Mambo 3 muhimu ambayo Xi amemuonya Trump wakiwa ana kwa ana kwenye mkutano Beijing

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817

1. Xi alimuonya Trump kuhusu "Thucydides Trap."​

"Can China and the US overcome the Thucydides Trap"
–Xi Jinping​

Nini maana ya Thucydides Trap?​
  • Nchi mpya yenye nguvu inapoinuka, nchi kubwa ya zamani huanza kuhofu kupoteza nafasi yake na mvutano huongezeka.​

China inaendelea kukua kwa nguvu kiuchumi, kiteknolojia, na kijeshi.

Marekani inaona ukuaji huo kama tishio kwa nafasi yake duniani. Marekani ina wasiwasi kwamba China inaweza kuipiku au kupunguza ushawishi wake duniani.

Xi alikuwa akijaribu kusema China haitaki kurudia historia ya vita (Thucydides Trap) kama Sparta na Athens.

Vita kati ya mataifa yenye nguvu kubwa si lazima itokee. Mataifa yanaweza kuepuka mgogoro kupitia mazungumzo, biashara, na ushirikiano.

2. Xi alimuonya Trump kuhusu suala la Taiwan.
​

“Ikiwa Marekani haitashughulikia vizuri suala la Taiwan, inaweza kusababisha migongano na hata vita”
–
Xi Jinping​

Xi alisisitiza Marekani isivuke mstari kuhusu Taiwan. Kwa mtazamo wa China Taiwan ni suala muhimu zaidi katika uhusiano wa China na Marekani.​
20260516_060052.jpg

Baada ya mkutano na Xi

3. Xi alimuonya Trump kuwa "United States is a declining nation.”​

20260516_055203.jpg

Hili la "U.S is a declining nation" limemuuma sana Trump, ikabidi aandike gazeti kumtupia lawama Biden.

Trump na Marekani wakubali tu kuwa dunia ya sasa ni ya ushindani na sio ya utawala wa taifa moja. Rising Dragon, fading Eagle.

Wakati Xi akitoa hoja zenye mashiko na nzito zinazogusa China na Marekani na mustakabali wa dunia, hizi ni baadhi ya quotes za Trump alipokuwa na Xi:

​
"It’s an honor to be your friend."

"You are a great leader."

"We’re going to have a fantastic future together.”​

Huu mkutano umedhihirisha kuwa Xi is smarter than Trump kwa mbali sana na Marekani haina lolote la kuitambia China kwa sasa.​
 
Trump ni rais ambae analisababishia taifa lake litumie nguvu kubwa mno katika kujisafisha!,kujitetea na kujiimarisha!. Naweza kusema trump ni rais mwenye upeo mdogo haendani na dunia katika kusukuma kete zake ni kama rais tu wengi wao wa huku bara la giza!, akiamini matumizi ya nguvu, hisia n.k
 
hili taifa kubwa la China ni kipi wanajivunia kwa kukivumbua wao na kuuzia dunia?
Kwa Marekani kuna
Nuclear Bombs
F35
Boeing
A.I
Android
Windows
Mac
IOS
ARV’s
Internet
reUsable Rockets

Na mengine mengi mengi mengi kwenye sector ya Afya kama chanjo kede kede amabyo yamefanya binadamu tuweze kufika hapa
Kwa Upande wa China ni kipi alichonacho ambacho amefaidisha Dunia na kufanya apate jeuri mbele ya USA?
 
Marekani ni bingwa wakununua watu na vitu akishakuona unakitu unaweza kumsaidia basi yupo radhi akuhonge hata uraia!, fatilia asili za hao waliogundua hivyo vitu wengi wao utakuta sio raia asilia wa huko!
 
Trump ni rais ambae analisababishia taifa lake litumie nguvu kubwa mno katika kujisafisha!,kujitetea na kujiimarisha!. Naweza kusema trump ni rais mwenye upeo mdogo haendani na dunia katika kusukuma kete zake ni kama rais tu wengi wao wa huku bara la giza!, akiamini matumizi ya nguvu, hisia n.k
Umesema vyema

Unajua nchi za Magharibi huwa zinashangazwa sana China, maana ni taifa ambalo limeibuka na kuwa na nguvu kiuchumi bila kutumia nguvu za vita kama wao.

Marekani wanaamini kwa kuwa Marekani ilinyanyuka na kuwa Superpower kwa njia ya mtutu basi ili kumaintain hilo waendelee kutumia matumizi ya nguvu. Dunia imebadilika

Tatizo lingine la Trump ni ego, mshindani wake kiuchumi anamwambia U.S is a declining state anamtupia lawama Biden

Kwa mtu mwenye upeo angeelewa Xi anachomaanisha na angemshukuru

Marekani kwa miaka 12 (Trump, Biden, Trump) imeongozwa na marais ambao hawaendani na dunia ya sasa

Raisi atakayekuja atakuwa na kazi ya ziada
 
Marekani ni bingwa wakununua watu na vitu akishakuona unakitu unaweza kumsaidia basi yupo radhi akuhonge hata uraia!, fatilia asili za hao waliogundua hivyo vitu wengi wao utakuta sio raia asilia wa huko!
Kwa sasa ni Raia wa Marekani na vitu vyote wametengeneza wakiwa Marekani,
Swali langu ni kipi hasa China alichonacho cha kuweza kutishia Dunia?
 
Kwa Marekani kuna
A.I
CEO wa NVIDIA Jensen Huang alipoulizwa: “How far is China behind the US in AI?” hili ndio jibu lake

“China is not behind! Remember that 50% of world’s best AI researchers are Chinese and many of those work at U.S.-based AI labs. This is a long race.
It would be a tremendous loss to miss the Chinese AI market."

-Nvidia CEO Jensen Huang

Nilichogundua unaipigia chapuo China ila “reality” China inategemea invention na innovation kutoka USA

Mpaka pale itakapokuja nchi ya kuiwekea vikwazo Marekani ila kwa sasa China bado ni mtengenezaji na muuzaji wa bidhaa kutoka Marekani
 
Hayo sio maneno yangu. Unabishana na Jensen Huang CEO wa NVIDIA?
 
Internet haikugunduliwa na mtu mmoja au nchi moja. Ni matokeo ya kazi ya watafiti wengi kwa miaka mingi
History umetoa kwenye kitabu kipi?

Swali jingine, wakati Marekani anafanya operation pale Straight of Hormuz na kuleta madhara ya Fuel Prices world wide nilitegemea China angeenda kumzuia
Wakati Marekani ananenda Kumteka Maduro nilitegemea China ingeenda kumzuia
Wakati Russia anawekewa vikwazo vya Kiuchumi nilitegemea Nchi kubwa na yenye uwezo kama China ingeingilia kati na kwenda kumzuia

Je mpaka leo ni kipi China amefanya cha kuionya Marekani kwa matendo yake hayo na kuiwekea vikwazo?
 
Kwa sasa ni Raia wa Marekani na vitu vyote wametengeneza wakiwa Marekani,
Swali langu ni kipi hasa China alichonacho cha kuweza kutishia Dunia?
China hatishii dunia china anaitishia marekani kwani hakutegemea likawa taifa lililoibuka nakuimarika kiuchumi,kisiasa na technology kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba kutishia ushawishi wakinguvu katika sekta hizo!, china inaendelea kujiimarisha nakuaminika duniani na hata bidhaa zake nyingi kukubalika Asia, Africa na mashariki ya kati.

Ukuaji wake wa jeshi unaipa kizungumkuti marekani!, ukweli ni kwamba ukiweza kuimarika ki technology na kiuchumi basi unaweza kuwa na nguvu kijeshi, china alishaweza hadi kupenyeza wapelelezi katika jeshi la marekani na mwengine miaka ya hivi karibuni walimshitukia akiwa ni pilot tena wa hizi ndege zao kubwakubwa wanazotambiana!.

Ndugu mambo ni mengi yanayomtishia marekani dhidi ya uchina hivyo hoja za kuwa tu na wavumbuzi wengi dunia ineshatoka huko!.
 
1. Xi alimuonya Trump kuhusu "Thucydides Trap."​

"Can China and the US overcome the Thucydides Trap"
–Xi Jinping​

Nini maana ya Thucydides Trap?​
  • Nchi mpya yenye nguvu inapoinuka, nchi kubwa ya zamani huanza kuhofu kupoteza nafasi yake na mvutano huongezeka.​

China inaendelea kukua kwa nguvu kiuchumi, kiteknolojia, na kijeshi.

Marekani inaona ukuaji huo kama tishio kwa nafasi yake duniani. Marekani ina wasiwasi kwamba China inaweza kuipiku au kupunguza ushawishi wake duniani.

Xi alikuwa akijaribu kusema China haitaki kurudia historia ya vita (Thucydides Trap) kama Sparta na Athens.

Vita kati ya mataifa yenye nguvu kubwa si lazima itokee. Mataifa yanaweza kuepuka mgogoro kupitia mazungumzo, biashara, na ushirikiano.

2. Xi alimuonya Trump kuhusu suala la Taiwan.
​

“Ikiwa Marekani haitashughulikia vizuri suala la Taiwan, inaweza kusababisha migongano na hata vita”
–
Xi Jinping​

Xi alisisitiza Marekani isivuke mstari kuhusu Taiwan. Kwa mtazamo wa China Taiwan ni suala muhimu zaidi katika uhusiano wa China na Marekani.​
View attachment 3589379
Baada ya mkutano na Xi

3. Xi alimuonya Trump kuwa "United States is a declining nation.”​

View attachment 3589378
Hili la "U.S is a declining nation" limemuuma sana Trump, ikabidi aandike gazeti kumtupia lawama Biden.

Trump na Marekani wakubali tu kuwa dunia ya sasa ni ya ushindani na sio ya utawala wa taifa moja. Rising Dragon, fading Eagle.

Wakati Xi akitoa hoja zenye mashiko na nzito zinazogusa China na Marekani na mustakabali wa dunia. Hizi ni baadhi ya quotes za Trump alipokuwa na Xi:

​
"It’s an honor to be your friend."

"You are a great leader."

"We’re going to have a fantastic future together.”​

Huu mkutano umedhihirisha kuwa Xi is smarter than Trump kwa mbali sana na Marekani haina lolote la kuitambia China kwa sasa.​
Umeandika na ka ushabiki kidogo. Technology yote ya china ni technologies za USA with some modifications!
UCHINA haijawahi gundua kitu from scratch! Ila wanaweza kuwa very innovative, wakiona kitu wanaiga na kukiboresha. Hawajawahi gundua lolote from scratch!

Kama alivyosema Japan kuwa "We do not have to invent the wheel, let innovate what others have invented/ discovered. Carnot cycle will remain as it is, let us revolve around that to suit our needs! Ndiyo wakabuni magari yao yote and the like in all fields of science and technology.
 
Back
Top Bottom