Mambo ambayo Shule na Vyuo vinapaswa kuzingatia ili kuwalinda Wanafunzi dhidi ya maambukizi ya #COVID19

Mambo ambayo Shule na Vyuo vinapaswa kuzingatia ili kuwalinda Wanafunzi dhidi ya maambukizi ya #COVID19

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
706
Reaction score
1,230
2411349_20200529_015635_0000.png

UTANGULIZI

Baada ya Serikali kutangaza kuwa wanafunzi wa Kidato cha Sita watapaswa kurudi shule ili wakajiandae na mitihani yao ya mwisho inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni kuanzia Juni 29 mpaka Julai 19, nimeona kuja na mawazo ambayo yatatoa mwongozo kwa namna wanafunzi, walimu na wafanyakazi wa shule wataweza kuchukua tahadhari dhidi ya COVID – 19.​

Ni wazi wazazi, walezi na jamii kwa ujumla imekumbwa na taharuki kubwa sana baada ya Serikali kutangaza maamuzi ya wanafunzi kurudi shule huku hali ya ugonjwa wa COVID-19 nchini ikiwa bado ni kizungumkuti. Kufungua Shule ni jambo zuri ila kuwalinda wanafunzi na maambukizi ni jambo kubwa zaidi.​

Kwa upande wa Serikali imewatoa wasiwasi wazazi na walezi kuwa wasiwe na hofu kwa wanafunzi kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama wakiwa mazingira ya shuleni.​


MAMBO AMBAYO SHULE INATAKIWA KUYAFANYA ILI KUHAKIKISHA USALAMA WA WANAFUNZI KWENYE MAZINGIRA YA SHULE​

Kuwajenga wanafunzi Kisaikolojia: Hili ndilo suala la kwanza na muhimu kwa shule.​
Wakuu wa shule wanatakiwa kuhakikisha wanawajenga wanafunzi kisaikolojia na kuwaondolea hofu ili waweze kuzingatia masomo na akili yao kuweza kurudi katika hali ya kawaida.​

Tutambue shule hazina facility za kujifukiza wala madawa, lakini pia wanafunzi wanaathirika zaidi kisaikologia pale wanapobaini yupo chumba kimoja na mgonjwa.​

Wahudumu wa Afya: Kila shule itatakiwa kuwa na mhudumu wa afya karibu kwa ajili ya kutatua changamoto za kiafya zitakazo jitokeza katika maeneo ya shule.​

Shule za bweni zenye vituo vya afya watatakiwa kuwepo muda wote eneo la kazi. Pia ni wakati muafaka kwa shule kuwa na mawasiliano ya karibu na taasisi na wataalamu wa afya ili kupata huduma kwa urahisi pindi dharura itakapotokea.​

Vituo vya kunawa mikono: Shule zinatakiwa kuweka miundombinu mingi ya wanafunzi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni. Sehemu muhimu za kuweka miundombinu hiyo ni darasani, maabara,bwenini,bwalo la chakula nk , viweze kutumika na walemavu na sanitizer zinaweza kutumika​

Mpangilio wa kukaa darasani na bwenini: Shule zitatakiwa kupangilia upya namna ambavyo wanafunzi wanakaa wakiwa madarasani, yaani kuongeza nafasi kati ya dawati hadi dawati. Pia kwakuwa vidato vingine vitakuwa bado havijafunguliwa hivyo ni vyema shule kuangalia namna ya kutumia madarasa mengi Zaidi ambayo sasa yako wazi.​

Mikusanyiko ya Asubuhi: Shule zitatakiwa kuachana na mikusanyiko hii kwa kipindi hiki, kama kutakuwa na ulazima basi zipangilia upya namna ambavyo wanafunzi watasimama wakiwa assembly, yaani kuongeza nafasi kati ya mtu na mtu.​

Huduma ya Chakula: Kuwe na mpangilio mpya wa namna ambavyo wanafunzi hususan wa bweni watapata huduma za chakula wakati wa mlo bila kusongamana​

Kukabiliana na dharura za kiafya: Ni vyema shule kuimarisha utaratibu wa kukabiliana na dharura za kiafya, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi na wafanyakazi ambao wanakuwa wagonjwa shuleni au wenye dalili zinazotia shaka wanapatiwa huduma maalum.​

Ni vyema shule zikaweka utaratibu bora wa kushughulika na yeyote anayeugua (ugonjwa wowote) kwa namna ambayo haitazua taharuki kwa wengine na kuwaathiri kisaikolojia.​

Wanafunzi wenye dalili wapimwe kabla ya kwenda, walio na corona wasiende shule na watakaoonesha dalili wakiwa shule/chuo kituo cha afya cha karibu kijulishwe Kuchangia vifaa vya shule: Pamoja na wanafunzi kuhimizwa kutochangia vifaa wakiwa madarasani na maabara, hili linaweza kuwa gumu kidogo kutekelezeka miongoni mwao, hivyo ni vyema kukawekwa vituo maalum vya kunawa mikono ili angalau kufanya mashirikiano haya yasiwe ya hatari sana.​

Udhibiti wa wageni: Ni vyema shule zikapunguza ama kusimamia kwa ukaribu sana maingiliano ya wanafunzi na wageni kutoka nje ya shule. Mfano, ni vyema kusimamia kwa karibu sana namna wanafunzi wanapokutana na wenzao kutoka shule nyingine katika midahalo, michezo nk.​

Jumbe za Tahadhari: Ni vyema shule ikatumia namna ya kukumbusha wanafunzi kuchukua tahadhari kwa kuweka mabango yenye ishara na jumbe za kujikinga. Hivi vinaweza kuwekwa katika maeneo mbalimbali kama ville milango ya kuingilia shule, mabwenini, madarasani, mabwaloni, maabara nk.​

Elimu ya Afya kwa Walimu: Shule zinapaswa kutumia wataalamu wa afya kutoa mafunzo kwa walimu kuhusu Covid-19 ili kuwaachia ujuzi ambao walimu hao wataendelea kuutoa kwa wanafunzi kila siku. Kunaweza pia kutengwa muda maalum ambapo wanafuzi watakuwa wakikumbushana (chini ya uongozi wa walimu) masuala mbalimbali yanayohusu kuzingatia hatua za kubaki salama dhidi ya Covid-19. Shule iandae programu maalumu na za mara kwa mara za njia za kujikinga ikiwemo uvaaji wa barakoa, unawaji mikono. Pia wanafunzi hususani wa shule wapewe onyo kuhusu matendo yanayoweza kuwaweka hatarini ikiwemo wizi wa barakoa​

Kupima wanafunzi: Kwa shule zenye uwezo, kama inawezekana, ni vyema kufanya check-ups (mfano: kupima joto, ama kuangalia dalili) za kila baada ya muda fulani ila kujua hali ya kiafya ya wanafunzi wakati wote.​

Lishe na Michezo: Ni vyema shule kuhimiza walimu na wanafunzi na kuwawezesha kula kwa afya, kufanya mazoezi na kupata wakati wa kutosha kupumzika.​


MAMBO AMBAYO MWANAFUNZI WA BWENI ATATAKIWA KUZINGATIA ILI KUHAKIKISHA USALAMA WAKE AWAPO SHULENI​

Kushirikiana vifaa: Ni vyema wanafunzi wa bweni wakajitahidi kutoshirikiana kutumia vifaa kama vile chanuo, mataulo, ndoo, sahani, vijiko, vikombe nk​

Kushirikiana sehemu ya kulala: Wanafunzi wana tabia ya kupenda kulala zaidi ya mtu mmoja kwenye kitanda. Kwa wakati huu ni vyema kuacha kuchangia vitanda na mashuka. Kuacha kuchangia vitu hivyo kunaweza kuwaweka mbali na hatari ya kuambukizana endapo mmoja atakuwa tayari ameathirika.​

Kunawa mikono: Kutokana na mazingira ya shule kuwa hatarishi kutokana na mwingiliano mkubwa, ni vyema wanafunzi kuchukua tahadhari na kunawa mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka​

Mawasiliano: Ni vyema wanafunzi kuhakikisha wanawasiliana na uongozi wa shule au wao kwa wao pindi wanapohisi hali tofauti ya kiafya kwao wenyewe ama kwa wenzao.​

Barakoa na Vitakasa Mikono: Ni vyema kila mwanafunzi akawa na barakoa za kutosha ambazo atavaa awapo kwenye mazingira yenye zaidi ya mtu mmoja. Pia Sanitizer kwa ajili ya kutakasa mikono endapo kutakuwa na uhaba wa maji tiririka.​

Kusoma kwa makundi: Ni kawaida kwa wanafunzi kusoma kwa namna ya majadiliano ya zaidi ya mtu mmoja. Kwa wakati huu ni vyema wafunzi wakatengeneza makundi ya wanafunzi wachache ambayo wataweza kusoma kwa kujadiliano huku wakiwa wamepeana nafasi yakutosha baina yao​


MAMBO AMBAYO MWANAFUNZI WA KUTWA ATATAKIWA KUZINGATIA ILI KUHAKIKISHA USALAMA​

Usafiri: Kwa wanafunzi wanaotumia usafiri wa umma, ni vyema wakachukuwa tahadhari kwa kuvaa barakoa wakati wote. Kwa wenye uwezo, ni vyema kubeba sanitizer zao ili kujitakasa kila wanaposhika maeneo yanayoguswa na wengi wawapo kwenye daladala nk.​

Pia wale wanaotumia mabasi ya shule, ni vyema nao kuzingatia uvaaji wa barakoa na kutumia vitakasa mikono wanapogusa sehemu ambayo inaguswa na wengi. Wasipande gari ambayo imejaa​

Kutembea: Wanafunzi wanaoishi karibu na maeneo ya shule lakini huwa wanaona ni vyema kutumia usafiri wa umma, ni vyema kubadili mazoea na kutembea waendapo shuleni.​

Hii itawasaidia kufanya mazoezi na kujiepusha kuwa kwenye mikusanyiko wakati wote.​

Masomo ya ziada: Wanafunzi wa kutwa wanaosoma masomo ya ziada ni vyema kuchukua tahadhari muhimu kwa sababu wawapo huko hukutana na wanafunzi wengine ambao wametoka mazingira tofauti. Hivyo ni vyema kuwa na barakoa na vitakasa mikono.​

Mikusanyiko isiyo na ulazima: Ni vyema kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima wawapo shule. Kama mikusanyiko sio ya kujenga kimasomo ni vyema kuachana nayo ili kujiweka mazingira salama. Mikusanyiko hukusanya wanafunzi ambao wametoka mazingira mbalimbali na kukutana shule kwa muda wote wa masomo hivyo ni hatari sana.​

Nyongeza kwa Wanafunzi wa chuo​

Kuepuka safari zisizo za msingi: Wanafunzi wa chuo wana uhuru wa kwenda popote hivyo ni muhimu wajitahidi kuzuia safari au mitoko isiyo ya lazima ili kudhibiti maambukizi​

Kuongeza matumizi ya TEHAMA: 'Discussion' zifanyike kwa njia ya mtandao ili kuepuka maambukizi na kuzingatia 'social distancing'.​

Manunuzi kwa njia za kimtandao: Pesa zinaweza kusambaza maambukizi ya COVID19 kutoka mtu mmoja hadi mwingine hivyo malipo kwa njia ya simu yanaweza zuia maambukizi.​

Serikali ya wanafunzi inaweza kushauri uongozi wa vyuo uweke utaratibu mzuri wa malipo ya ada na usajili ili kuepusha wanafunzi kwenda benki​

Pia, soma mwongozo wa Wizara ya Afya

JamiiTalks ​
 

Attachments

Umenena vyema sana, hakika wazazi na wanafunzi\wanavyuo wako kwenye taharuki mpaka sasa lakini hakuna namna lazima wafuate matakwa ya Serikali. Naamini wakizingatia haya yaliyowekwa hapa kwa ufasaha basi watakuwa sehemu salama mwisho wa siku.
 
Nimekuelewa vyema kabisa ila swali linakuja je, wanafunzi ambao ndio walengwa wanaona umuhimu wa hili? Maana huku mtaani tumeshaagana na Corona
 
Kwa kweli hili ni jambo muhimu sana ambalo shule na Wanafunzi wanatakiwa kulizingatia. Pia nashauri kuna haja baadhi ya masomo yanayojaza wanafuzi wengi katika darasa moja yapewe vipindi double. Yaani kama somo la kiswahili lina darasa moja lenye wanafunzi zaidi 90 linaweza gawanywa mara mbili na topic husika ikafundishwa kwa wanafunzi 45 kwa darasa ili kupunguza misongamano.

Zaidi ya hayo kuwe na ndoo za maji tiririka katika mageni ya shule, vyuo, madarasa, ofisi za waalimu na vyooni. Pia wanafunzi walazimishwe kuwa na sanitizer binafifsi ili kuepuka kila mtu kushika kikopo kimoja.

Wanafuzi wa dei au kutwa wajitahidi watafute hata chupa ndogo za kuweka maji ya moto zenye tangawizi na malimao, kwa wale wa boarding shule ijitahidi kuwachemshia mchanganyiko huu wanafuzi na kuwaamuru wayanywe Asubuhi wanapoamka na mida ya break.

Natambua kuchukua tahadhari kamili katika maeneo ya shule ni ngumu sana lakini kama ikidhamiriwa walau tunaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Yote kwa yote nawasihi na najisihi pia kuendelea kuchukua tahadhari kwa sababu hii kitu ipo bado.

May Allah protect all of us
 
Powerful message!

Lakini je Hizi shule zetu za kupiga kama wanaua nyoka, wanaweza kuwa na wataalamu wa saikolojia ili kuwasaidia wanafunzi kutoa hofu kipindi hiki
 
Mwanafunzi aliyotoka Manzese au Mbagala sidhani kama atakuelewa!
Kunyanduana hakuepukiki mkuu na hivi kila mmoja alikuwa kwao sasa kwa wale wenye uhusiano na walikuwa mikoa tofauti lazima kunyanduana. Nadhani kuna mitindo ambayo inapendekezwa kunyanduana japo sidhani kama wanaweza kuhimili bila hata kulambana mate.
 
Kwenye suala la saikolojia ni penyewe. Taharuki miongoni mwa wanafunzi inaweza kuwa kubwa sana endapo hawataandaliwa vyema na kuelimishwa kwa kina.
 
Nmependa Dada Ndalichako alivyo kazia hapa.

‘Marufuku wanafunzi kwenda na limao, tangawizi vyuoni, shuleni’

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema ni marufuku kwa wanafunzi kwenda shule na malimao, tangawizi na spiriti pamoja na shule kutoza wanafunzi malipo ya ziada.

Aidha, amesema yeyote ambaye atabainika kukiuka maelekezo ya serikali, kwa kutoza wanafunzi malipo ya ziada, atachukuliwa hatua ikiwamo kufutiwa usajili. Serikali kupitia Rais John Magufuli ilitangaza wiki iliyopita kwamba vyuo vyote nchini pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita watarejea masomoni kuanzia Juni Mosi, mwaka huu, baada ya nchi kuwa na unafuu mkubwa wa maambukizi ya virusi vya corona vinayosababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid-19).

Profesa Ndalichako alitoa kauli hiyo jana kutokana na tatizo lililoibuka hivi karibuni kwa baadhi ya shule, kutoa mwongozo wa vitu ambavyo wanafunzi wanatakiwa kwenda navyo na kutakiwa kulipa ada.

Alisema ni marufuku kwa wanafunzi kwenda na spiriti shuleni, kwani inaweza kuchoma shule na mabweni na pia inaweza kutumika kama kilevi.

“Watu waache kutumia tatizo la corona kama kitegauchumi, watu wanaanza kuagiza hela za ziada za kazi gani, wanafunzi walikuwa wamekwishalipa ada kabla ya kufunga shule na walienda nyumbani kwa sababu kulikuwa na changamoto ya mlipuko wa ugonjwa corona,” Profesa Ndalichako aliwaambia waandishi wa habari jana.

“Serikali imefanya juhudi na maambikizi yamepungua na ndio maana imeamua kufungua shule na vyuo, wanafunzi wanaenda kuendeleza pale pale walipoachia kwa fedha zao zile zile, hakuna malipo ya ziada.

“Nitumie nafasi hii kukemea shule ambazo zinataka kutumia corona kama kitegauchumi, hapa hakuna kitegauchumi, tulikuwa na tatizo kama taifa, tumeungana pamoja, tumeweka na maombi na Mungu wetu ametusikia, sasa tusianze kuumizana kwa sababu ambazo hazina msingi wowote,” aliongeza.

Aidha, alisema wizara itafuatilia shule zitakazotumia janga la corona kama kitegauchumi na kuwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.

“Wizara itafuatilia, shule ambazo zinataka kutumia janga la corona kama kitega uchumi kuweka michango michango ambayo haina uhalali wowote…wizara itachukua hatua ikiwa ni pamoja na kuzifutia shule usajili, kwa sababu tumekuwa tukiwaambia kila mara watu wanaoendesha shule wanatoa huduma kwa Watanzania wasiwe na roho ya kukomoana, imekuja changamoto ya corona watu wameona ni fursa, hili jambo halikubaliki,” alisema.

Aidha, alisema kwa wanafunzi ambao mpaka shule zinafungwa walikuwa hawajakamilisha ada, kufanya hivyo ili fedha hizo zitumiwe na shule kujiendesha.

“Wanafunzi ambao hawakuwa wamekamilisha kulipa ada, walipe ili shule ziweze kujiendesha vizuri, lakini wale ambao mpaka shule zinafungwa walikuwa wamelipa warejee shuleni kuendelea na masomo kama kawaida,” alisema.

Alisisitiza kuwa hata pale wanafunzi wengine watakapofungua shule, utaratibu utakuwa huo huo wa kutokuwa na malipo ya zaida.

“Ni lazima tuwaondolee hofu wananchi, unaposema mwanafunzi aje na limao ya unga, sijui hata inauzwa maduka gani, sasa tunapotoa taratibu ambazo hata utekelezaji wake unakuwa mgumu unazidisha hofu kwa jamii.

“Au unapomwambia mwanafunzi aje na kilo mbili za tangawizi mwanafunzi anayekwenda kukaa shuleni mwezi mmoja na wiki mbili, hilo koo lake litakuwa salama? Tuangalie pia na afya za watoto kwa kuzingatia kuwapa watoto vyakula vyenye vitamin C kwa wingi,” alieleza Waziri wa Elimu.

Alisisitiza kuwa ni vyema vyuo na shule, kuzingatia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona pindi watakapofungua shule. Alisema matumizi ya vitakasa mikono ni kitu cha zaida, na si lazima mwanafunzi kuwa navyo.

Credit: Habari leo
 
Ushauri huu utakuwa hauna kazi hapa kwetu labda tu kama ni njama zile za kuleta taharuki au kutumiwa na mabeberu.

Tayari mkuu wa nchi, waziri mkuu, waziri mwenye dhamana nk, wamesha tuthibitishia: Wagonjwa wamekuwa waliougua kwa kasi. Haiyumkiniki hii pungua pungua hadi sasa tokea Apr 29 tutakuwa tayari kwenye Corona kwishney!

Tahadhari lukuki zote hizi za nini tena?

Ikumbukwe mambo ya send off tulisha serebuka. Mbona kuturudisha nyuma tena wakuu?

Mabeberu washindwe na walegee!
 
Ushauri huu utakuwa hauna kazi hapa kwetu labda tu kama ni njama zile za kuleta taharuki au kutumiwa na mabeberu.

Tayari mkuu wa nchi, waziri mkuu, waziri mwenye dhamana nk, wamesha tuthibitishia: Wagonjwa wamekuwa waliougua kwa kasi. Haiyumkiniki hii pungua pungua hadi sasa tokea Apr 29 tutakuwa tayari kwenye Corona kwishney!

Tahadhari lukuki zote hizi za nini tena?

Ikumbukwe mambo ya send off tulisha serebuka. Mbona kuturudisha nyuma tena wakuu?

Mabeberu washindwe na walegee!
 
Ushauri huu utakuwa hauna kazi hapa kwetu labda tu kama ni njama zile za kuleta taharuki au kutumiwa na mabeberu.

Tayari mkuu wa nchi, waziri mkuu, waziri mwenye dhamana nk, wamesha tuthibitishia: Wagonjwa wamekuwa waliougua kwa kasi. Haiyumkiniki hii pungua pungua hadi sasa tokea Apr 29 tutakuwa tayari kwenye Corona kwishney!...
Mkuu unaleta utani kwenye masuala muhimu. Hata kama viongozi wanasema wagonjwa wamebaki wachache ila kuchukua tahadhari ni muhimu sana kwa watoto wetu. Wale wagonjwa madereva wanaorudishwa Tanzania kila siku kwenye mipaka wanapelekwa wapi!
 
Mkuu unaleta utani kwenye masuala muhimu. Hata kama viongozi wanasema wagonjwa wamebaki wachache ila kuchukua tahadhari ni muhimu sana kwa watoto wetu. Wale wagonjwa madereva wanaorudishwa Tanzania kila siku kwenye mipaka wanapelekwa wapi!

Mkuu suala hili mtu hawezi liwekea utani hata kidogo.

Hata kama viongozi wanasema wagonjwa wamepungua na hata kwisha kabisa, ni wajibu wetu sote kuwakemea kwa nguvu zote.

Kama wanasema ugonjwa umepungua hali si kweli, hatupaswi kuwafumbia macho asilani.

Upotoshaji wowote haupaswi kuvumiliwa.
 
Kwani huu ugonjwa si tulishauzika?😱
 
Kunyanduana hakuepukiki mkuu na hivi kila mmoja alikuwa kwao sasa kwa wale wenye uhusiano na walikuwa mikoa tofauti lazima kunyanduana. Nadhani kuna mitindo ambayo inapendekezwa kunyanduana japo sidhani kama wanaweza kuhimili bila hata kulambana mate.
aisee!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom