1. Xi alimuonya Trump kuhusu "Thucydides Trap."
"Can China and the US overcome the Thucydides Trap"
–Xi Jinping
Nini maana ya Thucydides Trap?
Nchi mpya yenye nguvu inapoinuka, nchi kubwa ya zamani huanza kuhofu kupoteza nafasi yake na mvutano huongezeka.
China inaendelea kukua kwa nguvu kiuchumi, kiteknolojia, na kijeshi.
Marekani inaona ukuaji huo kama tishio kwa nafasi yake duniani. Marekani ina wasiwasi kwamba China inaweza kuipiku au kupunguza ushawishi wake duniani.
Xi alikuwa akijaribu kusema China haitaki kurudia historia ya vita (Thucydides Trap) kama Sparta na Athens.
Vita kati ya mataifa yenye nguvu kubwa si lazima itokee. Mataifa yanaweza kuepuka mgogoro kupitia mazungumzo, biashara, na ushirikiano.
2. Xi alimuonya Trump kuhusu suala la Taiwan.
“Ikiwa Marekani haitashughulikia vizuri suala la Taiwan, inaweza kusababisha migongano na hata vita”
–Xi Jinping
Xi alisisitiza Marekani isivuke mstari kuhusu Taiwan. Kwa mtazamo wa China Taiwan ni suala muhimu zaidi katika uhusiano wa China na Marekani.
View attachment 3589379
Baada ya mkutano na Xi
3. Xi alimuonya Trump kuwa "United States is a declining nation.”
View attachment 3589378
Hili la "U.S is a declining nation" limemuuma sana Trump, ikabidi aandike gazeti kumtupia lawama Biden.
Trump na Marekani wakubali tu kuwa dunia ya sasa ni ya ushindani na sio ya utawala wa taifa moja. Rising Dragon, fading Eagle.
Wakati Xi akitoa hoja zenye mashiko na nzito zinazogusa China na Marekani na mustakabali wa dunia, hizi ni baadhi ya quotes za Trump alipokuwa na Xi:
"It’s an honor to be your friend."
"You are a great leader."
"We’re going to have a fantastic future together.”
Huu mkutano umedhihirisha kuwa Xi is smarter than Trump kwa mbali sana na Marekani haina lolote la kuitambia China kwa sasa.