1. Timu yetu ya Simba imecheza vizuri sana kilichotugharimu ni sub, kiukwel hatuna wachezaji wazuri wa sub ndio maana kipindi cha pili sikushangaa kuona Yanga wakipata bao la pili
2. Yussuf Kagoma ni mchezaji mzuri sana lakini Simba isimtegemee sana kwa sababu pancha nyingi sana
3. Kocha wetu anatuudhi sana kwa sub zake, Yanga wanajivunia sana viungo wao na sub wana watu lkn sisi sub zetu ni Balua na Okajepha
4. Kama Ateba angekuwa anacheza na Elie Mpanzu huku Kibbu Dennis prmbeni wale węhu wangetafutana leo
5 Kibbu Dennis ni mchezaji wa quality ya juu mno lakini kocha anamchukulia poa na kumfanyia sub wakati ambao tunahitaji matokeo
6 Hakuna cha maana alichokifanya Jean Charles Ahoua leo zaidi ya kumpa wakati mgumu Ateba
7 Chamou, Okajepha, Mutale, Ngoma watupishe dirisha dogo
8. Camara kafungwa goli la babu, mm simlaumu, Chama aliingia muda ule kwa maelekezo ya washirikina na ndio maana baada ya hapo hakuonekana tena
9 Mechi na Prisons ndio inakwenda kumharibia kibarua Fahdu kwa ubishi na kutoshaurika
10 Leo kazi imefanyika sana nje ya uwanja sina wa kumlaumu, mapambano yaendelee