Mambo ambayo nchi ya Marekani imezidiwa kwa mbali na nchi ya Tanzania

Mambo ambayo nchi ya Marekani imezidiwa kwa mbali na nchi ya Tanzania

Shule ngumu sana haya twende upande wa Pili wa shilling
haya ndiyo matokeo na faida ya kujibanza chooni wakati wenzako wanapiga shule darasani ...

kila jambo utaliona gumu na haliwezekani Tanzania 🐒
 
haya ndiyo matokeo na faida ya kujibanza chooni wakati wenzako wanapiga shule darasani ...

kila jambo utaliona gumu na haliwezekani Tanzania 🐒
Bora useme ww nikisema mm naitwa chawa
 
Umeamua kubisha sina cha kukusaidia
Screenshot_20241205-203445.jpg
Screenshot_20241205-203458.jpg
 
Umesahau mambo mengine muhimu zaidi. Hayo yote uliyoyaandika, Tanzania haiwezi kujivunia kwa sababu hayakutokana na utaalam, bidii au ujuzi wao. Hayo wa kusifiwa ni Muumba wa mbingu na nchi.

Lakini kuna mambo ambayo tunaweza kujisifu, ambayo ni matokeo ya bidii yetu, ambayo tunaizidi Marekani, na huenda tunazizidi nchi zote Duniani:

1) Kuteka na kuua wanaokataa kuwa machawa wa Rais.

2) Watawala hupora rasilimali asilia za nchi na kuwagawia wageni alimradi wao wakipata hongo iliyonenepa, na baada ya hapo machawa hushindana katika kuwasifu hao watawala.

3) Wananchi wake kuridhia kuongozwa na watu wenye akili na upeo mdogo.

4) Vyombo vya ulinzi na hasa polisi na TISS kuwa mali ya watawala, na hupambana na watu wanaomkosoa mtawala badala ya kushughulika na usalama wa wananchi na mali zao.

5) Tunawazidi katika kuyapa mambo ya kijinga uzito mkubwa kuliko yale ambayo ni ya muhimu, kama vile nchi kukosa pesa ya kutoa elimu bora au huduma bora za afya, lakini ina pesa tele za kuwazungusha wasanii Duniani kote wakilipwa posho ya dola 1,000 kwa siku baada ya kuwalipia gharama zote, au kuwa na pesa tele ya kununua magoli.

6) Tunawazidi kwa viongozi wetu kuwa wabinafsu, muda wote kutojishughulisha kufikiria ustawi wa Taifa, bali wanafikiria namna ya kubakia madarakani, iwe kwa njia za kishetani au njia halali.
Asante kwa maoni yako mkuuu
 
Ukweli upi kwa mfano unaweza kulinganisha developed country na developing country hata robo wewe au shule ulienda kusomea ujinga?
Sijalinganisha kiujumla nimechukua mambo sita kati ya mambo mengi waliotuzidi
 
Ingiwa nchi ya Marekani ina maendeleo makubwa ya kiteknolojia na kiuchumi, yapo mambo kadhaa ambayo Tanzania tumewaacha mbali mno.

1. Rasilimali za asili na utalii wa kiikolojia
Tanzania kuna hifadhi maarufu kama Serengeti, Ngorongoro crater, na Mlima Kilimanjaro, ambazo ni kivutio kikubwa cha utalii wa kiokolojia duniani.

● Biodiversity, Tanzania ina aina ya wanyama wakubwa wa porini kwa wingi na aina mbalimbali ya mimea ikilinganishwa na maeneo mengi ya Marekani.

11. Utulivu wa kijamii na kitamaduni
Utamaduni wa ujamaa mshikamano wa jamii na maisha ya kijamii ya mjini na vijijini ni imara zaidi nchini Tanzania kulinganisha na Tanzania.

● Amani na usalama wa kijamii, Tanzania kuna amani ya kijamii ukilinganisha na Marekani ambapo kuna ghasia za mara kwa mara kwenye jamii zao.

111. Chakula asili na lishe
● Chakula kisicho na kemikali, Tanzania kuna uzalishaji wa chakula cha asilia huku sehemu kubwa ya wakulima wakilima chakula pasipo kutegemea asili kulinganisha na Marekani ambao kilimo chao utegemea njia zisizo asilia.

1v. Hali ya hewa
Tanzania kuna hali ya hewa ya joto na unyevuunyevu,huku maeneo mengi ya Marekani yakipata hali mbaya za hewa kama kimbunga,baridi kali na vimbunga.

V. Gharama za maisha nafuu
Gharama za maisha nchini Tanzania kama malazi ,chakula na huduma za afya ni ndogo ukilinganisha na Marekani.

Vi. Matumizi madogo ya silaha
Tanzania ina viwango vya chini vya umiliki wa silaha na matukio machache ya uhalifu wa kutumia silaha tofauti na Marekani ambako matumizi ya silaha ni makubwa na matukio ya ghasia yanayojumlisha matumizi ya silaha ni ya juu.
Ww unachojua ni kuandika tuu ,akilo huna
 
Back
Top Bottom