Uchaguzi 2020 Mambo Kumi niliyoyasikia leo kwa mara ya kwanza kuhusu Tanzania kutoka kwa Tundu Lissu akiwa Mbarali

Uchaguzi 2020 Mambo Kumi niliyoyasikia leo kwa mara ya kwanza kuhusu Tanzania kutoka kwa Tundu Lissu akiwa Mbarali

Miradi mingi Kuna ufisadi wa kutupwa imeanzishwa mingi Kama sehemu ya kutakasishia Kodi zetu thus haipitishwi bungeni atuonyweshwi risiti na mikataba yake, hii uleta Sana shaka. Pili why kuzuia Uhuru wa habari kufanya Mambo gizani Kama wewe Ni msafi.
 
Mikutano ya kampeni Sio sehemu ya maswali Ni sehemu ya kunadi sera na kuomba kura sehemu ya maswali na majibu Ni bungeni alikokuwa huko angeuliza maswali yote apewe majibu na serikali hakuuliza anakuja kuuliza Nani kwenye mikutano ya kampeni

Mkutano wa kampeni Hakuna Spika Wala waziri anapotezea muda watu tu

Anadi sera zake aombe kura . Aondoke aende Kwingine
Sera mpya.ni lazima zijibu matatizo yaliyopo. Lazima watu wajue kwa nini kuna haja ya kuwa na uongozi mpya, sera mpya na sheria mpya. Kwa hiyo cha kwanza, ni lazima kasoro zianikwe wazi kwanza.

Anachokifanya Tundu Lisu ni perfect 100%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa tukimchagua kazi yake itakuwa kupita tu mitaani akiimba Uhuru na Maendeleo😂😂 maana pamoja na story zake tamu hasemi yeye atafanyaa nini tukimpatia nchi.
 
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Hapo kawapotezea muda tu watu wa mbalali
point ni 3 tu comrade:

1. Chini ya awamu ya 5, kuna viashiria vya grand corruption, tena sehemu ambayo haikutarajiwa kabisa.

2. Chini ya awamu ya 5, kuna viashiria vya nepotism.

3. Hakuna jipya ambalo awamu ya 5 inalifanya ambalo halijawahi kufanywa na awamu zilizopita. So, awamu hii isinyanyase watu kwa kisingizio cha eti kufanya mambo mapya!

Niongeze volume??
 
point ni 3 tu comrade:

1. chini ya awamu ya 5, kuna viashiria vya grand corruption, tena sehemu ambayo haikutarajiwa kabisa

2. chini ya awamu ya 5, kuna viashiria vya nepotism

3. hakuna jipya ambalo awamu ya 5 inalifanya ambalo halijawahi kufanywa na awamu zilizopita. so, awamu hii isinyanyase watu kwa kisingizio cha eti kufanya mambo mapya!

niongeze volume??
Hizo ndio sera za CHADEMA?
 
MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro), Hale (Tanga), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro), Pangani (Tanga), Rusumo (Kagera), Songwe (Mbeya), Kikonge(Ruvuma)

TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi.


NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU TAIFA MKWAJU MOJA SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki eka 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo

TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendela kujenga vingine vyote nchini, Magu si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.
Ndio uzuri wa demokrasia. Siri nje nje!
 
Hapo tu kwenye mkutano kashindwa kunadi sera
Una uhakika au unapiga ramli? Hakuna mkutano ambao Tundu Lisu hajanadi sera.

Kwanza hueleza mapungufu yaliyopo sasa, na kisha hueleza nini atafanya ili kuyarekebisha yaliyopo.

Yaliyoandikwa, mleta hoja, ameyachukua kwa kutegemea ametaka kuleta nini jukwaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa nasema Lissu atatia aibu kuliko wagombea wote waliowahi kugombea urais kupitia CHADEMA!
 
Baada ya Lisu kumaliza kueleza hayo mambo kumi ukimuuliza mwana mbalali sera za Chadema Ni Nini atajibu Nini hapo?
Sisi tunataka ushindi haijalishi tunanadi sera au tunafunua nyeti za mtu. Kikubwa tunaongea kile wananchi wanatamani kusikia.
 
Mimi huwa nasema Lisu atatia aibu kuliko wagombea wote waliowahi kugombea urais kupitia chadema!
Kabisa mkuu, Ila hatukutegemea kama kuna mtu anaweza kumkosoa jiwe hadharani maana tuliaminishwa kuwa yeye ndio Rais bora kuliko wengine. CCM oyee
 
Back
Top Bottom