Mambo Usiyoyafahamu Kuhusu ushoga na Jinsi Unaweza kuwaepusha Watoto Wako

Mambo Usiyoyafahamu Kuhusu ushoga na Jinsi Unaweza kuwaepusha Watoto Wako

Aisee mbona umekua mgumu sana kuelewa??
hakuna kitu sijakieleza lakini umekomaa kuniuliza yale yale ni ukosefu wa kujenga hoja ama ni nini?

Kwanza kwenye maelezo yangu ni wapi nimesema habari za Homons?? au ulikosea kuquote,

Kama watu wanasema ni homons ni wao sababu hadi sasa hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonesha sababu ya homosexual, ukisema ni kujiendekeza basi ujue ingekua tayari ni sababu lakini hakuna ziadi watu wana hisi hisi,

Unaelewa maana ya Sexual Orientation?? ndio maana nilikuuliza wewe ni mwanaume kwanini ukimuona Mwanamke unavutika nae?? hivyo hivyo na Gay kama ni Me akimuona Me atavutika nae na akimuona Ke atavutika nae, hizo blah blah za asili hazina nafasi tena, tofautisha kati ya kuzaana na matamanio ya ngono, msome jamani sio mnakaza fuvu tu, elimu ipo kiganjani mwako,

Kasome kuhusu Sexual Orientation, Sexual Behaviour, Sexual Identity, Genders na mengine mengi utakutana nayo huko, kubishana hakusaidii jaribu kusoma ili uelimike hata kama hutokubaliana na jambo angalau unakua una uelewa nalo,

Kwa taarifa yako Wanyama na Ndege wapo wanaopendana jinsi moja hii sio kwa kusimuliwa bali kwa kuona kwa macho yangu, Paka na Paka, Mbwa na Mbwa, Jogoo na Jogoo, again taarifa ipo kiganjani kwako, jaribu kuperuzi peruzi upate kuelimika ili uache kuuliza maswali yasiyo na tija.
We acha kulazmisha jamii ikuone wa kawaida, nyie ni wa ajabu na mnafurah kuona vitoto vikikua vinakuwa hvyo
 
Naona tu mashoga humu yanakuja kujitetea yako sawa, aya bna
 
Yaani kukojoa haraka ndio ugay[emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

We nae acha zako.

Huyu jamaa yako ana upungufu wa nguvu za kiume na confidence imeshuka sana.

Usikute hayo mahusiano yaliyopita yamemuathiri.

Kama yeye hataki badilika na kuchukua hatua atabaki hivyo hivyo na wewe kwako inakuwa kalaghabao[emoji2]

Unataka handsome mwenge pesa na kazi nzuti ila mzigo hawezi piga .Yule kapuku usiemtaka mnuka mijasho ndio anaesimamia ukucha[emoji1787][emoji2]

Daah wanawake nawaonea huruma yaani lazima mkutane na kasoro mahali.[emoji2]

Anyway mambo yenu nimewaachie wenyewe
Mxiyuuuu ovyoo
 
Basi Olewa tu na mwanaume mwenzako.
Kwanini huchukui huo uamuzi ?

Nadhani kama mtaamua kuishi pamoja hakuna atakaye wabughudhi kwakuwa ni watu wazima.

Unaonekana huwezi kuishi bila ya kushiriki pamoja na mwanaume mwenzako.

Kwenye Wanyama wengine msitake kuongopa.

Hakuna mnyama kwa mfano Simba dume anaye anzisha maisha na dume mwenziye na kushikilia Maliki ya eneo flani.

Wanyama wote ninao wajua wana anzisha familia na jinsia nyingine na kupelekea kuongeza familia kwa kuzaa watoto.

Ni swala la muda tu sijui nikuite kaka au dada,
sijui unapandelea kuitwa vipi
utakuja wakati huko mbeleni mtaruhusiwa kuonana na kutambulika na jamii watu mnaovutiwa na jinsia moja.

Ila kwa Tanzania, sio leo wala kesho, jamii ya sasa haitaki huo naweza kuiita upuuzi.

[emoji23][emoji23][emoji23] Bro mimi ni Mwanamke so ukiniita Dada utapatia zaidi, uamuzi nimeshachukua ninaishi na Mwanamke nishamchumbia na tuna Mtoto tayari,

Ni Happy Family kwa kweli tumebarikiwa Furaha, Amani na Upendo,

Naona unabadili upepo kila muda mwanzo ulikataa kua hakuna wanyama wanaoshiriki same sex naona umeenda kugoogle huko umejionea, sasa unakuja kusema hakuna wanyama wanaoishi pamoja as same sex, lol

Kuhusu Tanzania kuruhusu Ndoa ni suala litachukua muda lakini litatokea na ndio maana tunapigania kuweka mazingira sawa kwa new generation.
 
Mi siwakatazi Mashoga kufanya wanavyo jisikia. Kwani ni uamuzi wao na ni watu wazima.

Ni kwamba nashindwa kuhimili kuangalia matendo yao hadharani basi,
huko chumbani mi sifiki.

Na muwe mnafanya au hamufanyi mimi hainihusu.
Mimi nina fimbo na inahitaji kuingizwa sehemu ambayo nitapata matunda yake ( kuzaa watoto)

Mbegu za Binadamu zina thamani ya hali ya juu.

Mtu timamu hawezi kuzimwaga matakoni kwa yeyote hata awe mwanamke kwani ni kupoteza nguvu za bure.

Na pia kumnyima Binadamu haki yake ya kuzaliwa.

Nakuuliza na unijibu sio kwa ugomvi la hasha.

Hivi Baba yako ange chagua kutupa mbegu zake zilizo kuzaa wewe kwa Shoga wewe ungezaliwa ?

Kama ni hivyo huoni na wewe unakosea sana kwa kumshawishi Mwanaume azipoteze mbegu zake kwako na kusababisha wasizaliwe watoto halari kwake ?

Hijisikii guilty kwa hilo tendo au unawaza hisia zako tu ?

Mtu akidai haki zake za Msingi ambazo nilishakuorodheshea huko juu kuna tatizo gani??

Unaona ni sawa binaadam mwenzako anaishi kwa mateso kisa tu anachopenda yeye wewe hupendi wakati Dunia hii tumeikuta na tutaiacha? huo ni ubinafsi,

Hakuna sehemu Mashoga wamesema wanataka haki ya kufanyana hadharani sababu wale sio wanyama wana utashi na aibu pia,

Nilishakwambia tena suala la kuzaa lipo, Shoga anazaa, Msagaji anazaa sasa hivi technolojia imekua, watu wanapandikiza, kuna surrogate mothers pia, kwa hiyo kama wewe unaenda kwa Mwanamke ili uzae jua hata shoga akitaka kuzaa atazaa pia kikubwa mbegu na mayai,

Mfano wa wazazi wangu mnapenda sana kuutumia hua mnapenda sana kuutumia najua ni kukosa hoja sasa mnatapa tapa,

Labda nikuulize maswali rahisi, unajua wewe ulitoka wapi na kwanini upo hapa duniani?? ulijua kua wazazi wako wangekua wazazi wako kabla?? kwanini kuna wengine wana viungo vyote kamili na wengine wanazaliwa sio kamili?? kwanini kuna Tasa na Wagumba??

Twende pole pole hapo.
 
Ni ndefu kiasi ila jitahidi umalize.

Natumaini Wote Mu wazima wa afya, kwa walio wadhaifu basi Mungu awaponye na awatie nguvu tena.

Modes nimeamua kutumia ID tofauti na ambayo huwa natumia kwa sababu za privacy tu sababu ID nayotumia nafahamika personally na baadhi ya watu, kwa hivyo naomba msije ku reveal hata mkijua (the matter of privacy), nataka tu kutoa elimu kiasi kuhusu hili jambo kwa faida ya wote.

Kwanza niwape pole wazazi au familia ambazo wamekua na mmoja wa familia ama mtoto mbae labda ni gay/shoga na wameumizwa na jambo hilo,najua sio rahisi kuli handle, ni fedhea hasa katika jamii zetu, ila napenda kuwaambia msijione labda ni wazazi wabaya, au labda hamjui kulea, is not your fault.

Dhumuni kuu la kuanzisha hii thread si kwa ajili ya kuongelea uzuri au ubaya wake ila ni ili kutoa a simple knowledge ya jambo husika (gay) na ili pia niweze kuwapa mwanga wazazi na watu ambao jambo hili limekua likiwachanganya na kuwahudhunisha na labda jinsi ya kuokoa watoto pia. Kwa maana nimesoma maoni na mada nyingi ambazo huandikwa humu na maybe 80% ni very wrong na si kwa ubaya bali ni kwamba wengi hata hawajui jinsi inavokua na kwa kutokujua inafanya hata wasiweze kujua chanzo, na jinsi ya kuepukana na hilo. Nimeonelea mayb ni vyema kama mtapata kitu kutoka kwa real person who have real experience.

Karibu👇
Wengi wangependa kujua kuhusu mimi, watu wengi wamekua wakijiuliza mtu anakuaje gay, ukiniuliza nimekuaje gay sina jibu kamili kuhusu hilo swali, hata ukiniuliza nilianza lini kuwa gay sitakua na jibu sahihi.

KUHUSU MIMI
Ni kijana, kwa sasa nina 26 years, nimesoma hadi degree, ninafanya kazi nimeajiliwa mahali, sitarajii kuoa soon wala sijawahi kuwaza kuhusu hilo japo mama anaexpect soon nimletee daughter inlaw, hajui kama kijana wake ni gay na wala hajawahi kuhisi, sababu ukiniangalia kwa macho mimi mwanaume kamili, sina girlish behaviour, nina marafiki almost wote ni straight, na wao pia hakuna mtu anajua kua im gay, nina girlfriend pia, napenda kuvaa casual na sitembei kiajabu ajabu niko very normal in my formal life, ila nina boyfriend pia, lakini nina girlfriend pia wakuzugia (yes na hii siifurahii sababu nafanya kuridhisha marafiki na wazazi ili wasihisi chochote na pia sitaki kuwaudhi wala kuwadhalilisha ndugu zangu kwa jambo ambalo najua kabisa jamii yetu haipendi japo ndivyo nilivyo).

Sijawahi kufurahia kua gay hili niweke wazi, na siwezi taka mtu awe, and im not proud of it na siwezi taka mtu wangu wa karibu ajue that im gay, na wala siwezi taka mtu awe gay, ila siwezi kujizuia, ni automatically nimezaliwa hivyo, hakuna mahali nilijifunza au story za vijiweni labda nilifanyiwa vitendo vya ukatili hapana , nachojua ni tangu nikiwa mdogo sijawahi kuwa na hisia na msichana hata kidogo nimejaribu kujifunza sana jinsi gani nihamishe hisia zangu, lakini nimeshindwa, sababu mpaka leo ukiniwekea msichana mrembo sana mbele yangu na mwanaume handsome mbele yangu kitakachotokea ni kuwa mwanaume atateka akili yangu yote, msichana taona tu ni mrembo its fine, hata awe amevua nguo maybe sitaweza hata kumuangalia sababu nitaona is disgusting. Ila yule mwanaume nitakua ni kama vile ambavyo mwanamke akiona mwanaume handsome anavofeel. Natumai umepata picha japo kidogo.
Niliwahi kudhamilia kua straight ila nikashindwa, hisia kwa girls ni sifuri kabisa, natamani ningekua kama wanaume wengine ila nimeshindwa, yani automatically tu, na mahitaji ya mwili yako pale pale.

KABLA NIANDIKE MAMBO MENGINE MENGI, TAFADHARI ZINGATIA HUU USHAURI.

SOMA KWA MAKINI JINSI YA KUEPUSHA WATOTO NA MASWALA HAYA (hapa zaidi kwa wale ambao sio natural born ila wanataka kujaribu)

1- hakuna mzazi au mtu anaweza kuzuia kabisa lisitokee zaidi ya Mungu, hivyo jambo la kwanza kabla ya yote ni kuombea familia yako Mungu awaepusha kizazi chako.

2- Wengi hawapendi kuongea na vijana wao kuhusu masuala ya gender na masuala ya mahusiano na masuala ya sex, hii ni mbaya sana, sababu unampa uwanja mkubwa kijana ajifunze hayo mambo mtaani, wazazi msione aibu kuongea na watoto wenu, siongelei wakiwa wamekua, hapana ila wakiwa wadogo kabisa ongea nao, waambie wewe ni mwanaume na wewe binti, mwambie wewe mwanaume usikubali mtu akufananishe na mwanamke, muelezee yote yanayompasa kutenda kama mwanaume, mwambie mambo ya kuingiliwa sio yako, pia muelekeze kuhusu afya yake, matumizi ya condon, nchi za qwnzetu haya wanafundishwa hata shuleni , ila huku bado ni taboo kuongelea , ongeeni na watoto wenu kuhusu sex na yanayohusu jinsia yao.

3- Usikubali mtu yoyote amfananishe mtoto wako wa kiume na msichana, au kumsifia wewe ni mrembo, mwambie na umfundishe mtoto ako kabisa kua wewe ni wa kiume, wewe sio mrembo, mtu akikuambia hivo manaake anakutukana na anakudhalilisha, mtengenezee mindset mtoto wako ajione yeye ni mwanaume ,jambo lolote linalomfananisha na mwanamke achukulie ni matusi na dharau, nataka kusema tu kua hii mindset game inasaidia sana mtoto kujizuia hata kujaribu mambo furani sababu ameshaweka kwa akili yake kua ni kitu kibaya, na hii itafanya hata kuwa vigumu kushawishika. (nitelezea chini zaidi)

4- Mtoto akiwa mdogo, tafadhari wewe mama, dada, kaka, baba, ukiona anapenda vitu wanavyopenda wasichana, anapenda kujaribu jaribu viatu vya kike, rangi za kucha, sjui midoli ya princes , ama kuiga waschana either wanavotembea au kuongea, usifurahie , hapo kengele ilie kichwani mwako, hapo fanya jitihada zote kumnusuru mtoto katika umri huo mdogo, akipita hapo, basi huezi fanya kitu tena. Kuna watu watasema mbona wangu alikua hivyo na sasa sio gay, nakwambia ni gay ila incloset like me, ila huezi kujua sababu anafanya iwe privacy. Kama huamini, fanya jambo moja, hakiisha una unlock simu yake bila yeye kujua na fatilia emails, texts, whatsapp, browsing history etc, utapata kitu hakika.

Jambo la mwisho ni kufatilia mienendo ya watoto wenu, hapa nimesema kabisa , kama mtoto ni gay atakua gay tu huwezi zuia ila kwa kumtegemea Mungu peke ake, ila angalau ukifanya hayo ya juu , utamuokoa mtoto wako na familia yako kutoka kwenye fedheha na aibu ndogo ndogo na kubwa, sababu ni afadhari awe gay na usijue pia watu wasijue iwe siri yake kuliko ukute mwanao amevaa kama mwanamke anakatiza mitaani na makeups, ama uone watu wakimdhalilisha nitandaoni sababu ni gay, hiyo inaumiza zaidi.

HAYA CHINI NI MAONI YANGU NA EXPERIENCE YANGU NA PIA UFAFANUZI WA BAADHI YA MASWALA PENGINE UNAWEZA KUJIFUNZA KITU NA KIKAKUSAIDIA KUJUA JINSI YA KUHANDLE.

Kuna watu nimeona humu wanacomment kua gay unaweza mtibia hospitalini, kwamba unampeleka gay anaenda kupigwa bomba sababu akiingiliwa anakua anawashwa huko kwenye haja kubwa hivyo akiwashwa anatafta mtu wa kumuingilia, HII STORY SIO UKWELI

Kua gay ni suala la hisia zaidi , wala sio swala la kuwashwa, ni hisia, badala ya mtu kupenda jinsia tofauti anapenda jinsia yake, hii story ya vijiweni itafanya kweli wazazi wahangaike kupeleka mtoto wao akapigwe bomba ili aache kua hivyo na kumbe wanapoteza tu pesa na muda bure, hii story ya kuwashwa sjui hata watu wameitolea wapi.

Nimekua gay tangu niko mdogo, naongelea kihisia yani kupenda same gender, ila mala yangu ya kwanza kusex ilikua wakati nipo na 14 years, miaka hiyo yote hadi nafikia miaka 14 sikuwahi kuwashwa huko, na hata baada ya hiyo first time sijawahi kuwashwa , sababu hisia zinatoka ndani sio huko, ni kama msichana akimpenda mvulana , sijui kama hua anawashwa huko chini, nachojua ni hisia tu, anampenda mtu na anatamni kua nae, pia huko iko hivyo. Hakuna gay anaewashwa huko chini ndio atake kuingiliwa, hivyo hata ukipata mwanao yupo hivyo hio sio solutuon hata kidogo. Watu wanaopigwa bomba ni wale waliokua assulted , na wanatoa zile sparm kwa njia ile ili kuepusha maambukizi yoyote uko kwenye haja kubwa kama fungus au magonjwa mengine kama aliemuingilia alikua na magonjwa, na mtu akiwashwa huko basi ni kwa sababu amepata maambukizi either ya fungus au bacteria , ndio anakua anawashwa thats why anafaa akapigwe bomba, hata wasichana wakibakwa na wakalawitiwa pia hupigwa bomba kuepusha hizo infections.

Suala lingine watu wengi wamecomment ni suala la kusena ati vijana wanajiingiza kwenye ushoga sababu wanapenda maisha mazuri hivyo wanakubali kuingiliwa ili waishi maisha ya starehe na wanajiuza sjui na nini. Huyo anaefanya hivyo ni prostitute tu kama ilivyo kwa straight wanaoamua kujiingiza kwenye ukahaba ili wapate pesa. Nachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu anaejibadilisha kua gay, maybe yes hao wa hivyo wako ni kama straight people tu, sio kila msichana anajiuza ila wako wanaojiuza kwa sababu zao, the same kwa hawa gays pia wako wanaojiuza ila wengi pia hawajiuzi wala hawafanyi sababu wanataka pesa ama nini hapana.

Mfano kuhusu mimi, nimetokea familia yenye uchumi mzuri, nimesoma, ninakazi yangu nzuri yenye mshahara mkubwa, nina kila kitu cha muhimu ambacho vijana wengi au watu wengi wangependa kumiliki pia na vyote nimevipata kwa kupambana, na work very hard, namake sure sikati tamaa wala kutegemea favour ama kutarajia kitu kutoka kwa boyfriend, NO, unawezaje sema nimekua gay sababu nataka mteremko sjui maisha mazuri? Hivyo hiyo dhana muachane nayo, wazazi deal na hisia za mtoto, usijefikilia labda hujampatia maisha mazuri ndio kawa hivyo, hapana, tena wengi walitoka familia bora ndio wanakua hivyo, ni sababu wanazaliwa hivyo.

Pia kuna watu wanasema kwamba mtu anakua gay sababu labda aliingiliwa kwa nguvu akiwa mtoto labda aliingiliwa na mjomba ama sjui nani ndio akawa hivyo, hii pia ni uongo, kwa sababu kuna watu waliwahi kulawitiwa wakiwa wadogo au hata wakiwa wakubwa ila hawajawahi kubadilika na kuwa gays na wameendelea kua malijali mpaka sasa japo hilo swala la kulawitiwa lime waaffect psychologically (sio kua gays), hivyo hata mtu akibakwa hawezi kubadilika na kua shoga, akibadilika ujie alikua gay kitambo.


Lakini pia nataka mfahamu jambo moja, kua hili tatizo ni kubwa sana katika jamii yetu (nimetumia neno tatizo sababu linahesabika kama tatizo kwenye jamii), ni kubwa kuliko mnavodhani, watu wanawaangalia hao gays kama kina James delicious wanaojionesha na akiona watoto wake wako sawa anatukana hao wengine, hapana hujajua tatizo lilivyo bado. Sitaki kuongelea sana hao wanaojionesha sababu pia sijawahi kujiassociate nao wala sijawahi kua na rafiki anaejionyesha hivyo sijui sana. Ila fahanu haya kwa leo:-

Taelea hii mifano inayonihusu ili mjue kua hata ndoa haziko salama sana kama watu wanavoamini kwamba mtu akioa hawezi kua gay.

(1) Wanawake mlioko kwenye ndoa ombeeni ndoa zenu sana. Siwezi sema ni kwa % ngapi ila wanaume wengi ni bisexual, au bisexual curious, mimi binafsi nimewahi kua kwenye relationship na mume wa mtu sio mala moja. Ngoja niongelee hii sababu nimekua napatana sana na mtu ambae ni mume wa mtu mala nyingi, moja ambayo ilikua very serious relationship pia alikua mume wa mtu, from very happy family, alikua sometimes wanakuja wote na mke wake office ninapofanya kazi , hii ilikua inanikasirisha sana , hadi leo najiona mwenye makosa sana sababu mke wa jamaa alikua ananipenda sana na kuniheshimu bila kujua tunashare. Ila jamaa hakutaka kuniacha, alinipenda sana ila ilikua kwa siri sana sababu ni mheshimiwa pia, hivyo hata dating zetu ilikua tunasafiri kwenda mkoa mwingine ama hata kenya au nchi nyingine kwa ajili ya privacy. (alikua mtu wa kusafiri sana hivyo tulisafiri pamoja), hata sasa hivi bado yuko na mkewe na watoto family iko poa ila mkewe HAJAWAHI KUJUA HILI HADI LEO.


Nikawa kwenye uhusiano na mtu mwingine , huyu tulianza relationship kitambo pia, alikua hajaoa, funny thing ni hadi akanitambulisha kwa demu wake kama rafiki, girlfriend akaamini , hivyo hata akinikuta natumia gari la jamaa anajua ni shemeji, akikuta nimelala ndani ya nyumba anajua ni shemeji tu hadi harusi nilishiriki pale mlimani city sababu jamaa alitaka lazima niwepo, na kabla ya harusi yani siku moja kabla, alikuja kwangu tukasex kama kuniaga na kesho yake akafunga ndoa, hata alipooa japo tulikubaliana kuachana ila hatukuachana, hadi sasa ni happy family ila mke wake HAJAWAHI KUJUA.

Story ni nyingi ila wacha niishie hizo sababu zingine zitareveal kirahisi ID yangu maybe na za hao watu na nisingependa iwe hivyo, ila walioko kwenye ndoa wengi ni bisexual hasa hizi modern marriages. Watu sasa hivi wanaoa sababu tu jamii inataka waoe thats why hali ni mbaya, hata mimi mother akinipush sana nioe nitaoa , na cycle itaendelea like that, wapo vijana na watu wazima wengi ni gays ila huezi jua hata siku moja, kuna mtu tulikutana tu kwenye dating site moja ya huko nnje sababu hutumia zaidi dating site za kulipia kwa ajili ya privacy, siku tunakutana kwa mala ya kwanza sikuamini kama ni yeye, ni mtu maarufu sana na anaeheshimika sana ( ni kijana ) huko siasani. Pia mwingine huko kwenye music industry na nyimbo zake zinapendwa sana , ni za maadili.

Nataka kusema kua tatizo lipo more than you can imagine na sio rahisi kumjua mtu, hivyo kuliko kunyooshea vidole tu bila solution , ni vyema kuangalia ni kwa namna gani mtu anaweza kuzuia yasitokee kwake na kwa nwingine.

(2) Kuna watu hutongozwa na hawa gays kwenye mitandao, wala usijione unamkosi au labda umefanana na gays, hapana wewe ni straight. Kuna watu hulalamika kua ametongozwa na gay facebook au kwenye social medias, ukimuangalia huyo mtu utagundua kua ni very handsome na attractive , na gays wengi hudate na watu attractive zaidi , huwa hawafuati watu ambao wana sura personal, ndio sababu msione hao wanaotongozwa na gays huko labda wananyota mbaya au nao wanaonekana gays , hapana ila ni sababu wako attractive, tena gays wanapenda watu ambao sio gays, yani hata mimi watu niliodate nao naweza sema ni straight. Hivyo kama wewe ni handsome expect tu siku moja inaweza kukutokea na isikufanye uwaze sana na ujishushe thamani, mwambie tu im not gay then block that person. Hivyo wenye vijana ambao ni handsome wako attractive, msihisi kua labda vijana wenu ni gays hapana, ila tu nuombe Mungu awaepushe kufuatwa na gay, sababu ninachoweza kusema gays ni watu ambao wako na ushawishi mkubwa sana, unawesa hata kusex nae na mkimaliza ndio ukajiuliza imekuaje hadi ukafanya vile na unakua umechelewa tayari.

(3) Wanaume wengi ni curious, yani wameumbwa kutaka kujaribu vitu, hivyo imekua rahisi sana kushawishika, hata hawa ambao wako humu wanaongea kwa hasira na kufoka kuhusu gays tena hao ndio rahisi sana kuwashawishi, hasa wanaokunywa pombe, nina mshikaji wangu mmoja ambae ni gay, humuogopa sana sababu ana huo ujasiri wakutongoza atraight na wanaingia box, alishawahi kumtongoza straight guy akiwa na demu wake, jamaa alishindwa amfanye nini , girlfriend wake akacheka sanaaa wakaondoka. Ila hakukata tamaa na alimpata jamaa one day baada ya miezi mingi, hadi leo najiuliza sana.

La mwisho ni hili, watu mnapinga sana haya mambo ya NGO's za kusaidiwa hawa gays, ila hilo jambo lina faida sana hamjui tu, sio kwao tu kwa kila mmoja wenu, hata wewe straight ambae hauna mtoto gay, sababu hili jambo ni mzunguko. Gays ni watu ambao wako kwenye risk kubwa ya kupata maambukizi mbalimbali hasa HIV, Especially kwa wale ambao hawana elimu ya kutosha , Hizo NGO's zinasaidia kuwapa elimu na kuwapa dawa mbalimbali za kuzuia wasipatwe na magonjwa au kuambukizwa magonjwa , inawapa huduma muhimu hata kama wanaumwa ili kuzuia wasiambukize wengine, na hii ni muhimu sana, sababu hili la magonjwa linakuja kukuathili hadi wewe straight huko ambae hata huhusiki,.mzunguko uko hivi👇

gay na gay wanasex, mmoja anamshawishi wasitumie condom, bila kujua anamuambikiza mwenzake let say HIV, huyo mmoja anaenda tena kusex na mwingine, anamuambukiza pia, huyo mwingine ni straight ila curious , anenda kusex na gay anaambukizwa, nae anaenda kumuambukiza girlfriend wake, ambae huyo girlfriend ana mchepuko pia ambae ni mume wa mtu, nae anaambukizwa , nae anaenda kumuambukiza mke wake nyumbani, hatimae unafikiwa.
Au huyo gay alieambukizwa, anamshawishi kijana wako (vijana wengi straight wanashawishika kirahisi sababu ya kutaka kujaribu kuona inakuaje), kijana wako anasex nae anaambukizwa, nae anamuambikiza girlfriend wake na cycle inaendelea, ni hatari kwa taifa.

Serikali ruhusuni hizo NGO's kuokoa taifa, nawaambia ukweli gays wako wengi sana , na wale ambao ni uneducated au wanaojiuza wengi wanamagonjwa na hawapati msaada hata huko hospitali za kawaida, huko Kenya wameruhusu NGO's na zinasaidia sana , wako mpaka na special hospitals , psychologists ambao wanawasaidia pia kuishi normal na wale ambao wameshawishiwa kujaribu kuwafanya waache. NGO's haziko kwa ajili ya kuwamotivate , hapana, ziko kwa ajili ya kuzuia usambaaji wa magonjwa.

Naomba niishie hapa , kama kuna swali lolote uliza kwenye comment nitakujibu, tupo kujifunza na kusaidia kupunguza hili jambo, hivyo tafadhari tusitumie kugha za kuuudhi sana na nimejaribu kuelezea kidogo ili mpate kujua naongelea nini. Karibuni.
Unaturingishia huna marinda aisee 🤔🤔
 
Umetoa elimu bora sana... Tulinde watoto wetu wa kiune kwenye hali hii...

Hupaswi kumcheka jamaa huyu... Kumbuka bado na ww unazaa...
Hizi academy zinalainisha Sana watoto,mwanangu huwa namwita kamanda mwanajeshi nabkumlea kijeshi jeshi ni mpera mpera tu kumuepusha na hisia za kitofauti.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Bro mimi ni Mwanamke so ukiniita Dada utapatia zaidi, uamuzi nimeshachukua ninaishi na Mwanamke nishamchumbia na tuna Mtoto tayari,

Ni Happy Family kwa kweli tumebarikiwa Furaha, Amani na Upendo,

Naona unabadili upepo kila muda mwanzo ulikataa kua hakuna wanyama wanaoshiriki same sex naona umeenda kugoogle huko umejionea, sasa unakuja kusema hakuna wanyama wanaoishi pamoja as same sex, lol

Kuhusu Tanzania kuruhusu Ndoa ni suala litachukua muda lakini litatokea na ndio maana tunapigania kuweka mazingira sawa kwa new generation.
Hakuna Wanyama wanaofanya kama mnavyofanya ninyi Mashoga.

Yaani mmezidiwa ustaarabu hata na
Wanyama ambao hawana Busara lakini wameweza kutambua mema na mabaya kuliko ninyi.

Mema na mabaya yanatokana na uamuzi wa Jamii husika. Na sio lazima yawe ni Amri za Mungu, jamii zilizo staarabika zimejitungia kanuni na taratibu zinazo waongoza ktk namna ya kuishi

Kwakuwa mmechaguana watu wenye mihemuko sawa na kuamua kuishi pamoja sio kama Mume na Mke bali kama Marafiki na kuamua kuchezeana sehemu za siri, fanyeni hivyo kwa siri kama wanaovuta madawa ya kulevya.
Mkithubutu kuchezeana hadharani mtaadhibiwa.

Hapo ni kwamba mnachezeana tu sehemu za siri na kwingineko. Hakuna ndoa hapo, ndoa inatokana na fasili ya jamii husika.

Tanzania fasili ya ndoa inashirikisha watu wa jinsia mbili tofauti. Mwanamke na Mwanamme.

Kuhusu kuchezeana hadharani.
Mlivyo na akili ndogo, mkiruhusiwa tu kutambulika na jamii. Basi hapo mnaanza kuchezeana hadharani kwa fujo, Club za Mashoga zinaota kama Uyoga, sherehe za Mashoga kila upande ni full fujo.

Ushahidi upo, Nchi zote zilizoruhusu ushoga, Mashoga full time ni kukumbatiana na kubusiana hadharani.

Kuhusu kuzaa. Mashoga hawana uwezo wa Kuzaa wao kwa wao. Kama wewe Mwanamke huna uwezo wa kumzalisha Mwanamke unayejifanya umeoa.

Halafu bila soni unakuja hapa kuandika umeoa na umezaa na huyo rafiki yako wa Kike. Mke na Mke mnazaa vipi ?
Mtu akitoa kauli kama hiyo anaonekana wazi kuwa ni MWENDAWAZIMU.

Ila mkae mkitambua kuwa, hadi sasa hivi Ushoga umekataliwa ndani ya Jamii yetu.

Hivyo ni tendo haramu.
 
Ndugu mleta mada Bharka wala huna haja ya kuwa na wasiwasi kutokana na vitendo vyako vya Ushoga kwa sababu hivyo ndivyo ulivyo. Binadamu na viumbe wengine wanaendelea kubadilika kutokana na mazingira, hakika mbunifu Mkuu kuliko wote, aketie juu, uwezo wake na utashi mwanadamu hawezi fikia kamwe, ni kituko mwanadamu kuita alichokiona CHEMA haramu.
Ipo hivi hapo zama za kale wanadamu walikuwa wakiishi katika vikundi vya watu wachache wachache na mazingira ya hatari: Simba, Chui, Mamoth, Saber tooth tiger, Manyoka na noma na nusu MWANAMME MWENZIO. Hivyo kutokana na hatari kama wewe kidume uwe kidume kweli, wewe unategemewa kwenywe suala la ulinzi kulinda wanawake.

Sasa mambo sio kama zamani hatari karibia zote mwanadamu kazithibiti kwa teknolojia, sasa mwanadamu anaishi kwa mapatano na ukali kati ya wanaume umepungua mpaka kufika hatua ya wanaume kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Mambo ya kukaa kama box la umbo moja sasa hayapo tena, sasa ni kuwa kama maji kuchukua umbo lolote lile. Pia gay ni neno linalojumiisha aina zote za hisia mbali na heterosexual cocastic rudi shule kudai mleta mada sio gay.
 
Uchoko haujawahi kusababishwa na homoni uchoko ni laana ya ukoo ukijiona choko ujue baba ako alifirwa au ndugu yako yoyote anafirwa nawe ukifira choko jiandae mwanao au hata mjukuu wako kuwa choko
 
Uchoko haujawahi kusababishwa na homoni uchoko ni laana ya ukoo ukijiona choko ujue baba ako alifirwa au ndugu yako yoyote anafirwa nawe ukifira choko jiandae mwanao au hata mjukuu wako kuwa choko

Ndio mtazamo wako ulipo ishia njoo na fact kwaio ww unalaana
 
Katika hali ya Ukweli kila Mwanaume anahitaji kuanza maisha na Mwanamke ili kujenga familia.
Pia Kila Mwanamke anahitaji Mwanaume.
Ninaposema Mwanaume au Mwanamke ni wale waliokamilika kiakili na kimaumbile.

Ukitokea tofauti ujue kuna kasoro mahali imetokea ama ya Kimaumbile au ya kiakili (kisaikolojia)

Wanaume au wanawake wengi baada ya kupata musukosuko ya kisaikolojia kama kuachwa na wapenzi wao au kukosa wapenzi au kuumizwa kimapenzi utotoni, kutelekezwa au malezi mabovu, na pia madhara ya kimwli kama athari za ajali, kuzaliwa na mapungufu mengine.
Wamejikuta wanafanya maamuzi tofauti ili kujiriwadha na kuendelea kufurahia maisha.

Moja ya maamuzi ndio kama haya ya Kutafuta wapenzi wa jinsia moja au
hata kutafuta wapenzi wasio Binadamu.

Yako matukio baadhi ya Wanawake wanafunga Ndoa na wanyama na hasa Mbwa.
Yako matukio Wanaume wanafumaniwa wakilawiti wanyama kama Mbuzi na Ng'ombe.

Hayo yote ni matokeo ya frustration zilizo wapata baada ya kupitiwa na dharuba za kimaisha.

Mdada anafunga Ndoa na Mbwa dume na anaishi naye maisha ya Mume na Mke.
Hapo humwambii kitu, anatoa sababu kama zinazotolewa hapa na wahusika wa jinsia moja.

Kama mdau alivyo sema hapo juu, ulimwengu wa kisasa ni Free From Fear.
Watu wanajichagulia kuishi watakavyo. Ilimradi tu wasivunje sheria zilizowekwa ktk jamii zao.

Pamoja na hayo huwezi tu kutembea barabarani ukiwa uchi wa mnyama kwa kusema tu umejisikia kuwa huru kufanya hivyo.

Uhuru unamipaka yake, lazima uende na taratibu na kanuni za jamii husika.

Ndio maana Mashoga wanajisikia Guilty kujionesha mitaani. Na ni kweli ni waharifu kutokana na kanuni zetu za maisha tulizojiwekea.
Na wakikutwa wanaadhibiwa na jamii au mamlaka.

Hivyo ni ruksa kuishi namna utakavyo ila zingatia desturi za jamii yako ambayo imejirisha kiutafiti kuwa Ushoga una madhara kwa jamii na hauna faida.

Ushoga ni Uhalifu kama uhalifu mwingine hivyo ni juu yenu kuamua kuendelea nao mafichoni au kuachana na hayo maisha.
 
Katika hali ya Ukweli kila Mwanaume anahitaji kuanza maisha na Mwanamke ili kujenga familia.
Pia Kila Mwanamke anahitaji Mwanaume.
Ninaposema Mwanaume au Mwanamke ni wale waliokamilika kiakili na kimaumbile.

Ukitokea tofauti ujue kuna kasoro mahali imetokea ama ya Kimaumbile au ya kiakili (kisaikolojia)

Wanaume au wanawake wengi baada ya kupata musukosuko ya kisaikolojia kama kuachwa na wapenzi wao au kukosa wapenzi au kuumizwa kimapenzi utotoni, kutelekezwa au malezi mabovu, na pia madhara ya kimwli kama athari za ajali, kuzaliwa na mapungufu mengine.
Wamejikuta wanafanya maamuzi tofauti ili kujiriwadha na kuendelea kufurahia maisha.

Moja ya maamuzi ndio kama haya ya Kutafuta wapenzi wa jinsia moja au
hata kutafuta wapenzi wasio Binadamu.

Yako matukio baadhi ya Wanawake wanafunga Ndoa na wanyama na hasa Mbwa.
Yako matukio Wanaume wanafumaniwa wakilawiti wanyama kama Mbuzi na Ng'ombe.

Hayo yote ni matokeo ya frustration zilizo wapata baada ya kupitiwa na dharuba za kimaisha.

Mdada anafunga Ndoa na Mbwa dume na anaishi naye maisha ya Mume na Mke.
Hapo humwambii kitu, anatoa sababu kama zinazotolewa hapa na wahusika wa jinsia moja.

Kama mdau alivyo sema hapo juu, ulimwengu wa kisasa ni Free From Fear.
Watu wanajichagulia kuishi watakavyo. Ilimradi tu wasivunje sheria zilizowekwa ktk jamii zao.

Pamoja na hayo huwezi tu kutembea barabarani ukiwa uchi wa mnyama kwa kusema tu umejisikia kuwa huru kufanya hivyo.

Uhuru unamipaka yake, lazima uende na taratibu na kanuni za jamii husika.

Ndio maana Mashoga wanajisikia Guilty kujionesha mitaani. Na ni kweli ni waharifu kutokana na kanuni zetu za maisha tulizojiwekea.
Na wakikutwa wanaadhibiwa na jamii au mamlaka.

Hivyo ni ruksa kuishi namna utakavyo ila zingatia desturi za jamii yako ambayo imejirisha kiutafiti kuwa Ushoga una madhara kwa jamii na hauna faida.

Ushoga ni Uhalifu kama uhalifu mwingine hivyo ni juu yenu kuamua kuendelea nao mafichoni au kuachana na hayo maisha.
Kheeeh! Mbona kama wewe ndie mwenye hasira kuliko hao walengwa??

Sasa uhalifu wa Shoga ni upi au ndio kujitoa ufahamu mtu mzima wewe.
 
Hakuna Wanyama wanaofanya kama mnavyofanya ninyi Mashoga.

Yaani mmezidiwa ustaarabu hata na
Wanyama ambao hawana Busara lakini wameweza kutambua mema na mabaya kuliko ninyi.

Mema na mabaya yanatokana na uamuzi wa Jamii husika. Na sio lazima yawe ni Amri za Mungu, jamii zilizo staarabika zimejitungia kanuni na taratibu zinazo waongoza ktk namna ya kuishi

Kwakuwa mmechaguana watu wenye mihemuko sawa na kuamua kuishi pamoja sio kama Mume na Mke bali kama Marafiki na kuamua kuchezeana sehemu za siri, fanyeni hivyo kwa siri kama wanaovuta madawa ya kulevya.
Mkithubutu kuchezeana hadharani mtaadhibiwa.

Hapo ni kwamba mnachezeana tu sehemu za siri na kwingineko. Hakuna ndoa hapo, ndoa inatokana na fasili ya jamii husika.

Tanzania fasili ya ndoa inashirikisha watu wa jinsia mbili tofauti. Mwanamke na Mwanamme.

Kuhusu kuchezeana hadharani.
Mlivyo na akili ndogo, mkiruhusiwa tu kutambulika na jamii. Basi hapo mnaanza kuchezeana hadharani kwa fujo, Club za Mashoga zinaota kama Uyoga, sherehe za Mashoga kila upande ni full fujo.

Ushahidi upo, Nchi zote zilizoruhusu ushoga, Mashoga full time ni kukumbatiana na kubusiana hadharani.

Kuhusu kuzaa. Mashoga hawana uwezo wa Kuzaa wao kwa wao. Kama wewe Mwanamke huna uwezo wa kumzalisha Mwanamke unayejifanya umeoa.

Halafu bila soni unakuja hapa kuandika umeoa na umezaa na huyo rafiki yako wa Kike. Mke na Mke mnazaa vipi ?
Mtu akitoa kauli kama hiyo anaonekana wazi kuwa ni MWENDAWAZIMU.

Ila mkae mkitambua kuwa, hadi sasa hivi Ushoga umekataliwa ndani ya Jamii yetu.

Hivyo ni tendo haramu.
Calm Down bro, tatizo unaendeshwa kwa mihemko sana....

Nimekuuliza maswali huko juu hujajibu unabwabwaja kama mtu aliyerukwa na akili,

Jadili kwa upole, umakini na hoja kubwabwaja hakuleti maana,

Nakuongezea na Swali jingine,
Umesema wavuta madawa ya kulevya na wao wajitokeze kudai haki ya kuvuta madawa hadharani,
Je, Elezea Faida na Hasara ya Madawa ya Kulevya,


Umesema Ushoga ni Uhalifu, elezea hasara za Ushoga.
 
Calm Down bro, tatizo unaendeshwa kwa mihemko sana....

Nimekuuliza maswali huko juu hujajibu unabwabwaja kama mtu aliyerukwa na akili,

Jadili kwa upole, umakini na hoja kubwabwaja hakuleti maana,

Nakuongezea na Swali jingine,
Umesema wavuta madawa ya kulevya na wao wajitokeze kudai haki ya kuvuta madawa hadharani,
Je, Elezea Faida na Hasara ya Madawa ya Kulevya,


Umesema Ushoga ni Uhalifu, elezea hasara za Ushoga.
Sina hasira hata chembe.

Nasema katika jamii za Kitanzania
Ushoga ni uhalifu kama uhalifu mwingine.

Kama sio, basi tangaza kumwoa huyo mwanamke mwenzako na kaombe ruhusa ya kufunga ndoa kwa Mrajisi wa Wilaya yako halafu tuletee mrejesho hapa.

Utakataliwa, basi tambua kuwa ni uhalifu.

Mimi binafsi siwachukii Mashoga ila Ushoga, kwakuwa ni mapito ya maisha ya mtu na huenda akajirekebisha huko mbeleni na kuwa mtu wa kukubalika.

Ila lazima niseme ukweli kwamba katika Taifa la JMT Ushoga umepigwa marufuku kwakuwa utafiti wa Kisayansi umethibitisha kuwa hauna tija kwa ustawi wa jamii ya Kitanzania.
Na ni uhalifu kama uhalifu mwingine.
 
Back
Top Bottom