Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

EPISODE 6: The new Office

This is just an advice, when joining a new office it's important to avoid coming across as someone who knows too much. (u-much know unaweza kukucost)


Niliweza kujiunga na shirika jipya huku nikiwa nimejipanga kukabiliana na mazingira mapya yakazi, watu tofauti na wale niliowazoea lakini pia huku majukumu yaliongezeka kidogo na hata kasali kalikuwa na ahueni. Nilipokelewa pale kazini vizuri tu na kufanyiwa proper orientation. Utofauti ulikuwa mkubwa sana wakimazigira pamoja na structure ya uendeshaji wa ofisi kwani huku kwa sasa kulikuwa na idara nyingi nyingi ambazo zilikuwa na line managers ambapo mimi niliajiriwa pale idara ya ruzuku nikiwa ni mmoja wa maofisa usimamizi wa ruzuku (Program Officer – Grants). Nakumbuka kwenye ile nafasi tuliajiriwa wawili mimi pamoja na mwenzangu mmoja alikuwa kibonge hivi. Kwenye hii stori nitamwita Big.

Wiki ya tatu tu wakati nikiwa nimeanza kuzoea zoea kidogo mazingira nilipata very shocking news, that Dr KJ my former boss passed away. Nakumbuka nilikuwa nipo kwenye mkutano wakawaida wa wafanyakazi wa idara yetu nilipoona simu ya PS nikajua huyu labda kwa ni ijumaa hii basi ananitafuta labda twende kwenye mtoko maana aliniambia angenitafuta. Nikampotezea kwanza ili nimalize meeting. Kidogo nikana simu ya yule dereva na muhasibu wananipigia nikaona hii mbona kama haijawa sawa. Ikabidi nitoke nikapokee ya dereva ndio kuniambia Dr KJ is no more. Aisee nilipawtwa na mshtuko sana. Nikaconfirm kwa kumpigia mhasibu na PS. PS ndio akawa hajiwezi kabisa yaani anaongea huku analia tuu. Kwakweli ule zile habari ziliniumiza sana sikuweza tena kuendelea na kikao. Ikabidi niombe ruhusa pale niende msibani muda ule ule.

Kiufupi yale maradhi yaliyokuwa yanamsumbua KJ ndiyo yaliyopelekea kifo chake. Basi tukaorganize pale pamoja na wafanyakazi wengine tukaenda wote msibani. Kwahiyo ile weekend yote nilihudhuria msibar wa Dr KJ mpaka tulipomaliza kuzika. Wakati wa kuaga hakika nilitoa chozi la uchungu sana japo kisirisiri maana nilikumbuka mengi sana na mchango wake mkubwa katika kuniingixa kwenye ulimwengu wa ajira rasmi na decent. Japokuwa alikuwa na madhaifu yake lkn mchango wake kwangu ulikuwa mkubwa sana, Mr KJ aliniheshimisha sana mjini kwani maisha yalishanipiga sana ni yeye ndio aliyenipa ramani. Nakumbuka kuna kipindi baadhi ya madogo waliokuwa nyuma yangu kule chuoni ambaye pia alikuwa anawafundisha walinipigia simu za kunipongeza. Mwamba kama ilivyo kawaida ya masifa yake nasikia alikuwa anawaonyesha picha tuliyopiga ya wafanyakazi ya ofisi na kuwauliza darasani kama wananijua. Nasikia alikuwa ananifagilia kinoma noma kwamba amepata jembe ofisini kwake na alikuwa anafikiria hata kuniachia ofisi. Sema tu sifa zake ziliniletea matatizo kwa madogo maana aliwaambia mshahara anaolipa ni mkubwa sana (yeye aliwatajia mara nne ya kiasi alichokuwa ananilipa hahaha) kitu ambacho kilisababisha wale madogo wawe wananipiga sana mizinga. Kiufupi tu mwamba namkumbuka hadi kesho na kuna vitu ninavyo hadi leo kama kumbukumbu yake kwangu. RIP Dr, daima utaendelea kuwa mtu muhimu sana kwangu.

Anyway ya maamuzi ya Mungu hatupaswi kulalamikia sana tuendelee na stori yetu. Basi baada ya mazishi niliendelea na kazi kama kawaida. Sasa hii ofisi ilikuwa na watu sana ukilinganisha na kule nilipotoka. Mfano sisi kwenye department yetu pekee tulikuwa kama 16 hivi, hapo ongezea na wa idara nyingine. Kama nilivosema tuliingia mimi na Big tukiwa ndio newcomers –pale. Kwa kile kkipindi cha wiki mbili tu za mwanzo mwenzangu Big alikuwa ameshazoeana na watu wa karibia ofisi nzima na kwa muda mfupi akaanza mpaka kushirikishwa kwenye madili ya ofisi.

Unaju ile ofisi pamoja na shughuli nyingine ilikuwa pia inadili na mambo ya kugawa ruzuku kwa NGOs nyingine ili wakatekeleze miradi mbalimbali sasa kwa wazoefu wa pale kuna vimichezo walikuwa wanaicheza wanapiga piga vijisenti kwa njia za panya wanazozijua wao. Hii ilikuwa ni seriously unacceptable behavior na ukibainika unapiga hizo ilikuwa kwamba you are terminated on the spot. Na nakumbuka CEO wa lile shirika alikuwa hana msalie mtume katika hizo ishu. Kuna stori niliikuta pale kwamba CEO aliwahi kutimua department nzima ya grants kisa upigaji, akaanza kuajiri upya.hii idara ya grants ndio ambayo inahusika moja kwa moja na kureview proposals, ku-recoomen nani apate nani akose kulingana na vigezo na kusimamia miradi pale ofisini pamoja na kwenda field kuwakagua. Ilikuwa ni department ambayo imekaa kimtego mtego na kiushawishi sana na ilikuwa ukimaliza contarct yako ya miaka mine basi utapongezwa kwa kupewa zawadi ya pesa za kutosha before hujarenew mkataba. Yaani mimi tangu nilipofika pale before hata sijamaliza probation ya miezi mitatu nilishuhudia watu wanne wakitimuliwa. Balaa unaambiwa CEO alikuwa na informers wake nchi nzima utafikiri CIA ya Marekani.

Basi bhana turudi sasa kwa bwana Big. Big bhana nimeingia naye pale wiki moja tu keshazoeleka kwenye idara (halafu ile idara yetu wanaume tulikuwa watatu tu wengine wote wanawake). Wiki ya tatu ofisi nzima Bigii Bigii - Bigi Big Kweli. Big mtu wa mastory, Big mtu wa totoz, Big hana baya na mtu. Mda mfupi kila mtu pale ofisini anajua Big anashabikia utopolo kwa hapa bongo kwa nje anaipenda Liva. Mda mfupi tu k=watu wote tunajua big anapenda kwenda viwanja flani vya kujirusha weekend. Yaani ndani yam da fupi hata mwezi bado watu wote tunajua mambo mengi ya Big ya nje ya kazi, yaani mambo yake binafsi.

Iyo haikuwa kesi maana hizo ni character za mtu kiukweli hata mimi nilikuwa nainjoy kampani yake. Maana sometime Big alikuwa lesi hata kwenye kudai haki zake msingi. Mfano kuna siku sina hili wala lile nipo zangu napambana na majukumu yangu nashangaa naitwa kwa Meneja utawala. Kufika ofsini namkuta Big naye yupo. Mara yule meneja akaniuliza na wewe unataka mkopo? Ile ofisi walikuwa na utaratibu unaweza kukopa advance salali mpaka ya miezi 7 kwa hiyo utakuwa unakatwa kiasi cha pesa kulingana na muda wa mkataba mtakavyokubalina. Mimi nikashangaa, mkopo tena imekuwaje mbona mimi sijataka huo mkopo. Ndio yule meneja kunipa taarifa kwamba Bwana Big amejaza fomu za advance salary na kutaka mkopo wa miezi saba. Akaendelea kusema kwamba alipomwelekeza kwamba ni amalize probation bwana Big akawa anaforce kama vipi tupewe maana hata mimi nina shida na hela so nimemtanguliza yeye akajaribu.

Nikaona duu hii sasa soo. Kwa hiyo meneja ndio ananiuliza kama na mimi nataka au laa. Nikafikiri hapa Big ashaniingiza kwenye mambo yake bila ridhaa yangu lakini pia nikimtosa mooja kwa moja inaweza ikamjengea picha mbaya Big kwa yule meneja. Basi nikasema tuu ni kweli tulidiscuss pamoja na Big maana ni kipengere ambacho kipo kwenye mkataba na nilikubaliana na Big tukipata muda tufatilia so mimi bado sikupata muda muda wa kufatilia, ila kwa maelekezo hayo basi inabidi tusubiri. Yaani nilitoa sababu ya kijinga mpaka yule meneja kuna siku aliniambia kwa utani tulipozoeana kwamba siku zile alicheka sana kwani alijua fika Big kanichomekea. Kwenye hilo niliipenda ile spirit ya Big ya kuzitumia fursa vyenye vyedi.

Ila sasa bwana Big kuna mambo alikuwa anayaendea pupa sana mpaka kuna washkaji wengine pale ofsini wenye mapenzi mema walimtonya apunguze spidi ila akawa mjuaji. Sasa unajua sehemu yoyote ile kwenye michongo michongo watu wanakuwa makini hususani kwa newcomers kujaribu kuwasoma kama mnasomeka ama vipi. Basi zali la kusomeka likamdondokea bwana Big. Wataalamu wa zile kazi wakaona Big hana noma hata akielekezwa mchongo anasomeka. Mimi nikawa sisomeki yaani watu kama hawanielewi elewi hivi. Sijui niite ubaya au uzuri mimi nilijipa muda kwanza wa kuwasoma watu kabla watu hawajanisoma. Kwa hiyo mara nyingi nilikuwa msikilzaji sana na muongeaji kidogo hususani kwenye maswala ya kazi. Sikutaka kuanza kujichanganya kutoka weekend na washkaji wa pale ofisini kwa sababu zangu maalum.

Big alikuwa lesi sana unaambiwa kala hata probation haijaisha big ameshavuta usafiri.Nakumbuka mimi alinishirikisha ile plan yake ya kununua mkoko ila nikamwambia ndugu sikilizia kwanza ujue hapa hata ulikuwa na umedunduliza vijisenti vyako huko itakuwa ngumu watu kuelewa watakuweka kwenye kundi la wapigaji. Big akaniambia yeye anajua anachofanya. Nikamwambia hii italeta shida si unakumbuka ile ishu ya kulazimisha mkpo kule kwa meneja utawala anaweza akajiuliza pesa umepata wapi wakati mkopo hakuidhinisha. Big akaniambia nisijali kuhusu hizo mambo yeye amejipanga. Bai akavuta ile ndinga ilikuwa ni moja ya nding zinazokula sana wese ila ndio ilikuwa habari ya mjini kwa majanki wa enzi zile.

Big hana baya ile ndinga ilivotoka tu bandarini siku hiyo hiyo alikuja nayo ofsini na kila mtu huko parking alioneshwa. Mjengo mzima ukajua leo there is a new father car in town. Nyie si mmezo father house, sasa kuna father car ndio sisi tunaosema kujenga sijengi maana sijawahi kulala nje ila nimetembea sana kwa miguu na kuloana wacha ninunue gari. Kuna jamaa mmoja nae alikuwa ni mmoja wa washkaji wa Big ila yeye alikuwa pale mda mrefu akawa anampa madini sana Big namna ya kuyaendea mambo ofsini, ila Big akataka hadi kuvunja urafiki kwa kuona kuwa jamaa ameanza kumwangia.

Basi maisha yakaendelea pale job kama kawaida. Nakumbuka tulikuwa tumebakiza kama wiki mbili hivi kumaliza probation mimi na Big tulienda kwenye training Nairobi ya wiki tatu ili tukitoka uko tuwe tumekwiva kwa ajili kupiga mzigo kama full employees. Sasa tukiwa kule kwenye training Big akatumiwa email na line meneja wetu inatakiwa arudi ofisini mara moja. Akaniuliza kama na mimi nimetumiwa nikamwabia sijatumiwa. Sasa tukawa hatuelewi pale ni nini kinaendelea. Akili yangu mimi ikawaza labda ni matatizo ya kifamilia labda msiba unaomuhusu sana so wanaoshindwa kumwambia. Hii ikaingia hata kwenye akili ya big huenda kweli kuna tatizo la kifamilia. Akawacheki ndg zake hakuna taarifa yoyote. Siku ya pili asubuhi akapigiwa simu kutoka ofisini kwamba inabidi arudi faster. Tukachanganyikiwa sana pale, basi ikabidi jamaa abadili ticket apande mwewe arudi dar ofsini akisisitizwa akishuka eapoti hasiende hata nyumba aunganishe job.

Kufika ofsini bhana amefikia kwenye kikao chamenejiment. Kiufuoi jamaa yangu Big aliingia kwenye harakati za panya pale ofsini kwa speed sana. Alisomewa mashtaka yake na ushahidi wa kutosha kuhusu harakati za panya mpaka simu zilizorekodiwa na wadau wakipanga mambo yao. Jamaa yangu wakampiga on the sport na kuambiwa kama anahisi ameonewa anaweza kwenda mahamani ila kwa kumuhurumia mambo yasiwe na kuepukwa kufungwa achukue vyake asepe. Huo ndio ukawa mwisho wa mshkaji wangu sana Big.

Anyway weekend hii wakubwa wangu tunafanyeje? Mana kutwa nasikiliza vipindi vya redio tuu home mpaka masikio yataka kutoboka. Na watangazaji wanakera sana maana kutwa kututangazi tu kwamba huu ni mwezi wa matumizi na sherehe kwahiyo watu watumie pesa. Nyie wenzangu mnatumia wapi pesa zetu, basi mtu mmoja ajitokeze anipe mwaliko wa kushangilia pamoja Mnyama akimuua wydad kwake.​

See you badae kwenye episode 7
Oya mshikaji wake big uko wapi kama uko Mbeya please njoo inbox tukaenjoy

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
EPISODE 7: I once found myself in an awkward situation with my boss, but I successfully overcome it by responding ethically and professionally.

Kiukweli kutimuliwa kwa Big kulinichanganya sana. Nilikuja kuambiwa kwamba my colleague is no longer working with us siku nilipoingia ofsini baada ya kutoka training. Big alikuwa ni kampani yangu sana kati ya staff wote pale, labda kwa kuwa tuliingia mjengoni pamoja. Nikamcheki Big kwenye akawa hawezi hata kuongea analia tuu. Wkennd iliyofuata nikaonana nae akasema anapanga kuja ofsini kuomba radhi ili apewe second chance. Kweli wiki iliyofata alikuja ofsini pale kama mara tatu lkn wakubwa wakawa wanamfungia vioo, kimtindo flani Big alikubali kudhalilika mana kuna siku nasikia alipa magoti kwa boss kubwa akimshika miguu ili afikiriwe. Sikuhiyo mimi sikuwepo ila nilipata story. Nikakumbuka kujidhalilisha kwenye shida ni kawaida hata mimi nilishawahi kufanya kwa Dr KJ kama mnakumbuka. Shida inakuja inaumiza sana ujidhalilishe halafu na msaada wenyewe usipewe – aisee!!!

Wakati namiuwazia Big nikasema inawekana BIG aliingizwa kwenye mfumo wa wakubwa bila yeye kujua. Maana na mimi nalumbuka kuna awkward situation moja iliwahi kunikuta pale ofsini nikiwa kama na miezi miwili hivi kipindi ndio tunasubiri subiria tumalizane na probation. Ile situation sikuwa na hakika kama ulikuwa ni mtego ama vipi ila kiukweli ile situation ilinivuruga sana sio kidogo.

Labda niwarudishe nyuma kidogo niliwaambia kwamba ile ofisi ilikuwa na line managers wa idara tofauti tofauti ambao walikuwa ndio sehemeu ya Office Management Team (OMT). Hawa OMT ndio walikuwa ndio wanaomua mustakabali wa ofisi kwenye uendeshaji na mwellekeo wa ofisi. Na niwakumbushe tu niliwaambia kwamba idara yetu ndio ilikuwa ndo inadili na fedha za ruzuku kwenye kuamua nani aapate na asipate, so sisi officers ndio tulikuwa na madaraka ya kupitisha kulingana na mafaili (portifolio) unayofanyia kazi. Kwa hiyo kwenye kupata hizo grants mnoko wa kwanza kukubania usipate fedha ni sisi, au favour ya kwanza ya upendeleo ilikuwa inatoka kwetu. Tulikuwa ndio uti wa mgongo wa NGOs kupata au kokosa ruzuku.

Sasa nakumbuka line meneja wetu pamoja boss kubwa mwenyewe – CEO mara kwa mara walikuwa wanatuweka vikao vya kukumbushana kuhusu maadili ya kazi kwenye idara yetu. Kuna siku boss kubwa mwenyewe alituita mimi na mshikaji wangu Big ofisini kwake na kutuweka licheni ya masaa kama mawii na ushee akiongea na sisi kuhusu maswala ya integrit na being professional katika kazi.

According to Boss kubwa alisisitiza kwamba one strong reason why an employee must be ethical and professional in the workplace is to maintain and enhance the organization's reputation. Ethical and professional behavior contributes to a positive work environment, fosters trust among colleagues, clients, and stakeholders, and reflects positively on the company as a whole. Kwake yeye image ya shirika ilikuwa ni kitu cha msingi sana for organization sustainability. Alisisitiza san asana tujiepushe nay a kipuuzi kwani yeye aliamini kwamba unethical behavior can lead to legal issues; damage the organization's reputation, na kupoteza trust among employees and stakeholders. Yale mamneno binafsi yaliniingia sana nikajiongeza Boss kubwa himself sio mjinga mpaka atumie muda wake wote huo kuongea na sisi kitu ambacho angeweza kufanya HR au line meneja katika idara yetu. Basi kile kikao kikaisha ni kila mtu akabaki na akili kwa kumkichwa.

Siku moja wakati zoezi la kureview proposals za wadau ili kutoa au kutotoa ruzuku likiendelea nikapokea kimemo kutoka kwa one of my colligues wa pale idarani. Labda niseme hivi kuna wale ambao wenye wadau wao ambao wanapenda iwe isiwe lazima wapate ruzuku. Sasa unaweza kuta kwamba labda uyo mdau wako faili lake lipo kwa mtu mwingine, kwahiyo unaweza kufatwa na mwenye interest zake ili uangalie namna ya kumuwezesha huyo mdau. Hiyo ishu ilikuwa inafanyika kulingana na watu jinsi walivyoshibana huwezi tu tumfata kila mtu maana ni risks sana unaweza ukachomwa au ukajichomesha ikala kwako. Yule dada colleague wangu alinpatia kile kimemo na kuniambie kwa kunong’ona kwamba kimetoka kwa kibosile mmoja (line meneja wa department ingine). Kwamaana ya kwamba kuna meneja ameona wadau wake wapo kwangu kwa hiyo niwafanyie mipango wapate.

Wakati bado nafikiria nifanye nini mara yule kibosile akaingia kwenye pool yetu ambapo officers wa idara tunakaa akanicheki kisha akanikonyeza ile kwa kuniambia bila shaka ujumbe umeupata kisha akaendelea na mambo yake. Asee nilikuwa kwenye wakati mgumu sana ukifikiria ilikuwa ni 1st attempt halafu inatoka kwa kibosile. Gafla risala tuliyosomewa na Boss kubwa kwenye ile kicheni ya party ya mimi na Big ikajirudia kichwani mwangu. Nikajiuliza huu ni mtego au kweli yule kibosile ana maanisha. Nilichoamua kufanya sikuifungua kwanza ile memo nikaendelea na kazi maana nikasema nikiifungua yale majina niliyotakiwa kuyafanyia kazi yanaweza yakatibua kazi zangu pengi mengine ndo nimeshayanyima kwa kukosa vigezo. Basi nikauchuna nikaendelea kupiga mzigo.

Baada ya kama siku mbili hivi yule kibosile akamtuma mtu aniite niende ofsini kwake. Kiroho kikapiga paap nikaenda. Kufika kwake akaanza kujichekesha chekesha pale ili kujenga urafiki then akanichomekea kuhusu ile ishu. Akanilobby sana kwamba wale wadau ni muhimu sana sio kwamba yeye anainterest zake ila hata menejiment inajua kwamba wale ni watekelezaji wazuri wa miradi. Kwamba wameshafanya mitradi mingi tuu na ofisi kwahiyo sio vizuri wakakosa. Basi akapiga blabla zake pale na akaniuliza what is the status ya hao wadau wake kama wamekidhi au hawajakidhi?

Nikavuta pumzi pale kisha nikamwambia kiukweli sijui status yao maana kile kimemo mimi sikukifungua. Akaniambia eti hakuna shida maana muda bado tunao kama wiki hivi so nikifungue ni nihakikishe wote wana pata. Nikamuuliza wapo wangapi akaniambia wapo 11, si mchezo mwanawane. Basi nikawaza nikasema huyu kama ni mtego imekula kwake kama yuko real anataka niwabebe hao wadu wake basi leo ataniona mimi ni bonge la mkono. Unajua ipo hivi always trust your gut feelings (machale yako) iwe unconditionally au kwa kujiongeza. Mimi kikubwa kilichonifanya kwanza nione ule ni mtego ilikuwa ni approach ya yule dada mfanyakazi aliyeniapproach. Lazima very strategic katika kuwasoma watu unapoanza kazi mpya, huu uzoefu niliupata kule kwa Dr KJ. Wakati mshikaji wangu Big yuko bize kufatilia watoto wazuri wa kula nao bata and the likes mimi nilikuwa bize kufatilia nani anamichongo gani pale ofsini. Nikaja kubaini pale ndani kuna manyoka kibao sana wanaotumiwa na wakubwa kusoma tabia za watu hususani wageni, huyo dada nae alikuwa ni chawa pro max wa bosskubwa mwenyewe.

Then kingine nikajionea kwamba hoja anazotoa kibosile kwamba wale wadau wake ni wanafanya vizuri hata menejiment inawajua haina mashiko kwa sababu kama ni wazoefu na wabobevu basi kuandika proposal za pale isingekuwa shida. Maana pale pesa zilikuwa zinatolewa nyingi kulingana na uzoefu wako katka ufanyaji kazi na lile shirika so hawa wazoefu wanahaja gani ya kubebwa kama ni wazoefu na hata menejiment inatambua kazi yao.

Basi nikajilipua nikamjibu kibosile kile kimemo mimi nimeshakitupa tena nilikitupa makusudi kwa sababu sikuona umuhimu wa kujua majina ya mahirika ya hao wadau. Nilimwambia wazi kwamba anisamehee sana na kwakuwa ile ilikuwa ni assignment yangu ya kwanza basi nilikuwa nataka niifanye kwa weledi na fea ili niweze kujifunza kuimudu kazi yangu. Niliamua kujilipua kumjibu vile kwa sababu niijua risk yake ambayo kubwa ni uwezekano wa kuingia kwenye bifu kubwa na kibosile kisha kuanza kuwindana kama chui na paka pale ofisini. Maana nilijua kama sio mtego basi kibosile asingekubali mimi kumwangusha kwenye madili yake na yeye ili kujinasua lazima angeweka mikakati ya kuniwahi. Lakini nikaona potelea mbali ila niliingia na mbinu ya kujihami kama plan b. mazungumzo yetu yote niliyarrekodi dadeki kwa maana kama backup plan endapo ishu ingeniback fire.

Yule kibosile ni kama hakuamini vile nilivomtolea nje kavukavu ila akazuga zuga pale kwamba basi nisiwe na wasi wasi anaaamini hao wadau wake wapo vizuri na bila shaka wangekidhi vigezo. Basi tukaachana kila mmoja akiendelea na majukumu yake. Jioni wakati najiandaa kuondoka yule dada informer akaja kwenye desk yangu akanikuliza vipi mmemalizana vipi na kibosile? Kwanza nikashangaa amejuaje kama kulikuwa na kamkutano kasikokuwa na minutes hahaaa lkn nikaishia tu kumzingua pale nikasepa zangu. Basi ile ishu ikapita kama ivyo lkn kile kimemo nilikuwa nacho na baada ya kumaliza mafaili yote baada ya kama wiki nikacheki status za wale wadau wa kibosile. Walikuwa wadau kama 13 hivi na wengi wao karibia 9 walikuwa hawana vigezo kabisa yaani hawabebeki hata kwa mbeleko la chuma ila wnne ndio walikidhi walau vigezo. Na wakidhi tuu kwa sababu mimi sikuwa strikct sana kwenye kufatiia vigezo kama pesa za babaangu yani angekuwa mwingine strictly wale wote walikuwa wanapigwa chini. Basi nilicgofanya niliwarecommend wafanyiwe training ili sikunyingine wakidhi vigezo.

Sasa kumbuka hayo yote yaliyopita nilikuwa nayakumbuka wiki ile Big ametimuliwa ofsini nikasema inawezekana Big naye aliingizwa kwenye mfumo wa wakubwa. Kama vile Mungu siku moja wiki ile ile ambayo Big ametimuliwa line meneja wangu alitukuta na baadhi ya wafanyakazi tunagonga tea kicheni. Sasa sijui aliropoka au vipi akaniambia tena mbele za watu yaani Taidume sijui ulilaie ubavu gani maana ulivonusurika kila mtu ameshangaa. Hii ikanipa maswali sana nilipomuuliza ana maana ganiakazuga zuga tuu lkn wenye akili walielewa. Wafanyakazi wengine wakaniuliza kwani mzee uliponyokaje mimi nikawa nawazingua tu. Ndio kunijia akilini kwamba ile attempt ya kibosile na yule dada ulikuwa ni mtego mmoja mkali sana lakini nikashukuru Mungu nilisimamia weledi. Tena nakumbuka yule dada aliniambia wakati analitea kile kimemo kama na mimi nina wadau wangu wapo kwenye portifolio za wengine basi nimtajie majina yeye atanisaidie kuwafikishia ujumbe, Dah kuna watu wauwaji jamani lakini ndio hivo akili kumkichwa.

Badae sana nikaja kuthibitisha kwamba ule ulikuwa ni mtego na ambao nilivyopona ni kutokana kusimamia weledi kweny kazi nothing more.

Muendelezo soma Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa
 
Interesting story , japo nina swali kwanini umekaa mwaka mzima mtaani ilhali kazi ya kwanza kule uliondoka vizuri bila tatizo.

Kwanini wasikupe hata part time contract ?
Ni kweli hakuna ambapo niliondoka kwa ubaya kama ambavyo utaendelea kuona katika segments za mbele ila mambo sio rahisi kama unavofikiria. Mashirika niliyofanya mimi sio rahisi kurudi ukiwa hauna mchongo maana nafasi zinakuwa tayari zina watui Ila unaweza kurudi endapo kazi zitatangazwa upya, hayo mambo ya parttime ni nadra sana ktokea.
Ila mara nyingi nimekuwa nawaibukia kama nina shughuli zangu labda zinazohitaji proper office environment, strong internet, printing na vitu vingine vidogo vidogo. Mzee ishu ya ajira ni changamoto sana imagine mimi nina uzoefu usiopungua miaka saba napata changamoto vipi kwa fresh graduate?
 
Ni kweli hakuna ambapo niliondoka kwa ubaya kama ambavyo utaendelea kuona katika segments za mbele ila mambo sio rahisi kama unavofikiria. Mashirika niliyofanya mimi sio rahisi kurudi ukiwa hauna mchongo maana nafasi zinakuwa tayari zina watui Ila unaweza kurudi endapo kazi zitatangazwa upya, hayo mambo ya parttime ni nadra sana ktokea.
Ila mara nyingi nimekuwa nawaibukia kama nina shughuli zangu labda zinazohitaji proper office environment, strong internet, printing na vitu vingine vidogo vidogo. Mzee ishu ya ajira ni changamoto sana imagine mimi nina uzoefu usiopungua miaka saba napata changamoto vipi kwa fresh graduate?
Okay shukran kwa ufafanuzi mzuri.

Kila la kheri naamini utafanikisha tena kupata mahali maana nia yako imekua njema pote ulipopita kama ulivyosema.

Kuna kazi za grant office( hii ni kwa uzoefu wako niliona kwenye story hii

Zilitangazwa majuzi ulifanikiwa kuona na uapply?
 
Dah kuna watu wauwaji jamani lakini ndio hivo akili kumkichwa.
Hii hapa kwani si ungejiua mwenyewe sio hao watu kuwa wao ndio wauaji. Yaani everything kinachotokea kwako wewe ndiye chanzo sema kwa asili ya our mother brain huwa haitaki kukiri udhaifu Ila uimara tu ndio inaoupenda coz of ego. Yaani kila kitu sie ndio chanzo Cha Hilo Jambo kutokea. Sema Ile kukwepa responsibility or kukwepa maumivu ya kweli tunajaribu kutupia wengine mpira..

Ni sawa ukifanikisha maisha bila ya elimu ama konekesheni utajisifu kuwa ulipigana ,haikuwa rahisi,ulijinyima,ulilala stendi,ulikula ukoko kwa mama ntilie. Ila Sasa ukifeeli maisha huwezi sema Ile dry truth kuwa it was up to me Bali utasingizia umasikini wenu,hukusoma,huna konekesheni and the like. That's nature of our brain. Ndio Mana mwingine akitoboa wewe utasema alipata bahati ama zali Ila ubongo wako kumpa credits mwenzako kuwa amepigana ama amefanya Kama hayo ya kwako ulivyofanya huwezi sema. Ila Sasa njoo wewe fanikisha life nakuambia utatuambia ulivyohaso hata anodi Shwaznegger ameshasema alilala stendi Kama Mara tatu hivi mpaka akatoboa. So no asili ya binadamu na tricky ubongo unacheza with us , it's all about EGO. Yani igo yako inakuambia ama kukuaminisha kuwa you're the better than others or the rest ya dunia,unavimba unajisikia kuwa waweza tembea juu ya maji ama angani ukaonyesha ukuu na utukufu
 
Back
Top Bottom