MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA
MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro), Hale (Tanga), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro), Pangani (Tanga), Rusumo (Kagera), Songwe (Mbeya), Kikonge(Ruvuma)
TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi.
NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU TAIFA MKWAJU MOJA SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.
TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.
SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.
SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki eka 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu
NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo
TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!
KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendela kujenga vingine vyote nchini, Magu si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.