Mambo mawili yaliyonishangaza Tanga

Ulifata nini kwamgwe? Uliingilia michungwani? Vipi ulipita Ngojoro, Kambini je?
Sasa ngoja nikufungue.
kile kijiji ndio kilikua cha kibiashara enzi hizoo.Kilikua na utajiri mkubwa uliotokana na kiwanda cha kuchakata mkonge tunakiita Korona. Kipo mbele kidogo kuna kota za kambi.
Palizaa matajiri wakubwa tu wa Tanga mfano Sefu Mwarabu aliyekua anamiliki mabasi ya Zafanana.
Pia kulikua na utajiri wa kikoloni aka Rupia watu washatoka sana pale.
Kule mkundi ulifika? Kuna kisima cha kijerumani kina maajabu, wwakati wa mvua (masika) maji hupungua lakini wakati wa ukame (kiangazi) maji hujaa na kumwagika.
Siku nyingine ukija kwamgwe aka Bondo niambie nikutembeze nikuonyeshe maeneo ya historia.
 
Ndugu mtembezi, almost Tanzania yote iko hivyo tembea ujionee,
Mwaka 2014 niliwahi kwenda Itirima Simiyu aisee siyo mchezo
 
Acha kuleta uwongo unamdanganya nani ambaye hajafika Dodoma...soko la nyama la msalato machinjio yapo palepale kwa nyuma hatua chache tu sasa utasemaje wanakula mabaki ya mifupa😀😀
 
Acha kuleta uwongo unamdanganya nani ambaye hajafika Dodoma...soko la nyama la msalato machinjio yapo palepale kwa nyuma hatua chache tu sasa utasemaje wanakula mabaki ya mifupa[emoji3][emoji3]
Mkuu nimetoa reference!! Ni kipindi cha week cha Ripoti Maalumu cha ITV, ingia YOUTUBE uone maajabu!! Watoto wanaokota mifupa ilitupwa chini na kuanza kula palepale nyingine wanaweka kwenye mifuko wanapeleka nyumbani kupika. Mwandishi kaenda nao mpaka home wakamwonyesha wanavyopika. Kuna mwanasaikolojia mmoja aliojiwa akasema huu ni zaidi ya unyama kwani hata mbwa ambaye ni well trained hawezi kula mabaki ya mifupa

itv njoo mtusaidie link
 
Huko ndio kwa kina mwana FA na lulu diva hata kwao kupo hivyo hvyo ila mashauzi mengi mjini.
 
Jimbo linaloongozwa na CCM na Juma Aweso Waziri wa Maji.

Handeni wananchi wote ni CCM ili ujue na ujifunze madhara ya CCM kujikita mahali
Aweso kwao ni pangani huko ni kwa kina mwana FA
 
Na ndiyo mvaa bendera ya taifa shingoni anataka wapewe TIN namba.
 
Napapenda Tanga ila asilimia kubwa ya watu wakule wamezidi uvivu,umwinyi na mambo ya ushirikina,we cheki barabara tu yakuwasaidia wenyewe walikua wanagoma isijengwe haha sehemu itakua na maendeleo kweli
 
Handeni kuna umaskini wa kutupa kweli wala si uongo.

Sijui tunatokaje hapo.

Nimeshangaa nilipoenda Lushoto walau kule sijaona Nyumba ya nyasi, sijaona mwenda pekupeku.
 
Dah nmeiona hii ITV aisee watu n maskin
 
Nyinyi na report zenu za NBS mnautaja mkoa wa kagera kuwa ndo maskini zaidi kisa unachangia pato dogo la taifa kuliko population yake....

Lakini Tazama maisha ya vijijini kagera....
Kwa kagera ukiiacha biharamuro na Ngara vijijini watu wana maisha bora kabisa na decent hasa vijiji vya wahaya na wanyambo

Hakafu unakuta mtu wa Tanga anasema wahaya wahaya[emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Sehemu yoyote wanayoendekeza uchawi kuliko chochote hapawezi kuwa na maendeleo daima. Handeni ni nyumbani kabisa, mimi ni Mzigua lakini sijawahi kukanyaga ardhi yake na sitathubutu kwenda, nisamehewe kama nafanya makosa.
 
Sehemu yoyote wanayoendekeza uchawi kuliko chochote hapawezi kuwa na maendeleo daima. Handeni ni nyumbani kabisa, mimi ni Mzigua lakini sijawahi kukanyaga ardhi yake na sitathubutu kwenda, nisamehewe kama nafanya makosa.

Usiende mkuu Njoo nikuuzie ukoo upate na kiamba huku mgombani
 
Acha kuleta uwongo unamdanganya nani ambaye hajafika Dodoma...soko la nyama la msalato machinjio yapo palepale kwa nyuma hatua chache tu sasa utasemaje wanakula mabaki ya mifupa[emoji3][emoji3]
We Mgogo masario sijui masare ya chama njoo uwaulize watu wenye TV sio unaleta umatonya hapa
Dah nmeiona hii ITV aisee watu n maskin
Huyo mgogo alikua anabisha anafunika kombe na mwanaharamu hapiti. Mpe story kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…