Mambo 10 niliyoona kuhusiana na matamasha ya Simba Day na Yanga Day

Mambo 10 niliyoona kuhusiana na matamasha ya Simba Day na Yanga Day

Simba Hatuwezi Lazimishwa Siaza zikipumbavu kwenye Mpira
Hilo hatutakubari
Viongozi wa Simba wanajielewa
Nakubali. Mashabiki washikilie hapo hapo maana viongozi nao ni machawa au wamejaa uoga na wana vingi vya kupoteza. Mkiwasimamia mkawakumbusha hamtaki ujinga, watakuwa wanafikiria mara tatu kabla ya kutenda au kusema jambo lolote.

Jana kwa mara ya kwanza niliona kwa macho yangu serikali inatetemeka.
 
Hii ni tathmini yangu ya mambo 10 tuliyoyashuhudia katika matamasha ya Simba Day na Yanga Day.

1. Ni wazi mauzo ya jezi mpya za Yanga siyo mazuri. Jezi za Simba zimeuzika saana. Kuna tukio la Yanga la ugawaji jezi mpya bure kwa waliojitolea kutoa damu halafu anayesimamia ugawaji wa hizo jezi yeye mwenyewe amevaa jezi ya zamani.

2. Kitendo cha Simba kususia siasa katika mpira kitaigharimu. Simba ijiandae kupigwa shoti katika ligi ya ndani na hata kimataifa pamoja na ukweli kwamba hata mashabiki wa Yanga hawakuonyesha kuunga mkono siasa ila Azam TV walidhibitiwa ili hilo lisionekane.

3. Tamasha la Simba lilikuwa bora sana. Mpangilio, sauti, nidhamu ya muda, machaguo ya watumbuizaji, nk. Tamasha lilikuwa na class fulani hivi ya juu.

4. Tamasha la Yanga ni ama wanafanya maksudi, kutojali au hujma ili liwe baaaya. Sauti mbaya, kutojali muda, kejeli zilizopitiliza, watu wanapayukapayuka tu bila kuwa na mwongozo, machaguo yasiyo sahihi ya watumbuizaji, nk. Ni kama watu waliambiwa masaa manne kabla kuwa kuna tamasha, wakajiamua wafanye nini. Wachezaji wa Yanga walitokea uwanjani kabla hawajatambulishwa. Kuna wakati Zuchu ana perform, kule nyuma mafataki yanalipuka, wakati huo huo wachezaji wanafanya mazoezi, Zuchu anaamuru taa zizimwe (sijajua usalama wa wachezaji ulikuwaje wakati wanakimbia kwenye giza) ikafika wakati hawakusikilizi kwa hiyo inaonyesha haikufanyika rehearsal. Mechi nayo ilianza 8:48 pm, haya ni maajabu. Sina uhakika kama kwenye ndondo cup hili linafanyika.

5. Kutokana na kilichotokea katika Simba Day, Simba itaenda kupoteza mchezo wa ngao ya jamii. Picha litaanza Kayoko ndiye atatangazwa kuwa mwamuzi wa kati.

6. Simba iwaangalia kwa jicho la tatu wachezaji wafuatao....Kibu, Hamza na Sowah. Kama hujma itafanyika, itapitia hapa.

7. Simba itaendelea kuwa na makandokando hadi pale itakapomfukuza Mangungu

8. Manara ana wasiwasi na kikosi cha Yanga cha msimu huu ndiyo maana tofauti na kawaida yake aliweka akiba ya maneno

9. Yanga itatawala ligi ya ndani ila Azam naona anaweza kuwasumbua. Kimataifa nasita kutabiri ila sioni mwanga sana. Chikola anaenda kung'ara sana na unaweza kwenda kuwa usajili bora wa Yanga msimu huu.

10. Azam TV inaihujumu Simba, kuanzia kwenye mechi zake (matumizi ya camera, watangazaji, nk) hadi katika matamasha au shughuli za nje ya uwanja. Kwenye uzinduzi wa jezi nadhani walienda na camera 2 wakatupigia li wide moja karibia tukio zima. Juzi kwenye tamasha matukio mengi hayakuonyeshwa, kuanzia show ya mataa walienda kwenye drone ya mbali pekee na hawakutuonyesha kwa ukaribu kilichokuwa kinatokea uwanjani. Wakati wa muziki walikuwa wanaonyesha shot za mshabiki ambaye hafanyi lolote la maana kwa karibu nusu dakika bila sababu. Hawakuonyesha shot hata moja ya kikosi kizima muda wote wa utambulisho. Hii haiwezi kuwa bahati mbaya.
Shirikisho la mpira duniani linapinga mambo ya kuhusisha siasa na mpira kwahyo UNATAKA watu wakumbatie siasa afu uchunguzi ukifanyika timu ifungiwe? ...kuhusu mechi ya ngao hata hao yanga tuliowaona wenyewe hawana maajabu mzee subiri tarehe 16 usiongee ukamala.,...
 
Tatizo litakua ni refa kua Kayoko?
Hao wachezaji wa kuwaangalia jicho lao la 3??
ubovu wa kikosi cha Simba?
Mangungu?
Serikali kuipendelea Yanga??

Hayo mambo 10 wenzio huyapanga kwa ustadi kwa kuzingatia mada wanayotaka kuwasilisha.
 
Malalamiko FC.

Mmeanza mapema sana.

Subiria kukandwa

Mods edit heading, toa mambo 10 andika malalamiko 10.

Kichwa cha habari kinasema mabo 10..... Ila maelezo yako ya ndani yamejaa unabii feki, malalamiko yasiyo na tija na kuiponda tu Yanga kama ilivyo kawaida yako! Badala ya hayo mambo 10 uliyo yaona kwenye hayo matamasha mawili!

Shida ni nini?
Binadamu hamna jema. Nimewatabiria Yanga mangapi mema katika point hizo 10, yote hayo hamjaona?
 
Nilivutiwa na title ya thread yako kwasababu nilikuwa ninatamani kuona mtu/watu watakao analyse hizi siku za Yanga na Simba day kuanzia kwenye maandalizi hadi aina ya wachezaji na mechi zilizochezwa. Ila sijakipata kile nilichotarajia kwenye uzi huu.
 
This attack of Azam TV is not hidden. Yesterday I confirmed this. Those who were on duty behind the microphones had words that were intended to ruin the Simba concert.
But if we go back to the basics of football, Simba are struggling a lot and you still don't have a good team.
Yanga wana team bora sana
 
Waambie kwa kiswahili ili wengine waelewe vizuri.

Hii hoja ya hujma ya Azam nimeielezea mara nyingi sana na nimejiridhisha kwa kulinganisha jinsi wanavyorusha matangazo ya matukio na mechi za timu nyingine mfano Yanga.
 
Nilivutiwa na title ya thread yako kwasababu nilikuwa ninatamani kuona mtu/watu watakao analyse hizi siku za Yanga na Simba day kuanzia kwenye maandalizi hadi aina ya wachezaji na mechi zilizochezwa. Ila sijakipata kile nilichotarajia kwenye uzi huu.
Nashukuru kwa kusoma. Hoja zinaletwa ili zijadiliwe na siyo mleta mada amalize kila kitu na wengine wasome tu.
 
Waambie kwa kiswahili ili wengine waelewe vizuri.

Hii hoja ya hujma ya Azam nimeielezea mara nyingi sana na nimejiridhisha kwa kulinganisha jinsi wanavyorusha matangazo ya matukio na mechi za timu nyingine mfano Yanga.
Sawa kwa hili nakuunga mkono nadhani ni mipango maalum.
 
Sawa kwa hili nakuunga mkono nadhani ni mipango maalum.
Inawezekana ni migongano ya kibiashara kati ya wawekezaji walio nyuma ya hizo taasisi mbili. Azam TV wanatukosea sisi tunaonunua vifurushi vyao na hatuhusiki na hiyo migongano yao.
 
Inawezekana ni migongano ya kibiashara kati ya wawekezaji walio nyuma ya hizo taasisi mbili. Azam TV wanatukosea sisi tunaonunua vifurushi vyao na hatuhusiki na hiyo migongano yao.
Hii ndo sababu mkuu Yanga wao inakuwa rahisi kufanyiwa yale ya ziada kwasabau ya mikataba yao na hata vile walishawauzia Azam video contents wakati huko Simba nasikia mligomaga kufanya hivo.
 
Back
Top Bottom