Uchaguzi 2020 Mambo 5 niliyoyabaini uzinduzi wa kampeni kanda ya Nyasa CHADEMA

Uchaguzi 2020 Mambo 5 niliyoyabaini uzinduzi wa kampeni kanda ya Nyasa CHADEMA

Pamoja na kwamba tunaona Umati ni mkubwa na kujipa Moyo Kushinda ila tusijisahaulishe kuwa wengi ya hawa Watu hawajajiandikisha kwa Kura.
Watanzania walio wengi tayari wana vitambulisho vya kupigia kura. Tume imesema waliojiandikisha kupiga kura ni above 26 milion.
Kilichopelekea watu wengi kujiandikisha ni ulazima na umuhimu wa Kitambulisho cha kura kwenye huduma mbalimbali.
 
Hi video haiendi sambamba na maneno ya lisu na matendo ya mashabiki. Kisha mbona video haionyeshi mwendelezo kutoka kwa mashabiki mpaka Lisu alipo?

5 September 2020
Mbeya , Tanzania

Mkutano wa Kampeni wa Uchaguzi Mkuu 2020

MBEYA YAVUNJA REKODI UZINDUZI WA KAMPENI, SUGU ASEMA KURA ZIPO, MBOWE ATEMA CHECHE, LISU MSIIGE SERA
 
1. Salumu Mwalimu ana ushawishi na hoja, sauti ya mamlaka kuliko Lissu

2. Tundu Lissu anakera, anakera na anakera haaswa. Nadhani anafanya kusudi kumchokonoa Magufuli asiuze sera amjibu na hivyo apoteze muda

3. Sugu anashinda uchaguzi huu kwenye box la kura, mapema kabla ya saa nne asubuhi

4. Mbeya na kanda ya Nyasa wamefunika nchi nzima kwa mapokezi ya CHADEMA

5. CHADEMA bado imara sanaaaaaaaaaa

View attachment 1559760
Point namba mbili, imefuta point zote tano ulizoziandika.
 
Hii nchi bhana, akienda JIWE nako watu watajaa zaidi ya hao...

Jiwe sasa anatumia hela, Fiesta na vitisho kwa watumishi wa serikali.. Lissu mwenzio wanamfata tu watu wenyewe. Hapo ndio watu wanapochoka.
 
Tunduma , Songwe
Tanzania

Kampeni za CHADEMA zapamba moto

Lissu ndio chanzo cha Yote. Walianza kwa Nyalandu wakashindwa, wakaja na Membe wakafeli. Wamehamia kwa Hashimu Rungwe Spunda mzee wa ubweche.

Eti sasa Salim anafaa zaidi. Tunajua anafaa na ndiyo maana ni mgombea mwenza lakini Lissu ni baba lao.

Kawasambaratisha mmepoteana. Ya chamia yangeanikwa bila fukuto la Lissu?

Tathmini zenu kwani hata tunazihitaji? Yawezekana hata kina makondakta, katawi na kina hipi wanaona chamia anafaa zaidi kuliko jiwe. Ni mzuri!

Na bado!
 
Hii nchi bhana, akienda JIWE nako watu watajaa zaidi ya hao...
Jiwe hupelekewa watu kwa malori na wana lipwa. Chadema watu hujipeleka wenyewe na hutoa sadaka. Hivyo, Ccm wana jidanganya
 
Pamoja na kwamba tunaona Umati ni mkubwa na kujipa Moyo Kushinda ila tusijisahaulishe kuwa wengi ya hawa Watu hawajajiandikisha kwa Kura.

Ndio mbeya hii

Sugu aliongoza kwa kura nyingi nchi nzima 2015

Lowasa akipata nyingi kuliko maeneo yote.

Ccm bila kuiba ovaeral hata 25% haipati.
 
Hii nchi bhana, akienda JIWE nako watu watajaa zaidi ya hao...
No kweli kabisa lakini ukiangalia vizuri kwenye picha utagundua kuwa waliohudhuri kwenye mkutano huo was Lissu wengi wao in vijana wakiume ambao wengi wao huwa hawaendi kupiga kura. Nimefuatilia mikutano ya JPM wengi ni akinamama, vijana na akinababa ambao tafiti zinaonyesha kuwa makundi haya hushiriki kikamilifu katika kupiga kura. Hivyo ushindi ni mahesabu na sio mafuliko ya vijana wahuni tu.
 
Pamoja na kwamba tunaona Umati ni mkubwa na kujipa Moyo Kushinda ila tusijisahaulishe kuwa wengi ya hawa Watu hawajajiandikisha kwa Kura.
Mkuu GENTA, Hoja yako ni nn hasa?? Unataka wajajiandikishe au siku ile muhimu wakawapigie kura Wapendwa wao??
 
Hii nchi bhana, akienda JIWE nako watu watajaa zaidi ya hao...
Kwa Jiwe Mkuu ni kwamba Watu wanasombwa na magari toka mikoa ya jirani. Nilishuhudia Arusha wakati Kassim Majaliwa alipokuwa akiendesha kampeni. Watu waliletwa toka Manyara na K'manjaro. Vijana wa bodaboda waliwekewa mafuta na makada wa ccm.

Upande wa Upinzani wanajitokeza wenyewe na wale vijana wa bodaboda wanajiwekea wenyewe mafuta wenyewe.
 
Pamoja na kwamba tunaona Umati ni mkubwa na kujipa Moyo Kushinda ila tusijisahaulishe kuwa wengi ya hawa Watu hawajajiandikisha kwa Kura.
NEC wanadai waliojiandikisha ni 30 million. Hao ni nusu ya raia wote wa Tanzania. Hii inaonyesha kuwa ni Watanzania wengi waliojiandikisha safari hii.
 
Lengo lako kuu ni kuonyesha Lissu hafai. Hayo mengine imebidi usifu tu Chadema ili uweze kuchota watu akili. Lissu ni tishio kubwa kwa Magufuli na mnatumia kila aina ya mbinu ku-discourage wapiga kura lakini hamtashinda.

Lissu anawakera, Lissu anawatetemesha na Lissu anawafanya msilale kwa raha. Hata Magufuli sasa hivi amesha-panic vibaya sana. Serikali na organs zake wamechanganyikiwa na walikuwa hawajui kama Lissu anakubalika namna hii.
Lissu hawezi shinda uchaguzi endeleeni kumdanganya kama ambavyo mlimdanganya Lowassa 2015
 
Lissu hawezi shinda uchaguzi endeleeni kumdanganya kama ambavyo mlimdanganya Lowassa 2015
Hakuna asiyejua kuwa nguvu za dola zitatumika. Lakini pamoja na hizo nguvu za dola bado lolote linaweza kutokea. Watu walivyochoshwa na utawala huu ulivyofanya maisha yawe magumu hawana cha kupoteza na kitu kidogo sana kinaweza kikaamsha mshikemshike mbaya sana. Najua watawala wengi wanajua watanzania wengi ni watu waoga hivyo wanaamini kuwa vitisho vinaweza kuwanyamazisha lakini ogopa nchi yenye watu wa aina hii. Hujui saa wala dakika. Mitaani kila mtu anaugulia maumivu kimoyomoyo. Si CCM si mpinzani. Pengine wewe uko kwenye class nyingine na hujui ni nini mazungumzo yanayoendelea huku mitaani. Na mbaya zaidi ni kuwa wana CCM wengi ndiyo wamechoka na hii hali japo hawaonyeshi waziwazi.
 
Pamoja na kwamba tunaona Umati ni mkubwa na kujipa Moyo Kushinda ila tusijisahaulishe kuwa wengi ya hawa Watu hawajajiandikisha kwa Kura.
Unauhakika gani?? Sababu kwa mujibu wa tume ya uchaguzi wamevuka malengo kwa idadi ya watu waliojitokeza kwenye daftari la wapiga kura..
 
Back
Top Bottom