Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

TAI DUME pole kwa kamoko....tupe mwendelezo...
Baada ya timbwili la Kibondo ikawaje huko Kasulu?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
nimeshapoa mkuu. Ila jana nimeinjoi game maana mnyama alipiga game ya maana ambayo sikuiona ile performance kwa kama miezi 10 hivi. Naona tumeanza kujipata. I bet simba na wydad zinaenda robo. Mwendelezo jioni mkuu
 
Me nadhani ungejikita zaidi kwenye utunzi wa story. Haya mambo ya mpira waachie kina manara. Huwezi niambia timu inayovevenya mkia iende robo fainali, Haiwezi na haitaweza.

Hakuna cha Simba wala Yanga atakayetoboa kwenye makundi.
 
Tunza maneno Yako tutakutane tena JF[emoji1666]

Sent from my Pixel 4a (5G) using JamiiForums mobile app
 
Hao wazungu wanaotoa izo pesa (zinaonekana ni nyingi kweli kweli) wao wananufaika vipi? au wanazirudishaje? au kuna ajenda gani nyuma ya hizo pesa? au wao ni wanatoa Tu bila malengo/return yeyote?

Hizo NGO zikipewa izo pesa wanazifanyia nini hasa? Ungeota mfano baadhi ya mambo ambayo yanafanywa na izo NGO baada ya kupewa pesa TAI DUME
 
Kwenye kukujibu hili swali wacha nitulize na akili yangu kabisa maana hii hoja imekuwa ikileta ukakasai kwa wengi.

Wakati mwingine wafadhili, ikiwa ni serikali au watu binafsi kutoka nchi za Magharibi au wazungu, wanaweza kutoa misaada kwa sababu kadhaa, na kuna mifano mingi ya jinsi wanavyoweza kunufaika au kufuatilia malengo fulani. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa HAKUNA msaada ambao ni wa bure eti jamaa wanatupenda sana. isipokuwa KILA MSAADA unakuja na malengo malengo yake kutegemeana na muktadha wake. Mfano misaaada mingi inatolewa kwa sababu zifuatazo:​
  1. Diplomasia ya Maendeleo: Baadhi ya mataifa hutoa misaada kama njia ya kujenga uhusiano mzuri na nchi nyingine. Hii inaweza kuwa njia ya kuimarisha mafungamano ya kidiplomasia na kuimarisha ushawishi wa kimataifa.​
  2. Biashara: Kutoa misaada inaweza kuwa sehemu ya mkakati wa biashara. Kwa mfano, nchi inayotoa misaada inaweza kutarajia kufungua milango kwa biashara zake au kuboresha upatikanaji wa malighafi muhimu.​
  3. Usalama wa Kimataifa: Mataifa yanaweza kutoa misaada kwa lengo la kuhifadhi amani na usalama wa kimataifa. Kusaidia katika kuzuia migogoro na kutoa misaada ya kibinadamu inaweza kuchangia utulivu wa kimataifa. na hivyo wao kunufaika kibiashara.​
  4. Kuongeza Umaskini na utegemezi: Hapa wala usishangae. Baadhi ya misaada hutolewa kwa lengo la kudumaza akili na ubunifu wa wapewa misaada ili kuendelea kuwa tegemezi tofauti na tunavyohubiriwa kwamba misaada inakuboresha hali ya maisha ya watu katika nchi maskini. umasiki wetu unaweza kuwa faida kwao kwani wataendelea kukomba rasilimali zetu kwa kubadilishana na vitu vidogo vidogo sana mfano mavazi, chakula nk.​
Hizo NGO (Shirika Lisilo la Kiserikali) zinapopokea fedha, wanaweza kuzitumia kwa njia mbalimbali kulingana na malengo yao. Mifano ya shughuli wanazoweza kufanya ni pamoja na:​
  1. Maendeleo ya Jamii: Kujenga na kuboresha miundombinu ya jamii kama vile shule, vituo vya afya, na maji safi na huduma za usafi.​
  2. Afya na Lishe: Kutoa huduma za afya, kampeni za chanjo, na programu za lishe kwa jamii zilizoathiriwa.​
  3. Elimu: Kusaidia miradi ya elimu, ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya kufundishia, ujenzi wa madarasa, na kutoa ufadhili kwa wanafunzi.​
  4. Mazingira: Kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira, kama vile upandaji miti, utunzaji wa ardhi, na kuelimisha jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi.​
Ni muhimu kutambua kwamba wafadhili wanaweza kuwa na malengo mazuri, lakini pia kuna sababu za kimkakati nyuma yake zinazolengwa, ikiwa ni pamoja na maswala ya utegemezi na masuala ya utawala. Kwa hiyo, ni muhimu kuwa na uwazi na ushirikiano katika utoaji na matumizi ya misaada ili kuhakikisha kuwa inaleta matokeo chanya na endelevu na pia nchi masikini zenyewe ziwe na maamuzi ni aina gani ya misaada wanayoitaka. ILA CHA MUHIMU NI NCHI MASIKINI ZENYEWE ZIAMUE KUACHANA NA UTEGEMEZI NA KUTUMIA RASILIMALI ZAO KIKAKMILIFU ILI KUJIKWAMUA.​
 
EPISODE 9: Umeshawahi wahi kufanya kazi ambayo mda wote unakuwa bize kazini? Work-life balance is a must if don’t wish to go insane.
Baada ya kumaliza ile tripu ya Tabora na Kigoma salama at least nilikuwa nimeboresha uzoefu wa kazi za field kwenye hii ofisi mpya. Kumbuka kwamba nilibaki peke yangu baada ya kukubaliana na dadaB arudi home ila kutokana na kumsoma kwa mda mfupi na kuunganisha na uzoefu wangu wa kule kwa Dr KJ kazi ikawa rahisi sana kwangu. Hapo ndipo nikajua kwa nini waajiri wengi sikuhizi they prefer job experience than grade A academic certificates.

Nikarudi ofisini salama na kwa kushirikiana na dadaB tukasubb report pale na maisha mengine yakaendelea. Baada ya muda na mimi nikawa ni among senior officers pale hata nikawa trusted kuwa-mentor the new employees maswala ya kazi. Anyway it was good experience kwa kweli na niliinjoi sana kazi yangu.

Uzuri wa ile kazi ilikuwa ni kusafiri kitu ambacho nilikuja kugundua kumbe mimi napenda sana kusafiri tena hususani safari za mikoa ya mbali na vijijini nilikuwa napenda sana. Unajua kwenye kusafiri sio tu kuenjoy zile moments za kuwa kwenye gari au flight lakini inasaidia kuexplore new opportunitis na kuongexza network yako na watu tofauti tofauti unaokutana nao. Sasa pale ofisini ilikuwa ukikaa sana hujasafiri basi ni mwezi na nusu au miwili. Lakini kikawaida ilikuwa kila mwezi lazima mtu usafiri walau kwa si chini ya wiki, yaani safari ilikuwa ni lazima kulingana na nature ya kazi hususani kwenye idara yetu. Mimi ilifikia wakati mpaka nikawa nawatania watu kwamba sitakuja kuoa au kuruhusu mke wangu afanye kazi pale ofsini maana ndoa inaweza ikayumba hahaahaa sababu watu kila mara wapo safarini na hivyo mke anaweza kushindwa kutimiza majukumu ya nyumbani vizuri (jokes) with that job nilisafiri kila wilaya unayoijua wewe hapa Tanzania zilikzokuwepo kipindi kile. Utanitajia wapi nisipajue mimi.

Ofisi ilikuwa inakufacilitate kila kitu ukiwa safarini ili uweze kuendelea na majukumu yako ya kazi hata ukiwa nje ya ofisi. Mfano vitendea kazi bora kabisa laptops, vimodem kwa ajili ya internet vyenye unlimited bando nk. Kwanza ilikuwa ni marufuku staff kupanda mabasi haya abiria is either usafiri kwa gari ya ofisi sehemu ambako hakuna viwanja vya ndege au ukodi gari hata ktoka dar mpaka ifakara endapo usafiri wa ndege haupo na magari ya ofisi yapo na shughuli nyingine. Na ilikuwa lazima ulale sehemu yenye hadhi ya juu kulingana na eneo ulilopo ili kuwezesha usalama wako na pia mazingira rafiki ya kuendelea kupiga mzigo. Kifupi ilikuwa ukisafiri unasafiri na dawati lako maana kwa necha ya kazi ilikuwa huwezi kumuachia mtu akushikie shughuli zako maana utamuonea tuu, labda kama mtu ni mgonjwa, amefiwa au likizo za uzazi ilikuwa inaeleweka ila sio safari. Ukisafiri utawezeshwa kila kitu kusafiri na majukumu yako, hakuna kumuachia mtu ofsini.

Kwahiyo life pale ofsini ilikuwa ni mshike mshike, bize mda wote. Mtu kwenda weekend job au kuchelewa kutoka mpka saa tatu usiku ilikuwa ni kawaida sana. Yaani ilikuwa ukiangalia vimeo ulivyonavyo kwenye meza yako unajikuta tuu wenyewe kwa hiari yako jumamosi au jumapili unaingia job walau kwa masaa manne ukapunguze vimeo. Au mara kwa mara unatoka ofsini saa mbili au tatu usiku.

Mfano mimi kwenye portifolio yangu nikajikuta nina kama zaidi ya NGOs 700 ya kuzisimamia. Yaani hapo uhakikishe wameleta report zao za fedha na miradi, report zimekaa sawa, uindize report kwenye system tena kwa kuzitranlate kwa kingereza, kuhakikisha umewatumia fedha za quarter nyingine baada ya kujiridhisha na report ya fedha. Kisha uhakikishe uhakikishe hizo NGOs umezitembelea ili kwenda kuzikagua huko field kama wanatekeleza miradi sawa sawa au wapo wrong ili uwaelekeze. Wakati huo huo uhakikishe unatrain waliokosa funding ili nao wapate fedha maana ofisi ile ilikuwa na wafadhili wengi waliokuwa wanaweka fedha zao ili ziende kwa wadau huko mikoani, kwahiyo mnajikuta mna fedha lakini wanaopata ni wachache so in order to maintain reputation ya ofisi kwa donors ilikuwa ni lazima kwenda huko na huko mikoani kuwafundisha watu jinsi ya kuomba na kupata ruzuku kutoka kwetu kulingana na vigezo vetu ndio mana tukawa tunapokea hata proposal za Kiswahili ilimradi kutombagua mtu.

Sasa kwenye mazingira kama hayo unafanyaje? Watu tulikuwa bize muda wote ukiangalia kazi ni nyingi mpaka unatamani siku ingekuwa na masaa 30 walau unaweza kupata muda mzuri wa kupumzika. Kiukweli kuna watu ambaop hawakuwa na shida sana na kazi waliacha asee. Pia ukiachana na sababu za integrity kuachishwa kazi kama mshikaji wangu Big lakini wengi pia walitimuliwa sababu ya performance issue, hawakuweza kwenda speed ya ofisi. Na katika vitu ambavyo menejiment ilikuwa haiwezi kukuvumilia ni malalamiko kutoka kwa grantees kwamba umewaomba rushwa au umewacheleweshea fedha zao, hapo ulikuwa hueleweki. Kwahiyo unachotakiwa kufanya grantee akileta report yake leo baada ya wiki uwe umeshaireview na kuprocess fedha zake. Hata system ilikuwa inakukumbusha kwamba report ipo due hivyo unatakiwa kuishughulikia. Sasa mtu unasimamia miradi zaidi ya 500 what do you expect. Usipokuwa smart and organized unakuwa chizi. Work-life balance ni kama haikuwepo pale ofsini.

Nakumbuka kuna new employee ndio alikuwa ameajiriwa ana kama mwezi tuu akapiga chini kazi bila kupata kazi nyingine. Yule jamaa alivoajiriwa pale alikuwa amebakiza kama mwezi hivi afunge ndoa. Basi ameingia pale ofsini amekutana na mshike mshike wa kaxi na hakuna ugeni, kwani ugeni ulikuwa mwisho wiki ya kwanza. Sasa yule bwana harusi inaonekana maswala ya kushughulikia maandalizi ya harusi yake alikuwa anayasimamia yeye mwenyewe kwa kiasi kikubawa sijui hata kama alikuwa na kamati yule bwana maana simu yake ilikuwa bize sana na kila kitu anaulizwa yeye. Basi pale mjengoni tukamchangia kama kawaida tena mzigi wa kutosha tuu na kutokana na maandalizi yake akaruhusiwa awe anafanya kazi nusu siku.

Lakini tulikuwa tunabaki na bwana harusi mpaka usiku maana naona alikuwa akiangalia haoni pa kutokea lazima abaki ofsini kupunguza majukumu. Sasa sisi tulikuwa tunafanya kazi kwenye pool ambapo wote mnaonana na kusikilizana. Sasa kuna siku kazi zimepamba moto, basi simu ya bwana harusi ikawa inaita sana akawa hapokei. Mdada mmoja akamwambia bwana harusi pokea simu inaita basi akapokea nadhani sijui kuchanganyikiwa au vipi akaamkia “shikamoo”, sijui akajibiwa nini tukamsikia anasema “mdau nimekwambia atakuja mtu huko huko kuwatembelea wiki ijayo atawasaidia”. Sijui akajibiwa nini akamwambia yule mpigaji simu “ongea na huyu mwenzangu atakuasaidia” akawa amempa yule dada aliyemwambia apokee simu ili aongee na simu yake.

Yule dada akachukua simu akijua anaongea na grantee ii amsaidie bwana harusi kutatua changamoto yake akamuuliza mpigaji una shida gani nikusaidie? Akajibiwa mimi ni mchumba wake na ni mke mtarajiwa wa huyo mwenye simu lakini naona ananiambia vitu ambavyo ambavyo sivielewi, je yuko sawa kwani maana kuna vitu nataka kumwambia kuhusu gauni la harusi. Ndio yule dada kumwambia bwana harusi wewe anayepiga simu ni mkeo sio grantee hebu toka nje ukaongee naye. Aisee ofisi nzima tulibusrst kwa kucheka. Yaani bwana harusi alivurugwa na kazi mpaka akawa amesahau sauti ya mkewe mtarajiwa. Lakini pia inaonekana sijui alivurugwa kiasi gani mpaka akawa anaongelea maswala ya kazi wakati bi harusi anaongelea maswala ya gauni. Ikabidi atoke nje akaongee na mkewe badae akarudi.

Basi harusi ikapita lakini baada ya wiki kama tatu hivi bwana harusi akaandika barua ya kuacha kazi. Sasa HR hakutaka kuiprocess moja kwa moja akawa anamtaka kwanza afikirie mara mbili mbili uamuzi wake labda kama ni ishu ya maslahi na amepata sehemu nzuri zaidi. Basi HR akatufata watu ambao aliona kidogo tupo karibu na bwana harusi ili tuongee naye. Bwana harusi wala hakuficha akatuchana live japo hajapata kazi sehemu nyingine ila mazingira ya kazi pale yamemshinda maana yalikuwa ni busy mno with less work-life balance. Tuakajaribu kumsihi pale avumilie atazoea tuu akagoma kabisa. Jamaa etu mmoja akasema jamani tumuacheni huyu ni mtu mzima anajua analolifanya. Mimi nikaongezea nikasema tena huyu muhehe wa Iringa huko tusije tumalazimisha akajinyongea ofsini halafu ikawa balaa jingine. Basi bwana harusi akaresign kama alivyopanga, mhehe yule ni kweli alikuwa hana kazi maana baada ya hapo vilianzan vizinga kwa sana na tuu vile mkewe alikuwa karibu anajifungua basi alikuwa na uhitaji sana wa pesa. Kwa sisi washkaji zake tulimbusti tulivyoweza lakini nilijifunza kuna watu wana maamuzi magumu na misimamo asee. Unaachaje kazi huna kazi?

Nakumbuka tulimfikishia HR sababu za kwanini yule bwana harusi ameacha kazi na uzuri au ubaya kwenye taarifa za ofisi ya HR waligundua wengi tuu walionekana hawakuwa na performace nzuri kwa sababu hawakuwa na muda wa kutosha wa kuopumzika. So ikawekwa mikakati pale ili kuboresha work-life balance kwa wafanyakazi. Hata menejiment walikuwa wanajua kwamba work-life balance was essential for promoting employee well-being, maintaining job satisfaction, preventing burnout, and creating a positive and productive work environment. Ignoring work-life balance can have adverse effects on individuals and organizations alike, impacting health, relationships, and overall job performance.

Mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuongeza wafanyakazi, kwa hiyo ikatafutwa ofisi nyingine yenye uwezxo wa kuaccommodate wafanyakazi wengi zaidi lakini pia likizo ilikuwa ni lazima. Maana before hapo likizo ilikuwa ni optional kwamba mtu unaweza ukalipwa pesa ule mda wa likizo ili uendelee kupiga mzigo, na kwa jinsi kazi zilivokuwa nyingi mtu aliona bora auze baadi ya siku za likizo ili apunguze kazi huku akipokea mshiko. Hii hata mimi nikifanya sana. Basi maisha baada ya hapo yaliendelea kama kawaida na kiukweli work load ilikuwa imepungua sana na tulifanya kazi kwa utulivu na ufanisi mkubwa.

Wadau wangu nilifanya kazi pale kwa miaka mi4 before I shifted to another organization. Based on my job responsibilities as a Program Officer - grants, I have developed a diverse set of skills as followas
  1. Grant Management: Demonstrated ability to review, assess, and select grant applications in accordance with established procedures and regulations.​
  2. Communication Skills: Regularly communicated with grant applicants regarding the status of their applications, ensuring accurate and timely information.​
  3. Training and Facilitation: Organized and facilitated training sessions on project and financial management for CSOs/NGOs/partners nationwide.​
  4. Supervision and Leadership: Successfully supervised over 100 grantees annually in various sectors, including governance, youth, human rights, gender & women empowerment, health and disability.​
  5. Capacity Development: Designed and conducted capacity development sessions for grantees, covering project management, financial management, project monitoring and evaluation, and project report writing.​
  6. Partnership Management: Worked closely with local partners to identify and address capacity gaps in project grants management.​
  7. Monitoring and Evaluation: Conducted field visits to assess and monitor project implementation performance and collect success stories from partners.​
  8. Flexibility and Adaptability: Ensured flexibility and high quality of capacity development support provided to partners.​
  9. Report Writing: Prepared periodic reports for management purposes and other stakeholders.​
  10. Stakeholder Engagement: Collaborated with various stakeholders, including CSOs, CBOs, FBOs, and NGOs, throughout the grant management process.​
  11. Project Implementation Oversight: Monitored and assessed project implementation to ensure alignment with goals and objectives.​
  12. Time Management: Successfully handled multiple responsibilities and tasks within deadlines.​
  13. Analytical Skills: Evaluated grant applications, monitored project performance, and prepared reports, demonstrating strong analytical abilities.​
Nipeni connection wadau

Muendelezo soma Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa
 
EPISODE 3: I learnt how to be proactive and beliving in myself in handling difficult situations.

Kwakweli nimeshindwa kupata Kiswahili fasaha cha heading hapo juu ila kuna situation unaweza kutana nazo katika mazingira ya kazi yakapelekea either uwepo wako uonekane una positive impact au ni mzigo tu. Hayo mimi yalinikuta nikiwa na mwezi mmoja tu pale ofsini chini ya Dr KJ the boss.

Nakumbuka ilikuwa ni tarehe za wafanyakazi wa pale ofsini kulipwa mishahara na mimi nilikuwa almost nakaribia mwezi pale ofsini. Boss alikuwa na utaratibu wa kwenda nao benki wafanyakazi wote na baada ya kutoa cash kila mtu alipewa chake then tunatawanyika, sikukuta mtindo wa kuwekewa pesa benki. Yaani wote mnaenda benki, mnapewa chenu kisha mnasepa na maranyingi mshahara alikuwa anaotoa tar 23. Siku hiyo ilikuwa Alhamis.

Mpaka tarehe ya mshara inafika mimi sijui nitalipwa kiasi gani. Nikasema leo ngoja nione basi tukafika mpaka benki then kila mtu akapewa bahasha yake. Kile kibahasha nilipokikadiria kilikuwa na uzito sawa tuu na alichopewa yule PS, cha mhasbu kilikuwa kimejaa zaidi ya wote pale huku yule dereva akiburuza mkia. Nikatia kibunda change mfukoni nikatawanyika mpaka magetoni. Kufika home cha kwanza ilikuwa ni kuhesabu ile cash aisee kiukweli haikuwa haba japo haikufika six digits. Kujiridhisha nikampigia Mhasibu nikavunga kutaka kujua kama hapo makato ya serikali na NSSF yamekatwa, akaniambia kaka Taidume kwa sasa wewe chukua tu hiyo pesa usiwaze. Nikataka kujua kama iyo ni salalry au posho akaniambia kwa mimi ile ni posho maana sijaingizwa kwenye mfumo wa salary mpaka nitakapomaliza probation. Nikaona afadhali kumbe kuna uwezekano kasalali kakawa hata six figures.

Ijumaa wakati naendelea na majukumu yangu kama kawaida mara boss akaniita na akaniambia anategemea kusafiri hivyo kwa siku tatu kwenda Arusha kwa mambo yake hivyo akanipa majukumu mawili matatu niyasimamie wakati yeye hayupo. Pia akania next week pale ofisini tutapata ugeni (one among the key and prominent donor wa project za pale ofsini) kutoka Ulaya. Hao wageni wanakuja kufanya evaluation nna kuangalia namna funding zao zilivyofanya kazi na wangetembelea baadhi ya field areas ili kucollect achievement stories. So akanitaka niandae walau sehemu tatu za vijijini huko tunakofanya miradi na kuwataarifu beneficiaries ili maandalizi yaanze. Yeye alisema atawahi kurudi kwamba angeondoka Kesho yake Jumamos, Jumatatu angerudi by Jumanne angekuwa Ofsini. Ratiba ya wageni ilionesha wangekuja kufanya evaluation yao Alhamis ya wiki inayofata na Ijumaa na Jumamosi ni kwenda Field. Tukakubaliana hivyo.

Kumbe bhana bosi alikuwa anaenda zake zake Samunge kwenye kikombe cha babu nae ni mmoja walioamini kombe la upako la babu lingeweza kutibu maradhi yake. Hili nilifahamu kupitia PS kwani aliniambia ofisini kwa wengine ofisini ameaga jumatatu atampelekea mtoto wake hospitali lkn ni anamsindikiza boss kunywa kikombe cha babu. Nikamtania tu naona PS unafanya kazi yako vizuri sana basi tukacheka pale tukaagana. Kumbuka boss japo alikuwa anakuja kazini lakini kiukweli afya yake ilikuwa dhoofu sana na most of his responsibilities nilikuwa nazicover mm.

Jumatatu mimi niliendelea na majukumu yangu kikubwa ilikuwa ni maandalizi ya wageni na siku hiyo ofisini nilikuwa peke baada ya dereva, boss na PS wake kusafiri yule Muhasibu naye alitengeneza excuses anazozijua yeye mwenyewe so hakuja. Jumanne mpaka mchana boss na PS wake hawajafika ofisini, nikasema jioni nikitoka nitamcall dereva nijue wamerudi au lah. Kupiga namba ya dereva haipatikani, nikajaribu tena na tena ikawa hola. Nikajaribu kumpigie PS nae hapatikani vivo hivo kwa boss, wote hawapatikani. Mpaka naingia ofsini Jumatano hakuna anayepatikana. Yule Mhasibu alikuwa hana interest nao kwakweli kwa hiyo mpaka mimi nilipomwambia hawapatikani wote siku ya pili leo ndio na yeye kuanza kuwatafuta. Ikawa hawapatikani.

Tukajiuliza wamekumbwa na masaibu gani, ila sasa kipindi kile kule Samunge kulikuwa na foleni kubwa sana na kama mankumbuka mafuriko yale ya foleni ilipelekea watu kukwama njiani hata wiki na hakukua na mawasiliano ya simu, ndio hata mawaziri wengi akiwemo waziri wa ujenzi kipindi kile (RIP Mwamba) walitumia chopa. Basi maboss zangu nao walikuwa trapped on the same situation. Wamekwama njiani foleni haiendi wala hairudi, simu hakuna mawasiliano na walikuwa sehemu ambayo hata huduma za msingi kama chakula, malazi na maji ilikuwa shida. Yule dada mhasibu hakujua kama wameenda Samunge na mimi sikutaka kumwambia kwani wenyewe hawakuaga hivyo.

Sasa mimi tension yangu ilikuwa kwa donors ambao wanakuja maana kwenye ile ofisi boss KJ alikuwa ndio kila kitu kwenye kutoa updates na mm nilikuta wale donors fund zao zimeoperate karibia miaka miwili na nusu so wamekuja kufanya kitu kinaitwa midterm project evaluation. Nikawaza nikasema hapa lazima nifanye kitu ili kuokoa jahazi na pengine inakuwa kuwa ndio best opportunity for me to show my problem solving skills in difficult and challenging sitauations.

Basi nikamuuliza mhasibu kama ana access ya email ya boss ili tuone kama kuna updates zozote kutoka kwa wale wageni. Maana hiyo ilikuwa ni Jumatano asubuhi na kesho asubuhi ndio watakuwepo ofsini, maana pia walitegemewa kupokelewa eapoti na gari la ofisi. Dada mhasibu akajibu hana access na email ya boss, huku na huku nikamwambia kwani yeye kama muhasibu si ameshawahi kuwasiliana na watu wafinance upande wa Donor hususani maswala ya financial repors au updates. Akajibu anakumbuka amewahi kuwasiliana nao so tukatafuta hiyo email tukaipata.

Ikabidi mimi niconstruct email ya kumuomba emails za watu wanaotoka Ulaya kuja Tanzania kwa ajili ya evaluation. Hiyo ilikuwa kama saa sita mchana. Bahati nzuri yule jamaa wa finance naye alikuwa ni sehemu ya wanokuja kufanya evaluation na muda huo walikuwa wameshawasii Tanzania maana waliingia alfajiri sana ya Jumatano hiyo hiyo na muda huo walikuwa wamehsafika hotelini kwa kukodi tax. Basi nikampa namba yangu ya simu kwenye email na baada ya muda akanipigia mdada mzungu ambaye ndie alikuwa team leader wao. Kiufupi walikuwa wanatuma emails kwa boss tangu Jumatatu na walikuwa hawapati response yoyote. Kuna vitu walivyokuwa wanavitaka na hasa logistics za hapa Tanzania watafika hotel, ofsini nk ila walipoona kimya wakajiongeza wakafanikiwa kufika hotel ila hawakujua kesho wanakuja vipi pale ofisini. Basi nikamuomba anifoadie hizo email corresponses ili niendelee kuzifanyia kazi.

Mimi ikabidi nijiongeze nikawaomba samahani kuubwa sana na kuwaongopea kwamba boss alipata msiba kijijini kwao na aliondoka weekend kwa matarajio kwamba angerudi Jumatatu. Nikawapa pale blabla za unajua vijiji vya Tanzania hakuna mawasiliano ya simu na ni mbali kwelikweli. Hivyo kwa dharura hiyo I will be taking a lead. Uzuri wakaelewa wao wanachotaka ni updates za kazi sio kumkuta nani ofsini. Tukaagana kwa makubaliano kwamba ratiba ina baki ile ile no mabadiliko.

Sasa tukaanza kuumiza kichwa na mhasibu pale, ubaya kwamba yule muhasibu alikuwa hajui chochote kuhusu implementation za project ile sijajua kwa nini wakati yeye ndio alikuwa anaahold program budget. Nilichomwambia ni kwamba anipe financial report ya ile program ambapo angalau nikaweza kujua kipi kimefanyika so far kwa maana activity gani pesa ilitoka. Lakini pia ikabidi niingie kwenye mafaili kuanza kutafuta reports mbali mbali nilifanikiwa kupata in details kipi kimefanyiak. Nikajisemea mbona hawa nitawamudu tu at zile key points ninazo. Kingine nikamwomba mhasibu ampigie mama mmoja hivi ambae alikuwa ni member wa bodi nilimfahamu kwa sababu alikuwa amewahi kuja pale ofsini kama mara mbili hivi na niliona boss alimpa kazi ya kweda kupresent kwenye mkuta kwa niaba yake, niliona huyu anaweza kutujoin na kuongeza nguvu. Alipopigiwa nilimpa situation yetu akasema atakuja na mzee mwingine memba wa bodi pia ambae nae ni wa siku nyingi na anaijua miradi ya pale. Mpaka hapo nikaona hii ngoma tunaenda kotoboa.

Kwa kule field ikabidi niwapange wale trainees wangu wa Kilindi na Handeni ili wajiandae maana nao kama beneficiaries wanakuwa na sehemu yao. Niliamua kuwapeleka Kilindi na Handeni kwa sababu nilishiriki ile activity na ingekuwa rahisi kwangu kutoa majibu ya kuridhisha. Sasa ngoma ikawa fedha maana tunatoaje fedha bila approval ya boss na yule mhasibu alikuwa strict sana kwenye hizo taratibu. Maana wale wageni ilipaswa kukodi noa ya kutupeleka na kuturudisha dar lkn pia logistics za hapa mjini kwa wageni. Ikabidi nimpigie yule mama member wa bodi ambaye pia alikuwa ni signatory akakubali fedha itolewe ya kufacilitate hilo maana hao ndio wanaoleta pesa sasa kushindwa kuwapeleka site italeta picha mbaya, kwanza boss hayupo si itaonekana tunawakwepa? Mwisho wa siku mzigo ukatolewa wa kutosha.

Basi Alhamisi yake wageni nikawatumia usafiri wakafatwa na kuletwa ofisini, nashukuru Mungu kikao nilikiongoza vizuri na kilienda vizuri sana. Wale board members walisaidia kutoa ufafanuzi to rescue the situation. Then kesho yake tukaondoka nikiwa kiongozi wa msafara, pamoja na member wa board mmoja, muhasibu pamoja na wageni wetu wanne kwenda field. Kiufupi wale wageni walifurahi sana. Over the weekend wakawa wamerudi zao kwao by Jumatatu wakanitumia report yao ambayo ilikuwa nzuri tu kwetu. Kiufupi walikuwa very impressive na implementation ya projects na feedback tuliyowapa. Na walijicommitt kuongeza funding ili kufukia fukia magape ambayo yalihitaji more funding dadeki. It was a big experience for me and I was very proud of myself kwa kuhandle ile situation. Tuliposoma ile report na yule mhasibu pale ofisini tulipiga kelele za furaha utafikiri machizi.

Ilipofika Jumatano usiku kwenye saa 4 usiku hivi nikiwa nipo pahala nafatilia boli chama langu the gunners mara naona simu ya bosi inaita kwa fujo. Nikasogea pembeni kupokea maana mimi huwa napenda kucheki boli sehemu zenye vibe sana, ile kupokea boss akawa anaiuliza maswali mfululizo yasiyo pangiliwa vizuri kutaja kujua kama wageni walija? Walisemaje? Wameondoka? Wapo wapi? Yaani anauliza maswali sijajibu hata moja yeye ameshauliza kumi. Nikamwambia boss calm down ukitulia nipigie nikueleze vizuri nikawa namsikia anahemea juu juu simu yake ikakatika.

Kidogo PS wake ananipigia ndo kuniambia kwamba wamefika sehemu ambayo angalau kuna network na bosi alipanda kwenye kilima kidogo ili kupata network nzuri. Akaniambia yaani boss amejuta kwenda kwa babu maana walinasa njiani kwa siku mbili katikati ya safari wakilala kwenye gari. Akanipa pale situation yakule ilivokuwa worse ila chazaidi boss kilichomchanganya ni hao wageni. Mara kidogo nikasikia sauti ya boss kwa mbali inamwambie muulize wageni walikua. Basi nikatoa mrejesho wote jinsi ilivokuwa na jinsi walivoturecommend kwenye ile report yao angalau boss mcheche ukamuisha kabisa. Boss akaniomba nimfoadie ile report maana hakuiona kwenye email yake, na mm nikakumbuka kwamba wale wazungu ile report walinitumia mimi tu hawakumcopy mtu mwingine – sijui ilikuwaje lakini haikua kesi.

Basi ijumaa yake asubuhi sana boss aliwahi sana ofsini ili kufanya kikao na sisi na ile pia nimpe full picture. Kiukweli alikuwa ameedhoofika gafla sana sasa sjui sababu ya shurba za njiani kwenda kule kwa babu au mambo mengine. Basi nikatakiwa nitoe mrejesho pale na kwa mara kwanza nikaona tabasamu la boss ofisini. Aliisoma ile report ya wazungu mara mbili mbili. Na hapo hapo akaniuliza kama mkataba wangu wa kazi nilishasaini nikamwaba bado. Akaniuliza kwa nini nikamwambia bado sikuuelewa kwahiyo nilikuwa nasubiri muda mwafaka wa mimi nayeye kujadili vipengere ambavyo sijavielewa. Basi akawaruhusu wengine watoke nje mimi nayeye tukabaki. Akanitaka nimweleze kingere ambacho sikukielewa. Nikamwambia mwanzo nilikuwa nataka anieleweshe majukumu yangu lkn nashkuru kwa sasa nimeyaelewa ila kipengere cha remuneration hakipo kwenye mkataba. Akaniambia alikiacha makusudi kwa sababu hakuwa na uhakika wa anilipe kiasi gani kwani yeye analipa kutokana na utendaji kazi wa mtu. Pale pale akaniambia kutokana na utendaji wako kwanza nakuandikia barua ya kumaliza probation period na nitakulipa nusu ya mshahara wangu. Nilikuwa siju boss analipwa sh ngapi nikajisemea cha muhimu ni angalau kufikisha 6 figures bhana kwenye cheque – hahaaa. Basi niakprintiwa mkataba mwingine pale nikaanguka signature bila kuwaza.

JUMP TO PG # 154

NB:
Wakuu bado nasisitiza naandika uzi huu ili kushea yale niliyopitia na kujifunza katika mlolongo wa mambo mengi kwenye harakati zangu za kuajiriwa sehemu mbali nikiamini yanaweza kuwa na faida kwa wengine.

So far sina ajira kwa muda wa mwaka sasa na mimi nipo kwenye kundi la wanaosaka ajira. Kama kuna mdau ana connection kulingana na uzoefu, skills na knowledge yangu tunaweza kuwasiliana maana huku mtaani sio poa. Kwa sasa inaweza kuwa mapema kujua skills na experience nilizo nazo tuendelee kuwa pamoja huko mbele kuna uzoefu mwingi zaidi. Mpaka sasa nimeshea uzoefu niliopata katika ajira yangu moja tu wakati zipo tatu zaidi nilizopanga kushea nanyi.
Wewe ni mpambanaji[emoji119]
Ndio ile tunaita punda afe mzigo ufike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EPISODE 6: The new Office

This is just an advice, when joining a new office it's important to avoid coming across as someone who knows too much. (u-much know unaweza kukucost)

Niliweza kujiunga na shirika jipya huku nikiwa nimejipanga kukabiliana na mazingira mapya yakazi, watu tofauti na wale niliowazoea lakini pia huku majukumu yaliongezeka kidogo na hata kasali kalikuwa na ahueni. Nilipokelewa pale kazini vizuri tu na kufanyiwa proper orientation. Utofauti ulikuwa mkubwa sana wakimazigira pamoja na structure ya uendeshaji wa ofisi kwani huku kwa sasa kulikuwa na idara nyingi nyingi ambazo zilikuwa na line managers ambapo mimi niliajiriwa pale idara ya ruzuku nikiwa ni mmoja wa maofisa usimamizi wa ruzuku (Program Officer – Grants). Nakumbuka kwenye ile nafasi tuliajiriwa wawili mimi pamoja na mwenzangu mmoja alikuwa kibonge hivi. Kwenye hii stori nitamwita Big.

Wiki ya tatu tu wakati nikiwa nimeanza kuzoea zoea kidogo mazingira nilipata very shocking news, that Dr KJ my former boss passed away. Nakumbuka nilikuwa nipo kwenye mkutano wakawaida wa wafanyakazi wa idara yetu nilipoona simu ya PS nikajua huyu labda kwa ni ijumaa hii basi ananitafuta labda twende kwenye mtoko maana aliniambia angenitafuta. Nikampotezea kwanza ili nimalize meeting. Kidogo nikana simu ya yule dereva na muhasibu wananipigia nikaona hii mbona kama haijawa sawa. Ikabidi nitoke nikapokee ya dereva ndio kuniambia Dr KJ is no more. Aisee nilipawtwa na mshtuko sana. Nikaconfirm kwa kumpigia mhasibu na PS. PS ndio akawa hajiwezi kabisa yaani anaongea huku analia tuu. Kwakweli ule zile habari ziliniumiza sana sikuweza tena kuendelea na kikao. Ikabidi niombe ruhusa pale niende msibani muda ule ule.

Kiufupi yale maradhi yaliyokuwa yanamsumbua KJ ndiyo yaliyopelekea kifo chake. Basi tukaorganize pale pamoja na wafanyakazi wengine tukaenda wote msibani. Kwahiyo ile weekend yote nilihudhuria msibar wa Dr KJ mpaka tulipomaliza kuzika. Wakati wa kuaga hakika nilitoa chozi la uchungu sana japo kisirisiri maana nilikumbuka mengi sana na mchango wake mkubwa katika kuniingixa kwenye ulimwengu wa ajira rasmi na decent. Japokuwa alikuwa na madhaifu yake lkn mchango wake kwangu ulikuwa mkubwa sana, Mr KJ aliniheshimisha sana mjini kwani maisha yalishanipiga sana ni yeye ndio aliyenipa ramani. Nakumbuka kuna kipindi baadhi ya madogo waliokuwa nyuma yangu kule chuoni ambaye pia alikuwa anawafundisha walinipigia simu za kunipongeza. Mwamba kama ilivyo kawaida ya masifa yake nasikia alikuwa anawaonyesha picha tuliyopiga ya wafanyakazi ya ofisi na kuwauliza darasani kama wananijua. Nasikia alikuwa ananifagilia kinoma noma kwamba amepata jembe ofisini kwake na alikuwa anafikiria hata kuniachia ofisi. Sema tu sifa zake ziliniletea matatizo kwa madogo maana aliwaambia mshahara anaolipa ni mkubwa sana (yeye aliwatajia mara nne ya kiasi alichokuwa ananilipa hahaha) kitu ambacho kilisababisha wale madogo wawe wananipiga sana mizinga. Kiufupi tu mwamba namkumbuka hadi kesho na kuna vitu ninavyo hadi leo kama kumbukumbu yake kwangu. RIP Dr, daima utaendelea kuwa mtu muhimu sana kwangu.

Anyway ya maamuzi ya Mungu hatupaswi kulalamikia sana tuendelee na stori yetu. Basi baada ya mazishi niliendelea na kazi kama kawaida. Sasa hii ofisi ilikuwa na watu sana ukilinganisha na kule nilipotoka. Mfano sisi kwenye department yetu pekee tulikuwa kama 16 hivi, hapo ongezea na wa idara nyingine. Kama nilivosema tuliingia mimi na Big tukiwa ndio newcomers –pale. Kwa kile kkipindi cha wiki mbili tu za mwanzo mwenzangu Big alikuwa ameshazoeana na watu wa karibia ofisi nzima na kwa muda mfupi akaanza mpaka kushirikishwa kwenye madili ya ofisi.

Unaju ile ofisi pamoja na shughuli nyingine ilikuwa pia inadili na mambo ya kugawa ruzuku kwa NGOs nyingine ili wakatekeleze miradi mbalimbali sasa kwa wazoefu wa pale kuna vimichezo walikuwa wanaicheza wanapiga piga vijisenti kwa njia za panya wanazozijua wao. Hii ilikuwa ni seriously unacceptable behavior na ukibainika unapiga hizo ilikuwa kwamba you are terminated on the spot. Na nakumbuka CEO wa lile shirika alikuwa hana msalie mtume katika hizo ishu. Kuna stori niliikuta pale kwamba CEO aliwahi kutimua department nzima ya grants kisa upigaji, akaanza kuajiri upya.hii idara ya grants ndio ambayo inahusika moja kwa moja na kureview proposals, ku-recoomen nani apate nani akose kulingana na vigezo na kusimamia miradi pale ofisini pamoja na kwenda field kuwakagua. Ilikuwa ni department ambayo imekaa kimtego mtego na kiushawishi sana na ilikuwa ukimaliza contarct yako ya miaka mine basi utapongezwa kwa kupewa zawadi ya pesa za kutosha before hujarenew mkataba. Yaani mimi tangu nilipofika pale before hata sijamaliza probation ya miezi mitatu nilishuhudia watu wanne wakitimuliwa. Balaa unaambiwa CEO alikuwa na informers wake nchi nzima utafikiri CIA ya Marekani.

Basi bhana turudi sasa kwa bwana Big. Big bhana nimeingia naye pale wiki moja tu keshazoeleka kwenye idara (halafu ile idara yetu wanaume tulikuwa watatu tu wengine wote wanawake). Wiki ya tatu ofisi nzima Bigii Bigii - Bigi Big Kweli. Big mtu wa mastory, Big mtu wa totoz, Big hana baya na mtu. Mda mfupi kila mtu pale ofisini anajua Big anashabikia utopolo kwa hapa bongo kwa nje anaipenda Liva. Mda mfupi tu k=watu wote tunajua big anapenda kwenda viwanja flani vya kujirusha weekend. Yaani ndani yam da fupi hata mwezi bado watu wote tunajua mambo mengi ya Big ya nje ya kazi, yaani mambo yake binafsi.

Iyo haikuwa kesi maana hizo ni character za mtu kiukweli hata mimi nilikuwa nainjoy kampani yake. Maana sometime Big alikuwa lesi hata kwenye kudai haki zake msingi. Mfano kuna siku sina hili wala lile nipo zangu napambana na majukumu yangu nashangaa naitwa kwa Meneja utawala. Kufika ofsini namkuta Big naye yupo. Mara yule meneja akaniuliza na wewe unataka mkopo? Ile ofisi walikuwa na utaratibu unaweza kukopa advance salali mpaka ya miezi 7 kwa hiyo utakuwa unakatwa kiasi cha pesa kulingana na muda wa mkataba mtakavyokubalina. Mimi nikashangaa, mkopo tena imekuwaje mbona mimi sijataka huo mkopo. Ndio yule meneja kunipa taarifa kwamba Bwana Big amejaza fomu za advance salary na kutaka mkopo wa miezi saba. Akaendelea kusema kwamba alipomwelekeza kwamba ni amalize probation bwana Big akawa anaforce kama vipi tupewe maana hata mimi nina shida na hela so nimemtanguliza yeye akajaribu.

Nikaona duu hii sasa soo. Kwa hiyo meneja ndio ananiuliza kama na mimi nataka au laa. Nikafikiri hapa Big ashaniingiza kwenye mambo yake bila ridhaa yangu lakini pia nikimtosa mooja kwa moja inaweza ikamjengea picha mbaya Big kwa yule meneja. Basi nikasema tuu ni kweli tulidiscuss pamoja na Big maana ni kipengere ambacho kipo kwenye mkataba na nilikubaliana na Big tukipata muda tufatilia so mimi bado sikupata muda muda wa kufatilia, ila kwa maelekezo hayo basi inabidi tusubiri. Yaani nilitoa sababu ya kijinga mpaka yule meneja kuna siku aliniambia kwa utani tulipozoeana kwamba siku zile alicheka sana kwani alijua fika Big kanichomekea. Kwenye hilo niliipenda ile spirit ya Big ya kuzitumia fursa vyenye vyedi.

Ila sasa bwana Big kuna mambo alikuwa anayaendea pupa sana mpaka kuna washkaji wengine pale ofsini wenye mapenzi mema walimtonya apunguze spidi ila akawa mjuaji. Sasa unajua sehemu yoyote ile kwenye michongo michongo watu wanakuwa makini hususani kwa newcomers kujaribu kuwasoma kama mnasomeka ama vipi. Basi zali la kusomeka likamdondokea bwana Big. Wataalamu wa zile kazi wakaona Big hana noma hata akielekezwa mchongo anasomeka. Mimi nikawa sisomeki yaani watu kama hawanielewi elewi hivi. Sijui niite ubaya au uzuri mimi nilijipa muda kwanza wa kuwasoma watu kabla watu hawajanisoma. Kwa hiyo mara nyingi nilikuwa msikilzaji sana na muongeaji kidogo hususani kwenye maswala ya kazi. Sikutaka kuanza kujichanganya kutoka weekend na washkaji wa pale ofisini kwa sababu zangu maalum.

Big alikuwa lesi sana unaambiwa kala hata probation haijaisha big ameshavuta usafiri.Nakumbuka mimi alinishirikisha ile plan yake ya kununua mkoko ila nikamwambia ndugu sikilizia kwanza ujue hapa hata ulikuwa na umedunduliza vijisenti vyako huko itakuwa ngumu watu kuelewa watakuweka kwenye kundi la wapigaji. Big akaniambia yeye anajua anachofanya. Nikamwambia hii italeta shida si unakumbuka ile ishu ya kulazimisha mkpo kule kwa meneja utawala anaweza akajiuliza pesa umepata wapi wakati mkopo hakuidhinisha. Big akaniambia nisijali kuhusu hizo mambo yeye amejipanga. Bai akavuta ile ndinga ilikuwa ni moja ya nding zinazokula sana wese ila ndio ilikuwa habari ya mjini kwa majanki wa enzi zile.

Big hana baya ile ndinga ilivotoka tu bandarini siku hiyo hiyo alikuja nayo ofsini na kila mtu huko parking alioneshwa. Mjengo mzima ukajua leo there is a new father car in town. Nyie si mmezo father house, sasa kuna father car ndio sisi tunaosema kujenga sijengi maana sijawahi kulala nje ila nimetembea sana kwa miguu na kuloana wacha ninunue gari. Kuna jamaa mmoja nae alikuwa ni mmoja wa washkaji wa Big ila yeye alikuwa pale mda mrefu akawa anampa madini sana Big namna ya kuyaendea mambo ofsini, ila Big akataka hadi kuvunja urafiki kwa kuona kuwa jamaa ameanza kumwangia.

Basi maisha yakaendelea pale job kama kawaida. Nakumbuka tulikuwa tumebakiza kama wiki mbili hivi kumaliza probation mimi na Big tulienda kwenye training Nairobi ya wiki tatu ili tukitoka uko tuwe tumekwiva kwa ajili kupiga mzigo kama full employees. Sasa tukiwa kule kwenye training Big akatumiwa email na line meneja wetu inatakiwa arudi ofisini mara moja. Akaniuliza kama na mimi nimetumiwa nikamwabia sijatumiwa. Sasa tukawa hatuelewi pale ni nini kinaendelea. Akili yangu mimi ikawaza labda ni matatizo ya kifamilia labda msiba unaomuhusu sana so wanaoshindwa kumwambia. Hii ikaingia hata kwenye akili ya big huenda kweli kuna tatizo la kifamilia. Akawacheki ndg zake hakuna taarifa yoyote. Siku ya pili asubuhi akapigiwa simu kutoka ofisini kwamba inabidi arudi faster. Tukachanganyikiwa sana pale, basi ikabidi jamaa abadili ticket apande mwewe arudi dar ofsini akisisitizwa akishuka eapoti hasiende hata nyumba aunganishe job.

Kufika ofsini bhana amefikia kwenye kikao chamenejiment. Kiufuoi jamaa yangu Big aliingia kwenye harakati za panya pale ofsini kwa speed sana. Alisomewa mashtaka yake na ushahidi wa kutosha kuhusu harakati za panya mpaka simu zilizorekodiwa na wadau wakipanga mambo yao. Jamaa yangu wakampiga on the sport na kuambiwa kama anahisi ameonewa anaweza kwenda mahamani ila kwa kumuhurumia mambo yasiwe na kuepukwa kufungwa achukue vyake asepe. Huo ndio ukawa mwisho wa mshkaji wangu sana Big.

Anyway weekend hii wakubwa wangu tunafanyeje? Mana kutwa nasikiliza vipindi vya redio tuu home mpaka masikio yataka kutoboka. Na watangazaji wanakera sana maana kutwa kututangazi tu kwamba huu ni mwezi wa matumizi na sherehe kwahiyo watu watumie pesa. Nyie wenzangu mnatumia wapi pesa zetu, basi mtu mmoja ajitokeze anipe mwaliko wa kushangilia pamoja Mnyama akimuua wydad kwake.​

Episode 7 #254
Akaniuliza kama na mimi nimetumiwa nikamwabia sijatumiwa. Sasa tukawa hatuelewi pale ni nini kinaendelea. Akili yangu mimi ikawaza labda ni matatizo ya kifamilia labda msiba unaomuhusu sana so wanaoshindwa kumwambia. Hii ikaingia hata kwenye akili ya big huenda kweli kuna tatizo la kifamilia. Akawacheki ndg zake hakuna taarifa yoyote.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Dah
Hii episode ina mixture ya hisia.

RIP Dr KJ
Nimejikuta naumia sana[emoji3064].
Vipi kuhusu maisha ya ofisi baada ya Boss kufariki?
Ps,Accountant,ofisi iliendelea vizuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EPISODE 9: Umeshawahi wahi kufanya kazi ambayo mda wote unakuwa bize kazini? Work-life balance is a must if don’t wish to go insane.
Baada ya kumaliza ile tripu ya Tabora na Kigoma salama at least nilikuwa nimeboresha uzoefu wa kazi za field kwenye hii ofisi mpya. Kumbuka kwamba nilibaki peke yangu baada ya kukubaliana na dadaB arudi home ila kutokana na kumsoma kwa mda mfupi na kuunganisha na uzoefu wangu wa kule kwa Dr KJ kazi ikawa rahisi sana kwangu. Hapo ndipo nikajua kwa nini waajiri wengi sikuhizi they prefer job experience than grade A academic certificates.

Nikarudi ofisini salama na kwa kushirikiana na dadaB tukasubb report pale na maisha mengine yakaendelea. Baada ya muda na mimi nikawa ni among senior officers pale hata nikawa trusted kuwa-mentor the new employees maswala ya kazi. Anyway it was good experience kwa kweli na niliinjoi sana kazi yangu.

Uzuri wa ile kazi ilikuwa ni kusafiri kitu ambacho nilikuja kugundua kumbe mimi napenda sana kusafiri tena hususani safari za mikoa ya mbali na vijijini nilikuwa napenda sana. Unajua kwenye kusafiri sio tu kuenjoy zile moments za kuwa kwenye gari au flight lakini inasaidia kuexplore new opportunitis na kuongexza network yako na watu tofauti tofauti unaokutana nao. Sasa pale ofisini ilikuwa ukikaa sana hujasafiri basi ni mwezi na nusu au miwili. Lakini kikawaida ilikuwa kila mwezi lazima mtu usafiri walau kwa si chini ya wiki, yaani safari ilikuwa ni lazima kulingana na nature ya kazi hususani kwenye idara yetu. Mimi ilifikia wakati mpaka nikawa nawatania watu kwamba sitakuja kuoa au kuruhusu mke wangu afanye kazi pale ofsini maana ndoa inaweza ikayumba hahaahaa sababu watu kila mara wapo safarini na hivyo mke anaweza kushindwa kutimiza majukumu ya nyumbani vizuri (jokes) with that job nilisafiri kila wilaya unayoijua wewe hapa Tanzania zilikzokuwepo kipindi kile. Utanitajia wapi nisipajue mimi.

Ofisi ilikuwa inakufacilitate kila kitu ukiwa safarini ili uweze kuendelea na majukumu yako ya kazi hata ukiwa nje ya ofisi. Mfano vitendea kazi bora kabisa laptops, vimodem kwa ajili ya internet vyenye unlimited bando nk. Kwanza ilikuwa ni marufuku staff kupanda mabasi haya abiria is either usafiri kwa gari ya ofisi sehemu ambako hakuna viwanja vya ndege au ukodi gari hata ktoka dar mpaka ifakara endapo usafiri wa ndege haupo na magari ya ofisi yapo na shughuli nyingine. Na ilikuwa lazima ulale sehemu yenye hadhi ya juu kulingana na eneo ulilopo ili kuwezesha usalama wako na pia mazingira rafiki ya kuendelea kupiga mzigo. Kifupi ilikuwa ukisafiri unasafiri na dawati lako maana kwa necha ya kazi ilikuwa huwezi kumuachia mtu akushikie shughuli zako maana utamuonea tuu, labda kama mtu ni mgonjwa, amefiwa au likizo za uzazi ilikuwa inaeleweka ila sio safari. Ukisafiri utawezeshwa kila kitu kusafiri na majukumu yako, hakuna kumuachia mtu ofsini.

Kwahiyo life pale ofsini ilikuwa ni mshike mshike, bize mda wote. Mtu kwenda weekend job au kuchelewa kutoka mpka saa tatu usiku ilikuwa ni kawaida sana. Yaani ilikuwa ukiangalia vimeo ulivyonavyo kwenye meza yako unajikuta tuu wenyewe kwa hiari yako jumamosi au jumapili unaingia job walau kwa masaa manne ukapunguze vimeo. Au mara kwa mara unatoka ofsini saa mbili au tatu usiku.

Mfano mimi kwenye portifolio yangu nikajikuta nina kama zaidi ya NGOs 700 ya kuzisimamia. Yaani hapo uhakikishe wameleta report zao za fedha na miradi, report zimekaa sawa, uindize report kwenye system tena kwa kuzitranlate kwa kingereza, kuhakikisha umewatumia fedha za quarter nyingine baada ya kujiridhisha na report ya fedha. Kisha uhakikishe uhakikishe hizo NGOs umezitembelea ili kwenda kuzikagua huko field kama wanatekeleza miradi sawa sawa au wapo wrong ili uwaelekeze. Wakati huo huo uhakikishe unatrain waliokosa funding ili nao wapate fedha maana ofisi ile ilikuwa na wafadhili wengi waliokuwa wanaweka fedha zao ili ziende kwa wadau huko mikoani, kwahiyo mnajikuta mna fedha lakini wanaopata ni wachache so in order to maintain reputation ya ofisi kwa donors ilikuwa ni lazima kwenda huko na huko mikoani kuwafundisha watu jinsi ya kuomba na kupata ruzuku kutoka kwetu kulingana na vigezo vetu ndio mana tukawa tunapokea hata proposal za Kiswahili ilimradi kutombagua mtu.

Sasa kwenye mazingira kama hayo unafanyaje? Watu tulikuwa bize muda wote ukiangalia kazi ni nyingi mpaka unatamani siku ingekuwa na masaa 30 walau unaweza kupata muda mzuri wa kupumzika. Kiukweli kuna watu ambaop hawakuwa na shida sana na kazi waliacha asee. Pia ukiachana na sababu za integrity kuachishwa kazi kama mshikaji wangu Big lakini wengi pia walitimuliwa sababu ya performance issue, hawakuweza kwenda speed ya ofisi. Na katika vitu ambavyo menejiment ilikuwa haiwezi kukuvumilia ni malalamiko kutoka kwa grantees kwamba umewaomba rushwa au umewacheleweshea fedha zao, hapo ulikuwa hueleweki. Kwahiyo unachotakiwa kufanya grantee akileta report yake leo baada ya wiki uwe umeshaireview na kuprocess fedha zake. Hata system ilikuwa inakukumbusha kwamba report ipo due hivyo unatakiwa kuishughulikia. Sasa mtu unasimamia miradi zaidi ya 500 what do you expect. Usipokuwa smart and organized unakuwa chizi. Work-life balance ni kama haikuwepo pale ofsini.

Nakumbuka kuna new employee ndio alikuwa ameajiriwa ana kama mwezi tuu akapiga chini kazi bila kupata kazi nyingine. Yule jamaa alivoajiriwa pale alikuwa amebakiza kama mwezi hivi afunge ndoa. Basi ameingia pale ofsini amekutana na mshike mshike wa kaxi na hakuna ugeni, kwani ugeni ulikuwa mwisho wiki ya kwanza. Sasa yule bwana harusi inaonekana maswala ya kushughulikia maandalizi ya harusi yake alikuwa anayasimamia yeye mwenyewe kwa kiasi kikubawa sijui hata kama alikuwa na kamati yule bwana maana simu yake ilikuwa bize sana na kila kitu anaulizwa yeye. Basi pale mjengoni tukamchangia kama kawaida tena mzigi wa kutosha tuu na kutokana na maandalizi yake akaruhusiwa awe anafanya kazi nusu siku.

Lakini tulikuwa tunabaki na bwana harusi mpaka usiku maana naona alikuwa akiangalia haoni pa kutokea lazima abaki ofsini kupunguza majukumu. Sasa sisi tulikuwa tunafanya kazi kwenye pool ambapo wote mnaonana na kusikilizana. Sasa kuna siku kazi zimepamba moto, basi simu ya bwana harusi ikawa inaita sana akawa hapokei. Mdada mmoja akamwambia bwana harusi pokea simu inaita basi akapokea nadhani sijui kuchanganyikiwa au vipi akaamkia “shikamoo”, sijui akajibiwa nini tukamsikia anasema “mdau nimekwambia atakuja mtu huko huko kuwatembelea wiki ijayo atawasaidia”. Sijui akajibiwa nini akamwambia yule mpigaji simu “ongea na huyu mwenzangu atakuasaidia” akawa amempa yule dada aliyemwambia apokee simu ili aongee na simu yake.

Yule dada akachukua simu akijua anaongea na grantee ii amsaidie bwana harusi kutatua changamoto yake akamuuliza mpigaji una shida gani nikusaidie? Akajibiwa mimi ni mchumba wake na ni mke mtarajiwa wa huyo mwenye simu lakini naona ananiambia vitu ambavyo ambavyo sivielewi, je yuko sawa kwani maana kuna vitu nataka kumwambia kuhusu gauni la harusi. Ndio yule dada kumwambia bwana harusi wewe anayepiga simu ni mkeo sio grantee hebu toka nje ukaongee naye. Aisee ofisi nzima tulibusrst kwa kucheka. Yaani bwana harusi alivurugwa na kazi mpaka akawa amesahau sauti ya mkewe mtarajiwa. Lakini pia inaonekana sijui alivurugwa kiasi gani mpaka akawa anaongelea maswala ya kazi wakati bi harusi anaongelea maswala ya gauni. Ikabidi atoke nje akaongee na mkewe badae akarudi.

Basi harusi ikapita lakini baada ya wiki kama tatu hivi bwana harusi akaandika barua ya kuacha kazi. Sasa HR hakutaka kuiprocess moja kwa moja akawa anamtaka kwanza afikirie mara mbili mbili uamuzi wake labda kama ni ishu ya maslahi na amepata sehemu nzuri zaidi. Basi HR akatufata watu ambao aliona kidogo tupo karibu na bwana harusi ili tuongee naye. Bwana harusi wala hakuficha akatuchana live japo hajapata kazi sehemu nyingine ila mazingira ya kazi pale yamemshinda maana yalikuwa ni busy mno with less work-life balance. Tuakajaribu kumsihi pale avumilie atazoea tuu akagoma kabisa. Jamaa etu mmoja akasema jamani tumuacheni huyu ni mtu mzima anajua analolifanya. Mimi nikaongezea nikasema tena huyu muhehe wa Iringa huko tusije tumalazimisha akajinyongea ofsini halafu ikawa balaa jingine. Basi bwana harusi akaresign kama alivyopanga, mhehe yule ni kweli alikuwa hana kazi maana baada ya hapo vilianzan vizinga kwa sana na tuu vile mkewe alikuwa karibu anajifungua basi alikuwa na uhitaji sana wa pesa. Kwa sisi washkaji zake tulimbusti tulivyoweza lakini nilijifunza kuna watu wana maamuzi magumu na misimamo asee. Unaachaje kazi huna kazi?

Nakumbuka tulimfikishia HR sababu za kwanini yule bwana harusi ameacha kazi na uzuri au ubaya kwenye taarifa za ofisi ya HR waligundua wengi tuu walionekana hawakuwa na performace nzuri kwa sababu hawakuwa na muda wa kutosha wa kuopumzika. So ikawekwa mikakati pale ili kuboresha work-life balance kwa wafanyakazi. Hata menejiment walikuwa wanajua kwamba work-life balance was essential for promoting employee well-being, maintaining job satisfaction, preventing burnout, and creating a positive and productive work environment. Ignoring work-life balance can have adverse effects on individuals and organizations alike, impacting health, relationships, and overall job performance.

Mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuongeza wafanyakazi, kwa hiyo ikatafutwa ofisi nyingine yenye uwezxo wa kuaccommodate wafanyakazi wengi zaidi lakini pia likizo ilikuwa ni lazima. Maana before hapo likizo ilikuwa ni optional kwamba mtu unaweza ukalipwa pesa ule mda wa likizo ili uendelee kupiga mzigo, na kwa jinsi kazi zilivokuwa nyingi mtu aliona bora auze baadi ya siku za likizo ili apunguze kazi huku akipokea mshiko. Hii hata mimi nikifanya sana. Basi maisha baada ya hapo yaliendelea kama kawaida na kiukweli work load ilikuwa imepungua sana na tulifanya kazi kwa utulivu na ufanisi mkubwa.

Wadau wangu nilifanya kazi pale kwa miaka mi4 before I shifted to another organization. Based on my job responsibilities as a Program Officer - grants, I have developed a diverse set of skills as followas
  1. Grant Management: Demonstrated ability to review, assess, and select grant applications in accordance with established procedures and regulations.​
  2. Communication Skills: Regularly communicated with grant applicants regarding the status of their applications, ensuring accurate and timely information.​
  3. Training and Facilitation: Organized and facilitated training sessions on project and financial management for CSOs/NGOs/partners nationwide.​
  4. Supervision and Leadership: Successfully supervised over 100 grantees annually in various sectors, including governance, youth, human rights, gender & women empowerment, health and disability.​
  5. Capacity Development: Designed and conducted capacity development sessions for grantees, covering project management, financial management, project monitoring and evaluation, and project report writing.​
  6. Partnership Management: Worked closely with local partners to identify and address capacity gaps in project grants management.​
  7. Monitoring and Evaluation: Conducted field visits to assess and monitor project implementation performance and collect success stories from partners.​
  8. Flexibility and Adaptability: Ensured flexibility and high quality of capacity development support provided to partners.​
  9. Report Writing: Prepared periodic reports for management purposes and other stakeholders.​
  10. Stakeholder Engagement: Collaborated with various stakeholders, including CSOs, CBOs, FBOs, and NGOs, throughout the grant management process.​
  11. Project Implementation Oversight: Monitored and assessed project implementation to ensure alignment with goals and objectives.​
  12. Time Management: Successfully handled multiple responsibilities and tasks within deadlines.​
  13. Analytical Skills: Evaluated grant applications, monitored project performance, and prepared reports, demonstrating strong analytical abilities.​
Nipeni connection wadau

Tukutane next episode
Hakika umejaa madini na potentially kubwa kwenye hiyo sector
 
EPISODE 8: Nilikuja kuelewa kwamba uki-mess up kwenye mawasiliano umeharibu kila kitu.

That is to say kwa shughuli ambazo nilikuwa nazifanya pale ofisini, effective communication was crucial in such projects because it helped me to build and maintain positive relationships, ensures transparency, and fosters collaboration among diverse stakeholders. Chukua hiyoutajishuluru badae kama ulikuwa unapuuzia.

Nitawapeni kisa kidogo kilichowahi kunitokea au kukishuhudia pale ofsini. Ulifika muda ambao sasa staff tulitakiwa kwenda field mikoani kufanya shughuli mbalimbali kadiri ya majukumu ya idara. Kama nilivogusia kule juu kwama kwa kuwa idara yetu ilikuwa inadili moja kwa moja na usimamizi wa ruzuku kwa viNGO vingine karibia Tz yote basi moja ya kazi zangu ilikuwa ni kwenda huko mikoani kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali. Mfano kwa wale waliopata ruzuku na wanaoendelea kutekeleza miradi niliwajibika kwenda kuangalia au kufatilia jinsi wanavyotekeleza shughuli zao, matumizi ya fedha, kukusanya success stories na mafanikio lkn kikubwa ni kutatua kwa pamoja changamoto zinazowakabili. Lakini pia kwa kuwa wengi walikuwa wanakosa ruzuku kutokana na kushindwa kumeet vigezo basi niliwajibika kuwakusanya kwenye mikoa yao na kuwafanyia training kama kama ya siku nikikaa nao na kuwapitisha katika namna bora ya kuandika projects zenye mashiko na namna ya kujaza fomu za ruzuku. Kiukweli ni kazi ambayo ilinipa exposure ya kusafiri Tanzania nzima mpaka huko vijijini mno. Pia ilinipa exposure ya kujua kumbe nchi hii ina watu masikini sana, chamuhimu ni utembee uone.

Nakumbuka field yangu ya kwanza nilikuwa na dada mmoja ambaye yeye alikuwa ana uzoefu wa kutosha tuu pale ofsini, hivyo utaratibu ulikuwa kama wewe ni mgeni basi trip tatu za mwanzo unaambata na mzoefu ili ukajifunze kwa vitembo badae ukikaa sawa ndio unaweza kuanza kwenda mwenyewe. Baada ya maandalizi pale ofsini na huko field safari ikaanza. Nakumbuka tulipangiwa mikoa miwili, Tabora na Kigoma na ilibidi huko kuzipitia wilaya karibu zote na tulikuwa tuna muda wa wiki 4, yaani ilikuwa mtu ukipotea unapotea kwelikweli kulingana na ukubwa wa mikoa unayopangiwa. Basi tukakwea mwewe pale mpaka Tabora maana tulipanga yuanzie kazi hapo. Pale Tabora tukafanya kazi kwa muda wiki mbili then tukaenda kumalizi mkoa wa Kigoma. Kigoma pale kulikuwa na wadau wengi sana kufanya nao hivyo ilitulazimu kukaa wiki tatu.

Kwakuwa mimi ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza basi yule dada (tumwite dada B) alikuwa anatake lead ili mimi nijifunze. KKwahiyo kama kwenye trainings alikuwa anatake lead yeye au kama ni kwenye kutembelea ofisi kwa ajili ya ukaguzi nako alikuwa anatake lead. Ile kazi haikuwa ngumu sana mimi kuimasta kwa sababu kama kufacilitate trainings nilifanya sana kule Dr KJ kama mnakumbuka. Sana sana kidogo nilichelewa kumaster zile procedure za kuhandle ukaguzi kwa wadau tuliowapa ruzuku lakini baada ya kuambatana na dada B wiki moja tuu ikawa tayari ninaweza, ofcourse kujiongeza pia ni muhimu.

Ile kazi ilikuwa inaushawishi na mitego sana. Maana mnaweza kwenda kufanya ukaguzi mahali yaani mnanyeyekewa kama miungu watu. Kuwa donor kuna raha na karaha zake sometimes. Raha ni pale ambapo mnapokelewa huku watu wakionyesha kuwajali, wengine mnavyowapa taarifa mnaenda basi utakuta wamewalipia mpaka lodge au hotel za kulala. Lakini wengine unaweza ukakuta hawajiamini kwenye utekelezaji miradi na matumizi ya fedha basi wanatengezeza mazingira ya kupeana vibahasha njenje. Hatari ambayo ilikuwepo ni kwamba huwezi jua zipi ni fedha za moto na zipi sio za moto lkn kwakuwa tulikuwa tunaishi kufata misingi ya kazi basi haikuwa tatizo sana. Sometimes kwa sisi vijana unatengenezewa mpaka mazingira ya kupewa vitoto vizuri vya kike ilimradi ughafirike mambo ya wadau yaende. Hii ilikuwa mimi mwenyewe bila kusimuliwa ilikuwa Urambo huko, lakini hii sio stori kwa leo. Ila wengi sana kwa nilivoshuhudia na nilivosikia story walinaswa kwenye mtego huu. Hapo juu niliwa BOSS KUBWA la ofici alikuwa na networks zake kama CIA/FBI kwenye kuwadaka staff wanaotaka rushwa.

Basi Tabora tukamaliza vizuri tu tukavamia mkoa wa Kigoma. Tulipomaliza kufanya nkazi Kigoma mjini pale tukaanza wilayani. Tukasema tukaanzie kibondo kwanza. Ili kwenda Kibondo na Kasulu ilibidi tukodi na escort ya polisi maana kipindi hicho kulikuwa na ujambazi sana wa kuteka magari porini huko. Nasikikia wale jamaa walikuwa waasi wa Burundi huko so waliikuwa wanafanya sana uhalifu upande wa Tz kwa kuiba mifugo, kuteka mabasi nk. Nasikia walikuwa wakilianzisha mbungi wanakuja kama wapo vitani mpaka jeshi la JW ikabidi liweke escort zone kwenye yale maeneo yenye hatari. Bahati nzuri tukafika Kibondo bila shida. Basi tukakutana na wenyeji wetu pale ili kucheki kama maandalizi ya shughuli ya kesho yamekaa sawa.

Pale Kibondo tulikuwa na training ya siku tatu kwa ajili ya viNGO vilivyokosa ruzuku so tulipanga tuwasaidie ili waweze kupata ruzuku. Basi asubuhi tumefika pale kama kawaida sasa kwa kuwa mimi nilishakwiva ile session nikawa mimi ndio natrain. Sasa unajua hizi session wale wadau walikuwa wanazipendaga sana maana walikuwa wanakula pale breakfast and lunch nzito na wanapewa pesa ndefu kwa siku za kujikimu na nauli kwa wanaotoka mbali kwa hiyo kiasi cha chini mtu alikuwa anapata kati ya elfu 25 mpaka 50 kwa siku times 4 days. Kwa vijijini kule ilikuwa ni pesa ndefu sana miaka hiyo hivyo kuhudhuria zile trainings ilikuwa ni dili kwao na wazamiaji hawakukosekana. Kwahiyo ni kawaida sana kuanza kuchelewa kuanza session kwa ajili kwnza ya kuchuja wazamiaji.

Sasa bhana kwenye lile swala la kuhandle wazamiaji dada B alikuwa anakereka sana yaani alikuwa analose temper yake haraka. Mimi hilo nililinote mapema sana kama ndio udhaifu wake. Yaani yeye kukishakuwa na mzamiaji hana simile wala lugha ya stara, yaani ile “tokaa kwenye kipindi changu” zilikuwa ni lugha za kawaida akiwabalasa wadau wetu. Duu mimi nikawa naona haipo sawa so mara nyingi nikawa namtuliza na kujaribu kuintervene. Sasa bhana wakati tukiwa tunajiandaa na session pale Kibondo mjini (mji una vumbi ule balaa hahaa) ile asubuhi uzamiaji ukawa kama kawaida. Dada B kama kawaida alipaniki sana.

Sasa wazamiaji wa Kibondo pale siku iyo walikuwa ni wengi sana karibu nusu nzima ya darasa walizamia. Mchujo ulikuwa mkali sana. Sasa dada B akalivalia njuga lile swala kwa hasira sana. Ukaanza mchujo wa nguvu pale tulijikuta mpaka muda wa session bado watu hawataki kutoka. Watu wabishi wale sikuwahi kuona b4 khaa. Mimi nikamshauri dadaB wacha tuendelee na training lkn hao waliozamia tusiwalipe na kama tusipowalipa keshi na keshokutwa hawatafika, bidada akanigomea akasema wacha apambane nao mpaka kitaeleweka. Senior kasema hivyo mimi junior ntasemaje? Kiukweli alifanikiwa kupambana nao isipokuwa kulibaki wazee watatu. Wale wazee wala hawakuwa waongeaji sana wao walikuwa tu wanamsikiliza kisha wanamjibu tuu mama sisi hatutoki tutahudhuria.

Dada B alikwazika sana na zile kauli zao akawa anawafokea sana wale wazee kama watoto. Badae wale wazee wakakonyezana wakaondoka kisha wakasimama wote watatu kwa pamoja wakaondoka bila kuaga. Mh, mimi ile situation nikaona haipo sawa nikamwambia dadaB naona kama wale wazee wameondoka na kinyongo nikajibiwa achana nao waache waende zao mimi najiamini na nasimamia kanuni za kazi yangu na sitishiki maana nalindwa na damu ya Yesu. Na akaniambia unaona mdogo wangu na hizi ndio sehemu ya changamoto tunazokutana nazo huku field hivyo jiandae kuziweka kwenye report tukiridi ofsini.

Mimi nikamsikiliza pale lakini nikaona haipi sawa. Nikachomoka pale nikawatoka kuwawahi wale kabla hawajatokomea. Nikawakuta mahali wamekaa chini mti sijui wanaongea vitu gani. Basi nikawasalimia pale na kuanza kuongea nao lakini kubwa ilikuwa kuwaomba watusamehe tulighafirika tuu kutowajuisha hivyo kama hawatajali wanipe majina na namba za simu ili tukirudi baada ya mwezi mmoja tuwaalike na wao. Mimi niliongea tu vile ile kuwaondolea kile kinyongo maana kwenye miji ya watu bhana unatakiwa uwe unaishi kwa kujiongeza ongeza kidogo.

Wale wazee bhana ni kama niliamsha mashetwaini yao maana walianza kufoka na kulaani utafikiri mimi nimeenda pale kuwafukuza tena. Waliaani na kutoa maneno makali sana. Basi mimi ili kutuliza hali ya hewa nikawaomba omba msamaha pale nikarudi kuendelea na session. Wakati naongea na wale wazee ilikuwa ni muda wa breakfast kule kwenye session. Dada B akaniuliza ulikuwa wapi nikamwambia nilikuwa na wale wazee pale kwenye mti. Alipowaona nikamwambia tuwaite tu waje wanywe chai kisha waende maana inaonekana kama wana njaa akaniambia achana nao. Wale wazee hawakuondoka pale kwenye mti walikuwa wanatazama sana upande ule ambao sisi tulikuwa tunakunywa chai. Breakfast siku ile naikumbuka vizuri sana ilikuwa chai ya maziwa, viazi, chapati na supu ya kuku wa kienyeji. Basi tukawa tumekaa meza moja mimi, dada B na wenyeji wetu wawili tunaendelea kupata msosi. Wale wazee wapo tuu pale kwenye mti tunawaona.

Tulipomaliza kunywa chai tukaingia ukumbini mimi nikawa naendelea na session. Nusu mbele dada b akaanza kukohoa kohoa pale. Mara kikohozi kikawa kinazidi mpaka kupelekea kutoka nje. Mara kikohozi kikawa kikavu sana kama kile cha mgonjwa wa TB. Alikuwa anakohoa mpaka mimi ikabidi nisitishe kwanza session kwenda kumwangalia. Nafika nje nakuta ameshikwa na mmama mmoja nadhali alikuwa ametoka toilet. Toba kumcheki dadaB ameshikilia shingo macho yamemtoka hawezi hata kuongea. Nilipagawa sana tukimuuliza nini hawezi kujibu anatutumbulia macho tuu. Sasa kwenye ile session kulikuwa na mama mmoja mlokole akaanza kukemea pale mapepo kwa muda mda mrefu kama dk 20 nzima lakini hali ya dadaB ndio ikawa inazidi kuwa mbaya. Sasa

Mimi akili yangu ikiwa imepagawa maana naona workmate anaondoka huyu hivyo nikawa namtafuta dereva wa gari tuliyokodi toka Kigoma kuja nayo KIbondo aje tumkimbize hospitali. Yule jamaa hakuwepo alikuwa kwenye misele yake maana tulimwambia sisi atufufate saa tisa aturudishe lodge. Nikipiga simu yake akawa hapokei. Sasa wakati tunahangaika kupata usafiri mwingine na wale walokole wanaendelea na maombi yao pale kukema kuna mzee mmoja ambaye alikuwa mkimya sana muda wote akawanyamazisha wale wakole waache maombi yao. Wakawa wanabisha nbasi yule mzee mkimya akawa mkali akiwaambia mkiendelea na makelele yenu mtampoteza huyu dada. Basi wakatulia. Yule mzee akamsogelea dadaB akamzunguka pale kama mara saba kisha akawa anapiga makofi huku akiangalia mawinguni kama anafukuza fukuza vitu hewani. Baada ya muda tukaona dadaB anaanza kupiga chafya mfululizo. Gafla akatapika bonge la mwiba wa samaki yaani ule mwiba mkubwa kama sindano kubwa ya kushonea nguo majumbani. Kila mmoja akashangaa pale, na mara baada ya kutapika dadaB alipa nafuu kubwa sana.

Wote pale tukashangaa akiwemo dada B mwenyewe kwamba ule mwiba wa samaki umtoka wapi. Maana usku wake nakumbuka kabisa dadaB alikula chipi na mishikaki na asubuhi ile alikuwa kuku sio samaki. Tukaona hayo ni mazingaombwe. Yule mzee mkimya akasema hili jambo bado halijaisha huko njiani mtakapokuwa mnarudi hamtakuwa salama cha muhimu watafuteni wale wazee watatu muongee nao. Wale wazee bila aibu waliikuja pale maana walikuwa bado wapo pale pale kwenye tena wanafatilia kila linalotokea. Wale wazee wala hawakupepesa maneno walituchana live walikuwa wamepanga wakati tungekuwa tunamkimbiza dada B hospitali basi gari ingepata ajali napengine kupelekea kifo. Awali walipanga kutufanyizia wote ila kadili ya maelezo yao mimi walinisamehee kwa sababu nilonekana muungwana. This is very true story maana wazee wa chai hamkawii kuhoji hapa. Yaani wallikuwa na ushujaa wakutueleza kila plan yao walivoichora bila kuogopa wala kufikatena wakisisitiza wao wanaheshimika hawajawahi kudharauliwa na watu wepesi kama sisi.

Basi tukawaomba msamaha pale nakumbuka dadaB aliomba msamaha sana mwisho wakaamua kutegua mitego yao. Nao walifanya kama yule mzee mkimya walimzunguka dadab na kufukuza fukuza vitu hewani, jamani haya mazingaombwe yapo nyie achene. Kwiukweli kabisa ile shughuli iliitibuka pale. DadaB hakuweza tena kufanya iile kazi pale. Hata mimi sikuwa kiakili. Ikabidi tuahirishe tu kwa siku hiyo. Jioni wakati tupo lodge nikamwona dadaB hayupo sawa kabisa kisaikolojia. Kwakuwa yeye ndio alikuwa victim mkubwa nikamshauri kama vipi afanye utaratibu arudi Dar akapumzike nap engine akaangalie afya yake ya kiakili. Dada b nikama nilikuwa kwenye akili yake nayeye alikuwa anafikiria ni namna gani angenishawishi aondoke tuu. Ila tulikubaliana tufanye siri ofisini wasijue basi aka niacha mimi nimalizie kupiga mzigo Kigoma. Watu wa Kigoma kama mpo humu salamaleko.

Baada ya pale sasa nilipobaki mwenyewe kumalizia kazi sehemu zilizobaki ikabidi niintroduce mtindo ambao mwenyeji wangu ndio nilimpa mamlaka ya kuchuja wazamiaji pamoja na kuwalipa washiriki. Nilikuwa na nidhamu sana na uchaguzi wa nini cha kuongea ili kutotibua hali ya hewa. Utashangaa kwa nini niliwaachia wenyeji wangu walipe washiriki ni kwa sababu kwenye hizi mambo yakulipa mara nyingi tulikuwa tunaingia loss sana yaani ni kama unapigwa viini macho hata uwe makini mara nyingi ilikuwa inatokea unajikuta unapata loss yaani kuna mtu watu unakuwa umewali mara mbili. Hii mimi imeshanitokea sana. Kwahiyo nikasema wacha haya mambo wacharurane wenyewe.

Go to #290 for next episode
Yaani wallikuwa na ushujaa wakutueleza kila plan yao walivoichora bila kuogopa wala kufikatena wakisisitiza wao wanaheshimika hawajawahi kudharauliwa na watu wepesi kama sisi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Funzo
Watu wa mjini msiende vijijini kwa pupa..
Unakuta mtu ulokole wa kuunga unga,hasali inavyopaswa lakini anaenda chokoza nyuki.
Hata kama mtu anakukwaza,kuna namna nzuri ya kumuapproach...tujifunze hekima ya maneno na busara.

Ni kweli tumepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka na hakuna kitakachotudhuru ila uhalali wa kuitumia mamlaka hiyo inategemea na mahusiano yetu na Mungu.

Ni aidha uwe umejicommit sana kwa Mungu,si kwa kuungaunga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini Dada B alijifunza kutokutumia Jina la YESU Bure, huo ukax aliowaletea hao walozi wazee watatu ni kinyume cha mafunzo ya Jesus, so alifungua mlango wa kukandwa mwenyewe, ila ulimwengu wa Kiroho upo deep sana hutakiwi kujiaminisha juu juu, miezi kama minne imepita dada mmoja coworker tulienda kumdai mteja rejesho si akaanza kumletea maneno ya dharau mteja (Alikua ni mwanamke mwenzie) Wacha wacharuane na mataashtiti kama yote tukambebea vitu bana Sasa nikawa namshauri mwenzangu apunguze maneno makali na dharau akawa asikii wakafikia hatua ya kutishiana kiroho, dada mteja akawa anamtishia job mate wangu kumnyoosha kishirikina huku job mate wangu anaringishia Upako wa mwamposa mara mafuta mara nini, baada ya siku tatu job mate wangu alianza kuumwa ugonjwa usiojulikana mwezi mzima ndio akapoa, yaani nikajifunza Jina la Mungu halitumiki hivi hivi lazima ujiridhishe uko sawa sawa kabla ya kulitaka likulinde inahotaji hekima ya hali ya juu sana, Mungu atupe roho ya kutuangazia kwa kweli. Hicho kisa cha Dada B kimenifanya niwekee mkazo kuwa muungwana kwa kila mtu hata kama anakukwaza tutafute namna ya kutokuwachokoza maana upande wa pili haucheleweshagi kichapo[emoji119]
Inaonyesha pia wale wakemea pepo hawakuwa strong.

Yaani ulimwengu wa roho, especially sisi wafuasi wa Kristo,Kuna kanuni zake.
Waty hawataki kutengeneza mahusiano mazuri na Mungu lakini wanataka watumie nguvu zake.

"Nasi twajua ya kwamba katika mambo yote,Bwana hufanya kazi na wale wampendao katika kuwapatia...."

Kumpenda Bwana kuambatane na kumtafuta kwa bidii,ndipo tutakapomuona.
Katika bidii ya kumtafuta,kuna gharama ambazo watu wengi hawapo tayari kugharamika.

Na ili ujazwe nguvu na mamlaka ni lazima uwe tayari kumtafuta Mungu...
Siyo mtu anaomba kwa matukio tu...
Nje na hapo,hana ratiba na Mungu.
Anamuhitaji Mungu anapopata shida tu.
God is supposed to be there in our daily routine.
....
Ona hawa Wana maombi
Wanaambiwa waache kuomba.

Si kwamba shetani ana nguvu kuliko Mungu no!
Ila wao binafsi hawakuwa na nguvu ya Mungu ya kutosha...

Mimi nikimess up na Mungu huwa naogopa sana, na kwenye ishu za kukemea mapepo sifanyi kama najijua kwa muda huo mahusiano yangu na Mungu yameyumba.
Ukifosi kufanya, utafanya mwenyewe, Mungu hayupo na wewe,, huna nguvu za Roho Mtakatifu.. you're just doing for showoffs hapo hakuna pepo utamtoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom