Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Karibu nimepokea hizo Ahsante naomba nimrudishie Mungu utukufu wote maana yeye ndio anastahili huo.Tofauti kubwa ya jina la biashara na ltd kampani ni nani anadaiwa baada ya jambo lolote paya kutokea kwa kampuni ukomo wa deni ni mali za kampuni lakini jina la biashara ambalo mara nyingi ni mtu binafsi mmoja halina ukomo kwenye biashara ile tu inaweza kuinga mpaka kwenye mali zote za mhusika. Pili unaweza kufungua jina la biashara mtu mmoja (Sole propriater) ingawa unaruhusiwa mpaka watu 20 wakati kwenye kampuni lazima wawe watu wawili nakuendelea. Hizo ni sababu chache ila hata kwenye maswala ya kodi kuna matakwa yake ambayo yako tofauti kidogo
ASANTE SANAAAAAAA 🤝
 
Mimi niko mwenyewe. Nataka nisajili kampuni kama main shareholder. Sema nataka iwe limited liability. Inawezekana?
 
Kwa sheria zetu limited company must have at least two shareholder unaweza kuwa main shareholder sema unaweza kuwa hata na 95% ila huyo wa pili atakuwa na asilimia 5%. Na director lazima wawe atleast wawili

Mimi niko mwenyewe. Nataka nisajili kampuni kama main shareholder. Sema nataka iwe limited liability. Inawezekana?
 
Kwenye hili eneo elimu kweli inahitajika na ni kila siku hongera kwa kutuelimisha na shukrani kwa kazi nzuri
 
Kwa sasa unaweza kuorodhesha mpaka kazi 40 ambazo zinaweza kufanywa na kampuni. Ila angalizo usifanye biashara yoyote ambayo huwezi kusimamia kwa karibu maana ndio chanzo cha biashara nyingi kufeli kuwa na mfumo mzuri wa kutambua kitu kinavyoingia na kutoka katika biashara yako unaweza kuwa na vitabu, mifumo ya kielectroniki yaani software zinazoweza kukuonyesha manunuzi, mauzo na stock. Biashara ambazo unaweza kuongeza kwenye list yako kwa mtaaji huo kama unasehemu nzuri kidogo nafikiri ni biashara ya uwakala wa Bima, Uwakala wa makampuni makubwa ya bidhaa ya vyakula (mfano Maziwa Asasim, Tanga fresh) uwakala katika taasisi za fedha kale kamashine mfano ka CRDB kana vitu vingi ndani yake yaani unalipa malipo yote yaliyopo, bado unaweza kuwawekea watu fedha zao unapata commission mtu hapa hawezi kukuibia.
Wadau wanaweza kujazia nyingine hapo

Natamani sana kuwa na kumpuni japo mtaji wangu ni mdogo kama 2mill, naumizwa sana na jinsi TRA wanavyonikadilia kodi lakini pia nahitaji kuwa huru, ndo maana natamani kuwa na kampuni ili wanikadilie kwenye faida, sasa mkuu kwa mtaji kama huo wa 2mill naweza kuanzisha kampuni ya nini tofauti na hii ya maduka? Biashara ambayo inaweza kunifanya kuwa free, ili niachaane na hii ambayo nikisafiri kwa mwezi tu nakuta biashara iko hoi, yaani kuendelea kwake vizuri mpaka mimi niwepo. Asante sana.
 
Sasa toka tunahimizana toka January sasa tumefika June hiyo ambapo ni mwisho wa kupeleka hesabu za mwaka 2018. Najua tuna hulka ya kupeleka haya mambo siku za mwisho embu tujitahidi kufanya michakato hii mapema zaidi ili tuweze kutimiza malengo. Muda wa kufunga hesabu umefika
 
Kwa sasa unaweza kuorodhesha mpaka kazi 40 ambazo zinaweza kufanywa na kampuni. Ila angalizo usifanye biashara yoyote ambayo huwezi kusimamia kwa karibu maana ndio chanzo cha biashara nyingi kufeli kuwa na mfumo mzuri wa kutambua kitu kinavyoingia na kutoka katika biashara yako unaweza kuwa na vitabu, mifumo ya kielectroniki yaani software zinazoweza kukuonyesha manunuzi, mauzo na stock. Biashara ambazo unaweza kuongeza kwenye list yako kwa mtaaji huo kama unasehemu nzuri kidogo nafikiri ni biashara ya uwakala wa Bima, Uwakala wa makampuni makubwa ya bidhaa ya vyakula (mfano Maziwa Asasim, Tanga fresh) uwakala katika taasisi za fedha kale kamashine mfano ka CRDB kana vitu vingi ndani yake yaani unalipa malipo yote yaliyopo, bado unaweza kuwawekea watu fedha zao unapata commission mtu hapa hawezi kukuibia.
Wadau wanaweza kujazia nyingine hapo
mkuu mie nahitaji kufungua Group of Companies naomba unipe moja mbili tatu kulingana na uzoefu wako
 
Kusajili kampuni inakuwezesha kuwa na mtu mwingine zaidi ya wewe. Maana kampuni ni kitu kamili ( Entity) na sheria nyingi za kodi zinaonyesha kulinda zaidi kampuni zaidi kuliko aina nyingine za biashara. Yani zile za watu binafsi (Sole Proprietor ) au zile za Ubia (Partnership). Kwa kuwa kampuni inaweza kushitaki na kushitakiwa ( Entity) na hivyo kuwezesha kuwa na ukomo kwa hisa zake tu ( Limited to its share) na hivyo inaweka cover fulani kuliko aina nyingine. Na faida nyingine kubwa ni uwezo wa kutoa matumizi ya biashara katika faida unayotengeneza. Na huo uhuru wa kuweza kukadiria kodi mwanzoni wa mwaka tofauti ya ile ambayo biashara nyingine unakadiriwa tu then unalipa. Ila uhuru huo unalimit usije ukapungua zaidi ya 20% unaweza kukutana na penalty.
ukitaka kusoma zaidi unaweza kutembelea link hii Advantages and Disadvantages of the Corporate Form of Business
Mkuu kwanza nikushukur sana kwa kutoa hili darasa at least nimepata mwangaza.
Sasa kuna maswali mengi nahitaj kujua.
Je naweza kufanya kazi za kitaalam/contractor na kuchukua tenda kwa kutumia Sole proprietor au partnership company?Je na zenyewe zipo kisheria?
 
Habarini za leo wanajamii,
Leo nimeona kidogo nitumie fani yangu ya ushauri wa maswala ya biashara na uchumi niweke mambo muhimu katika uendeshaji wa biashara kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania.

Hapo miaka ya nyuma kulitokea na watu wengi waliosajili makampuni (LTD Companies) na wengine walienda mbali kidogo wakapata na Tax Indentification Number (TIN) kutoka mamlaka ya mapato (TRA). Sasa wanapotaka kuanza kufanya kazi wanakutana na penaty kubwa na fine.

Ni Moja ya kushukuru Mungu sijui waheshimiwa walipita hapa katika budget ya mwaka 2018/2019 wametoa TAX AMNESTY kwenye fine na penalty kwa kipindi cha miezi sita toka July 1 to Nov 30, Sasa Maelekezo yametoka na form ziko online na kwenye ofisi za TRA hii ni nia nzuri mno ya serikali na mimi natoa kongole kwa jambo hilo. Hii uliyo na rangi hii ni maongezo toka kwenye original post

Ni kutokana na kadhia hiyo nataka kutoa ushauri kidogo kwa yeyote mwenye kampuni vitu hivi vitatu ni vya muhimu sana hata kama kampuni yako haiyafanya biashara.

Mosi hakikisha kila mwaka unapeleka majeresho yako (Annual returns) brela kwenye tarehe ile ambayo ulisajiliwa na hizi ni vyema ziambatane na hesabu zilizokaguliwa ( Audited financial). Kuanzia February 01, 2018 swala hili linafanyika kwenye mtandao wa Brela kama utahitaji msaada wa kufanya unaweza kuwasiliana nami PM .

Mbili hakikisha unapelewa returns zako TRA zile za provisional returns ambazo zinatakiwa kupelekwa kuanzia tarehe 01 January mwisho wake ni tarehe 31 March. Haya ni makisio unayotegemea kuwa nayo kwa kipindi cha mwaka huo. Na hapa ndio kumekuwa na mtihani kwa wale waliokuwa na kampuni lala kuwa mimi sijafanya biashara kabisa, Kama hutegemei kufanya bishara weka au fill Nil returns ( RETANI ZERO) inakubalika ila unajulikana na kutofanya hivyo inakarabisha fine.

Na haya makadirio unaweza kuyabadilisha kwa wakati wowote hali yako ya biashara itakapobadilika. Hivyo hivyo kwenye VAT unatakiwa kupeleka returns zako za VAT kila mwezi hata kama ujafanya biashara kama umesajiliwa kwa VAT. Na Vile vile hakikisha kuwa mahesabu yako ( Audited Financial) zinawakilishwa kila mwaka kabla ya tarehe 30 June.

Tatu kodi zote nyinginezo kama withholding tax, PAYE na SDL zinapelekwa ila hapa utata umekuwa mkubwa kwenye withholding tax kwenye pango (rent) kwa mujibu wa sheria ni yule anayelipa ndio anatakiwa kukata na kupeleka TRA kwahiyo kama pango lako kwenue mkataba ni laki tano kwa mwezi na wewe umelipa miezi mitatu. Unatakiwa umpe mwenye nyumba 1,350,000/ halafu hiyo 150,000/ Unapeleka TRA, hivyo ndio sheria inavyotaka.

Naomba kuwakilisha
Mkuu Asante kwa darasa lako muhimu.
Je kwa sisi ambao hatuna kampuni na wala hatujawah kupata tenda yoyote lakini tunahitaji kuanzisha kampuni for future,unatushauri vipi?
 
Karibu uzoefu wangu hapo sio mkubwa kihivyo ila ambayo nimewahi kufanya ni ambapo mtu anafungua business names ambazo zinakuwa 100% owned by company limited.
Nyingine hii sasa ni ya kishule shule ambapo hiyo kampuni moja inamilki zaidi ya asilimi 66% nayo inakuwa parent kampuni. Au unafungua makampuni mengi yenye share holder wale wale ila yote unatengeneza mahesabu moja as a group of companies. na maswala ya kodi inakuwa moja.

mkuu mie nahitaji kufungua Group of Companies naomba unipe moja mbili tatu kulingana na uzoefu wako
 
Hii inawezekana ila risk ni kubwa mno kama unataka kufanya biashara ya contractor ndio maana watu wanaona ni vyema kuwa na kampuni. Kwa sababu ukiwa sole proprietor au Partnership liabilty haina ukomo yaani inaingia mpaka kwenye mali zako binafsi. Ndio maana watu wanaanzisha limited company ambapo liability zitaishia au ziko limited kwenye mali za kampuni na sivyo vinginevyo. Sasa fikiri umefanya kosa ambalo limesababisha hasara umeshitakiwa ukiwa na kampuni mali za kampuni tu ndio ukomo wakufidia hilo ila ukiwa na hiyo partnership au sole propriator tutaenda kwanza kwa mali zake zikiisha tutakuja mali binafsi mpaka zote ziishe hazijatosha tunaendelea kukudai tuu mpaka kieleweke. Naamini nimeelezea vyema kama bado hujanipata maswali zaidi yanakaribishwa

Mkuu kwanza nikushukur sana kwa kutoa hili darasa at least nimepata mwangaza.
Sasa kuna maswali mengi nahitaj kujua.
Je naweza kufanya kazi za kitaalam/contractor na kuchukua tenda kwa kutumia Sole proprietor au partnership company?Je na zenyewe zipo kisheria?
 
Hii inawezekana ila risk ni kubwa mno kama unataka kufanya biashara ya contractor ndio maana watu wanaona ni vyema kuwa na kampuni. Kwa sababu ukiwa sole proprietor au Partnership liabilty haina ukomo yaani inaingia mpaka kwenye mali zako binafsi. Ndio maana watu wanaanzisha limited company ambapo liability zitaishia au ziko limited kwenye mali za kampuni na sivyo vinginevyo. Sasa fikiri umefanya kosa ambalo limesababisha hasara umeshitakiwa ukiwa na kampuni mali za kampuni tu ndio ukomo wakufidia hilo ila ukiwa na hiyo partnership au sole propriator tutaenda kwanza kwa mali zake zikiisha tutakuja mali binafsi mpaka zote ziishe hazijatosha tunaendelea kukudai tuu mpaka kieleweke. Naamini nimeelezea vyema kama bado hujanipata maswali zaidi yanakaribishwa
Dah mkuu umenisaidia kunifungua masikio Sasa hapo nimepata mwangaza mzuri sana kuhusu kampuni.
 
Mkuu asante kwa elimu as nikiwa kama kijana nakaribia kufungua carwash ambayo nimepiga cost so far inaweza kurange mtaji kwenye mili5 mpaka 7 natamani sna niiendeshe iwe chini ya kampuni je inawezekana?na bora kipi kuanza kwa kusajili busnes name au kufungua kampuni iendeshwe chini ya kampuni?Thanks in advance
 
Kampuni inaweza kufuguliwa hata na mtaji wa elfu 20. Ila kwa sababu ya compliance costs mbalimbali ningekushauri uanze na business name ujijenge kidogo mambo yakikaa vizuri fungua kampuni. Maana ukifikiria hiyo ulipe Final account preparation na Audit inaweza kuwa 1.2m. Moja ya kanuni ya kukua ni anza mdogo fikiria makubwa hatimaye utafika huko. Ndio maana mtoto humchukua miezi tisa kukua lakini akizaliwa hakimbii hapo hapo anachukua muda. Isome biashara yako ielewe ikuze.

Thanks mkuu nashukuru sna Siku moja ntafika oficn kwa ajili ya consultation
 
Back
Top Bottom