Mambo muhimu ambayo Mzee Mkapa hajaweka wazi katika kitabu chake ''My Life, My Purpose''

Mambo muhimu ambayo Mzee Mkapa hajaweka wazi katika kitabu chake ''My Life, My Purpose''

Benjamin Mkapa amejichokoza kwa kuandika kitabu. Ipo siku wanaomfahamu watamchokoza kwa kuandika kitabu chake akiwa hai. Hapo ndipo tutakapoona Serikali ikipiga marufuku maandishi na kufanya usomaji wa maandishi kuwa jinai.
 
FUSO,

Sasa hapo hicho kitabu kingekuwa kikubwa sana na ingekuwa shida kukisoma so vingine lazima viachwe mku la sivyo kitadondosha kabati za watu siunajua kabati zingine zilishaliwa namchwa!!!
 
Hawezi kuandika kila kitu Mkuu - ndio maana nikasema mambo muhimu!
Kuhusu uchaguzi wa 2005 mnaweza kupata dondoo katika Kitabu cha Makwaia wa Kuhenga cha mwaka 2007. Kina ukarasa wenye mambo mengi kuhusu uchaguzi huo
 
Mkapa Ndiye aliyesababisba ushenzi wote unaoendelea mpaka leo!

Ilo la idala ya usalama wa taifa kukataa ni kweli ila kikwete alikuwa akiungwa mkono na JWTZ na Salim alikataliwa na jeshi na ndiye alikuwa apewe nchi so ndio ugumu ulipoanzia apo kwa Mkapa.
NE OKITOKEA 2020 KWA JIWE? ikawa kinyume ,KITENGO kikamkubali na Mabakamabaka wakamkataa??😁😁😂😂
 
Kutokuwepo hivyo vitu haimaniishi hicho kitabu ni batili. Huwezi kuweka kila kitu wazi kwenye autobiography maana kuna mambo ambayo hutapenda watu wayajue kuhusu wewe au ukiyasema yataumiza watu wengine ambao ulishirikiana nao. Niliwahi soma autobiography ya Charlie Chaplin ambapo alisema wazi kuna mambo ambayo hatayasema kabisa.

Pia kuna kitabu cha jamaa mmoja muingereza wa karne ya 19 ambaye alikua anaandika matendo yake ya ngono kila alipofanya na baadae aliyakusanya na kuandika kitabu. Pamoja na kuwa anonymous lakini kuna maelezo, majina na matukio mengine hakuwa tayari kuyaweka wazi.

Sidhani kama Mandela, Mengi au Edwin Mtei wameandika kila kitu Chao kwenye vitabu vyao. Hata mimi mpaka hapa nilipofikia na sina umaarufu wowote lakini kuna matukio ambayo siwezi kuyaweka wazi maana ni ya aibu na yanahusisha watu wengine ambao sidhani kama wangependa yajulikane.
 
Nitajalibu kujibu maswali yako yote ingawa kwa awamu
swali la pili:::kipindi cha 2005 Kund la EL na JK Rostam kinara alikuwa ni edo,hapa nadhanj ndio maana umeuliza kwann mkwere not edo..Sababu kwann sio El 2005 na n jk ilikuwa ni la kidin au mgombea atoke zenji...kwa kigezo hiki ndipo wana wanamtandao wakapiga kampen atoke uku lakin muislam ndipo jk akapenya na walijua itakuwa rahisi kumdhibiti ila kama angepita masai pangekuwa na hekaheka sana...

Mkuu sorry nimeingilia jibu lako hapa, 1995 hao hao wanamtandao walimsimamisha JK mpaka pale mzee mzima JKN alipoingilia lakini tunaambiwa mkwere alitoboa ila busara za Mzee zikatumika.. Hapo utaona bado wanamtandao hawakuwa na mgombea wakuaminika zaidi ya JK since 1995.. To make it short, wanamtandao walimtegemea sana JK awe raisi ili wapate mwanya wa kuiteka nchi na baada ya hapo ingekuwa rahisi kwao kuendelea kupandikiza maRaisi waliowataka wao kwa maana ya after JK the next Lowassa.
 
yes ilikuwa kubwa sana kiongozi, Mzee alikuwa anaivaa kama kikoi yaani inapita shingoni begani hadi kifuani chini ya mkono.... kuna kuda akiwa na press ilikuwa inaonekana kwa nadra nadra ....pembeni pembeni kwa suti.
utembee na kilo 5 shingoni hahahahha hii porojo ya moto sana imenishinda kumeza.
 
Kwa wale waliokisoma hicho kitabu, ile hadithi ya kukatwa mitama ya hatari na mtoto wa kufikia mpaka center bolt ikapinda, IMO au imesshaulika kwa makusudi?
 
Benjamin Mkapa amejichokoza kwa kuandika kitabu. Ipo siku wanaomfahamu watamchokoza kwa kuandika kitabu chake akiwa hai. Hapo ndipo tutakapoona Serikali ikipiga marufuku maandishi na kufanya usomaji wa maandishi kuwa jinai.
hakuna kitabu kitaandikwa... kumbuka hata hichi unachokiona kimepitiwa sana ndipo kibali cha kuwa published kikatoka, mambo hayapo kilahisi hivyo so hata kama Nkapa angetaka kuweka wazi mambo yote system isingeruhusu kwa usalama wa nchi!,
Pawaga
 
Hivi uuzwaji wa nyumba za serikali ulilenga yeye kujinufaisha na hekalu huko oysterbay? basi ni bora nyumba za serikali zirudishwe kwa namna yoyote ile ili kukwepa aibu ya maafisa waandamizi kwenda kupanga uswahilini
 
Fuatilia uteuzi wa Kikwete ulivyokuwa utapata habari kamili, wakati ambapo majina ya mwisho yalikuwa Kikwete, Salim Ahmed Salim na Prof. Mwandosya. Kikwete alikuwa na taarifa chafu ambayo Mkapa aliamua "kuipuuza", lakini kuipuuza huku kulikuwa na walakini.
why kikwete!!!
Mwandosya alikuwa mkali mno kiasi kwamba hata Nkapa alipata wasiwasi nini kingemtokea baada ya kustaafu ukizingatia alikuwa kafanya ufisadi mno, na pia kwa wakat ule alihitajika rais either awe ambaye ni muislam kwakuwa incumbent alikuwa mkristo or atokee znz so automatically Mwandosya akawa disqualified

Salim ahmed salim, alikuwa mdini mno pia zanzibar ambapo walimchujia kutokana na kwamba alikuwa na ukalibu mno na waarabu waliokuwa wanaiyumbisha zanzibar pia alitumia nguvu yake wakat akiwa OAU kuwasaidia waraab waliokuwa wanataka kuiangusha znz, pia Salim alikuwa sio chaguo la wanamtandao
Pawaga
 
Synthesizer,

je unahisi mkapa baada ya kukiandika kitabu chake ali publish au ilibidi kwanza kipitie sehemu kupata ruhusa ya kuwa published ?kama kuna sehem ilibidi kipitie unahisi wewe ungekuwa mwanajopo wa hiyo sehem ungeluhusu yote aliyoandika yatoke!!!!
Nadhan mkapa alaumiwe kwa kutoweka mambo yake binafs sio mambo mazito kama uliyosema na wanayosema wengine, Na pia nadhan kwa level binafsi kajitahidi sana kufunguka mpaka kamtaja demu wake wa kimarekan ambaye aliendelea na mahusiano nae hata baada ya kuingia state house ila akiweka wazi mno mambo yaliyotokea enzi zake hapatatosheka mf ishu ya mwembechai na znz baada ya uchaguz.....
 
Mm nafikili kama ajaweka ndo maana tunakuaga na kipengele cha kuferi kwa mwandishi tukiwa tunachambua kazi za fasihii andishi, then mambo mengine yanabaki nyuma kwa masirah ya taifa,
 
Kwa wale waliokisoma hicho kitabu, ile hadithi ya kukatwa mitama ya hatari na mtoto wa kufikia mpaka center bolt ikapinda, IMO au imesshaulika kwa makusudi?
Kwa ulinzi wote huo wa rais, hiyo fursa ya kumkata mitama aliipata wapi? unaweza kujikuta ahera ndani ya sekunde..
 
Back
Top Bottom