Mambo muhimu ya kufanya pindi tu unapopokea taarifa za msiba wa mzazi wako au ndugu yako wa karibu

Hakika Mungu alikuongoza katika hilo. Ki ukweli pamoja na kwamba kufiwa kuna umma, lakini kuwa mstahamilivu na jasiri katika kupokea taarifa za kutisha namna hii humsaidia mtu kupata muda wa kufanya maombi fulan ambayo baadae huwa na msaada mkubwa kwa muombaji.
 
Hahaha huu nao ni ushauri mzuri wa kuzingatia. Ubarikiwe sana mkuu kwa ushauri ulioshiba.
 
Kweli mkuu, kwanza nafikiri imani zote zinashauri mtu kufanya ibada mwenyewe akiwa hai, kuliko kutegemea kuombewa baada ya kifo.

Ndio maana hata waislam wanasisitiza mtu uswali kabla haujaswaliwa. Lakini pia hii haiondoi ile nafasi ya kumuomba Mungu amsamehe marehemu madhambi yake nk. Maana hatuwezi kujua pengine Mungu ataweza kutumia maombi ya waombaji wema kumsamehe marehemu.

So hiyo namba 4 ni moja kati ya njia ya kumfariji mfiwa. Kwani hakuna mtu ambae hupenda kuona ndugu yake anaenda mahali pabaya huko mbinguni.
Japo mtu anaweza kujua kwamba baba yake, mama yake, mke au mume wake alikuwa haendi kanisani wala msikitini lkn akifanya maombi huhisi faraja kwamba anakuwa amemsaidia ndugu yake kuepukana na adhabu ya Mungu huko alipokwenda.
 
Kiuhalisia ukifiwa haya mambo hayapo
Inategemea mtu na mtu. Ya kwa wengine obvious inaweza kuwa ngumu kwa muda ule anaopewa taarifa kutokana na uzito wa msiba. Lkn baada ya kutulia kama dakika 5 hivi akili kidogo inarudi mahala pake na muhusika anaanza kufanya haya niliyoyaandika. Soma comment namb #18 utaelewa mkuu.
 
Leo nimemkumbuka baba yangu hadi chozi kukaribia kunitoka alafu nakutana na mada kama hii.

Uchungu wa kufiwa unatofautiana ndugu, na mbinu za kumfariji mfiwa pia haziwezi kuwa sawa
Ya ni kweli kabisa mkuu, ila inategemea mtu na mtu.
 
Nakataa kukubaliana na ww moja kwa moja japo umeshauri vtu vya msingi,ndugu kumbuka tone ya msiba hubadilika kulingana na mambo yanavoendelea Mara tu baada ya kupokea taarifa,kwnz Ni taarifa mbaya ambazo huwez kuzibadili ili walau ziwe Ni jokes,waweza yazingatia hayo uloyashauri ila ikafika mda wa kuaga Mara ya mwisho tone ikabadilika akili zinakuja kurud unajikuta wodini,au Ile umejitahd kuicontrol mood ila wafiwa wenzio wakakuaminisha through body language kuwa wanaumia Sana Sana,pengine Ni wadogo zako au mama yako/baba yako napo mood ikakudrive harshly,kumbuka hayo yote huja mfiwa akiwa kwny hali mbaya Sana mentally and emotionally,hapa ndipo nyimbo za faraja na maneno mazuri mtu huhisi km ana kupigiwa kelele flan hv,acha tuuu,RIP daddy
 
Kufuata hayo mambo ukifiwa??
Labda msiba tu msiba
Sio msiba unaohusu damu yako
Ila pia watu tunatofautiana moyo na viwango vya mqpenzi
 
Ni kweli mkuu kuondokewa kuna uma, na hata mimi yalinikuta mwaka mmoja tu uliyopita tena nikiwa nje ya nchi. Kama hautojali sogea kidogo hapo juu kwenye post namb #18 nimeeleza hali ilivyokuwa.

Hakika ni uchungu lkn kuna njia ukikumbuka kuzitumia za kumtegemea Mungu kwa kile kilichotokea, basi Mungu huyo huyo atakusaidia kukupa faraja fulan ambayo hakuna mtu yeyote atakaeweza kukupa.

RIP kwa wazazi wetu wote waliotangulia mbele ya haki.
 
Wewe kariri tu kifo ni tukio la kawaida la asili. Hakuna anaeishi milele.
Mkuu hata ukariri vipi hili swala moja wapo likikufika, ukariri wako utakutoka kwa muda. Yani angalau baada ya dakika kadhaa ndo akili itakaa sawa na kukupa uhalisia kwamba kweli kufa kupo na wote tutakufa.
 
Kufuata hayo mambo ukifiwa??
Labda msiba tu msiba
Sio msiba unaohusu damu yako
Ila pia watu tunatofautiana moyo na viwango vya mqpenzi
Yah ni kweli inategemea mtu na mtu, lkn pia ni neema fulan kama ukiwa unapenda kumuomba Mungu akuongoze kwenye hayo pindi tu unapopokea habari ya msiba wa mtu wako wa karibu.
 
Hapo kwenye namba 4 huwa ni faraja tu za huku duniani kuwekana sawa kisaikolojia, hakuna kitu utafanya kumshawishi Mungu mtu akishamaliza safari yake!
Soma Ebr 9:27
 
Hapo kwenye namba 4 huwa ni faraja tu za huku duniani kuwekana sawa kisaikolojia, hakuna kitu utafanya kumshawishi Mungu mtu akishamaliza safari yake!
Soma Ebr 9:27
Yah ni kweli kabisa, ila si kuna ile kufarijiana kama ulivyosema mkuu.
 
Huu ushauli ni mzuli japo ni mgumu kuutekeleza pindi unapoletewa taarifa ya msiba wa mtu wako wa karibu
 
Huu ushauli ni mzuli japo ni mgumu kuutekeleza pindi unapoletewa taarifa ya msiba wa mtu wako wa karibu
Ndo mana tukasema inategemea na mtu. Ila ukiwa unamuomba Mungu kwamba siku likitokea tukio la aina hiyo akuongoze katika haya manne, basi uwezekano wa kuyafanya kupitia Mungu upo.
 
Jambo la 4..tumia muda mwingi kumuombea marehemu(hili suala limekaa kiimani sana)
 
Hili suala limekaa kiimani sana Kumuombea marehemu apumzike salama..hii naona haina mantiki yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…