cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Kabisaaa maelezo mazuri na yamenyooka mnoo, apite asome hapaaa.Kwa Umri wake ni kuiga,
Atakua amezungukwa na Wadada wa kileo na ukute mtoto wa kiume yupo peke yake kwa hiyo akiona dada zake wanachofanya na yeye anawaiga na shule amekua na marafiki wa kike sababu ndio kampani aliyoizoea tangu nyumbani kwa maana hiyo ana jifeel comfortable akizungukwa na wa kike kuliko wa kiume,
Hapo waanze tu kumuonesha kwa upole kua yeye ni wa kiume akipaka lipstick wamfute wamshikishe fimbo wamwambie apigane kung fu ili kuilinda familia yake, wamuoneshe yeye ni protector wa familia anatakiwa kua strong, n.k
Kuna ndugu yangu nilienda kumtembelea kwake mwaka jana nikamkuta na kilio cha binti yake wa miaka 10 anataka kua mkaka, hataki nguo za kike, anacheza michezo ya kupigana, mpira, hadi kuongea anaongea kibabe, nikamwambia anipe nikakae nae likizo ya mwezi mmoja, bahati nzuri hakubisha,
Siku namrudisha mama ake alilia kumuona mwanae amevaa nguo za kike na amesuka nywele nzuri na vishanga juu,
Mazingira wakati mwengine humshape mtoto kutoka A kwenda B and Vice Versa.
Sent using Jamii Forums mobile app