Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.
1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha Quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee noma
2. Mavazi ya staha kwa wanawake
Napenda sana dress code kwa wanawake. Wanavaa mavazi ya staha. Sehemu za ibada huwezi kuvaa kihuni-huni ukaingia
3. Kutengana wanawake na wanaume kwenye ibada zao
4. Kuruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa mtu mwenye uwezo wa kuwatunza.
5. Utoaji wa sadaka usiotia umasikini
6: Kuharakisha mazishi.
7. Kutomtenga muumini (Hapa uswali ama usiswali ilimradi wewe ni muislamu ukifa hamna longolongo utazikwa mahali popote! Njoo kwetu!
8: Kuharakisha ndoa! Hamna longolongo!
Uislam kama ulivyo Ukristo, Uhindu, Ubudha, Uyahudi n.k vyote vina mabaya na mazuri yake.
Katikahjayohayo uyaitayo mazuri ya uislam ukiyachumbua kwa akili huru utaona ni udhaifu tu unaopuliziwa mafuta mazuri na kuvalishwa viungo bandia, pia ndivyo ilivyo kwenye dini nyingine.
Ila ukiona mmoja yupo mbelembele kujinasibu yeye ni mzuri kuliko wengine , basi akili kichwani ni wakati wa kuitumia.
Sikatai, Uislam ni mzuri sana na unajali mno, ndiyo maana umeagiza mtu kama kama atashikwa na hamu ya kimwili, ikatokea akamuingilia mnyama kimwili basi akimchinja mnyama huyo ahakikishe nyama yake haiuzi au hailiwi eneo hilo, anatakiwa akaiuze au akawape watu mbali kabisa. Pia kama mtu ataiingilia maiti ya mwanamke kimwili, uislam unaelekeza mtu huyo anatakiwa kufanya nini baada ya tendo hilo.
Wakristo wana mapungufu mengi ambayo yanatokana na utayari wa wakristo kiimani, hivyo kuna makundi ya watu yanataka kujinufaisha wao binafsi kupitia utayari, upole na Ujinga wa Wakristo.