Mambo usiyoyajua kuhusu Biblia

Mambo usiyoyajua kuhusu Biblia

King Jim

Member
Joined
Aug 12, 2024
Posts
6
Reaction score
16
BIBLE'S CONSPIRACIES 1.

MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU BIBLIA
ambayo yatakushangaza hata kama umekuwa Mkristo uliyapata kipaimara na kubatizwa.

Namba 6 itakushangaza!

Tafadhari USISOME kama hukupitia Bible School.

Imeandikwa na King Jim

images (5).jpeg


1. Biblia ndio kitabu kilichokamilika zaidi nilichowahi kusoma na hakijakosewa bali unahitaji uelewa sahihi kufafanua kila kifungu ndani ya Biblia, anayesema Biblia inamapungufu ameshindwa kuitafsiri tu mwenyewe.

images (1).jpeg


1. Biblia sio kitabu pekee Kitakatifu katika ulimwengu huu bali moja tu ya vitabu takatifu hasa baada ya waandishi wa Biblia kusaidiwa kuandika na Roho wa Mungu. Kuna vitabu vingine kama Kitabu cha Uzima na Kitabu cha Hukumu.
Biblia imeandikiwa kizazi cha Adam tu.

2. Adamu sio binadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu bali Adam ndiye mtu wa kwanza kuumbwa kwa mfano wa Mungu. Sayansi italidhibitisha hili hasa baada ya kugundua mafuvu yaliyoishi miaka millioni iliyopita ilihali Adam alitokea miaka 6000 tu iliyopita.

3. Mtumishi Ayubu aliishi katika kizazi cha kabla ya Adam. Kitabu chote cha Ayubu kimeongelea mambo ya ajabu ambayo kwa sasa hivi hayapo ambayo yalikuwepo kabla ya Adamu na pia hakuna reference ya utawala na tarehe ya uandishi kama ilivyo kwa vitabu vingine. Mfano kutajwa kwa viumbe kamaLeviathan ambao ni kama ma Dinosaurs 🦕 Job 41:1

4. Shetani ndio alikuwa mwokozi kama Yesu wa kipindi cha kabla ya Adamu ila akawadanganya watu badala ya kuwaonesha upendo wa Mungu kama alivyotumwa ndio akapotea mazima mpaka kuwa Ibilisi. Ref John 16:11

images (3).jpeg


5. Shetani hakutaka kumpindua Mungu kama mlivyojifunza Sunday School. Bali shetani alitupwa chini baada ya kuwadanganya watu kuwa yeye ndo wao Mungu. From Isaiah 14: 14 Ukifikiria vizuri utaona shetani sio mpuuzi kiasi hicho na story yao hai-make sense

6. Yesu ni Mungu na hakuwahi fahamika kabla ya kuzaliwa kwake duniani yaani hakuna malaika aliyemfahamu wala kumuona Yesu kabla hajazaliwa na Mariamu hapa duniani isitoshe hata shetani mwenyewe alikuwa hamjui ndio maana akahitaji uthibitisho kumuuliza "kama kweli wewe ni mwana wa Mungu."

7. Paulo alioa ila aliachika na hakuwa Bachelor kama tunavyodhania kwasababu Paul alihudhulia Sanhedrin ambapo huwezi kuhudhuria kama hujaoa.

images (4).jpeg


8. Dunia yetu hii sio uumbaji pekee wa Mungu na wala sisi pekee sio watu wa Mungu. Imagine the whole Galaxy and focusing only on Earth.

9. Hakuna watakatifu mbinguni wanao ombea watakatifu duniani, wote waliokufa baada ya Yesu wapo peponi na wanasubiri ujio wa Yesu tena rejea mfano wa Lazaro na Tajiri.

10. Kuna mashetani yanatisha sana kuliko hata shetani mwenyewe ila yamefungwa minyororo bali shetani ameachwa anazurula huku na kule.
Refer 2 Peter 2:4

11. Kuna malaika wengi sana walioanguka out of the influence ya shetani na case yao haimuhusu Ibilisi na walizaa na binadamu viumbe wa ajabu ndio sababu ya Mungu kuingamiza dunia ya zamani kwa maji. Mwanzo 6 yote

12. Kizazi chetu ni kiovu lakini sio sababu ya sisi kutoona utendaji mkuu wa Mungu tunayemsoma kwa Biblia kama tunavyoelekezwa kwamba sisi hatuna imani kama waliotangulia japo wengi wanamuamini Yesu na hawajawahi muona sembuse walio mkataa Musa aliyetoka kugawanya bahari!

13. Sadaka zetu huenda ndio zikawa Pocket Money zetu mbinguni kwani Biblia imesema tuweke akiba sehemu isiyo haribika, na sote tunajua akiba ni kwa matumizi ya baadae.

images (6).jpeg
 
Mtumishi Ayubu aliishi katika kizazi cha kabla ya Adam.
Hii sio kweli, Ayubu si mpka nchi ilitajwa ila ilikua kabla hata ya Abraham. Na ilikua ni kama fumbo/parable kuliko uhalisia.
Adamu sio binadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu bali Adam ndiye mtu wa kwanza kuumbwa kwa mfano wa Mungu.
Hapa umeongea ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia.
Mfano kutajwa kwa viumbe kamaLeviathan ambao ni kama ma Dinosaurs 🦕 Job 41:1
Hawa kweli walikuwepo kabla ya Adam ila hata Zaburi amewaongelea kama reference licha ya kuwa zaburi kiliandikwa recent kuliko Ayubu. So Ayubu kuwaongelea ni reference tu ya mambo aliyosikia enzi na enzi. Hata isaya aliongelea wanyama kama centaur (Farasi mtu) na Cockatrice ambao ni wa enzi za wanefili ila haimaanishi isaya alikuwepo kabla ya Adam.
6. Yesu ni Mungu na hakuwahi fahamika kabla ya kuzaliwa kwake duniani yaani hakuna malaika aliyemfahamu wala kumuona Yesu kabla hajazaliwa na Mariamu hapa duniani isitoshe hata shetani mwenyewe alikuwa hamjui ndio maana akahitaji uthibitisho kumuuliza "kama kweli wewe ni mwana wa Mungu."
Sio kweli, Yesu alifahamika kabla hajazaliwa. Mfano Mwanzo 13 Yesu alifahamika kwa Abraham pale alipompa kikumi kama Mfalme Melchizedek. Pia nebuchadnezzar alimtambua Yesu kwenye moto wa kina shadrack. Pia kitabu cha petro kinaeleza Yesu alikuwepo enzi za Nuhu kuhubiri roho zilizopotea!!

Kama wote walimtambua sembuse shetani au malaika?
10. Kuna mashetani yanatisha sana kuliko hata shetani mwenyewe ila yamefungwa minyororo bali shetani ameachwa anazurula huku na kule.
Refer 2 Peter 2:4
Sio kweli hawa wametunzwq Euphrates na Tigris kwa kazi maalum kipindi cha mwisho, soma ufunuo kuanzia 16 wanatajwa kazi yao itakua nini wakifunguliwa minyororo.

Hawa ndio walitajwa kwenye Yuda 13 kuwa waliacha kazi yao wakaenda kuzini na binadamu na hivyo kuzaa giants!!
 
13. Sadaka zetu huenda ndio zikawa Pocket Money zetu mbinguni kwani Biblia imesema tuweke akiba sehemu isiyo haribika, na sote tunajua akiba ni kwa matumizi ya baadae
Hapana, pocket money ili ununue nini? Akiba ni ya matendo, ukiwa na imani, upendo, uadilifu, ujazo wa roho mtakatifu, maisha yenye ushuhuda hizo ndio akiba otherwise maskini hawataingia mbinguni. Abraham alimtoa Isaka ila tunaambiwa ndio baba wa imani SIO sababu ya kutoa PESA.

Na wanatheolojia wanasema kwa nia ya sadaka ile ndio Mungu akaona asimzuie mwanaye kufa msalabani sababu aliona moyo wa Abraham kutozuia wake.

So to hell with pesa, matendo ndio hazina
 
Hapa sijaelewa wakuu naomba ufafanuzi

Ufunuo wa Yohana 5:6
[6]Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
And I beheld, and, lo, in the midst of the throne and of the four beasts, and in the midst of the elders, stood a Lamb as it had been slain, having seven horns and seven eyes, which are the seven Spirits of God sent forth into all the earth.
 
Ebu nisaidie ufafanuzi wa hiyo namba 7 kuhusu Paulo
 
Ukichukua ndoo ya maji safi, ukadondosha tone la kinyesi ndani ya ndoo, maji yote yanageuka kuwa machafu.

Umeandika Kweli kidogo ukatia na makanyaboya ya uongo kibao hivyo kufanya yote uliyoandika kuwa uongo.
 
Back
Top Bottom