Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

EPISODE 14: Unajali sana kuhusu muonekano mzuri kazini? Jiangalie upya

Muda ulipowadia nilianza kazi kwenye lile shirika la wazungu baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu. Asikuambie mtu kufanya kazi kwenye haya mashirika international kuna vetting kubwa sana ambazo new employee unafanyiwa ili kujiridhisha na uhali wa vibali vya wewe kufanya kazi nchini ikiwemo maswala ya criminal records, nakumbuka ilibidi mpaka kupata police report, wenyewe wanaita background and reference check.

Nakumbuka siku ya kwanza kufika pale kazini nilipokelewa vizuri tu nikatambulishwa pale kisha nikaonyeshwa ofisi ambapo ndio nitakkuwa nafanyia kazi zangu. Kisha nikapewa utaratibu pale wa mambo muhimu ya pale ofisini kama vile muda wa kula nk. Then nikapatiwa baadhi ya document nizisome huku nikiambiwa kwamba kesho yake nitaanza orientation walau ya siku mbili ili kujua shughuli mbali mbali za pale ofsini. Kweli siku ya pili yake nikafanya skype meeting na makao makuu ulaya na Nairobi. Then zikaendelea orientation za pale ndani ofsini, kwa kweli hizi orientation zinasaidia na inatakiwa uzitumie vizuri kuuliza maswali. Hapa niseme hivi proffesionally, asking questions to your supervisors or coleagues helps in Building Relationships. What I mean is, asking questions demonstrate your interest in the job and a commitment to understanding the company's culture and processes. It also provides an opportunity to build a positive working relationship with your supervisor, as they see you as engaged and eager to contribute. Proactively seeking information through critical questions shows that you are proactive and take initiative. This can leave a positive impression on your supervisors or coleagues signaling that you are committed to your role and willing to go the extra mile.

Hata kwa watu ambao mnaitwa kwenye interview ya kazi yoyote jitahidi usitoke bila kuuliza swali. Kwa uzoefu wangu wa kufanya interview mbalimbali za kazi kunai le nafasi inatolewa kwa job applicant kuuliza maswali kama yapo. Sasa ile nafasi inatakiwa uitumie vizuri sana kwa kuuliza maswali hususani yanayohusiana na nafasi husika unayoomba au kuhusu kampuni/shirika unalotarajia kuajiriwa nalo. Asking insightful questions leave a positive impression on the panelists. This demonstrates that you are not only interested in the position but you are also thoughtful and strategic in your approach. It indicates your genuine curiosity about the company's operations, work culture, and future direction. Hapo utakuwa umejitengenezea nafasi nzuri yaw ewe kuonekana wa tofauti na kuwa na nafasi kubwa ya kuwin hiyo job, unaona kazi hiyo? Sio tu unaishia kusema “I don’t have any question for now”, utafeli. Jitutumue uulize maswali kama “Can you describe the company culture and how employees collaborate here?” Au hata “What opportunities are there for professional development and growth within the company?” Shauri yako. Such question demonstrates your long-term commitment and ambition. It shows that you are not just looking for a job but you are also interested in building a career within the company.

Turudi kwenye point yetu ya leo maana hayo mengine hapo juu yameingilia tuu mada. Basi nikamaliza wiki pale na kila kitu kikaenda sawa. Lakini kitu kimoja nikanote kwamba asee mimi pale ofisini ndio nilikuwa more than formal, yaani nilikuwa napiga dress code zile za kiexecutive kwa wiki ile tuu nilibadili suti kama mbili. Wengine walikuwa wanadress very casual kwa wanaume ila wanawake walau wengi wao walikuwa ni smart casual. Country representative ni mdingi wa kizungu alikuwa amesafiri wakati mimi nafanyiwa orientation japo niliweza kuskype nae, siku alipoingia ofisini nilishangaa sana kwani jamaa alikuwa amepiga kinjunga kimoja matata sana. Ndio amekuja ofisini ivo halafu ndio top pale. Basi jamaa alikuwa anapita kwa kila staff anagawa vichoclate kama zawadi na kinjunga chake hana habari. Mimi ukiangalia hapo nimepiga suti kasoro tai halafu nipo level za kawaida tuu.

Nikajiuliza hii inakuwaje. Jamaa ambaye nilikuwa nashea nae ofisi moja yeye alikuwa ni mtu wa kupiga jinzi sana sio jumatatu sio ijumaa. Mimi kote nilikokuwa nimepita pita before, jinzi ilikuwa labda ijumaa, ila nikanotes jamaa anazigongelea karibia kila siku. Kuna bro mwingine yeye alikuwa anapenda kupiga track au pensi za kuvuka magoti. Kiufupi pale swala la dress code sijui kuchomekea, suti, sijui nguo gani haikuwa ishu kabisa wewe jisitiri vyovyote unakvyoweza ili mradi usije uchi. Wadada kupiga vipedo ilikuwa ni jambo la kawaida sana. Kuna jamaa mmoja alikuwa anabeba vyuma so alikuwa na mwili mkubwa na mitatuu sana basi jamaa alikuwa anapenda sana kuvaa singlendi nadhani ili tuone mitatuu yake vizuri. Kuna kidada kimoja kilikuwa kibalck byuti hivi, kile kidada nadhani kilikuwa kimepitiliza maana alikuwa anajiachia na vinguo vifupi sana na alikuwa anavaa vipini vya ulimi, pua na kwenye nyusi kwa kweli mimi nilikuwa namuona kituko kwa kweli hahahaa. Si mnakumbuka stori ya rasi yule aliyenipa mchongo? Basi pale ofsini nilimkuta mwingine yeye ndio na mirasta mirefu mpaka mgongoni.

Kiufupi hakuna aliyekuwa anafatilia swala la mavazi na wala haikuwa kesi, kila mtu alivaa kulingana na anavyojiskia ili mradi huvunji sheria za nchi. Kwaupande wangu kwa kweli niliona vitu tofauti sana kwanza nilizoea kwamba ni kawaida kwa mabosi wa ofisi kunyuka suti au pamba za gharama sana. Madada wakitokelezea sketi au wenyewe mnaita suruali za ofisi zile za vitambaa. Lakini pale mambo yalikwa valuvalu. Ikabidi na mimi nianze kujisthukia pale kwanza kuvaa suti au kuchomekea sio hobi yangu, nilikuwa nalazimisha tuu kwa sababu ya mazingira niliyopitapita ya kazi. Kwanza nakumbuka nilipokuwa shule hususani primary na sekondari nilikuwa napewa adhabu mara nyingi sababu ya kutochomekea shati.

Ikapidi na mimi niadapt fasta utaratibu wa pale, nikajifanyia tathmini kwenye kabati langu la nguo nikaona nina upungufu mkubwa sana wa nguzo za ofisini kwa wakati huo. Weekend moja nikaenda kufanya manunuzi ya nguo za ofisi. Guess what! Nilinunua pensi cardet na jinzi za kutosha pamoja na Tshirts nyingi nyingi tuu mpaka nilipoona nimedhika. Nikasema sasa nimekamilika maana nilipanga kwa asilimia kubwa niwe napiga zangu pensi maana kiukweli ndio vazi ninaloplienda sana. Kiukweli napenda sana kuvaa pensi sijali hivi vimiguu vispoku kama vya diamond, hahaha pensi kwangu mimi ni is favorite cloth. Kwanza hata katika maisha ya kawaida ni nadra sana kunikuta weekend nimetoka nikiwa nivaa suruali asee labda sijui iwe ishu gani. Hata wakati nafanya kazi kwenye ile ofisi ya kugawa ruzuku ambapo mara kwa mara wafanyakazi tulikuwa tunalazimika kwenda job hadi weekend ilikuwa nava pensi mpaka kupewa jina la mzee wa pensi.

Basi officially na mimi nikawa ni mzee wa kupiga pensi mara nyingi sana pale ofisini isipokuwa kama nitakuwa na kazi za nje ya ofisi kama mikutano au kutoa trainings mbali mbali ndio kidogo nilikuwa natokea smart casual. Yaani hata washkaji wa mtaani baadhi walikuwa wanajua labda nimejiajiri mjini maana ilikuwa ukoniona naenda zangu job nimekula pensi yangu, tshirt na begi langu unaweza sema naenda kuuza mitumba kariakoo. Hayo ndio yalikuwa maisha mapya ya kazi.

Ila nikaja kugundua kitu kimoja, wafanyakazi wa pale walikuwa very oraganized and very punctual kwenye muda when it comes to accomplishing their tasks. Yaani wale wafanyakazi walikuwa wamejijenge utaratibu ambapo kama mmekubaliana kitu ni lazima kifanyike kwa wakati. Hususani kwenye swala muda walikuwa very pancyual. Yaani ugomvi mkubwa na boss pale ulikuwa ni kwenye kutozingatia muda. Ni bora uharibu kazi boss anaweza akakuelewa lakini sio kuchelewa kwenye swala la muda. Yaani pale ukifika na uswahili wako kikao kinaanza saa tatu wewe unakuja saa tatu na nusu asee utaleta tafrani kubwa na wafanyakazi wa pale hususani boss. Pale ilikuwa mpaka kufikia saa mbili kila mtu ameshafika job labda uwe na dharura kwelikweli. Hakuna cha kusema sijui foleni ama nini, kama ni fole toka kwako saa 9 usiku ilimradi saa mbili ikukute umeshasaini na umeanza kupiga kupiga mzigo.

Pale ofisini kama nilivosema hakuna mtu atakaekufuatilia umevaa nini. Wale jamaa I salute them pamoja na kuonekana hawako serious kwenye mavazi lakini walikuwa vicha sana. In long run baada ya kama miezi miwili hivi nikagundua kwamba ili ukubalike pale na wakuindorse kama mfanyakazi baada ya probation period you were required to have a set of personal qualities including Professionalism & Integrity, Adaptability & Innovation as well as Teamwork & Collaboration. Kwa uzoefu nilioupata pale, in summary, these three sets of qualities contribute synergistically to a company's overall development. Professionalism and integrity build trust, adaptability and innovation ensure the company stays relevant in a changing setting, and teamwork and collaboration maximize the collective potential of the workforce. Together, these attributes create a foundation for sustained growth and success.

Kingine kilichonishangaza pale ofisini ni kwamba most of the employers hat boss hawakuwa na elimu za kutisha sana. Pale sana sana kulikuwa na degree hoders na hata dipoma zilikuwepo pia. Mwanzoni nilikuwa najua mashirika kama yale ya kimataifa yanaajiri PhD holders na labda kwa uchache ni masters. Lakini ni tofauti sana, Nyie wenye PhD na masters zenu mara nyingi mnachukuliwa kwenye short term consultation tasks kama outsourcing. I came to realize that, most of international organizations often prioritize what candidates can contribute to the organization over academic grades. Kwaufupi, while academic achievement is certainly important, international organizations focus on a broader set of criteria to ensure that candidates have the practical skills, experiences, and qualities necessary to thrive in the complex and diverse environments in which they operate. Hata katika utafutaji wao wa wafanyakazi mara nyingi unaweza ukajikuta unapitia hatua zaidi ya mbili za interview na interview zao mara byingi zinakuwa ni kuassess skills set, innovation na problem solving skills.

Nimewapata hiyo introduction fupi ili nikirudi kwenye next episodes niweze kushea nanyi mengine makubwa niliyojifunza kwa muda ambao nilifanya kazi na lile shirika la kimataifa. Kifupi wenzetu hawaangalii sana muonekano wako wan je but what yo provide to the organization.

See you.​

Muendelezo soma Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa
 
EPISODE 11: Nilijifunza kuacha kuwahurumia kabisa watu wenye ulemavu

Hii experience najua itawashangaza wengi au labda watu kutokunielewa kabisa. Kabla ya kujifunza kwamba sipaswi kabisa kuwahurumia watu wenye ulemavu namimi pia nilikuwa ni mmoja wa watu katika kundi ambalo nawaonea huruma sana watu wenye ulemavu.

Kikawaida nilikuwa nikiona au nikikutana na mtu mwenye ulemavu wowote kama vile wasioona, wanaotambaa, wenye magongo, viziwi au hata albino nilikuwa nawahurumia sana Nilikuwa nafikiria ni watu wenye shida sana na wanahitaji kuhurumiwa na kupewa misaada hivyo nilikuwa najitoa sana hasa hasa kwa wale ombaomba wa barabarani. Nakumbuka kuna omba omba alikuwa anatega kituo ambacho mimi ndio ilikuwa nashukia au napita kwenda na kurudi kwenye mihangaiko yangu, yule jamaa alikuwa anatembelea mikono (ni kama anatambaa vile) basi nilikuwa mara kwa mara namsapoti na kiasi kidogo cha pesa mpaka akanizoea yule mlemavu.

Yaani ilikuwa hawa omba omba wa wenye ulemavu mitaani hususani wanawake nilikuwa mara nyingi sana nawapa vijisenti kidogo maana nilikuwa nawahurumia sana. Hali hii iliendelea kunitawala sana na ilifikia hatua kama nikipata nafasi ya kuongea na mtu mwenye ulemavu basi ilikuwa ni yale maongezi ya kumpa moyo yaliyotawaliwa na majonzi. Yaani niliona hawa walemavu ni kama vile wanahitaji kufarijiwa kila mara na kama Mungu anawatumia kutukumbusha wengine ukuu wake.

Sasa bhana baada ya kuona kule serikalini hakuna tena dalili ya kurejeshwa job (maana niliachishwa kazi kabla sijaanza kuifanya hahaha) nikajikita kwenye kutafuta mchongo mwingine ili maisha yasije kunipiga mjini hapa. Huku na huku nifanikiwa kupata kazi kwenye shirika moja ambalo lenyewe lilikuwa linadili na maswala ya kuwainua watu wenye ulemavu na mambo mengine yanayohusiana na haki zao.

Pale niliajiriwa kama Program advocacy coordinator hivo ilikuwa ni managerial position ambacho kwenye idara yangu nilikuwa na staff kama wanne hivi ambao walikuwa wanareport kwangu direct, na pia nilikuwa naingia kwenye vikao vya menejimenti, hapa nilipanda ngazi katika career yangu. Sasa kwenye organization unadili moja kwa moja na watu wenye ulemavu ambapo wengi tulikuwa nao pale ofsini kama staff wenzangu nawengine walikuwa ni wanufaika wa program mbali mbali za pale ofsini.

Kama ilivyokawaida kazi zangu pia zilikuwa zinahusisha sana safari za mikoani katika kutimiza majukumu mbaalimbali ya program za pale ofisini. Basi ilikuwa katika zangu watu ambao na-engage naokwa asilimia kubwa walikuwa ni wenye ulemavu. Ilikuwa nikienda mikoani nakutana na walemavu, nikifanya seminars workshops basin i walemavu, nikialikwa kwenye mikutano basin i walemavu yaani ilikuwa ni walemavu walemavu kila kitu.

Sasa baada kufanya kazi na watu wenye ulemavu tena wa aina tofautitofauti kwa muda mrefu na mimi nikaaza kuwafahamu tabia zao kwa undani, lakini pia niliweza kujifunza mambo mengi sana yanayohusiana na watu wenye ulemavu. Niliweza kuzielewa hisia zao, mitazamo yao, mahitaji yao na mikakati mbali mbali ambao walikuwa nayo kibinafsi, kisera au kiprogamu yenye lengo la kutetea haki zao na kuwainua kujikwamua na hali ngumu za maisha.

Kwanza kabisa nikaja kugundua kumbe hawa jamaa ni binadamu kama binadamu wengine despite their disabilities. Kwamba mapungufu yao ya kimwili au kiakili hayawafanyi wasiwe na hisia, matamanio au mipango katika maisha yao ya kila kitu. Kikubwa sana katika hilo nikaja kuelewa kwamba watu wenye ulemavu hawataki kabisa kuonewa huruma. Yaani vile nilivyokuwa nikiwachukulia kama watu wenye kuonewa huruma na kuongea nao kwa lugha flani hivi ya kuwasikitia hicho wenyewe walikuwa hawaki kabisa.

Nakumbuka wakati naanza kufanya kazi pale ilikuwa kila kitu nafanya kwa kuwapendelea watu wenye ulemavu. Mathalani kwenye mikutano kwa kuwa mimi ndio nilikuwa organizer na facilitator mkuu basi nikatoa maagizo labda waaanze kwanza kula watu wenye ulemavu, au naweza agiza malipo waanza kulipwa wenye ulemavu, ukiniuliza sababu nakuwa sababu yenye mashiko isipokuwa ni kasumba tuu ya kuona kama wanahitaji zaidi sympathetic treatment. Nakumbuka wengi wao walikuwa hawapendi hizi privilege nilizokuwa nawapa. Nakumbuka kuna siku jamaa wawili wenye ulemavu waliniita chemba na kunichana live kwamba nakosea sana ninavyowapa upendelea wa wazi mambo mengine ambayo hayana athari moja kwa moja napaswa kuwachukulia kwa usawa na watu wengine ambao hawana ulemavu.

Nilishangaa sana inakuwaje mimi nawapa upendeleo halafu wao wanakataa? Basi ikabidi nianze kuwasoma sasa kwa ukaribu zaidi. Nikaja kugundua yafuatayo:

kwanza, Watu wenye ulemavu hawataki kuonewa huruma pasipo sababu za msingi. Kwamba wanataka kama hakuna umuhimu na sababu yoyote ya maana basi wewe wachukulie ni kama watu wengine tuu na sio kama kundi spesho. Mimi nimesafiri nao sana, nimeenda nao sana maeneo ya mitoko na kupitia hayo n imejua tabia zao nyingi sana. Wanapenda kubishana mpira, wanajichanganya kwenye starehe, wanapenda kuabudu na kufanya kazi. Hiyo ni mifano michache tuu niliyoianisha.

Nakumbuka kwenye moja ya safari zangu nilisafiri na jamaa mmoja ambaye yeye alikuwa hana miguu kabisa. Sasa kwenye hizi safari ujue mnakuwa na mda mwingi wa kufanya mambo mengi pamoja kwenye tripp kama vile kula nk. Sasa yule jamaa nikaja gundua ni mtu wa kupenda sana kutoka usiku kwenda kwenye viwanja vya starehe. Sasa siku moja nikasema ngoja nitoke na mshikaji nikampe kampani. Basi tumefanya mambo yetu pale mara jamaa akaopoa demu mmoja mkare sana. Yule manzi alikuwa pisi kwelikweli na jamaa aliondoka naye. Asubuhi nikawa namtania namtani kaka ile pisi hata mimi niliielewa jamaa akacheka sana akaniambia zile ndio pigo zake na anazo nyingi tuu na nikisema tushindane Taidume huwezi kuwin. Ila nilichokuja kugundua jamaa alikuwa ni muhongaji mzuri sana dadeki.

Pili, Watu wenye ulemavu wanakereka sana kuona wenye ulemavu wengine wanavyoomba omba mitaani kwani wanadai wanawadhalilisha. Pale ofsini kulikuwa na program ambazo zilikuwa zinawakutanisha walemavu wanaoomba omba mitaani ambazo zilikuwa zinakuwa na lengo la kuwekana sawa na kupeana mikakati ya kujiinua. Kwenye vile vikao nilikuwa naingia na wale omba omba walikuwa wanatoa shuhuda kwamba wanapata pesa nyingi sana. Akikupigia hesabu sometimes kiwango cha chini mtu anaondoka hata 50k kwa siku. Sasa wakawa wanapeana makavu wenyewe kwa wenyewe kwamba kama mtu umeomba omba kwa mwaka mmoja tu si unakuwa na pesa za kutosha na hata kuwa na uwezo wa kuanzisha biashara ya heshima tuu. Hapo nikaja gundua kwamba wale omba omba wa mitaani wengi wao ile wameishaifanya ni ajira na hawawezi kuacha.

Hii ikanifanya nikumbuke siku moja kipindi cha nyuma wakati nipo nafanya kazi kwenye lile shirika la kugawa ruzuku, nilipita pale Rombo green view shekilango kula ilikuwa ni kama saa saba hivi mchana. Basi wakati nasubiri msosi pale liliingia kundi la omba omba wasioona kama nane wakiwa na wale watoto wanaowaongoza. Basi mimi kwenye akili yangu nikawa nawaza pale leo tumevamiwa ila nikawa nimetenga buku wakipita mezani kwangu pale niwape. Gafla nikaona kuna meza ni kama zilikuwa reserved wakaenda wale ombaomba kukaa na vitoto vyao. Haikuchuka hata dakika 10 nikaona misosi ya maana ya inapekwa kwenye zile meza zao nikama wametoa oda na ndivyo ilivyokuwa. Maana nilipoletewa msosi wangu nilimuuliza yule muhudumu mbona wale ombaomba wameletewa chakula haraka je mnawasaidia kuwapa na misosi. Akanijibu kwamba wale ni wateja wao wakubwa na huwa wanakulaga pale lunch. Nikashangaa sana pale na bei za misosi rombo ya kipindi kile zilikuwa zimesimama. Kwa wale ombaomba sikutegemea kama wangemudu kula pale.

Tatu, Watu wenye ulemavu hawahitaji kuhurumiwa bali kutengenezewa mazingira mazuri yatakayowafanya waweza kujumuika pamoja na raia wengine katika shughuli mbalimbali. Nilikuja kugundua watu wenye ulemavu ni very potential. Wapo wenye vipaji na vipawa vikubwa katika field mbali mbali lakini wengi vipawa vyao wanashindwa kuvionesha na kuwanuifa kwa sababu tuu wengi wetu tumeishia tuu kwenye kuwaonea huruma badala ya kuwatengenezea mazingira wezeshi ili waweze kuonesha uwezo wao. Tena kwenye hili nina idea nzuri sana ya tv program yenye kuhusisha watu wenye ulemavu, ambayo nina uhakika itabamba sana. So kama kuna wadau wa hizo connection tuwasiliane nishee hiyo idea na kama wana uwezo wakaifanyie kazi, mimi sitaki hata kumi hapo – nipo siriasi.

Amini ama usiamini kwamba mazingira wezeshi (accessibility) plays a crucial role in empowering people with disabilities to showcase their talents and contribute to economic empowerment. By removing barriers and creating an inclusive environment, society can tap into the diverse skills and abilities of individuals with disabilities. Kwa kutowekeza katika mazingira wezshi tuapote viongozi wazuri, tunapoteza wafanyabiashara wakubwa, tunapoteza wasanii mahiri kabisa, tunapoteza wasomi wabobevu kisa tu wamezaliwa na ulemavu au kupata ulemavu katika hatua za ukuaji. Sio fair kabisa

Kwahiyo katika maana hiyo nikaachana kabisa na tabia ya kuwaonea huruma watu wenye ulemavu na badala nikajikita kushiriki kikamilifu kutengeneza mazingira ili kuwawezesha kwa nafasi nilizokuwa nazo. Mfano sasa hivi kuna wale watu wanaowatumia watoto wenye ulemavu kuomba omba mitaani. Asee siku hizi nakuwa mkali sana kwanini yule mtoto asikazaniwe kupelekwa shule instead ya kuzungushwa kwenye jua muda wa kusoma. Nimekuwa nikiwakkaripia wengi sana kuachana na tabia hizo na mara nyingi sitoi pesa ila naweza nikamnunulia chakula.

Nakumbuka hata yule mlemavu aliyekuwa anaomba omba pale kituo cha daladala mtaani kwangu kuna siku moja nikaongea nae na kumshauri kwavile lile eneo analokaa pale kituoni kumechangamka sana nikamwambia aanzish biashara yoyote. Akadai nimpe mtaji, nikamchana live kwamba nikimpa mtaji mimi au mtu mwingine hawezi kuwa na uchungu na biashar. Nikamwambia wewe anzisha biashara yoyote hata kuuza pipi mimi nitakuwa mmoja wa wateja wako na nitakuletea wateja. Ikawa kila nikipita namkomalia ishu ya biashara. Kuna kipindi nikawa nimesfairi kama wiki hivi. Nilivyorudi nikakuta ameanzisha biashara ya kuuza maji ya kandoro anauzia kwenye ndoo. Huwezi amini alipata wateja wengi sana hususani madereva na makonda wa daladala. Hapo usiniulize kama nilikuwa nanunua ama sinunui ila nakumbuka nilimfanyia mpango nikamuunganisha na jamaa yangu mmoja alikuwa anafanya kazi tigo wakampa mwamvuli na benchi. Nilihama ile mitaa lakini naamini aliiendeleza na kukuza biashara yake.

Kabla sijamaliza hii episode ngoja niwapeni shule ndogo. Tunatakiwa sana kuheshimu utu wa mtu mwenye ulemavu. Watu wengi sana wanawadhalilisha watu wenye ulemavu bila kujua kupitia au kutokana na majina tunayowaita mitaani kila siku. Ni kawaida sana kusikia mtu akimwita mtu mwenye ulemavu kipofu, kiwete, kilema, asiyesikia, zeruzeru nk. Ndugu zangu haya ni baadhi tuu ya majina yanayotweza utu wa mtu mwenye ulemavu.​
  • Usahihi upo hivi, kwanza unapotaka kutaja majina ya walemavu anzia na neno “mtu” au “watu”.​
  • Mfano,​
  • Mtu asiyeona badala ya kipofu. Ukiita kipofu wenyewe hawataki watakupiga na zile fimbo zao.​
  • Mtu mwenye ulemavu wa viungo/miguu badala ya kiwete. Ukiita kiwete wenyewe wanakuwa wakali kweli kweli.​
  • Mtu kiziwi badala ya asiyesikia. Ukiita asiyesikia wanasema wao sio watukutu maana mitoto mitukutu ndio huwa haisikii.​
  • Mtu mwenye ualbino badala ya zeruzeru.​
  • Mtu mwenye ulemavu badala ya kilema/vilema.​
Nadhani nimetoa shule kidogo hapo. See you next episode hakutakuwa na arosto jamani.​
Usipo kuwa na pesa.. unakua na hasira za haraka sanaa..
 
Umeanza mambo ya UMUGHAKA .
Intro ya nini kaka? Huu muda ungeshusha tu story. Na pia unachanganya sana lugha. Nadhani bora chapa kiswaz tu au twende ngeli tu.
Apo kwenye ngeli hapana Mkuu nibora muende huko Telegram [emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mimi siwezi kucopy na kupest kule online dictionary English to Swahili
 
Back
Top Bottom