Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mimi kukiri wala si issue.Nimeishia kucheka.
Hiyo siku ni unknown, ila tu katika pitapita zako unazosoma, itafika wakati utakiri tu.
Inawezekana kabisa nikapata sababu za kukiri Mungu yupo. Watu wengine huwa wanalemewa na matatizo na kuishia kukubali kuwepo kwa Mungu kama kimbilio la kuwapoza moyo kisaikolojia.
Au wengine hupata mafanikio makubwa sana wakajiona hawajaweza kupata mafanikio wao wenyewe, lazima wamesaidiwa na Mungu.
Kwa hivyo, hata kama Mungu hayupo, mtu anaweza kukiri Mungu yupo.
Hivyo, kukiri tu si jambo muhimu. Kwa sababu halithibitishi Mungu yupo.
Issue ni, hata nikikiri, huyo Mungu atakuwepo kweli? Inawezekana kuthibitisha yupo? Inawezekana kuondoa contradictions katika hoja za kuwepo huyo Mungu?
Mpaka sasa hoja za kimantiki zinaonesha hayupo.