Mkuu asante kwa bandiko. Nilishaliona siku nyingi lakini it worth to put it here for discussion. Mimi huwa nadhani kunamambo mengi sana ambayo binadamu hatujayajua kutuhusu. Nasema hivi kwa sababu kuna ndoto ambazo mimi nikiota, basi kesho yake kuna tukio litanitokea hata nijaribu kuwa mwangalifu namna gani. Ni hivi: nikiota nimengalia juu angani halafu nikaona nyota nyingi lakini moja ina rangi nyekundu, basi kesho yake ni lazima nitaumia wakati nafanya kazi na damu itatoa. Hili limenitokea tangu nikiwa mdogo mpaka sasa. Siyo kila nikiumia na damu kutoka huwa nimekuwa nimeota jana yake, ila kila nikiota basi lazima nitaumia na damu kutoka.