Mambo muhimu ambayo Mzee Mkapa hajaweka wazi katika kitabu chake ''My Life, My Purpose''

Afu kuna tuhuma kwamba alipewa cheni ya dhahabu ya kilo 5 huko buli sasa badala ya kuikabidhi IKULU yeye akawa anaivaa shindoni akaifanya yake kumbe ni ya Taifa.

Hiyo cheni ya Taifa basi ilikuwa nzito mno, ‘kilo 5’ sio masikhara.... ndio maana shingo imemtitia Che Nkapa.
 
kaka ni kweli alipewa, kuna ule mkufu wa kuvaa wa dhahabu na nyepesi nyepesi zinasema akapewa na mziko wa kilo nyingi tu kaa 5 hivi kama zawadi.... haya mambo si ya kwangu ila yapo mtaani, kwa hiyo ni wajibu wake ayatolee ufafanuzi.

Jiwe la kilo tano, lakini mkufu wa kilo tano kisha akawa anakaa hilo hapa na.
 
FUSO,

Mzee baba story nyingine unaona kabisa ni uongo,wala haiitaji ufafanuzi.

Sasa cheni kilo 5 mtu anaivaaje shingoni?!!! Mweeh
 

Utetezi wa Mkapa kuhusu EPA ni wa kipumbavu kabisa!

Eti watu walinidanganya!

Rais mzima tunaejua ana akili “anadanganywa” nchi inaibwa?

Yaani kabisa unaletewa stori mezani unashindwa kujua huu ni wizi na huu si wizi?

Mimi na akili zangu hizi,huniletei stori nisijue hiki ni kipigo na hiki si kipigo!

Plus,hata kama hakujua kweli,then baada ya wizi kwanini hakuadhibu mtu!?

Jamaa lina utetezi wa mavi kabisa!

Limenifanya nikalidharau kabisa!

Bure kabisa!
 
Yaaani mtu aandike kitabu halafu humo ndani ajikandye au aonyeshe udhaifu wake, ni ngumu sana labda vitabu vinavyowahusu kina Clinton na Blair, sio viongozi wa kiafrika.
 
Kwenye TISS kumuondolea sifa kikwete sio kweli,isipokua TISS ndio ilimsaidia kikwete kutangazwa mshindi,hii ni baada ya BM,CDF , IGP na PM wa kipindi kile,walimuogopa kikwete na kutaka kutomtangaza kwa kuhofia mabaya yao,na walikaa kikao cha siri ktk kambi 1 wapo.lakini mchezo kuo ulishtukiwa na TISS wakamtonya jk,na jk ilibidi aombe baraka kwa bibi na bibi hakusita,akawakulupusha kwenye kikaochao cha siri.kwa aibu iliwabidi wakamtangaze mshindi.
 
Wabongo bana

Mtu anaanza kuchambua kitabu kabla hajakisoma
Hahaha
Kakiona kwenye TV na muda huo huo akawa keshajua ndani pameandikwa nini.

Yale yale ya mtu katika mazungumzo ya kahawa anakupa story za Brazil au Japan wakati hajawahi kupanda ndege hata siku moja.
 
Sikiliza, Mkapa alifanya kila awezalo kumzuia JK 2005 lakini nguvu ya wanamtandao ilimfanya asalimu amri mbele yao dakika ya mwisho.
Kweli kabisa,hakuna mtu aliepambana kuupata urais akiwa mwenyewe ni jk.kwasababu tu jk michezo ya kisiasa anaijua vizuri sana.
 
Kweli kabisa,hakuna mtu aliepambana kuupata urais akiwa mwenyewe ni jk.kwasababu tu jk michezo ya kisiasa anaijua vizuri sana.
Zungumza ulijualo! Rostam na Mzee wa Bati utawapeleka wapi
 
Hapo umebugi ile mbaya!!!! SI KWELI
 
Kwa akili zako unafikiri kuna mtu anaweza kusema mambo yake yote? Hakika bado watu wana akili nyembamba sana kama ndio fikra zinakutuma kuwa utaelezwa kila kitu! Huwezi kuanika kila kitu mzee, hilo liko wazi na wote tunajua hilo. Mtu atayekwambia kila kitu ni mtu aliyetokwa na akili, mwendawazimu
 
Mkuu hivi unaijua nguvu ya taasisi ya uraisi pamoja na nguvu anazopewa anae kalia kiti cha uraisi?
Unajua hizo nguvu zinakuwapo hadi siku anapo apishwa mrithi wake?

Jeuri ya kumtisha raisi na kumfanya afuate matakwa yako kilazima kwa katiba ya Tanzania hakuna mtu alie nayo ambae si raisi alie madarakani.

Jeuri hiyo Kikwete hakuwa nayo, Lowassa hakuwa nayo, na Membe wala mtu mwingine yeyote hatakuwa nayo kama katiba hii aliyo acha Nyerere haitabadilishwa.
 
Baada ya Mwalimu J.K Nyerere kuondoka duniani ule u-Mr. Clean wote wa Banjamin Mkapa nao ukaondoka duniani na badala yake akageuka kuwa Mr. Fisadi. Kwa kweli katika awamu ya kwanza ya uongozi wake alifanya kazi kubwa sana. Alikuwa na washauri wazuri katika nyanja mbalimbali hususani katika uchumi na sera za maendelo. Kwa jinsi hali ya nchi ilivyokuwa hoi wakati rais Mwinyi anaondoka madarakani bila jitihada alizozifamya Mkapa katika kufufua uchumi wa nchi na ku-suppress mfumuko wa bei nadhani tungekuwa bado tunacheheme sana.

Huyu mzee alifanya kazi kubwa sana ya kuliinua taifa letu katika kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi wake kama rais wa JMT. Kwa hilo sitosita kamwe kumpongeza! Na kama hiyo nafasi ndio angepewa mkwere kipindi hicho (1995) nadhani leo kama taifa tungekuwa tunaogelea kwenye dimbwi la ufukara na wala siyo umaskini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…