Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Pamoja na kwamba tunaona Umati ni mkubwa na kujipa Moyo Kushinda ila tusijisahaulishe kuwa wengi ya hawa Watu hawajajiandikisha kwa Kura.
Mkuu wapiga kura kwa mujibu wa tume ya uchaguzi wako 29m+. Watanzania tuko 59m+, yaani wapiga kura ni nusu ya watanzania wote, yaani kila watanzania wawili mmoja kajiandikisha kupiga kura! Kwa maneno marahisi hakuna mtu aliye juu ya miaka 18+ ambaye hajajiandikisha kupiga kura.
Sasa hapa ni aidha ukubali kuwa tume ya uchaguzi imepika data za wapiga kura, au ukubali kwa shingo upande kuwa wote hao wana vitambulisho vya kura. Iwapo utakubali kuwa idadi ya wapiga kura ni 29m+, basi hoja yako kuwa watu hawana vitambulisho inakufa natural death. Na iwapo itabidi ukatae hiyo idadi ya tume kuwa ni ya kupika, basi hata matokeo watakayotangaza yatakuwa ya kupika. Hiyo inaitwa ukikaa nchale, ukisimama nchale. Habari ndio hiyo mtani. Iwe iwavyo, huu ni udhibitisho kuwa ccm haina uwezo wa kushinda uchaguzi wowote kihalali nchi hii zaidi ya 55%.