Mambo ambayo nchi ya Marekani imezidiwa kwa mbali na nchi ya Tanzania

Mambo ambayo nchi ya Marekani imezidiwa kwa mbali na nchi ya Tanzania

Fuatilia nukuu zako kwangu utaelewa kwamba sikubishana kusema hakuna baadhi ya mambo mmewazidi wamarekani.

Unabishia hoja ambayo mimi sijaisema.

Mimi nimesema tu Watanzania wanawaongelea Wamarekani kuliko Wamarekani wanavyowaongelea Watanzania.
Sasa kwa ukubwa wa marekani kuna taifa ambalo halilizungumzii taifa hili kubwa?
 
Tanzania AKA the Cradle of Mankind hatuna Mengi na Mengi tunazidiwa kwa macho / perception ya mtu /watu wa sasa...,

Ila Bongo tuna jambo moja tu ambalo sio USA to bali tunawazidi jamii nyingi sana Ulimwenguni nalo ni UNDUGU....., Heko kwa Waasisi kwa hili..., kwa nchi yenye Black and Whites au waliopigana CIVIL Wars ni ngumu sana kushindana na SISI..., ila ndio hivyo hata hilo tupo mbioni kulipoteza kwa UPUUZI wa wachache.... Walisema Wahenga You dont know you have it, till you loose it...
 
Sasa kwa ukubwa wa marekani kuna taifa ambalo halilizungumzii taifa hili kubwa?
That is irrelevant and tautological.

Mimi nakwambia Marekani ni taifa kubwa kila mtu analizungumzia, Watanzania wanaizungumzia Marekani zaidi ya Wamarekani wanavyoizungumzia Tanzania.

Wewe unaniukiza "Sasa kwa ukubwa wa Marekani kuna taifa ambalo halizungumzii taifa hili kubwa?".

You are making my point.
 
Hivyo vyote havijamsaidi mtanzania,mimi huwa napima maisha bora kwa nchi kwa juangalia mortuality ratr au life expectancy ya raia ,kama watu wanakufa below 60 unajisifu kula organic food ni ujinga
Kuna wabongo hawali kuku wa kisasa waishi maisha marefu halafu jioni wanachinjika kwenye ajali ya hovyo ya bus kwa sababu ya miondombinu mibovu!
 
Safi kabisa,mfumo dume umetawala pamoja na kuhubiri usawa wa jinsia
Hadi leo kwao wanawake wanalipwa mshahara pungufu kwa kazi ileile sawa na wanaume. Hapo pia tumewapita kwa mbali ikiwemo nchi nyingi za Ulaya. Uko sahihi, wanahubiri usawa wa kijinsia wasioufuata kabisa!
 
That is irrelevant and tautological.

Mimi nakwambia Marekani ni taifa kubwa kila mtu analizungumzia, Watanzania wanaizungumzia Marekani zaidi ya Wamarekani wanavyoizungumzia Tanzania.

Wewe unaniukiza "Sasa kwa ukubwa wa Marekani kuna taifa ambalo halizungumzii taifa hili kubwa?".

You are making my point.
Sawa kama mataifa yote yanaizungumzia Marekani kwann ss iwe shida?
 
Ingiwa nchi ya Marekani ina maendeleo makubwa ya kiteknolojia na kiuchumi, yapo mambo kadhaa ambayo Tanzania tumewaacha mbali mno.

1. Rasilimali za asili na utalii wa kiikolojia
Tanzania kuna hifadhi maarufu kama Serengeti, Ngorongoro crater, na Mlima Kilimanjaro, ambazo ni kivutio kikubwa cha utalii wa kiokolojia duniani.

● Biodiversity, Tanzania ina aina ya wanyama wakubwa wa porini kwa wingi na aina mbalimbali ya mimea ikilinganishwa na maeneo mengi ya Marekani.

11. Utulivu wa kijamii na kitamaduni
Utamaduni wa ujamaa mshikamano wa jamii na maisha ya kijamii ya mjini na vijijini ni imara zaidi nchini Tanzania kulinganisha na Tanzania.

● Amani na usalama wa kijamii, Tanzania kuna amani ya kijamii ukilinganisha na Marekani ambapo kuna ghasia za mara kwa mara kwenye jamii zao.

111. Chakula asili na lishe
● Chakula kisicho na kemikali, Tanzania kuna uzalishaji wa chakula cha asilia huku sehemu kubwa ya wakulima wakilima chakula pasipo kutegemea asili kulinganisha na Marekani ambao kilimo chao utegemea njia zisizo asilia.

1v. Hali ya hewa
Tanzania kuna hali ya hewa ya joto na unyevuunyevu,huku maeneo mengi ya Marekani yakipata hali mbaya za hewa kama kimbunga,baridi kali na vimbunga.

V. Gharama za maisha nafuu
Gharama za maisha nchini Tanzania kama malazi ,chakula na huduma za afya ni ndogo ukilinganisha na Marekani.

Vi. Matumizi madogo ya silaha
Tanzania ina viwango vya chini vya umiliki wa silaha na matukio machache ya uhalifu wa kutumia silaha tofauti na Marekani ambako matumizi ya silaha ni makubwa na matukio ya ghasia yanayojumlisha matumizi ya silaha ni ya juu.
Unaota ndoto mbaya sana, amka ndugu yangu.
Siku ukifika USA naamini utashangaa kwamba hata State Moja inaweza kuitoa TZ knockout katika huo mlolongo wako uliotitirika nao, karibu tujumuike katika kubeba 'box'.
 
Unaota ndoto mbaya sana, amka ndugu yangu.
Siku ukifika USA naamini utashangaa kwamba hata State Moja inaweza kuitoa TZ knockout katika huo mlolongo wako uliotitirika nao, karibu tujumuike katika kubeba 'box'.
Endelea kubeba maboksi mm hapana
 
Back
Top Bottom