Mambo muhimu ambayo Mzee Mkapa hajaweka wazi katika kitabu chake ''My Life, My Purpose''

Afu kuna tuhuma kwamba alipewa cheni ya dhahabu ya kilo 5 huko buli sasa badala ya kuikabidhi IKULU yeye akawa anaivaa shindoni akaifanya yake kumbe ni ya Taifa.

Hiyo cheni ya Taifa basi ilikuwa nzito mno, ‘kilo 5’ sio masikhara.... ndio maana shingo imemtitia Che Nkapa.
 
kaka ni kweli alipewa, kuna ule mkufu wa kuvaa wa dhahabu na nyepesi nyepesi zinasema akapewa na mziko wa kilo nyingi tu kaa 5 hivi kama zawadi.... haya mambo si ya kwangu ila yapo mtaani, kwa hiyo ni wajibu wake ayatolee ufafanuzi.

Jiwe la kilo tano, lakini mkufu wa kilo tano kisha akawa anakaa hilo hapa na.
 
FUSO,

Mzee baba story nyingine unaona kabisa ni uongo,wala haiitaji ufafanuzi.

Sasa cheni kilo 5 mtu anaivaaje shingoni?!!! Mweeh
 
NI watu wachache sana ambao wakiandika vitabu kuhusu maisha yao, huwa wanaweka mambo yote makuu yaliyotokea katika maisha yao, kwa kuwa labda wanahofia yatawachafua au yatawapotezea umaarufu. Hivyo basi mara nyingi vitabu kuhusu maisha ya watu ambavyo vimehaririwa na wao wenyewe, hutokea kuwa kama namna tu ya publicity stunts za namna ya kujisafisha mbele ya jamii.

Je, tunaweza kusema hivyo kuhusu kitabu cha Mkapa? Mimi binafsi sijakisoma bado, lakini bado nina shauku sana kujua kama Mkapa ameweka wazi mambo ambayo sisi kama jamii tunaona yameacha maswali mengi kuliko majibu. Kwa mfano, amegusia jinsi alivyopishana vikali na Mwalimu Nyerere kuhusu suala la ubinafsishaji? Na je, Mkapa ameeleza ukweli kuhusu suala la rada iliyoleta mgogoro kama vile EPA? Je, suala la uuzaji nyumba za serikali? Suala la Mradi wa Makaa ya Mawe Kiwira?

Mkapa amegusia kuhusu maisha ya familia na tuhuma za uchawi kwa wazee wake, lakini vipi suala lake la maisha ya ndoa ambalo tumekuwa tukisikia kila namna ya habari, ameliongelea ili kuiweka jamii sawa? Ni kweli Mkapa alioa mtu ambae alikuwa mke wa Basil Mramba au ni porojo tu? Vipi hisia zake pale ambapo hadi watoto walimzomea "fisadi fisadi", ameeleza alijisikiaje kuona hadi watoto wakimtuhumu ufisadi?

Na vipi tuhuma zilizomkabili kuhusu uuzwaji wa NBC ambazo zilifanya karibu uasi wa Bunge utokee, amezigusia? Na vipi tuhuma na mkanganyiko kulelekea mwishoni mwa maisha ya Nyerere, akituhumiwa kumsusa Nyerere akiwa mgonjwa, je ametoa ufafanuzi juu ya hilo? Na vipi mgogoro wa Bulyanhulu watu kufukiwa na yeye kupewa kilo ya dhahabu, na pia kukubali asilimia 5% ya hisa kwa ajili ya Tanzania wakati Nyerere alikataa asilimia 49%, ametoa sababu zinazofanya watu waone kweli hakuwa muuza nchi? Vipi suala la kwamba katika uteuzi wa Kikwete kuwa mgombea wa uraisi wa CCM alikubali japo TISS walimpa taarifa iliyomuondolea sifa Kikwete kuwa mgombea wa wa uraisi? Je ni kweli alimpitisha Kikwete kwa nguvu kwa kuwa Kikwete alitishia kujiunga na Chadema, na wakakubaliana Kikwete amlinde atakapokuwa raisi?

Sasa haya ni baadhi ya mambo ambayo wengine tukisikia Mkapa kaamua kuandika kitabu, tunategemea ayagusie. Vinginevyo inakuwa ni kitabu cha kujikosha na kujisafisha mbele ya jamii. Na kama hajayaweka, basi mie binafsi labda niandike kitabu "Benjamini Mkapa: Your Life, Tanzania's Purpose".

Pengine wewe unajua mengine ya muhimu ambayo unahisi Mkapa alipaswa kuzungumzia katika hiki kitabu alichaoandika, "My Life, My Purpose".

Utetezi wa Mkapa kuhusu EPA ni wa kipumbavu kabisa!

Eti watu walinidanganya!

Rais mzima tunaejua ana akili “anadanganywa” nchi inaibwa?

Yaani kabisa unaletewa stori mezani unashindwa kujua huu ni wizi na huu si wizi?

Mimi na akili zangu hizi,huniletei stori nisijue hiki ni kipigo na hiki si kipigo!

Plus,hata kama hakujua kweli,then baada ya wizi kwanini hakuadhibu mtu!?

Jamaa lina utetezi wa mavi kabisa!

Limenifanya nikalidharau kabisa!

Bure kabisa!
 
Kuna mifumo 5 ya uandishi nitaitaja; Poetry, Drama, prose, non fiction na media.
Kwa mfumo ambao BWM alioamua kuandika Kitabu chake ni "Non fiction".

Non-fiction can be creative, such as the personal essay, or factual, such as the scientific paper. Sometimes the purpose of non-fiction is to tell a story (hence the autobiography), but most of the time the purpose is to pass on information and educate the reader about certain facts, ideas, and/or issues.

Kwa hiyo mfumo huo hapo hauwezi kuchanganya gossip kama ambazo mtoa mada umeziweka kwenye uzi wako. Hayo unayotaka wewe yatapatikana kwenye vitabu vya Eric Shigongo.
Yaaani mtu aandike kitabu halafu humo ndani ajikandye au aonyeshe udhaifu wake, ni ngumu sana labda vitabu vinavyowahusu kina Clinton na Blair, sio viongozi wa kiafrika.
 
NI watu wachache sana ambao wakiandika vitabu kuhusu maisha yao, huwa wanaweka mambo yote makuu yaliyotokea katika maisha yao, kwa kuwa labda wanahofia yatawachafua au yatawapotezea umaarufu. Hivyo basi mara nyingi vitabu kuhusu maisha ya watu ambavyo vimehaririwa na wao wenyewe, hutokea kuwa kama namna tu ya publicity stunts za namna ya kujisafisha mbele ya jamii.

Je, tunaweza kusema hivyo kuhusu kitabu cha Mkapa? Mimi binafsi sijakisoma bado, lakini bado nina shauku sana kujua kama Mkapa ameweka wazi mambo ambayo sisi kama jamii tunaona yameacha maswali mengi kuliko majibu. Kwa mfano, amegusia jinsi alivyopishana vikali na Mwalimu Nyerere kuhusu suala la ubinafsishaji? Na je, Mkapa ameeleza ukweli kuhusu suala la rada iliyoleta mgogoro kama vile EPA? Je, suala la uuzaji nyumba za serikali? Suala la Mradi wa Makaa ya Mawe Kiwira?

Mkapa amegusia kuhusu maisha ya familia na tuhuma za uchawi kwa wazee wake, lakini vipi suala lake la maisha ya ndoa ambalo tumekuwa tukisikia kila namna ya habari, ameliongelea ili kuiweka jamii sawa? Ni kweli Mkapa alioa mtu ambae alikuwa mke wa Basil Mramba au ni porojo tu? Vipi hisia zake pale ambapo hadi watoto walimzomea "fisadi fisadi", ameeleza alijisikiaje kuona hadi watoto wakimtuhumu ufisadi?

Na vipi tuhuma zilizomkabili kuhusu uuzwaji wa NBC ambazo zilifanya karibu uasi wa Bunge utokee, amezigusia? Na vipi tuhuma na mkanganyiko kulelekea mwishoni mwa maisha ya Nyerere, akituhumiwa kumsusa Nyerere akiwa mgonjwa, je ametoa ufafanuzi juu ya hilo? Na vipi mgogoro wa Bulyanhulu watu kufukiwa na yeye kupewa kilo ya dhahabu, na pia kukubali asilimia 5% ya hisa kwa ajili ya Tanzania wakati Nyerere alikataa asilimia 49%, ametoa sababu zinazofanya watu waone kweli hakuwa muuza nchi? Vipi suala la kwamba katika uteuzi wa Kikwete kuwa mgombea wa uraisi wa CCM alikubali japo TISS walimpa taarifa iliyomuondolea sifa Kikwete kuwa mgombea wa wa uraisi? Je ni kweli alimpitisha Kikwete kwa nguvu kwa kuwa Kikwete alitishia kujiunga na Chadema, na wakakubaliana Kikwete amlinde atakapokuwa raisi?

Sasa haya ni baadhi ya mambo ambayo wengine tukisikia Mkapa kaamua kuandika kitabu, tunategemea ayagusie. Vinginevyo inakuwa ni kitabu cha kujikosha na kujisafisha mbele ya jamii. Na kama hajayaweka, basi mie binafsi labda niandike kitabu "Benjamini Mkapa: Your Life, Tanzania's Purpose".

Pengine wewe unajua mengine ya muhimu ambayo unahisi Mkapa alipaswa kuzungumzia katika hiki kitabu alichaoandika, "My Life, My Purpose".
Kwenye TISS kumuondolea sifa kikwete sio kweli,isipokua TISS ndio ilimsaidia kikwete kutangazwa mshindi,hii ni baada ya BM,CDF , IGP na PM wa kipindi kile,walimuogopa kikwete na kutaka kutomtangaza kwa kuhofia mabaya yao,na walikaa kikao cha siri ktk kambi 1 wapo.lakini mchezo kuo ulishtukiwa na TISS wakamtonya jk,na jk ilibidi aombe baraka kwa bibi na bibi hakusita,akawakulupusha kwenye kikaochao cha siri.kwa aibu iliwabidi wakamtangaze mshindi.
 
Wabongo bana

Mtu anaanza kuchambua kitabu kabla hajakisoma
Hahaha
Kakiona kwenye TV na muda huo huo akawa keshajua ndani pameandikwa nini.

Yale yale ya mtu katika mazungumzo ya kahawa anakupa story za Brazil au Japan wakati hajawahi kupanda ndege hata siku moja.
 
Sikiliza, Mkapa alifanya kila awezalo kumzuia JK 2005 lakini nguvu ya wanamtandao ilimfanya asalimu amri mbele yao dakika ya mwisho.
Kweli kabisa,hakuna mtu aliepambana kuupata urais akiwa mwenyewe ni jk.kwasababu tu jk michezo ya kisiasa anaijua vizuri sana.
 
Zungumza ulijualo! Rostam na Mzee wa Bati utawapeleka wapi
 
JWTZ hawakuwa na tatizo na Salim. Salim alikataliwa na Zanzibar, ambao siku zote walimwona yuko upande wa Waarabu waliopinduliwa mwaka 1964 kwenye Mapinduzi ya Zanzibar. Tatizo ni pale ambapo Kikwete alitoa shinikizo kwamba asipopitishwa na CCM ataenda Chadema na akamwambia Mkapa nikienda Chadema nitashinda na historia itaandikwa CCM ilifia mikononi mwa Mkapa. Nasikia Mkapa akakubali, lakini kwa kuwa hakumwamini Prof. Mwandosya kuwa asingechukua hatua dhidi ya mambo ya "kifisadi" aliyofanya akiwa Raisi, wakakubaliana na Kikwete kwamba atashinikiza jina lake lipitishwe kwa masharti kwamba akistaafu mambo yake aliyofanya akiwa raisi yasiguswe, kutia ndani Kiwira, nyumba za serikali nk. Wakati huo Mkapa alikuwa na tuhuma nyingi sana za ufisadi, kutia ndani tetesi kwamba ABSA walimpa hoteli huko Afrika Kusini kama zawadi ya ubinafsishaji wa NBC. Na Mkapa zawadi kutoka makampuni binafsi alikuwa hazionei aibu kuzipokea!
Hapo umebugi ile mbaya!!!! SI KWELI
 
Kwa akili zako unafikiri kuna mtu anaweza kusema mambo yake yote? Hakika bado watu wana akili nyembamba sana kama ndio fikra zinakutuma kuwa utaelezwa kila kitu! Huwezi kuanika kila kitu mzee, hilo liko wazi na wote tunajua hilo. Mtu atayekwambia kila kitu ni mtu aliyetokwa na akili, mwendawazimu
 
JWTZ hawakuwa na tatizo na Salim. Salim alikataliwa na Zanzibar, ambao siku zote walimwona yuko upande wa Waarabu waliopinduliwa mwaka 1964 kwenye Mapinduzi ya Zanzibar. Tatizo ni pale ambapo Kikwete alitoa shinikizo kwamba asipopitishwa na CCM ataenda Chadema na akamwambia Mkapa nikienda Chadema nitashinda na historia itaandikwa CCM ilifia mikononi mwa Mkapa. Nasikia Mkapa akakubali, lakini kwa kuwa hakumwamini Prof. Mwandosya kuwa asingechukua hatua dhidi ya mambo ya "kifisadi" aliyofanya akiwa Raisi, wakakubaliana na Kikwete kwamba atashinikiza jina lake lipitishwe kwa masharti kwamba akistaafu mambo yake aliyofanya akiwa raisi yasiguswe, kutia ndani Kiwira, nyumba za serikali nk. Wakati huo Mkapa alikuwa na tuhuma nyingi sana za ufisadi, kutia ndani tetesi kwamba ABSA walimpa hoteli huko Afrika Kusini kama zawadi ya ubinafsishaji wa NBC. Na Mkapa zawadi kutoka makampuni binafsi alikuwa hazionei aibu kuzipokea!
Mkuu hivi unaijua nguvu ya taasisi ya uraisi pamoja na nguvu anazopewa anae kalia kiti cha uraisi?
Unajua hizo nguvu zinakuwapo hadi siku anapo apishwa mrithi wake?

Jeuri ya kumtisha raisi na kumfanya afuate matakwa yako kilazima kwa katiba ya Tanzania hakuna mtu alie nayo ambae si raisi alie madarakani.

Jeuri hiyo Kikwete hakuwa nayo, Lowassa hakuwa nayo, na Membe wala mtu mwingine yeyote hatakuwa nayo kama katiba hii aliyo acha Nyerere haitabadilishwa.
 
Baada ya Mwalimu J.K Nyerere kuondoka duniani ule u-Mr. Clean wote wa Banjamin Mkapa nao ukaondoka duniani na badala yake akageuka kuwa Mr. Fisadi. Kwa kweli katika awamu ya kwanza ya uongozi wake alifanya kazi kubwa sana. Alikuwa na washauri wazuri katika nyanja mbalimbali hususani katika uchumi na sera za maendelo. Kwa jinsi hali ya nchi ilivyokuwa hoi wakati rais Mwinyi anaondoka madarakani bila jitihada alizozifamya Mkapa katika kufufua uchumi wa nchi na ku-suppress mfumuko wa bei nadhani tungekuwa bado tunacheheme sana.

Huyu mzee alifanya kazi kubwa sana ya kuliinua taifa letu katika kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi wake kama rais wa JMT. Kwa hilo sitosita kamwe kumpongeza! Na kama hiyo nafasi ndio angepewa mkwere kipindi hicho (1995) nadhani leo kama taifa tungekuwa tunaogelea kwenye dimbwi la ufukara na wala siyo umaskini
 
Back
Top Bottom