Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

ASANTE SANAAAAAAA 🤝
 
Mimi niko mwenyewe. Nataka nisajili kampuni kama main shareholder. Sema nataka iwe limited liability. Inawezekana?
 
Kwa sheria zetu limited company must have at least two shareholder unaweza kuwa main shareholder sema unaweza kuwa hata na 95% ila huyo wa pili atakuwa na asilimia 5%. Na director lazima wawe atleast wawili

Mimi niko mwenyewe. Nataka nisajili kampuni kama main shareholder. Sema nataka iwe limited liability. Inawezekana?
 
Kwenye hili eneo elimu kweli inahitajika na ni kila siku hongera kwa kutuelimisha na shukrani kwa kazi nzuri
 
Kwa sasa unaweza kuorodhesha mpaka kazi 40 ambazo zinaweza kufanywa na kampuni. Ila angalizo usifanye biashara yoyote ambayo huwezi kusimamia kwa karibu maana ndio chanzo cha biashara nyingi kufeli kuwa na mfumo mzuri wa kutambua kitu kinavyoingia na kutoka katika biashara yako unaweza kuwa na vitabu, mifumo ya kielectroniki yaani software zinazoweza kukuonyesha manunuzi, mauzo na stock. Biashara ambazo unaweza kuongeza kwenye list yako kwa mtaaji huo kama unasehemu nzuri kidogo nafikiri ni biashara ya uwakala wa Bima, Uwakala wa makampuni makubwa ya bidhaa ya vyakula (mfano Maziwa Asasim, Tanga fresh) uwakala katika taasisi za fedha kale kamashine mfano ka CRDB kana vitu vingi ndani yake yaani unalipa malipo yote yaliyopo, bado unaweza kuwawekea watu fedha zao unapata commission mtu hapa hawezi kukuibia.
Wadau wanaweza kujazia nyingine hapo

 
Sasa toka tunahimizana toka January sasa tumefika June hiyo ambapo ni mwisho wa kupeleka hesabu za mwaka 2018. Najua tuna hulka ya kupeleka haya mambo siku za mwisho embu tujitahidi kufanya michakato hii mapema zaidi ili tuweze kutimiza malengo. Muda wa kufunga hesabu umefika
 
mkuu mie nahitaji kufungua Group of Companies naomba unipe moja mbili tatu kulingana na uzoefu wako
 
Mkuu kwanza nikushukur sana kwa kutoa hili darasa at least nimepata mwangaza.
Sasa kuna maswali mengi nahitaj kujua.
Je naweza kufanya kazi za kitaalam/contractor na kuchukua tenda kwa kutumia Sole proprietor au partnership company?Je na zenyewe zipo kisheria?
 
Mkuu Asante kwa darasa lako muhimu.
Je kwa sisi ambao hatuna kampuni na wala hatujawah kupata tenda yoyote lakini tunahitaji kuanzisha kampuni for future,unatushauri vipi?
 
Karibu uzoefu wangu hapo sio mkubwa kihivyo ila ambayo nimewahi kufanya ni ambapo mtu anafungua business names ambazo zinakuwa 100% owned by company limited.
Nyingine hii sasa ni ya kishule shule ambapo hiyo kampuni moja inamilki zaidi ya asilimi 66% nayo inakuwa parent kampuni. Au unafungua makampuni mengi yenye share holder wale wale ila yote unatengeneza mahesabu moja as a group of companies. na maswala ya kodi inakuwa moja.


mkuu mie nahitaji kufungua Group of Companies naomba unipe moja mbili tatu kulingana na uzoefu wako
 
Hii inawezekana ila risk ni kubwa mno kama unataka kufanya biashara ya contractor ndio maana watu wanaona ni vyema kuwa na kampuni. Kwa sababu ukiwa sole proprietor au Partnership liabilty haina ukomo yaani inaingia mpaka kwenye mali zako binafsi. Ndio maana watu wanaanzisha limited company ambapo liability zitaishia au ziko limited kwenye mali za kampuni na sivyo vinginevyo. Sasa fikiri umefanya kosa ambalo limesababisha hasara umeshitakiwa ukiwa na kampuni mali za kampuni tu ndio ukomo wakufidia hilo ila ukiwa na hiyo partnership au sole propriator tutaenda kwanza kwa mali zake zikiisha tutakuja mali binafsi mpaka zote ziishe hazijatosha tunaendelea kukudai tuu mpaka kieleweke. Naamini nimeelezea vyema kama bado hujanipata maswali zaidi yanakaribishwa


 
Dah mkuu umenisaidia kunifungua masikio Sasa hapo nimepata mwangaza mzuri sana kuhusu kampuni.
 
Mkuu asante kwa elimu as nikiwa kama kijana nakaribia kufungua carwash ambayo nimepiga cost so far inaweza kurange mtaji kwenye mili5 mpaka 7 natamani sna niiendeshe iwe chini ya kampuni je inawezekana?na bora kipi kuanza kwa kusajili busnes name au kufungua kampuni iendeshwe chini ya kampuni?Thanks in advance
 
Kampuni inaweza kufuguliwa hata na mtaji wa elfu 20. Ila kwa sababu ya compliance costs mbalimbali ningekushauri uanze na business name ujijenge kidogo mambo yakikaa vizuri fungua kampuni. Maana ukifikiria hiyo ulipe Final account preparation na Audit inaweza kuwa 1.2m. Moja ya kanuni ya kukua ni anza mdogo fikiria makubwa hatimaye utafika huko. Ndio maana mtoto humchukua miezi tisa kukua lakini akizaliwa hakimbii hapo hapo anachukua muda. Isome biashara yako ielewe ikuze.

 
Thanks mkuu nashukuru sna Siku moja ntafika oficn kwa ajili ya consultation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…