Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Sasa kuna siku kazi zimepamba moto, basi simu ya bwana harusi ikawa inaita sana akawa hapokei. Mdada mmoja akamwambia bwana harusi pokea simu inaita basi akapokea nadhani sijui kuchanganyikiwa au vipi akaamkia “shikamoo”, sijui akajibiwa nini tukamsikia anasema “mdau nimekwambia atakuja mtu huko huko kuwatembelea wiki ijayo atawasaidia”. Sijui akajibiwa nini akamwambia yule mpigaji simu “ongea na huyu mwenzangu atakuasaidia” akawa amempa yule dada aliyemwambia apokee simu ili aongee na simu yake.

Yule dada akachukua simu akijua anaongea na grantee ii amsaidie bwana harusi kutatua changamoto yake akamuuliza mpigaji una shida gani nikusaidie? Akajibiwa mimi ni mchumba wake na ni mke mtarajiwa wa huyo mwenye simu lakini naona ananiambia vitu ambavyo ambavyo sivielewi

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Hii stori imenichekesha[emoji23]
Kuna kibarua niliwahi kufanya almanusura niwehuke.

.......
Hii ni moja kati ya nyuzi nzuri sana nimesoma mwaka huu.
Uzi unaojenga,,
Kwa episodes nilizosoma,tayari zimenisaidia kujievaluate,madhaifu yangu,ubora wangu,,na zinaendelea kunipa mwanga wa mambo mengi especially carrier wise.


Mungu akubariki Mkuu,,
Huu uzi ni uzi bora kabisa kusoma ,hasa graduates kama mimi ambao bado tunapambana kwenye soko la ajira.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ukiacha mambo ya mpira unakuaga na hekima hivi!
Kongole sana mkuu.
 
Kumbe ukiacha mambo ya mpira unakuaga na hekima hivi!
Kongole sana mkuu.
Mpira ni moja ya burudani ninayoipenda sana.

Mimi si mtu wa kujichanganya mtaani, hivyo nyuzi za mipira ndizo zinazonipa vibe humu jf.

Ni mtu niliyeamua kujiwekeza kumtafuta Mungu sana,,,still nipo kwenye hizo struggles
Wale tunaokutana nje na humu huwa wanashangaa sana .. eti mimi mpole sana tofauti na ID yangu..hahaa,, ni vile mtu anasoma tu mabaya.

Kushabikia Mpira kidogo, si mbaya, tunachangamsha nafsi😂
 
Kuna clip fupi ya speech ya Mwalimu Christopher Mwakasege
Anasema Jifunze kuongea na Mungu kila siku.

Kama jinsi tunavyoamka na kuwajulia hali wazazi wetu, na ndugu zetu jamaa na marafiki.. hivyohivyo God wants the same, even more.

Hata kama huna chochote unachoona kinafaa kusema, basi mwambie tu Mungu Shkamoo.
Ataweza kucheka lakini atajua umemkumbuka.

Siyo ulikurupuka, hujaongea naye..
Njiani umekumbwa na mabalaa sasa
Ndio unaenda kumtafuta.


Kulala na Biblia pekee haitoshi,
Mtu anaweka Biblia pembeni ya kitanda
,Haisomi, imekaa kama pambo... Ila anaitegemea imsaidie siku majinamizi yamembananisha.
Kuitamka tu toka Katika jina la Yesu haitoshi.
Kusema nalindwa na damu ya Yesu pekee haitoshi.. we have to show it by actions.. yaani imani inaenda na matendo.


Tunatakuwa tujenge urafiki na Mungu
Ushirika na Mungu una mambo mengi sana ikiwepo kiu, heshima(hofu) Kwa
Mungu
Kujenga urafiki naye(utii)
Mawasiliano yetu na Mungu ni maombi,, muda wote,, siyo muda
Wa matukio tu.

Hivi vyote ni gharama.
Unakutana na mtu, he/she can't sacrifice even a single day for fasting prayers, achilia mbali maombi ya kawaida..
Neno ambalo ndilo kuna nguvu na msaada wote hasomi..
Mzani wetu unaegemea kwenye mambo mambo mengine ila mambo ya Mungu ni sifuri, tunadonoa..
Na mwisho wa siku mamlaka ya kimungu kufyatua mapepo tunataka tuitumie rahisi tu.

Tumtii Mungu kwanza, Kwa kufuata maagizo na kanuni.. hapo sasa ndipo tutaweza kumfyatua shetani.

Ulimwengu wa kishetani pia una principles zake..
Rejea mfano wa paragraph ambayo wale wazee walikuwa wakimzunguka
DadaB na kuwa kama wanafukuza vitu hewani.

Vivyohivyo ulimwengu wa Mungu.
Zipo kanuni na gharama
.

Wengi hatupendi kuzijua wala kuzifuata
We just want shortcuts.
 
Upo deep sana Mkuu, nimejikuta nimemezwa na hili andiko lako.

Kunayo namna napaswa kumtafuta Mungu kwa nia.
 
Somo Zuri sana mkuu limenifungua zaidi macho katika kukazia Ile amri ya pili Usilitaje Bure Jina la Mungu wako, wengi tunakosea sana hii amri, Mungu aturehemu🙏
 
Upo deep sana Mkuu, nimejikuta nimemezwa na hili andiko lako.

Kunayo namna napaswa kumtafuta Mungu kwa nia.
Kumbuka, Mungu anatupenda wote ila
Wale wamtafutao Mungu Kwa bidii ndio watakaomuona

Ni muhimu sana kutunza uhusiano wetu na Mungu.
Uhusiano ni ile hali ya kuambatana na Mungu,,, huwezi kuambatana na kitu kama hakuna vitu vinavyoendana.

Dhambi inatufanya tufanye vitu tofauti na Mungu hivyo ile hali ya kuambatana inapotea.

Hivyo ili kuimarisha mahusiano yetu na Mungu lazima kuwe na
-Moyo wa ibada
-Ushirika na Mungu
-Muda/Sadaka

Moyo wa ibada utakusaidia kutambua ukuu, mamlaka na uweza wa Mungu. Ukishajua hayo.. utatamani kumjua Mungu zaidi, utamhofu na hali ya kumpenda itakuja.

Ushirika utakupa kujua mapenzi ya Mungu, na mpango wa Mungu kwako. Na ukisoma neno anakuambia"For I know the plans I have for you, says the Lord , ni mawazo mema, wala si mabaya"Yer 29:11
Ukijua haya, hutamlaumu Mungu, utamfurahia.. katika kila jambo utakuwa na shauku kujua mapenzi/mipango yake.
Mapenzi ya Mungu kutimizwa ni muhimu zaidi kuliko yale yetu ..
Hata katika sala ya Bwana, Yesu alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wake kusali ukisoma injili kama ilivyoandikwa na Mathayo Mtakatifu 6 kuanzia verse 15 nadhani..
Tunaona kwenye sala, kipaumbele Cha Kwanza ni mahusiano yetu na Mungu"Baba Yetu uliye mbinguni"
Cha pili ni jina lake litukuzwe
Inakuja mapenzi yake kutimizwa
Mahitaji yetu Yanafuata baadaye baada ya yale muhimu ya Mungu kwanza.

Ni muhimu kuwa na muda wa kujifunza neno,na kupata muda wa maombi.
Kumbuka Neno ndilo lilifanya kila kitu, na Neno halimrudii bila kutimiza mapenzi yake(Mungu) alilolituma ,, rejea Zaburi.
Ukijua hili utang'ang'ana kujifunza .. pia utamrudia kwenye maombi na kuhojiana naye,,
Shida ijayo, muambie.
Neno pia ukilijaza kwa wingi litakusaidia kumpiga shetani, kukwepa hila zake.
Rejea mfano wa watu wa Gym mambo ya body fitness..
Yaani Kuna ratiba, na zinazingatiwa.. hawaskip hata siku Moja.
Siku akiacha, basi uwezekano wa kurudi kwenye default mode ni mkubwa.

Vivyohivyo kwako apply hivyo upande wa muda wa kujifunza na maombi.
There is no substitute for prayers.

Sadaka hupiga kelele mbele za Mungu., Zinamkumbusha
Rejea sadaka za Cornelio... Acts 10.
Sadaka zake zilipiga kelele to the extent Bwana akashindwa kukaaa kimya, his prayers with sacrifices forced God to answer his prayers.

Sadaka si kupeleka pesa Kanisani pekee.
It's more than that..
Waweza kutoa sadaka kwa namna mbalimbali kulingana na maelekezo ya Roho Mtakatifu mwenyewe ndani yako.
Sadaka ya kujitoa mwenyewe pia ni nzuri sana pia(Fasting) and it works better... Ila ina gharama,, watu wanaikwepa.

....
Haya machache yatakusaida katika safari yako ya kumtafuta zaidi Mungu
Na Bwana akutie nguvu,anajua nia yako.


Lakini kazana kuomba...
Nia pekee haitoshi...
Kitu gani kitakuwezesha? Ni nguvu za Mungu Kwa maombi.
Hata Petro alikuwa na nia nzuri sana juu ya Yesu, kabla hajamsaliti... Akasema ikiwezekana hata kama itamlazimu kufa Kwa ajili ya Yesu then he's ready... We all know what happened.. alimkana Yesu mara3.
What I want to say is, nia ya kitu pekee haitoshi kutufanya tutoboe..we need prayers.
 
Amina Sana, barikiwa sana Mkuu.
 
Tupe baba, leo kuna nondo adimu sana, nimefurahi zaidi keenye nondo za maisha ya kiroho hususani mtumishi Saint Anne tunamtafuta Mungu sana tukiwa na shida then shida zikiisha tunamsahau kabisaa walonz wakitushtua kidogo tu tunaanza kulitaja jina la Mungu ambalo kimsingi hatumwabudu ipasavyo! Mwisho wa siku sasa ni kilio
 
Nami nitakutafuta siku moja nikuone live ulivyo mpole.
 
Nami nitakutafuta siku moja nikuone live ulivyo mpole.
Aisee😂
Inahitaji ujasiri
Mimi sijui huo upole wanauonea wapi maana sina upole wowote.

Karibu Mkuu
Mimi napatikana kwenye biashara zangu za cake na perfume,,, kama ni mdau wa hivi vitu tutaonana tu.

Hata kama si mteja,
Twaweza onana pia, sina ubaguzi.
Inategemea tu na namna tunawasiliana hapa jukwaani.
 
Amin.
Tujitahidi kuyaweka haya kwenye matendo.
Kama vile mwili pasipo roho, umekufa . Vivyohivyo na imani pasipo matendo imekufa.
 
😁😁tutakaribia
 
Eti Mungu shikamoo dah seriously??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…