Mkuu mimi nimepata mawaidha ya tajiri maarufu Ali Mufuruki akiwaasa graduates kujishusha ili kupata angalau sehemu ya kuanzia.
Aliwaambia graduates wafanye kazi, hata kama ni kuosha magari mjini, ilimradi wanajua mpango wao ni kufanya nini kuitoa katika maisha. Wasione aibu kufanya kazi yenye maslahi kwa sababu wao ni graduates.
Na nishaishi maisha ya aina zote ya kwetu ushuani na Uswahilini nilikojitosa tu kuona maisha, nikafunga mkanda mpaka New York City kutafuta maisha bila kumjua mtu.
Kwa hivyo, somo la kujishusha katika maisha ili kupata pa kuanzia, nalielewa sana.
Nishawahi kukaa sehemu ambazo wale watu wa pale wangejua mimi ni nani wangenichukukia tofauti kabisa, lakini mimi hata sikutoa credentials zangu nilikuwa nimejishusha tu, na hata hapo kuna watu walikuwa wananiangalia k8magutu magutu wanaona huyu mbona kama hapa kajiegesha tu lakini si wa hapa?
Kumbe nilikuwa nasoma tu katika darasa la maisha.[emoji16][emoji16]