukaribu kilichokuwa kinatokea uwanjani. Wakati wa muziki walikuwa wanaonyesha shot za mshabiki ambaye hafanyi lolote la maana kwa karibu nusu dakika bila sababu. Hawakuonyesha shot hata moja ya kikosi kizima muda wote wa utambulisho. Hii haiwezi kuwa bahati mbaya.