Kuna coisedence zingine za ajab sana. Nyumban kwangu napokwenda au kurud toka mihangaikon kuna umbali flan huwa napenda kutembea baada ya kushuka gari kituoni kama nimepanda dala dala
Sasa kuna siku moja ikatokea nikiwa natembea nikapokea simu toka kwa mshkaji wangu Elly, nikwa naongea ghafla nyoka akapita mbele yangu.
Sku nyingine tena nikiwa natembea njia hiyo, nikawa naongea na huyo huyo mshkaji Elly, ghafla tena mbele akapita nyoka.
Siku nyingine tena ikawa hivyo.
(Huyu ni mtu tuna uhusiano wa kikaz so ni obvious kuongea nae mara kwa mara).
Baada ya tukio la mara ya 3 kujirudia, nikaapa sitakaa kumoigia wala kupokea simu ya mshkaji nikiwa natembea maeneo hayo. Ikawa ndio sheria. Nitaongea nae nikiwa popote pemfine ila sio kwwnye hako ka njia. 😂😂