Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mkuu Nyumbalao naomba ufafanuzi kuhusu tarehe ya mwisho ya kuwasilisha return za VAT kwa kila mwezi, maana kuna jamaa amekwenda kutafuta Tax Clearance wakampa bill ya penalty ya zaidi ya mil 11 sababu alichelewesha returns
Kwani Returns za VAT ni kila mwezi au ulisema kwa kila miezi mitatu?
 
Kwani Returns za VAT ni kila mwezi au ulisema kwa kila miezi mitatu?
Returns za VAT ni kila mwezi na saa hizi kuna mfumo mpya unatumia barcode ulioanza kutumika mwezi uliopita ambao risiti unayopewa jitahidi iwe na vitu hivi vitatu JINA, TIN na VRN ili mfumo upitishe kwa urahisi.
 
Kwa wale waliokuwa wamechelewa kupeleka hesabu za mwaka 2021 ambapo mwisho ilikuwa juzi TRA wameongeza muda mpka tarehe 05 unaweza kuchukua fursa hiyo ikakusaidia tutopigwa penalty ambayo sio lazima.
 
Leo ndio siku ya mwisho ya kupeleka returns za mwaka 2021 TRA baada ya kuongeza siku tano kwahiyo kama ujapeleka una fursa ya kufanya hivyo fanya hivyo
 
Leo ndio siku ya mwisho ya kupeleka returns za mwaka 2021 TRA baada ya kuongeza siku tano kwahiyo kama ujapeleka una fursa ya kufanya hivyo fanya hivyo
Mkuu salama?
Kwanza nikupe pongezi kwa kazi njema unayoifanya ya kuelimisha watu kwa kile ambacho Mungu amekubariki nacho, ni maombi yangu kuwa Mungu akubariki zaidi na zaidi...

Pili, naomba kujuzwa ni taratibu zipi nafuata kama nataka kubadili mkurugenzi wa kampuni (yaani kujiondoa kabisa na kuweka mwingine). Thanks in advance!!
 
Tukiwa tunakaribia mwisho wa mwaka napenda kuwakumbusha wadau wote kuwa ni vyema kucheck vitu kadhaa hata kwa uchache moja makadirio yako uliofanya mwezi wa tatu umeshalipa yote na ndio ni hali halisi au unatakiwa kuongeza au kupunguza?. Pili kama umesajiliwa na VAT je mauzo yako uliyoweka ni sawa na EFD. Tatu umefaili PAYE NA SDL kama inavyotakiwa na wafanyakazi wako wana TIN maana January itakuwa bila TIN hizo returns haziendi. Nne ukiwa na maghala umejipanga kupeleka Storage facilities returns kama sheria mpya inavyotaka hapa ni wenye hizi storage facilities zenye kubeba bidhaa zenye dhamani ya zaidi ya Tshs 10m kwa mwaka. Nawatakieni kumaliza mwaka salama na Heri na Fanaka kwa mwaka Mpya.
 
Mkuu salama?
Kwanza nikupe pongezi kwa kazi njema unayoifanya ya kuelimisha watu kwa kile ambacho Mungu amekubariki nacho, ni maombi yangu kuwa Mungu akubariki zaidi na zaidi...

Pili, naomba kujuzwa ni taratibu zipi nafuata kama nataka kubadili mkurugenzi wa kampuni (yaani kujiondoa kabisa na kuweka mwingine). Thanks in advance!!
Kikawaida unafanya maamuzi ya bodi (Board resolutions) na kwa kuwa haya mambo yanafanyika online siku hizi ukiwa umeshauhisha kampuni yako unamteua mwingine kama idadi itakuwa imeshuka maana kwa sheria za Tanzania lazima uwe na wakurugenzi walau wawili. Karibu tukusaidie kwa vitendo zaidi kama bado unapata shida na hayo maelekezo.
 
Nashkuru kwa response yako japo imekuja too late, nilishafanikisha mkuu.
 
Elimu nzuri sana jamii forums big up
Tukiwa tena tunaanza mwaka kwa biashara zetu mipango yako iendane vilevile na jinsi gani utakavyolipa kodi. Kitu ambacho watu wengi huwa wanakisahau ni kitu kinachoitwa Tax plan, Tafuta wataalamu wakushauri namna nzuri ya kukabiliana na taratibu na mipango ya kikodi. Kwa wale ambao hawajasajiliwa kwenye VAT tafadahli hakikisha kuwa unafanya makadirio kabla ya mwezi wa tatu na kupeleka na kuandaa hesabu kabla ya tarehe 30 Mwezi wa sita kwa hesabu za 2022. Nawatakieni kila la heri katika mwaka huu mpya
 
Kuna mabadiliko makuu mawili makubwa ambayo yametokea kwa sasa hasa kuanzia mwezi wa pili 2023.
1. Ni kuwa leseni zote za biashara za daraja B nazo zitakuwa zinapatikana online kwenye website https://tausi.tamisemi.go.tz/
2. Tra wameboresha mfumo na kuwa mambo mengi sasa ya kikodi yanaweza kufanyika online na wamekuja na mfumo uliboreshwa unaitwa taxpayportal nao unapatikana kwenye TRA | Taxpayer Portal.
Kwa kweli mfumo umeboreshwa unajitahidi kupatikana na kama unachangamoto zozote nasi tupo kukusaidia kuzitatua ili uweze kulipa kodi stahiki bila shida
 
KARIBU SANA
Kwa sasa baada ya TRA kuwa na mfumo mpya www.taxpayerportal.co.tz na tunapoelekea mwisho wa mwaka ni muhimu kuzingatia yafuatayo. Kama uko VAT registered returns zako zinafana na kwenye mashine yako na ingawa manunuzi yanachukuliwa moja kwa moja ni muhimu kuangalia kama hayo ndio matumizi yako sawia.
 
Kuna mabadiliko makuu mawili makubwa ambayo yametokea kwa sasa hasa kuanzia mwezi wa pili 2023.
1. Ni kuwa leseni zote za biashara za daraja B nazo zitakuwa zinapatikana online kwenye website Tausi Portal
2. Tra wameboresha mfumo na kuwa mambo mengi sasa ya kikodi yanaweza kufanyika online na wamekuja na mfumo uliboreshwa unaitwa taxpayportal nao unapatikana kwenye TRA | Taxpayer Portal.
Kwa kweli mfumo umeboreshwa unajitahidi kupatikana na kama unachangamoto zozote nasi tupo kukusaidia kuzitatua ili uweze kulipa kodi stahiki bila shida
Mkuu,hii tausi uki log in kwako inakubali??

Me naona huu mfumo ni takataka kabisa,nina mwezi sasa haikubali kuingia.
 
Mkuu,hii tausi uki log in kwako inakubali??

Me naona huu mfumo ni takataka kabisa,nina mwezi sasa haikubali kuingia.
Ndio unakubali ukikishinda kwa number tumia ile ya kujibu maswali ndio umekuwa unafanya kazi. kam kuna specific tatizo nione inbox nitakusaidia zaidi. Ila kwenye kuingia au kusajili hapo ndio kwenye issue
 
Kwanye ku sign in ndo tatizo mkuu
 
Ndio unakubali ukikishinda kwa number tumia ile ya kujibu maswali ndio umekuwa unafanya kazi. kam kuna specific tatizo nione inbox nitakusaidia zaidi. Ila kwenye kuingia au kusajili hapo ndio kwenye issue
Hapo hiyo NIN haifanyi kitu kabisa.

Sasa najiuliza wanaosimamia huu mfumo kwamba hawaoni hii shida au makusudi tu wanapotezea.
Screenshot_20231114-112711_Chrome.jpg
 
Hapo hiyo NIN haifanyi kitu kabisa.

Sasa najiuliza wanaosimamia huu mfumo kwamba hawaoni hii shida au makusudi tu wanapotezea.View attachment 2813360
Ha inabidi uanzie hapa kwanza kwa kutumia Question ukiienda hiyo ya NIN moja kwa moja hupati hiyo otp then ndio utaenda na hiyo NIN kwenye taaratibu zinazofuata watakuliza maswali ambayo wewe tu unaweza kutoa majibu yake
1700136810197.png

1700136900993.png
 
Nilikushauri utumie njia ya maswali ndio unaweza kupata suluhisho kwa sasa
 
Back
Top Bottom