Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

UTANGULIZI
Wakuu habari.

Naandika hii story yangu ikiwa ni mwaka sasa nipo mtaani nikiendelea na harakati za kusaka ajira mpya toka mkataba wangu wa ajira ulipoisha mnamo Desemba 2022. Nimeamua kushea uzoefu wangu kwa mtindo wa Masimulizi (katika episodes) kwa kuamini pengine inaweza kuwa na mafunzo kwa waajiri, waajiriwa au wanaotegemewa kuajiriwa. Naomba moderatoes wa JF wauache huu uzi wangu hapa hapa kwenye Jukwa la Ajira kwani muktadha wa simulizi hii maswala ya kubadilishana uzoefu katika swala la ajira na sio mambo ya entertainment. Twende kazi.

Episode 1: Sikuogopa kujidhalilisha ili kupata reliable connection

Mwaka 2011 nilipomaliza my 1st degree kama ilivo kwa wanachuo wengine, nilikuwa na expectation kubwa sana ya kupata ajira nzuri ndani ya muda mfupi. Hii ilijengwa na kiburi kwamba mwaka mmoja before sijamaliza niliwaaproach ndugu na wadau kwenye network yangu kwamba mwakani namaliza. Kila mmoja alinipromise kunisaidia kupata job au kuniconnect na waajiri mbali mbali. Swala likawa ni kwamba wewe maliza tu chuo then utuambie ili tukafanyie mipango.

Kimbebe kilikuja baada ya kumaliza. Nilitulia kwanza mwezi mmoja then nikaanza kucheki walionipromise job kwamba I am available. Asee nilipigwa dana dana za kutisha na mwishowe wengine wakawa hata hawapokei simu zangu. Nikiwaibukia nyumbani au maeneo yao ya kazi wanaishia kunipa nauli ya kurudia na kuniambia ajira ngumu cha muhimu wewe endelea kumuomba Mungu. It was very disappointing situation at that time na nikafikia hatua ya kuanza kuwachukia bila sababu as if wao ndio wanaonisababishia ugumu wa kuajiriwa, hahahaaa.

Basi nikaanza kuumiza kichwa how to go about finding the job. Nikaaply sana kazi kupitia job adverts za mtandaoni lakini mimi mwenyewe nikaona as a fresh graduate I didn’t have the skills and required experiences. Nikaanza kuona hata elimu yenyewe may be course niliyosoma haina maana bora lile boom ningelitumia kwa kuanzisha hata kimradi cha kuchoma popcorn mtaani.

Hali ilikuwa mbaya to most of the graduates maana kila nikiwacheki wana nao wanalalamika kama mimi tuu isipokuwa wachache sana wenye connection tena za familia zao za kuzaliwa. Hapo nikakumbuka wakati naenda kuanza form 5 way back bro wangu aliwahi kuniambia “dogo huko shule nenda kawe na marafiki wa aina mbili, either wenye akili sana darasani au wale wanaotoka kwenye familia bora”. Nilikuja kumwelewa kipindi hiki ni nini bro alichomaanisha. Kwamba wale wenye akili sana darasani watakuinfluence kufauru na wale wanaotoka maisha bora ni future asset katika connection za ajira.

Sasa mimi kutoka na usela wangu mavi wa teenager sikuwa na hata mmoja kati ya hao. Roho ilikuja kuniuma zaidi nilipogundua nilipokuwa advance niligombana na jamaa mmoja ambaye kwao walikuwa wapo poa sana wa kutokea mkoa wa Iringa, nilipooulizia habari zake nikasikia kwa kipindi kile natafuta ajira alikuwa ni msimamizi wa kampuni ya usafirishaji mizigo(malori) na walikuwa na ofisi zao bandarini (clearing and forwarding). Laiti yule jamaa ningemfanya best friend ukute ingekuwa rahisi kwa yeye kunipa mchongo. Anyway, les forget about him.

Nakumbuka siku moja nikiendelea kusaga visigino katika harakati zangu za kutembeza bahasha, kwenye foleni nikamwona lecturer wangu mmoja hivi, tumuite Dr KJ (PhD ya kihaya hiyo) kwenye shangingi lake akiendeshwa na dereva wake kama kawaida. Huyu lecturer nilimkumbuka kwa sababu alikuwa na sifa sana kwenye vipindi vyake na alikuwa anafundisha somo la project Management.

Yaani huyu Muhaya alikuwa anatumia nusu ya muda wake kwenye lecture kujisifia. Ataanza kuwananga maprof kwamba japo yeye ana PhD ila hakuna prof anaemzidi akili na pesa chuo kizima, kwanza yeye anaendeshwa na mshahara anamlipa dereva wake ni sawa na wa tutorial assistant wa pale chuo. Alikuwa mdhalilishaji sana kwa wanafunzi hususani watoto wa kike au wanaofeli somo lake.

Ila watu walichompendea jamaa alikuwa sometimes anagawa sana maokoto akiwakuta wanafunzi njiani ila ndio mjue mtadhalilishwa. Jamaa alikuwa anatembea na dola au Euro akidai pesa za madafu ni nzito, hatukujua anapata wapi zile dola dola. Nakumbuka kuna semester alimlipia ada jamaa mmoja alikuwa anasoma kwa shida sana alikuwa hana boom. Alimlipia ada ya semester ya mwisho ila yule jamaa cha moto alikiona maana Dr KJ kwenye kila kipindi alichofundisha kwenye madarasa yake lazima amtolee mfano yule jamaa mpaka mlipiwa ada akawa famous chuo hahahaaa.

Basi bhana nilipomwona kwenye foleni Dr KJ vitu vingi vingi vikapita kama mshale kwenye mawazo yangu. Kwamba huyu jamaa anaweza akawa asset lakini anaweza akanidhalilisha vibaya sana na nitamuanzaje yupo kwenye gari. Je atanikumbuka maana wanafunzi tulikuwa wengi sana. Lakini nikifikiria pale geto nadaiwa kodi mwenye nyumba keshanivumilia kama two months (niliamua kukomaa mjini sikutaka kwenda mkoani).

Wakati naendelea kuwaza foleni ikaanza kutembea, asee sijui ni nini kilinikuta nikajikuta naikimbilia ile gari na kwenda kuisimamia kwa mbele nikiizuia isiende huku nikimwonyeshea ishara dereva apaki pembeni. Dereva alipoona anaweka foleni akamuuliza bosi wake wafanyeje hahaaa maana nacheka kama ni mazuri. Basi Dr KJ kwa wasiwasi akamwambia aweke pembeni.

Basi nikasogea upande wa Dr KJ akawa hataki kushusha kioo, akanielekeza niende upande upande wa dereva. Nikajua tuu boss anaogopa labda nitamdhuru so he decided to sacrifice his driver- hahahaa. Basi nikaenda upande wa dereva aliposhusha kioo nikamsalimia.

Mimi: shikamoo Dr KJ

Yeye: Unanifahamu?

Mimi: Ndio wewe ni mwalimu wangu wa somo flani nimemaliza mwaka jana.

Yeye: (Bado akiwa na wasiwasi) Nitaamini vipi na kwanini unanisimamisha kama jambazi?

Mimi: (Bila kujiuma uma) Naomba unisamehe sana Dr, ni kuvurugwa na hapa nimeona kama bahati
kukuona. Dr mimi nipo katika harakati za kutafuta kazi, nimekusimamisha ili nikuachie CV yangu maana naamini wewe network yako ni kubwa pengine unaweza ukaniconnect na wadau wako.

Yeye: (Akacheka sana huku akiniita niende upande wake). Kwa hiyo unatafuta kazi gani?

Mimi: Kwa sasa nahitaji sehemu yoyote ya kujishikiza ili nipate uzoefu, lakini uzuri wewe ni mwalimu wangu wa PM so unaweza ukaona ni wapi zile theory wapi naweza kuziapply.

Akaniangalia sana kisha akaniuliza unajua nini kuhusu project management na principles for effective project management? Nikamshushia madude kwa style ambayo nadhani ilimkamata kisawa sawa. nIkamsisitizia kwamba mimi sijawahi kushikwa kwenye somo lake. Baada ya kumjibu pale akaniambia. Mbona unaonekana una njaa sana? Shika hii nenda kale mimi nina mambo mengi sana na hapa unanichelewesha tuu. Sikupokea kwanza ile pesa ila nikamwambia Sir please just take my CV may you can see how you can help.

Akaniuliza, sasa CV yako umeandika nini wakati hujawahi kufanya kazi popote? Halafu sina muda wa kutembea na makaratazi kwa gari yangu. Akawa anafunga kioo, asee nikaking’anga’ania. Akaniambia unataka nini sasa pesa nimekupa umekataa. Nikamwambia, kama huwezi kutembea na makaratasi basi naomba email address yako ili nikutumie. Akaniangaliaa, kisha akatoa business card akanipa. Mimi nikaicheki nikaona ile biz card sio yake ni ya mdada. Nikamwambia mbona sio yako. Akaniambia “vizuri sana upo makini, mpigie huyo dada simu kesho muda kama huu”. Hiyo ilikuwa ni kama saa tisa hivi. Kisha akanipa ile pesa, akasepa zake.

Mwendelezo=>

Sehemu ya 2

Sehemu ya 3
Dr KJ hakuomba tobo? Maana umemshobokea hadi aibu
 
Mkuu Tai Dume, kwa kweli uzi wako una somo zuri sana kuhusu skills na experience unazo pata kazini ukiwa mtu wa kujituma.
Tungependa kujua kidogo ni misaada ya namna gani hasa mlikua mnatoa kwa hao wastahiki.
Pia nimeona kua kwenye hizi NGO pia sehemu kubwa ya pesa zinakwenda kwenye gharama za idara na kidogo zinawafikia walengwa.
Kutafuta success stories ni moja ya njia ya secure kazi za hao watumishi wa NGOs wakiwa local au wakitoka huko ugenini wote wako desperate kuhakikisha wafadhili wana endelea kuto pesa.
 
EPISODE 9: Umeshawahi wahi kufanya kazi ambayo mda wote unakuwa bize kazini? Work-life balance is a must if don’t wish to go insane.
Baada ya kumaliza ile tripu ya Tabora na Kigoma salama at least nilikuwa nimeboresha uzoefu wa kazi za field kwenye hii ofisi mpya. Kumbuka kwamba nilibaki peke yangu baada ya kukubaliana na dadaB arudi home ila kutokana na kumsoma kwa mda mfupi na kuunganisha na uzoefu wangu wa kule kwa Dr KJ kazi ikawa rahisi sana kwangu. Hapo ndipo nikajua kwa nini waajiri wengi sikuhizi they prefer job experience than grade A academic certificates.

Nikarudi ofisini salama na kwa kushirikiana na dadaB tukasubb report pale na maisha mengine yakaendelea. Baada ya muda na mimi nikawa ni among senior officers pale hata nikawa trusted kuwa-mentor the new employees maswala ya kazi. Anyway it was good experience kwa kweli na niliinjoi sana kazi yangu.

Uzuri wa ile kazi ilikuwa ni kusafiri kitu ambacho nilikuja kugundua kumbe mimi napenda sana kusafiri tena hususani safari za mikoa ya mbali na vijijini nilikuwa napenda sana. Unajua kwenye kusafiri sio tu kuenjoy zile moments za kuwa kwenye gari au flight lakini inasaidia kuexplore new opportunitis na kuongexza network yako na watu tofauti tofauti unaokutana nao. Sasa pale ofisini ilikuwa ukikaa sana hujasafiri basi ni mwezi na nusu au miwili. Lakini kikawaida ilikuwa kila mwezi lazima mtu usafiri walau kwa si chini ya wiki, yaani safari ilikuwa ni lazima kulingana na nature ya kazi hususani kwenye idara yetu. Mimi ilifikia wakati mpaka nikawa nawatania watu kwamba sitakuja kuoa au kuruhusu mke wangu afanye kazi pale ofsini maana ndoa inaweza ikayumba hahaahaa sababu watu kila mara wapo safarini na hivyo mke anaweza kushindwa kutimiza majukumu ya nyumbani vizuri (jokes) with that job nilisafiri kila wilaya unayoijua wewe hapa Tanzania zilikzokuwepo kipindi kile. Utanitajia wapi nisipajue mimi.

Ofisi ilikuwa inakufacilitate kila kitu ukiwa safarini ili uweze kuendelea na majukumu yako ya kazi hata ukiwa nje ya ofisi. Mfano vitendea kazi bora kabisa laptops, vimodem kwa ajili ya internet vyenye unlimited bando nk. Kwanza ilikuwa ni marufuku staff kupanda mabasi haya abiria is either usafiri kwa gari ya ofisi sehemu ambako hakuna viwanja vya ndege au ukodi gari hata ktoka dar mpaka ifakara endapo usafiri wa ndege haupo na magari ya ofisi yapo na shughuli nyingine. Na ilikuwa lazima ulale sehemu yenye hadhi ya juu kulingana na eneo ulilopo ili kuwezesha usalama wako na pia mazingira rafiki ya kuendelea kupiga mzigo. Kifupi ilikuwa ukisafiri unasafiri na dawati lako maana kwa necha ya kazi ilikuwa huwezi kumuachia mtu akushikie shughuli zako maana utamuonea tuu, labda kama mtu ni mgonjwa, amefiwa au likizo za uzazi ilikuwa inaeleweka ila sio safari. Ukisafiri utawezeshwa kila kitu kusafiri na majukumu yako, hakuna kumuachia mtu ofsini.

Kwahiyo life pale ofsini ilikuwa ni mshike mshike, bize mda wote. Mtu kwenda weekend job au kuchelewa kutoka mpka saa tatu usiku ilikuwa ni kawaida sana. Yaani ilikuwa ukiangalia vimeo ulivyonavyo kwenye meza yako unajikuta tuu wenyewe kwa hiari yako jumamosi au jumapili unaingia job walau kwa masaa manne ukapunguze vimeo. Au mara kwa mara unatoka ofsini saa mbili au tatu usiku.

Mfano mimi kwenye portifolio yangu nikajikuta nina kama zaidi ya NGOs 700 ya kuzisimamia. Yaani hapo uhakikishe wameleta report zao za fedha na miradi, report zimekaa sawa, uindize report kwenye system tena kwa kuzitranlate kwa kingereza, kuhakikisha umewatumia fedha za quarter nyingine baada ya kujiridhisha na report ya fedha. Kisha uhakikishe uhakikishe hizo NGOs umezitembelea ili kwenda kuzikagua huko field kama wanatekeleza miradi sawa sawa au wapo wrong ili uwaelekeze. Wakati huo huo uhakikishe unatrain waliokosa funding ili nao wapate fedha maana ofisi ile ilikuwa na wafadhili wengi waliokuwa wanaweka fedha zao ili ziende kwa wadau huko mikoani, kwahiyo mnajikuta mna fedha lakini wanaopata ni wachache so in order to maintain reputation ya ofisi kwa donors ilikuwa ni lazima kwenda huko na huko mikoani kuwafundisha watu jinsi ya kuomba na kupata ruzuku kutoka kwetu kulingana na vigezo vetu ndio mana tukawa tunapokea hata proposal za Kiswahili ilimradi kutombagua mtu.

Sasa kwenye mazingira kama hayo unafanyaje? Watu tulikuwa bize muda wote ukiangalia kazi ni nyingi mpaka unatamani siku ingekuwa na masaa 30 walau unaweza kupata muda mzuri wa kupumzika. Kiukweli kuna watu ambaop hawakuwa na shida sana na kazi waliacha asee. Pia ukiachana na sababu za integrity kuachishwa kazi kama mshikaji wangu Big lakini wengi pia walitimuliwa sababu ya performance issue, hawakuweza kwenda speed ya ofisi. Na katika vitu ambavyo menejiment ilikuwa haiwezi kukuvumilia ni malalamiko kutoka kwa grantees kwamba umewaomba rushwa au umewacheleweshea fedha zao, hapo ulikuwa hueleweki. Kwahiyo unachotakiwa kufanya grantee akileta report yake leo baada ya wiki uwe umeshaireview na kuprocess fedha zake. Hata system ilikuwa inakukumbusha kwamba report ipo due hivyo unatakiwa kuishughulikia. Sasa mtu unasimamia miradi zaidi ya 500 what do you expect. Usipokuwa smart and organized unakuwa chizi. Work-life balance ni kama haikuwepo pale ofsini.

Nakumbuka kuna new employee ndio alikuwa ameajiriwa ana kama mwezi tuu akapiga chini kazi bila kupata kazi nyingine. Yule jamaa alivoajiriwa pale alikuwa amebakiza kama mwezi hivi afunge ndoa. Basi ameingia pale ofsini amekutana na mshike mshike wa kaxi na hakuna ugeni, kwani ugeni ulikuwa mwisho wiki ya kwanza. Sasa yule bwana harusi inaonekana maswala ya kushughulikia maandalizi ya harusi yake alikuwa anayasimamia yeye mwenyewe kwa kiasi kikubawa sijui hata kama alikuwa na kamati yule bwana maana simu yake ilikuwa bize sana na kila kitu anaulizwa yeye. Basi pale mjengoni tukamchangia kama kawaida tena mzigi wa kutosha tuu na kutokana na maandalizi yake akaruhusiwa awe anafanya kazi nusu siku.

Lakini tulikuwa tunabaki na bwana harusi mpaka usiku maana naona alikuwa akiangalia haoni pa kutokea lazima abaki ofsini kupunguza majukumu. Sasa sisi tulikuwa tunafanya kazi kwenye pool ambapo wote mnaonana na kusikilizana. Sasa kuna siku kazi zimepamba moto, basi simu ya bwana harusi ikawa inaita sana akawa hapokei. Mdada mmoja akamwambia bwana harusi pokea simu inaita basi akapokea nadhani sijui kuchanganyikiwa au vipi akaamkia “shikamoo”, sijui akajibiwa nini tukamsikia anasema “mdau nimekwambia atakuja mtu huko huko kuwatembelea wiki ijayo atawasaidia”. Sijui akajibiwa nini akamwambia yule mpigaji simu “ongea na huyu mwenzangu atakuasaidia” akawa amempa yule dada aliyemwambia apokee simu ili aongee na simu yake.

Yule dada akachukua simu akijua anaongea na grantee ii amsaidie bwana harusi kutatua changamoto yake akamuuliza mpigaji una shida gani nikusaidie? Akajibiwa mimi ni mchumba wake na ni mke mtarajiwa wa huyo mwenye simu lakini naona ananiambia vitu ambavyo ambavyo sivielewi, je yuko sawa kwani maana kuna vitu nataka kumwambia kuhusu gauni la harusi. Ndio yule dada kumwambia bwana harusi wewe anayepiga simu ni mkeo sio grantee hebu toka nje ukaongee naye. Aisee ofisi nzima tulibusrst kwa kucheka. Yaani bwana harusi alivurugwa na kazi mpaka akawa amesahau sauti ya mkewe mtarajiwa. Lakini pia inaonekana sijui alivurugwa kiasi gani mpaka akawa anaongelea maswala ya kazi wakati bi harusi anaongelea maswala ya gauni. Ikabidi atoke nje akaongee na mkewe badae akarudi.

Basi harusi ikapita lakini baada ya wiki kama tatu hivi bwana harusi akaandika barua ya kuacha kazi. Sasa HR hakutaka kuiprocess moja kwa moja akawa anamtaka kwanza afikirie mara mbili mbili uamuzi wake labda kama ni ishu ya maslahi na amepata sehemu nzuri zaidi. Basi HR akatufata watu ambao aliona kidogo tupo karibu na bwana harusi ili tuongee naye. Bwana harusi wala hakuficha akatuchana live japo hajapata kazi sehemu nyingine ila mazingira ya kazi pale yamemshinda maana yalikuwa ni busy mno with less work-life balance. Tuakajaribu kumsihi pale avumilie atazoea tuu akagoma kabisa. Jamaa etu mmoja akasema jamani tumuacheni huyu ni mtu mzima anajua analolifanya. Mimi nikaongezea nikasema tena huyu muhehe wa Iringa huko tusije tumalazimisha akajinyongea ofsini halafu ikawa balaa jingine. Basi bwana harusi akaresign kama alivyopanga, mhehe yule ni kweli alikuwa hana kazi maana baada ya hapo vilianzan vizinga kwa sana na tuu vile mkewe alikuwa karibu anajifungua basi alikuwa na uhitaji sana wa pesa. Kwa sisi washkaji zake tulimbusti tulivyoweza lakini nilijifunza kuna watu wana maamuzi magumu na misimamo asee. Unaachaje kazi huna kazi?

Nakumbuka tulimfikishia HR sababu za kwanini yule bwana harusi ameacha kazi na uzuri au ubaya kwenye taarifa za ofisi ya HR waligundua wengi tuu walionekana hawakuwa na performace nzuri kwa sababu hawakuwa na muda wa kutosha wa kuopumzika. So ikawekwa mikakati pale ili kuboresha work-life balance kwa wafanyakazi. Hata menejiment walikuwa wanajua kwamba work-life balance was essential for promoting employee well-being, maintaining job satisfaction, preventing burnout, and creating a positive and productive work environment. Ignoring work-life balance can have adverse effects on individuals and organizations alike, impacting health, relationships, and overall job performance.

Mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuongeza wafanyakazi, kwa hiyo ikatafutwa ofisi nyingine yenye uwezxo wa kuaccommodate wafanyakazi wengi zaidi lakini pia likizo ilikuwa ni lazima. Maana before hapo likizo ilikuwa ni optional kwamba mtu unaweza ukalipwa pesa ule mda wa likizo ili uendelee kupiga mzigo, na kwa jinsi kazi zilivokuwa nyingi mtu aliona bora auze baadi ya siku za likizo ili apunguze kazi huku akipokea mshiko. Hii hata mimi nikifanya sana. Basi maisha baada ya hapo yaliendelea kama kawaida na kiukweli work load ilikuwa imepungua sana na tulifanya kazi kwa utulivu na ufanisi mkubwa.

Wadau wangu nilifanya kazi pale kwa miaka mi4 before I shifted to another organization. Based on my job responsibilities as a Program Officer - grants, I have developed a diverse set of skills as followas
  1. Grant Management: Demonstrated ability to review, assess, and select grant applications in accordance with established procedures and regulations.​
  2. Communication Skills: Regularly communicated with grant applicants regarding the status of their applications, ensuring accurate and timely information.​
  3. Training and Facilitation: Organized and facilitated training sessions on project and financial management for CSOs/NGOs/partners nationwide.​
  4. Supervision and Leadership: Successfully supervised over 100 grantees annually in various sectors, including governance, youth, human rights, gender & women empowerment, health and disability.​
  5. Capacity Development: Designed and conducted capacity development sessions for grantees, covering project management, financial management, project monitoring and evaluation, and project report writing.​
  6. Partnership Management: Worked closely with local partners to identify and address capacity gaps in project grants management.​
  7. Monitoring and Evaluation: Conducted field visits to assess and monitor project implementation performance and collect success stories from partners.​
  8. Flexibility and Adaptability: Ensured flexibility and high quality of capacity development support provided to partners.​
  9. Report Writing: Prepared periodic reports for management purposes and other stakeholders.​
  10. Stakeholder Engagement: Collaborated with various stakeholders, including CSOs, CBOs, FBOs, and NGOs, throughout the grant management process.​
  11. Project Implementation Oversight: Monitored and assessed project implementation to ensure alignment with goals and objectives.​
  12. Time Management: Successfully handled multiple responsibilities and tasks within deadlines.​
  13. Analytical Skills: Evaluated grant applications, monitored project performance, and prepared reports, demonstrating strong analytical abilities.​
Nipeni connection wadau

Tukutane next episode
inaonyesha umepiga sana Hela Mkuu...haijatosha kujiajiri
 
Mkuu TAI DUME story yako ni nzuri sana na imejaa mafundisho kwa watu wa aina mbalimbali. Ila nakushauri kwamba ongea yote ila usisahau kipengele cha kula tunda kimasihara, ni kipengele muhimu sana kwa story zinazobamba hapa Jf. Ongelea hata mahusiano ya boss na PS au unda story ya aina hiyo wewe na demu wako wa kitaa au wateja wenu hapo kazini ilimradi kisikosekane tu.
Asante.
TAI DUME itifaki izingatiwe mkuu.
 
EPISODE 6: The new Office

This is just an advice, when joining a new office it's important to avoid coming across as someone who knows too much. (u-much know unaweza kukucost)


Niliweza kujiunga na shirika jipya huku nikiwa nimejipanga kukabiliana na mazingira mapya yakazi, watu tofauti na wale niliowazoea lakini pia huku majukumu yaliongezeka kidogo na hata kasali kalikuwa na ahueni. Nilipokelewa pale kazini vizuri tu na kufanyiwa proper orientation. Utofauti ulikuwa mkubwa sana wakimazigira pamoja na structure ya uendeshaji wa ofisi kwani huku kwa sasa kulikuwa na idara nyingi nyingi ambazo zilikuwa na line managers ambapo mimi niliajiriwa pale idara ya ruzuku nikiwa ni mmoja wa maofisa usimamizi wa ruzuku (Program Officer – Grants). Nakumbuka kwenye ile nafasi tuliajiriwa wawili mimi pamoja na mwenzangu mmoja alikuwa kibonge hivi. Kwenye hii stori nitamwita Big.

Wiki ya tatu tu wakati nikiwa nimeanza kuzoea zoea kidogo mazingira nilipata very shocking news, that Dr KJ my former boss passed away. Nakumbuka nilikuwa nipo kwenye mkutano wakawaida wa wafanyakazi wa idara yetu nilipoona simu ya PS nikajua huyu labda kwa ni ijumaa hii basi ananitafuta labda twende kwenye mtoko maana aliniambia angenitafuta. Nikampotezea kwanza ili nimalize meeting. Kidogo nikana simu ya yule dereva na muhasibu wananipigia nikaona hii mbona kama haijawa sawa. Ikabidi nitoke nikapokee ya dereva ndio kuniambia Dr KJ is no more. Aisee nilipawtwa na mshtuko sana. Nikaconfirm kwa kumpigia mhasibu na PS. PS ndio akawa hajiwezi kabisa yaani anaongea huku analia tuu. Kwakweli ule zile habari ziliniumiza sana sikuweza tena kuendelea na kikao. Ikabidi niombe ruhusa pale niende msibani muda ule ule.

Kiufupi yale maradhi yaliyokuwa yanamsumbua KJ ndiyo yaliyopelekea kifo chake. Basi tukaorganize pale pamoja na wafanyakazi wengine tukaenda wote msibani. Kwahiyo ile weekend yote nilihudhuria msibar wa Dr KJ mpaka tulipomaliza kuzika. Wakati wa kuaga hakika nilitoa chozi la uchungu sana japo kisirisiri maana nilikumbuka mengi sana na mchango wake mkubwa katika kuniingixa kwenye ulimwengu wa ajira rasmi na decent. Japokuwa alikuwa na madhaifu yake lkn mchango wake kwangu ulikuwa mkubwa sana, Mr KJ aliniheshimisha sana mjini kwani maisha yalishanipiga sana ni yeye ndio aliyenipa ramani. Nakumbuka kuna kipindi baadhi ya madogo waliokuwa nyuma yangu kule chuoni ambaye pia alikuwa anawafundisha walinipigia simu za kunipongeza. Mwamba kama ilivyo kawaida ya masifa yake nasikia alikuwa anawaonyesha picha tuliyopiga ya wafanyakazi ya ofisi na kuwauliza darasani kama wananijua. Nasikia alikuwa ananifagilia kinoma noma kwamba amepata jembe ofisini kwake na alikuwa anafikiria hata kuniachia ofisi. Sema tu sifa zake ziliniletea matatizo kwa madogo maana aliwaambia mshahara anaolipa ni mkubwa sana (yeye aliwatajia mara nne ya kiasi alichokuwa ananilipa hahaha) kitu ambacho kilisababisha wale madogo wawe wananipiga sana mizinga. Kiufupi tu mwamba namkumbuka hadi kesho na kuna vitu ninavyo hadi leo kama kumbukumbu yake kwangu. RIP Dr, daima utaendelea kuwa mtu muhimu sana kwangu.

Anyway ya maamuzi ya Mungu hatupaswi kulalamikia sana tuendelee na stori yetu. Basi baada ya mazishi niliendelea na kazi kama kawaida. Sasa hii ofisi ilikuwa na watu sana ukilinganisha na kule nilipotoka. Mfano sisi kwenye department yetu pekee tulikuwa kama 16 hivi, hapo ongezea na wa idara nyingine. Kama nilivosema tuliingia mimi na Big tukiwa ndio newcomers –pale. Kwa kile kkipindi cha wiki mbili tu za mwanzo mwenzangu Big alikuwa ameshazoeana na watu wa karibia ofisi nzima na kwa muda mfupi akaanza mpaka kushirikishwa kwenye madili ya ofisi.

Unaju ile ofisi pamoja na shughuli nyingine ilikuwa pia inadili na mambo ya kugawa ruzuku kwa NGOs nyingine ili wakatekeleze miradi mbalimbali sasa kwa wazoefu wa pale kuna vimichezo walikuwa wanaicheza wanapiga piga vijisenti kwa njia za panya wanazozijua wao. Hii ilikuwa ni seriously unacceptable behavior na ukibainika unapiga hizo ilikuwa kwamba you are terminated on the spot. Na nakumbuka CEO wa lile shirika alikuwa hana msalie mtume katika hizo ishu. Kuna stori niliikuta pale kwamba CEO aliwahi kutimua department nzima ya grants kisa upigaji, akaanza kuajiri upya.hii idara ya grants ndio ambayo inahusika moja kwa moja na kureview proposals, ku-recoomen nani apate nani akose kulingana na vigezo na kusimamia miradi pale ofisini pamoja na kwenda field kuwakagua. Ilikuwa ni department ambayo imekaa kimtego mtego na kiushawishi sana na ilikuwa ukimaliza contarct yako ya miaka mine basi utapongezwa kwa kupewa zawadi ya pesa za kutosha before hujarenew mkataba. Yaani mimi tangu nilipofika pale before hata sijamaliza probation ya miezi mitatu nilishuhudia watu wanne wakitimuliwa. Balaa unaambiwa CEO alikuwa na informers wake nchi nzima utafikiri CIA ya Marekani.

Basi bhana turudi sasa kwa bwana Big. Big bhana nimeingia naye pale wiki moja tu keshazoeleka kwenye idara (halafu ile idara yetu wanaume tulikuwa watatu tu wengine wote wanawake). Wiki ya tatu ofisi nzima Bigii Bigii - Bigi Big Kweli. Big mtu wa mastory, Big mtu wa totoz, Big hana baya na mtu. Mda mfupi kila mtu pale ofisini anajua Big anashabikia utopolo kwa hapa bongo kwa nje anaipenda Liva. Mda mfupi tu k=watu wote tunajua big anapenda kwenda viwanja flani vya kujirusha weekend. Yaani ndani yam da fupi hata mwezi bado watu wote tunajua mambo mengi ya Big ya nje ya kazi, yaani mambo yake binafsi.

Iyo haikuwa kesi maana hizo ni character za mtu kiukweli hata mimi nilikuwa nainjoy kampani yake. Maana sometime Big alikuwa lesi hata kwenye kudai haki zake msingi. Mfano kuna siku sina hili wala lile nipo zangu napambana na majukumu yangu nashangaa naitwa kwa Meneja utawala. Kufika ofsini namkuta Big naye yupo. Mara yule meneja akaniuliza na wewe unataka mkopo? Ile ofisi walikuwa na utaratibu unaweza kukopa advance salali mpaka ya miezi 7 kwa hiyo utakuwa unakatwa kiasi cha pesa kulingana na muda wa mkataba mtakavyokubalina. Mimi nikashangaa, mkopo tena imekuwaje mbona mimi sijataka huo mkopo. Ndio yule meneja kunipa taarifa kwamba Bwana Big amejaza fomu za advance salary na kutaka mkopo wa miezi saba. Akaendelea kusema kwamba alipomwelekeza kwamba ni amalize probation bwana Big akawa anaforce kama vipi tupewe maana hata mimi nina shida na hela so nimemtanguliza yeye akajaribu.

Nikaona duu hii sasa soo. Kwa hiyo meneja ndio ananiuliza kama na mimi nataka au laa. Nikafikiri hapa Big ashaniingiza kwenye mambo yake bila ridhaa yangu lakini pia nikimtosa mooja kwa moja inaweza ikamjengea picha mbaya Big kwa yule meneja. Basi nikasema tuu ni kweli tulidiscuss pamoja na Big maana ni kipengere ambacho kipo kwenye mkataba na nilikubaliana na Big tukipata muda tufatilia so mimi bado sikupata muda muda wa kufatilia, ila kwa maelekezo hayo basi inabidi tusubiri. Yaani nilitoa sababu ya kijinga mpaka yule meneja kuna siku aliniambia kwa utani tulipozoeana kwamba siku zile alicheka sana kwani alijua fika Big kanichomekea. Kwenye hilo niliipenda ile spirit ya Big ya kuzitumia fursa vyenye vyedi.

Ila sasa bwana Big kuna mambo alikuwa anayaendea pupa sana mpaka kuna washkaji wengine pale ofsini wenye mapenzi mema walimtonya apunguze spidi ila akawa mjuaji. Sasa unajua sehemu yoyote ile kwenye michongo michongo watu wanakuwa makini hususani kwa newcomers kujaribu kuwasoma kama mnasomeka ama vipi. Basi zali la kusomeka likamdondokea bwana Big. Wataalamu wa zile kazi wakaona Big hana noma hata akielekezwa mchongo anasomeka. Mimi nikawa sisomeki yaani watu kama hawanielewi elewi hivi. Sijui niite ubaya au uzuri mimi nilijipa muda kwanza wa kuwasoma watu kabla watu hawajanisoma. Kwa hiyo mara nyingi nilikuwa msikilzaji sana na muongeaji kidogo hususani kwenye maswala ya kazi. Sikutaka kuanza kujichanganya kutoka weekend na washkaji wa pale ofisini kwa sababu zangu maalum.

Big alikuwa lesi sana unaambiwa kala hata probation haijaisha big ameshavuta usafiri.Nakumbuka mimi alinishirikisha ile plan yake ya kununua mkoko ila nikamwambia ndugu sikilizia kwanza ujue hapa hata ulikuwa na umedunduliza vijisenti vyako huko itakuwa ngumu watu kuelewa watakuweka kwenye kundi la wapigaji. Big akaniambia yeye anajua anachofanya. Nikamwambia hii italeta shida si unakumbuka ile ishu ya kulazimisha mkpo kule kwa meneja utawala anaweza akajiuliza pesa umepata wapi wakati mkopo hakuidhinisha. Big akaniambia nisijali kuhusu hizo mambo yeye amejipanga. Bai akavuta ile ndinga ilikuwa ni moja ya nding zinazokula sana wese ila ndio ilikuwa habari ya mjini kwa majanki wa enzi zile.

Big hana baya ile ndinga ilivotoka tu bandarini siku hiyo hiyo alikuja nayo ofsini na kila mtu huko parking alioneshwa. Mjengo mzima ukajua leo there is a new father car in town. Nyie si mmezo father house, sasa kuna father car ndio sisi tunaosema kujenga sijengi maana sijawahi kulala nje ila nimetembea sana kwa miguu na kuloana wacha ninunue gari. Kuna jamaa mmoja nae alikuwa ni mmoja wa washkaji wa Big ila yeye alikuwa pale mda mrefu akawa anampa madini sana Big namna ya kuyaendea mambo ofsini, ila Big akataka hadi kuvunja urafiki kwa kuona kuwa jamaa ameanza kumwangia.

Basi maisha yakaendelea pale job kama kawaida. Nakumbuka tulikuwa tumebakiza kama wiki mbili hivi kumaliza probation mimi na Big tulienda kwenye training Nairobi ya wiki tatu ili tukitoka uko tuwe tumekwiva kwa ajili kupiga mzigo kama full employees. Sasa tukiwa kule kwenye training Big akatumiwa email na line meneja wetu inatakiwa arudi ofisini mara moja. Akaniuliza kama na mimi nimetumiwa nikamwabia sijatumiwa. Sasa tukawa hatuelewi pale ni nini kinaendelea. Akili yangu mimi ikawaza labda ni matatizo ya kifamilia labda msiba unaomuhusu sana so wanaoshindwa kumwambia. Hii ikaingia hata kwenye akili ya big huenda kweli kuna tatizo la kifamilia. Akawacheki ndg zake hakuna taarifa yoyote. Siku ya pili asubuhi akapigiwa simu kutoka ofisini kwamba inabidi arudi faster. Tukachanganyikiwa sana pale, basi ikabidi jamaa abadili ticket apande mwewe arudi dar ofsini akisisitizwa akishuka eapoti hasiende hata nyumba aunganishe job.

Kufika ofsini bhana amefikia kwenye kikao chamenejiment. Kiufuoi jamaa yangu Big aliingia kwenye harakati za panya pale ofsini kwa speed sana. Alisomewa mashtaka yake na ushahidi wa kutosha kuhusu harakati za panya mpaka simu zilizorekodiwa na wadau wakipanga mambo yao. Jamaa yangu wakampiga on the sport na kuambiwa kama anahisi ameonewa anaweza kwenda mahamani ila kwa kumuhurumia mambo yasiwe na kuepukwa kufungwa achukue vyake asepe. Huo ndio ukawa mwisho wa mshkaji wangu sana Big.

Anyway weekend hii wakubwa wangu tunafanyeje? Mana kutwa nasikiliza vipindi vya redio tuu home mpaka masikio yataka kutoboka. Na watangazaji wanakera sana maana kutwa kututangazi tu kwamba huu ni mwezi wa matumizi na sherehe kwahiyo watu watumie pesa. Nyie wenzangu mnatumia wapi pesa zetu, basi mtu mmoja ajitokeze anipe mwaliko wa kushangilia pamoja Mnyama akimuua wydad kwake.​

Episode 7 #254
Dah, Big hakumsikiliza Big mwenzie kwenye 10 crack commandments;

never let no one know, how much dough you hold.
 
Mkuu habari...hawa jamaa Danish refugee council nimeona wanataka grants mgmt officer. Unaweza apply hapo

emoji1241.png
Grants Management Officer Job Vacancy at Danish Refugee Council (DRC)


Mkuu habari...hawa jamaa Danish refugee council nimeona wanataka grants mgmt officer. Unaweza apply hapo

[emoji1241] Grants Management Officer Job Vacancy at Danish Refugee Council (DRC)

Thank you chifu. Hii ngoja nikimbizane nayo sasa hivi
 
Mkuu Tai Dume, kwa kweli uzi wako una somo zuri sana kuhusu skills na experience unazo pata kazini ukiwa mtu wa kujituma.
Tungependa kujua kidogo ni misaada ya namna gani hasa mlikua mnatoa kwa hao wastahiki.
Pia nimeona kua kwenye hizi NGO pia sehemu kubwa ya pesa zinakwenda kwenye gharama za idara na kidogo zinawafikia walengwa.
Kutafuta success stories ni moja ya njia ya secure kazi za hao watumishi wa NGOs wakiwa local au wakitoka huko ugenini wote wako desperate kuhakikisha wafadhili wana endelea kuto pesa.
Mkuu Percival asante kwa kuona kuna kitu unaweza kuokota kwennye huu uzi.

Nikirudi kwenye maswali yako,
1. Hilo shirika halitoi misaada bali linatoa fedha kama ruzuku kwa NGOs nyingine baada ya kuleta proposals za kutekeleza miradi (projects) mbalimbali hususani za kusimamia utekelezaji wa sera na sekta mbali mbali kwenye level ya halmashauri, mfano Afya, maji, elimu nk. Lakini pia kuna miradi ya kudai au kusimamia upatikanaji wa haki za makundi mbali mbali kama wanawake, watoto, walemavu, wazee, vijana nk.

2. Mgawanyo wa fedha zilizokuwa zinaigia pale ofsini ulikuwa ni 30% kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi kama vile mishahara, ununuzi wa assests za ofisi n.k.

3. Kwenye kutekeleza miradi kama niliyoitaja hapo juu success stories na case studies for best practices ni muhimu sana. Ni moja ya uthibitisho kwamba fedha zilizopelekewa kwa wadau zimetumika kadili ilivyopangwa na zimeleta matokeo chanya. Kumbuka shirika likipewa fedha za ruzuku hawazirudishi fedha kwa riba au zinapokelewa tu kama msaada, bali wanatakiwa kulipa matokeo chanya.

Nafikiri nimekujibu.
 
Back
Top Bottom