Mambo 10 niliyoona kuhusiana na matamasha ya Simba Day na Yanga Day

Mambo 10 niliyoona kuhusiana na matamasha ya Simba Day na Yanga Day

Hii ni tathmini yangu ya mambo 10 tuliyoyashuhudia katika matamasha ya Simba Day na Yanga Day.

1. Ni wazi mauzo ya jezi mpya za Yanga siyo mazuri. Jezi za Simba zimeuzika saana. Kuna tukio la Yanga la ugawaji jezi mpya bure kwa waliojitolea kutoa damu halafu anayesimamia ugawaji wa hizo jezi yeye mwenyewe amevaa jezi ya zamani.

2. Kitendo cha Simba kususia siasa katika mpira kitaigharimu. Simba ijiandae kupigwa shoti katika ligi ya ndani na hata kimataifa pamoja na ukweli kwamba hata mashabiki wa Yanga hawakuonyesha kuunga mkono siasa ila Azam TV walidhibitiwa ili hilo lisionekane.

3. Tamasha la Simba lilikuwa bora sana. Mpangilio, sauti, nidhamu ya muda, machaguo ya watumbuizaji, nk. Tamasha lilikuwa na class fulani hivi ya juu.

4. Tamasha la Yanga ni ama wanafanya maksudi, kutojali au hujma ili liwe baaaya. Sauti mbaya, kutojali muda, kejeli zilizopitiliza, watu wanapayukapayuka tu bila kuwa na mwongozo, machaguo yasiyo sahihi ya watumbuizaji, nk. Ni kama watu waliambiwa masaa manne kabla kuwa kuna tamasha, wakajiamua wafanye nini. Wachezaji wa Yanga walitokea uwanjani kabla hawajatambulishwa. Kuna wakati Zuchu ana perform, kule nyuma mafataki yanalipuka, wakati huo huo wachezaji wanafanya mazoezi, Zuchu anaamuru taa zizimwe (sijajua usalama wa wachezaji ulikuwaje wakati wanakimbia kwenye giza) ikafika wakati hawakusikilizi kwa hiyo inaonyesha haikufanyika rehearsal. Mechi nayo ilianza 8:48 pm, haya ni maajabu. Sina uhakika kama kwenye ndondo cup hili linafanyika.

5. Kutokana na kilichotokea katika Simba Day, Simba itaenda kupoteza mchezo wa ngao ya jamii. Picha litaanza Kayoko ndiye atatangazwa kuwa mwamuzi wa kati.

6. Simba iwaangalia kwa jicho la tatu wachezaji wafuatao....Kibu, Hamza na Sowah. Kama hujma itafanyika, itapitia hapa.

7. Simba itaendelea kuwa na makandokando hadi pale itakapomfukuza Mangungu

8. Manara ana wasiwasi na kikosi cha Yanga cha msimu huu ndiyo maana tofauti na kawaida yake aliweka akiba ya maneno

9. Yanga itatawala ligi ya ndani ila Azam naona anaweza kuwasumbua. Kimataifa nasita kutabiri ila sioni mwanga sana. Chikola anaenda kung'ara sana na unaweza kwenda kuwa usajili bora wa Yanga msimu huu.

10. Azam TV inaihujumu Simba, kuanzia kwenye mechi zake (matumizi ya camera, watangazaji, nk) hadi katika matamasha au shughuli za nje ya uwanja. Kwenye uzinduzi wa jezi nadhani walienda na camera 2 wakatupigia li wide moja karibia tukio zima. Juzi kwenye tamasha matukio mengi hayakuonyeshwa, kuanzia show ya mataa walienda kwenye drone ya mbali pekee na hawakutuonyesha kwa ukaribu kilichokuwa kinatokea uwanjani. Wakati wa muziki walikuwa wanaonyesha shot za mshabiki ambaye hafanyi lolote la maana kwa karibu nusu dakika bila sababu. Hawakuonyesha shot hata moja ya kikosi kizima muda wote wa utambulisho. Hii haiwezi kuwa bahati mbaya.
umejitahidi kuandika mambo ya kweli ila umeongeza na ushabiki kwa kiasi fulani na hivyo kufanya maoni yako yakose mashiko.
 
Hii ndo sababu mkuu Yanga wao inakuwa rahisi kufanyiwa yale ya ziada kwasabau ya mikataba yao na hata vile walishawauzia Azam video contents wakati huko Simba nasikia mligomaga kufanya hivo.
Wananikwaza sana maana wanafanya kama wamelazimishwa.

Niliwahi kutoa ushauri kuwa idara ya habari ya Simba iwe na mtu au watu maalumu wa kufuatilia jinsi matukio ya Simba yanavyorushwa. Ikibidi, anatakiwa akae nao katika chumba cha kurushia matangazo.
 
umejitahidi kuandika mambo ya kweli ila umeongeza na ushabiki kwa kiasi fulani na hivyo kufanya maoni yako yakose mashiko.
Ni tathmini binafsi kwa hiyo sitegemei kila mtu akubaliane na mimi. Ningeweka ushabiki unaosema, ungeona nasifia sana kikosi cha Simba ila sijafanya hivyo hata katika point moja.
 
Wananikwaza sana maana wanafanya kama wamelazimishwa.

Niliwahi kutoa ushauri kuwa idara ya habari ya Simba iwe na mtu au watu maalumu wa kufuatilia jinsi matukio ya Simba yanavyorushwa. Ikibidi, anatakiwa akae nao katika chumba cha kurushia matangazo.
Wao wanaiona Simba kama Mbeya City kaka huo ushauri hauwezi fanyiwa kazi yoyote.
 
Wao wanaiona Simba kama Mbeya City kaka huo ushauri hauwezi fanyiwa kazi yoyote.
Ni wazi wana ushirikiano mzuri na Yanga. Mechi za Yanga huwa wanakuwa na hadi camera za kuchukua reaction za mashabiki.

Naamini mkataba wao na Simba una vipengele ambavyo Simba inaweza kutumia kukazia ubora wa matangazo, tena kwa kulinganisha na urushaji wao wa matangazo wa mechi zingine ili kupata usawa.

Kwenye uzinduzi wa jezi nilishangaa walienda kwenye chumba cha picha yule mzee akawa anatoa maelezo ya picha za ukutani live wakati lile lilitakiwa litengenezewe kamakala kafupi badala ya kulipua vile. Nilishangaa sana.
 
Ni tathmini binafsi kwa hiyo sitegemei kila mtu akubaliane na mimi. Ningeweka ushabiki unaosema, ungeona nasifia sana kikosi cha Simba ila sijafanya hivyo hata katika point moja.
Ni maoni mazuri ila nilivyoona mimi 5-8 imekaa kishabiki, ushabiki sio kupendelea timu yako hata kuandika/kusema jambo lisilo na ushahidi au uhakika.

hoja zako nyingine ziko vizuri.
 
Ni maoni mazuri ila nilivyoona mimi 5-8 imekaa kishabiki, ushabiki sio kupendelea timu yako hata kuandika/kusema jambo lisilo na ushahidi au uhakika.

hoja zako nyingine ziko vizuri.

5. Kwenye hoja hii nimeangalia kitu deep sana nje hata ya mpira. Sitakielezea ila wanaojua wanajua nasema nini.

6. Ni tahadhari. Nilianza kusema Zimbwe angekwenda Yanga labda miaka miwili iliyopita na leo limetimia.

7. Ni wazi huyu kiongozi hafai kuwepo hapo Simba na sababu zipo nyingi.

8. Pamoja na makandokando yake mengi, utambulisho wake wa wachezaji ulikuwa unasema mengi.
 
Simba Hatuwezi Lazimishwa Siaza zikipumbavu kwenye Mpira
Hilo hatutakubari
Viongozi wa Simba wanajielewa
Huyu ni Rais wa nchi alikua nawasalimu raia wake,,kusanyiko la watu elfu 60 ni kubwa,,na hakuiombea CCM kura.

Msimu uliopita kwenye kusanyiko kama hili alifanya hivyohivyo kwa matamasha yote mawili, ni huyuhuyu Rais wa nchi aligharamia safari za timu zetu,Simba,yanga na timu za taifa.
 
5. Kwenye hoja hii nimeangalia kitu deep sana nje hata ya mpira. Sitakielezea ila wanaojua wanajua nasema nini.

6. Ni tahadhari. Nilianza kusema Zimbwe angekwenda Yanga labda miaka miwili iliyopita na leo limetimia.

7. Ni wazi huyu kiongozi hafai kuwepo hapo Simba na sababu zipo nyingi.

8. Pamoja na makandokando yake mengi, utambulisho wake wa wachezaji ulikuwa unasema mengi.
FIFA wanasema football is a game of fair play,,matatizo ya ndani ya timu yanaihusu timu yenyewe.
 
Hii ni tathmini yangu ya mambo 10 tuliyoyashuhudia katika matamasha ya Simba Day na Yanga Day.

1. Ni wazi mauzo ya jezi mpya za Yanga siyo mazuri. Jezi za Simba zimeuzika saana. Kuna tukio la Yanga la ugawaji jezi mpya bure kwa waliojitolea kutoa damu halafu anayesimamia ugawaji wa hizo jezi yeye mwenyewe amevaa jezi ya zamani.

2. Kitendo cha Simba kususia siasa katika mpira kitaigharimu. Simba ijiandae kupigwa shoti katika ligi ya ndani na hata kimataifa pamoja na ukweli kwamba hata mashabiki wa Yanga hawakuonyesha kuunga mkono siasa ila Azam TV walidhibitiwa ili hilo lisionekane.

3. Tamasha la Simba lilikuwa bora sana. Mpangilio, sauti, nidhamu ya muda, machaguo ya watumbuizaji, nk. Tamasha lilikuwa na class fulani hivi ya juu.

4. Tamasha la Yanga ni ama wanafanya maksudi, kutojali au hujma ili liwe baaaya. Sauti mbaya, kutojali muda, kejeli zilizopitiliza, watu wanapayukapayuka(mechi ya simba ilipangwa kuanza saa ngapi na ikaanza saa ngapi?
 
Matamasha ya Yanga, Singida, Costa, KMC nk yangefanyika pamoja kwa siku moja ili kuokoa muda. Baada ya hapo ndiyo Mnyama Simba aungurume kufunga kazi
Tena kweli na ungeongeza na zile timu zingine 4. Wazo zuri na waliite GSM Day.
 
Back
Top Bottom