Mambo ambayo Shule na Vyuo vinapaswa kuzingatia ili kuwalinda Wanafunzi dhidi ya maambukizi ya #COVID19

Mambo ambayo Shule na Vyuo vinapaswa kuzingatia ili kuwalinda Wanafunzi dhidi ya maambukizi ya #COVID19

Status
Not open for further replies.
Mna wadunisha sana hawa wanafunzi, watu wazima mnataka walindwe kama watoto wadogo, wakati wametoka mitaani ambako walikuwa wanachangamana kama kawida.Wajilinde kwanza wao, huu ugonjwa hadi watoto wadogo wanauelewa nao,umetangazwa kila sehemu na kwa kila namna.

Kidato cha sita ambaye mwaka huu anaingia chuo kikuu,kama hawezi kujilinda wala hana uelewa wa kutosha kuhusu huu ugonjwa pamoja na matangazo yote haya huyo ni zezeta.

Waafrika tumeanza kudeka sana,eti kwa ugonjwa huu mtu anahitaji usaidizi wa psychologists wakati mitaani maisha yanendelea kama kawaida, na hata walipokuwa nyumbani walikuwa wanazurura tu mitaani bila hata kuchukua tahadhari zozote.
 
Bado mnataka kujengaa hofu ya corona?
Nachojua Serikali inasema Corona imetoweka lakini bado wanasisitiza kuchukua thadhari.

Hata hivyo leo Uganda imewarudisha nchini wagonjwa 11 wa Corona watanzania. Hapo vipi!
 
Hakuna aliyesema corona imeisha Tanzania..
Nachojua Serikali inasema Corona imetoweka lakini bado wanasisitiza kuchukua thadhari.

Hata hivyo leo Uganda imewarudisha nchini wagonjwa 11 wa Corona watanzania. Hapo vipi!
 
Madudu tu, subiri kidogo mtapata mnachotafuta! Kawaulize North Korea
 
Corona sio Tanzania tu. Hata huko duniani imeanza kuisha nguvu. Si unaona hausikii tena matangazo kama mwanzo.
Na ligi zimeanza kuchezwa.

Huko marekani napo wameshasahau corona wanaandamana tu. Kwanini kila siku tuimbe corona corona?
Unajua unaweza usiseme kitu na ukakimaanisha
 
wanafunzi wa vyuo nadhani waendelee kusubili kwanza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom