Mambo 10 yanayothibitisha kwamba Mungu yupo

Mambo 10 yanayothibitisha kwamba Mungu yupo

Mkianza kuleta mambo ya hukumu ndio mnachanganya watu, Mungu yupo ila hukumu haipo msiwatishe watu, dini hizi za watu zinafanya watu wakae mbali zaidi na Mungu zimekuwa zikiwatisha sana watu

Ukigeuka huku hukumu, ukienda kule mapepo , ukihudhuria misibani huko ndio kabisa kujazana hofu ni kwingi hofu tupu wakati kuna namna tunaweza ishi bila kutiana hofu,
Hukumu isipokuwepo huko mbinguni itakuwaje kwa watu waliodhulumiwa hapa duniani?
Mfano mdogo tu mtu kamuua baba yako na labda ana mamlaka huwezi kumfanya chochote hapa duniani, Mwenyezi Mungu asipohukumu huko akhera je wewe na huyo baba yako aliyeuliwa mtapata wapi haki yenu?

Au mtu kakuibia kisha kakimbia hujampata kusipokuwa na hukumu huko mbinguni wewe utafurahi?
HUKUMU ipo na haiepukiki
 
🤣Kuimagine kitu haikifanyi iwepo...we imagine vyote hivyo ila maisha ndo hayo hayo ndo maana hata huyo mchungaji anakuambia toa sadaka yeye anajenga hoteli ananunua magari ma body guard why? Anajua maisha ndo hayo...hizi fikra ndo zile za maskini unakuwa huna Cha kufanya unaishia kusema Mungu atalipa..na hizi ndo zinatufanya tuwe maskini...watu wanajilimbikizia Mali za umma we unasema utalipwa akhera nchi inakuwa maskini miaka nenda rudi kisa story za mroma na muarabu..

Wamarekani wangesema mungu atalipa anayofanya Hitler au Osama we unadhani dunia ya Leo ingekuwaje?
 
Ndio hakipo.

Je wewe unakubali kwamba Dragons šŸ‰ watemao moto midomoni mwao wapo?

Sisi hatudai, narudia tena kukwambia sisi Atheists hatudai hakuna Mungu.

Hivi wewe una elewa kiswahili?

Sisi Atheists tunapinga madai yenu ya kwamba "Kuna Mungu" kwa kukanusha na kusema "Hakuna Mungu"

Atheists HATUDAI hakuna Mungu, Bali TUNAKANUSHA madai yenu ya kusema kuna Mungu, kwa kusema hakuna Mungu.

Maana ninyi waamini Mungu ndio mlioanzisha kusema Mungu yupo.

Na sisi Wakana Mungu tunakanusha kwa kusema Mungu hayupo.

Kwa hivyo nyie Theists ndio mnapaswa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Mkishindwa kuthibitisha kwamba Mungu yupo, Ni kwamba Mungu hayupo.

Una elewa?
Dogo hapa mpaka utanielewa tu.

Ukisema kwamba nyinyi(atheists) mnakanusha na kupinga madai ya kwamba kuna Mungu, je ni kipi kinachofanya mpinge/mkanushe? Je ni kwa sababu mnajua kiuhakika hakuna Mungu ndio maana mnapinga hayo madai?
 
Hawaamini asili , wanaamini Mungu kupitia dini za za asili , hata ukristo ni dini ya asili ya wayahudi yaani waisrael na warumi . Hata uislam ni dini ya asili ya waarabu . Mifano michache nikupe wajapan dini ya asili ni Shinto na Tao , Wachina ni Buddha na Confunsionism , India ni Hinduism hii ndio oldest wanazo nyingi sana , Korea ni Shaman , Kila watu wana dini zao za asili , sema sasa wakoloni na dini zao za kuleta a.k.a mapokeo wamezipamba na kuzifanya zionekane Bora kuliko za Mwafrika kitu ambacho ni uongo mtupu.Kuamini dini ya asili yako ndio sahihi zaidi .Wakoloni walikuja na hila kuua dini za asili ili zao zionekane bora. Mfano mwingine mzungu asili yake ni kusali kanisani, mwarabu asili yake ni kusali msikitini Buddha ni Hekaluni, Wao wakristo na waislam kusali kwenye dini zao za asili ni sahihi ila Mwafrika kusali kwenye dini zake za asili wanakwambia dhambi, shetani, shirki kitu ambacho ni uongo mkubwa lengo ni kupata wafuasi hiyo ni ufupi .
Unaposema dini ya asili una maaanisha nini?
 
Suala la uwepo wa Mungu Muumba wa Mbingu na nchi halihitaji mjadala. Ni mpumbavu pekee atapinga uwepo wa Mungu.
 
Mimi sio dogo you halfwit.

Kwani wewe ni kipi kinacho kufanya useme kuna Mungu?

Ndio.
Kumbe mnapinga madai ya kuwepo Mungu kwa sababu mnajua hakuna Mungu na si kwa sababu tu kwamba sisi wenye kudai kuna Mungu hatujathibitisha madai, sasa mbona nikisema kuwa atheists wanadai hakuna Mungu unakataa? Kama mnajua wenyewe kiuhakika kuwa Mungu hakuna na mnasema kabisa kuwa HAKUNA MUNGU KAMA YUPO THIBITISHA? sasa kwanini mkatae madai yenu?
 
Mkianza kuleta mambo ya hukumu ndio mnachanganya watu, Mungu yupo ila hukumu haipo msiwatishe watu, dini hizi za watu zinafanya watu wakae mbali zaidi na Mungu zimekuwa zikiwatisha sana watu

Ukigeuka huku hukumu, ukienda kule mapepo , ukihudhuria misibani huko ndio kabisa kujazana hofu ni kwingi hofu tupu wakati kuna namna tunaweza ishi bila kutiana hofu,
Mafundisho kuhusu hukumu ya Mungu si ya kutisha watu, bali ni ya kutuongoza katika njia ya haki..

Biblia inaeleza wazi kuhusu siku ya hukumu (Mhubiri 12:14; Ufunuo 20:11-15). Hivyo tunapozungumza kuhusu hukumu, lengo sio kutisha watu bali kuwaonya kwa upendo ili waweze kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na hatimaye wapate uzima wa milele.
Ukiendesha gari barabarani ukaona alama ya onyo kwamba mbele kuna hatari, siamini kama utawalalamikia walioweka hiyo alama na kusema wasikutishe. Badala yake utapunguza mwendo na kuanza kuendesha kwa usalama. Vivyohivyo, mafundisho kuhusu hukumu ni kama tu alama za onyo/tahadhari barabarani.
 
Thibitisha uwepo wa huyo Mungu?
Uwepo wa Mungu upo ktk aina 5.
1. Nature inatangaza kuwa Mungu yupo
2. Sayansi na teknolojia inavumbua Ukuu wa Mungu
3. Biblia inaeleza na kumfunua huyo Mungu jinsi alivyo.
4. Ukitaka kumjua huyo Mungu unapitia kwa Yesu Kristo.
5. Ukitaka kuona udhihirisho wa Mungu nenda kanisani au kwenye mikutano/ Semina za Injili.
 
Huu ujinga usini nitag tena siku nyingine.
 
Uwepo wa Mungu upo ktk aina 5.
1. Nature inatangaza kuwa Mungu yupo
2. Sayansi na teknolojia inavumbua Ukuu wa Mungu
3. Biblia inaeleza na kumfunua huyo Mungu jinsi alivyo.
4. Ukitaka kumjua huyo Mungu unapitia kwa Yesu Kristo.
5. Ukitaka kuona udhihirisho wa Mungu nenda kanisani au kwenye mikutano/ Semina za Injili.
Safi sana
 
Back
Top Bottom