Mambo matatu Muhimu kabla hatujamsahau Hayati Dkt. Magufuli

Hayati JPM kama angaliweza kutii sheria na katiba kwa kuzingatia masuala muhimu ya kiutu na kidemokrasia, utawala wake ungaliweza kuweka alama muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Uthubutu wake wa kufanya maamuzi magumu ili kulinda rasilimali za nchi yetu na kwa maslahi mapana ya nchi yetu ni sifa kubwa ambayo alikuwa nayo.

Kurudisha nidhamu ya utendaji na ufanisi katika ofisi za umma pia ni kongole nyingine kwake. Kukemea kwa uwazi vitendo vya rushwa, uonevu na ukandamizaji wa kimatabaka pia ilikuwa ni "credit" nyingine kwake. Na hata pia uthubutu wake wa kuanzisha ama kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati kama vile mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere.

Taifa linapaswa kuwa na "succession plan" na kuanza kuandaa viongozi waliopo ili waje kuwa baadaye viongozi wazuri hapo baadaye. Wananchi wengi hawatamani kuwa na Rais aina ya JPM kutokana na mabaya yake, ila wanatamani kuwa na Rais kama yeye kutokana na mazuri yake.

Kama tunataka kiongozi mwenye haiba ya JPM kwa upande wa mazuri yake, yaani mwenye uthubutu wa kufanya maamuzi magumu, na watu wakatambua kuwa yupo "serious" na hata kuupelekea umma kutii kwa dhati, basi naweza kuwataja Tundu Lissu ama Mwigulu Nchemba, pengine pia yupo Kassim Majaliwa.

Hawa ni watu ambao wanaweza kuanza kuandaliwa ili kama wakifanikiwa kushika uongozi wa juu wa nchi wasigeuke kuwa viongozi katili na madikteta. Kama ni uthubutu wa kukemea, kuamua na kufanya maamuzi magumu hii sifa wote wanayo.
 
Mimi sina ugomvi na Kodi yeyote
Tatizo ni kurudisha watu walioshindwa madarakani basi.

Kodi, tozo sina ugomvi Nazo ukitaka maendeleo tegemea hayo.

Sio Kila kitu kitakuja ni kitamu kama pipi vingine vinaanza na uchungu alafu vinakuwa pipi baadae
Ndio maana kwenye mtori nyama zinakuwa chini
Mama Samia fanya kazi.
 
Bora purukushani za jpm zilitufanya tufanye kazi, lakini yeye alideal na mijizi, sio kukomba tozo kwa wabanchi wa kawaida.
Pamoja na jitihada hizo miradi mikubwa tuliiona.

Sasa huyu aliyepo kipi kipya amekianzisha mwenyewe? Miradi yote jpm aliacha ameilipia, ndo sasa wanamsingizua madeni lakini miradi yote ililipiwa.

Walijuwa wananchi watahoji ili ikabidi kuwasepesha wanaojua siri hizo.

Walobaki wanaojua hawawezi fungua midomo yao.
Kizuri cha jpm alikuwa akilipia mradi anatueleza kuwa kashalipa kazi imebaki kwa mkandarasi.

Walivyo wa ajabu kuna siku mtasikia eti hela imeenda kumaliza daraja la busisi. Wakati jpm alituekeza hadaiwi hata mia. Na miradi mingine yote alitueleza.sasa wap wana kipi kipya?
 
Tanesco wana kiwanda cha mita?
Mbona kampuni za simu hazigawi bure simu?
Tanesko Haina kiwanda cha mita lkn serikali inaweka ruzuku kwenye bei ili wananchi wapate umeme wazione fursa na wazitumie huko ndiko kugawana keki ya taifa Leo una rudisha bei ya umeme juu lkn,matumizi mengine yapo juu huenda zaidi ya kawaida.
 
Tanesco wana kiwanda cha mita?
Mbona kampuni za simu hazigawi bure simu?
Simu huwezi kupewa bure kwa sababu unaweza kubadilisha mtandao wakati wowote. Pia simu sio kwa ajili ya mawasiliano tu unaitumia na kwa mambo mengine hivyo huwezi kupewa bure. Line ndio unaweza kupewa bure na buku zinayouzwa ni sawa na bure.

Tanesco wanachofanya kuuzia watu mita na nguzo ni sawa na mtu anawachangisha watu ili ajenge duka mtaani kisha awazuie bidhaa.
 
Taifa letu lina hasara sana kuwa na watu wengi kupita kiasi ambao ni wajinga wa aina yako.
 
Akili yako bwana
 
Lete Ushaidi kuwa huyo mungu wenu magufuli miradi yote alikuwa ashailipia hela? Huyo sindio alikuwa anawadanganya mazuzu Kama wewe kuwa miradi yote anajenga kwa fedha za ndani!
 
Huyo kilazaa The Boss hawezi kuelewa
 
Kwa Magufuli mbona iliwezekana kulipia umeme 27,000 kila kona?
Acha uongo binti, umeme kipindi Cha magufuli kwa mijini ilikuwa 321000/= Wengine tulivuta kwenye mabanda yetu tuna Ushaidi wa hilo,vijinini ndio ilikuwa 27000/=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…