Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha Quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee noma

2. Mavazi ya staha kwa wanawake
Napenda sana dress code kwa wanawake. Wanavaa mavazi ya staha. Sehemu za ibada huwezi kuvaa kihuni-huni ukaingia

3. Kutengana wanawake na wanaume kwenye ibada zao

4. Kuruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa mtu mwenye uwezo wa kuwatunza.

5. Utoaji wa sadaka usiotia umasikini

6: Kuharakisha mazishi.

7. Kutomtenga muumini (Hapa uswali ama usiswali ilimradi wewe ni muislamu ukifa hamna longolongo utazikwa mahali popote! Njoo kwetu!

8: Kuharakisha ndoa! Hamna longolongo!
Madhehebu yameuharibu sana Ukristo. Kuanzia dhehebu kubwa la Katoliki hadi Madhehebu madogo
 
Madhehebu yameuharibu sana Ukristo. Kuanzia dhehebu kubwa la Katoliki hadi Madhehebu madogo
Yaani imekuwa vurugu hata huelewi ufuate lipi. Mbaya zaidi kwa watu wasiolijua vizuri neno wanayumbishwa sana. Ukizingatia wabongo wavivu kusoma wanaelewa kwa kuambiwa, basi ni kupotoshwa tu. Kikubwa ni bidii katika kutenda yanayompendeza Mungu tu
 
Islam is true religion the rest the human made bussiness.
Kila moja ashinde mechi zake period. Cha kusema one religion is a true religion na zingine siyo ni kujidanganya tu. Wewe umezaliwa na wazazi Waislamu endelea kuwaenzi, na aliyezaliwa na wazazi Wakristu naye aendelee kuwaenzi pia. Mwisho wa siku Waislamu na Wakristu wote wanamuamini Mungu mmja kupitia kwa Abraham
 
Hapana kaka nimewaza tu yani tunaweza dumisha upendo kwa kulala pamoja wote na mme wetu[emoji81]
Nina hakika baada ya usiku moja kesho ni fujo.
Hasa ikitokea nafsi ako ikihisi unazidiwa na mwenzio...
[emoji2211][emoji2211] swaum njema.
 
Nina hakika baada ya usiku moja kesho ni fujo.
Hasa ikitokea nafsi ako ikihisi unazidiwa na mwenzio...
[emoji2211][emoji2211] swaum njema.
Hamna kaka tukilala wote hamna fujo, fujo tukiwa separate....

Swaum njema pia
 
Hata mimi kuna vitu nimeona vimenivutia mno kama misiba hata kama siyo ndugu yao utaona wanajitolea mzika na kumsalia.

Siku kama hizi za mfungo wanalisha maskini ili wasishindwe funga ,misikiini wanachanganyika maskini na tajiri, kiongozi na kapuka
Hakuna masikini anae weza kushindwa kufunga,miezi mingine alikuwa anakula nini?
 
Back
Top Bottom