Hayati JPM kama angaliweza kutii sheria na katiba kwa kuzingatia masuala muhimu ya kiutu na kidemokrasia, utawala wake ungaliweza kuweka alama muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Uthubutu wake wa kufanya maamuzi magumu ili kulinda rasilimali za nchi yetu na kwa maslahi mapana ya nchi yetu ni sifa kubwa ambayo alikuwa nayo.
Kurudisha nidhamu ya utendaji na ufanisi katika ofisi za umma pia ni kongole nyingine kwake. Kukemea kwa uwazi vitendo vya rushwa, uonevu na ukandamizaji wa kimatabaka pia ilikuwa ni "credit" nyingine kwake. Na hata pia uthubutu wake wa kuanzisha ama kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati kama vile mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere.
Taifa linapaswa kuwa na "succession plan" na kuanza kuandaa viongozi waliopo ili waje kuwa baadaye viongozi wazuri hapo baadaye. Wananchi wengi hawatamani kuwa na Rais aina ya JPM kutokana na mabaya yake, ila wanatamani kuwa na Rais kama yeye kutokana na mazuri yake.
Kama tunataka kiongozi mwenye haiba ya JPM kwa upande wa mazuri yake, yaani mwenye uthubutu wa kufanya maamuzi magumu, na watu wakatambua kuwa yupo "serious" na hata kuupelekea umma kutii kwa dhati, basi naweza kuwataja Tundu Lissu ama Mwigulu Nchemba, pengine pia yupo Kassim Majaliwa.
Hawa ni watu ambao wanaweza kuanza kuandaliwa ili kama wakifanikiwa kushika uongozi wa juu wa nchi wasigeuke kuwa viongozi katili na madikteta. Kama ni uthubutu wa kukemea, kuamua na kufanya maamuzi magumu hii sifa wote wanayo.