Mambo ambayo nchi ya Marekani imezidiwa kwa mbali na nchi ya Tanzania

Sawa kama mataifa yote yanaizungumzia Marekani kwann ss iwe shida?
Kwani wapi nimesema ni shida?

Uzi unaongelea mambo ambayo nchi ya Marekani imezidiwa na Tanzania.

Mimi nimesema Marekani imezidiwa na Tanzania jinsi Watanzania wanavyoijadili Marekani kila siku, Wamarekani hawaizungumzii Tanzania kama Watanzania wanavyoizungumzia Marekani.

Nimechangia mada ya mleta uzi mambo ambayo Tanzania inaizidi Marekani.

Huelewi wapi?
 
Haya nimekuelewa
 
Me: "I'm from Tanzania"
American: "Did you say Tasmania?".

Wamarekani wengi hata hawajui Tanzania iko wapi kwenye ramani.
Wengi mno, 'average' Americans wanaoijua TZ ni wachache mno kwanza kuna wengi wanaodhani kuwa Africa ni nchi moja.
Ni sawa na Watanzania uwaulize kuhusu Tonga au Tuvalu wengi watakutolea mijicho tu.
 
Wengi mno, 'average' Americans wanaoijua TZ ni wachache mno kwanza kuna wengi wanaodhani kuwa Africa ni nchi moja.
Ni sawa na Watanzania uwaulize kuhusu Tonga au Tuvalu wengi watakutolea mijicho tu.
Siyo tatizo wenyewe ni taifa kubwa!!ila haindoi ukweli kuwa kuna mambo tumewazidi
 
Tanzania imeizidi Marekani kwa kupokea misaada kutoka Marekani kuzidi Marekani inavyopokea misaada kutoka Tanzania.
 
Tanzania imeizidi Marekani kwa kupokea misaada kutoka Marekani kuzidi Marekani inavyopokea misaada kutoka Tanzania.
Hilo ni kweli ila ilikuwa mada ya jmos ambayo tayari nimeshaiandaa unavujisha pepaa mzee
 
Una ma tatizo ya akili, watu hawawezi kula milo mitatu, unasema bongo kuna Amani! Bongo njaa tu, na ufisadi, majizi, madikiteta ndio yapo ikulu, yanalazimisha kukaa ikulu, nchi zenye Amani na furaha ni UK, Korea kusini, china, Afrika ni ukimya tu wa umaskini!
 
Asante kwa maoni yako ww usiye na matatizo ya akili
 
kwenye rasilimali za asili naomba nibishe

ifahamike kwamba marekani ni nchi kubwa sana(karibia 1/3 ya bara zima la afrika)

ina biomes nyingi tofauti na hapa hivyo biodiversity lazima ni kubwa

inazalisha mafuta ghafi kuliko nchi yeyote ile

na wao wana wanyama maarufu; grizzly bears, the alaskan moose, the american bison, the gray wolf. wanavutia sana

nadhani hata ukigoogle list ya most biodiverse countries hutoikuta tz 20 bora
 
Umeamua kubisha sina cha kukusaidia
 
Kuna wabongo hawali kuku wa kisasa waishi maisha marefu halafu jioni wanachinjika kwenye ajali ya hovyo ya bus kwa sababu ya miondombinu mibovu!
Bora ajali,kipindupindu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…