Mambo ya ajabu yaliyonifanya nikashindwa kuishi vijiji vya kanda ya Ziwa

Kwa vijijini ni maeneo mengi sana ukabila hasa upande wa biashara Tanganyika hii unahusika sana tena sana. Hata kule kusini kuna hao Wamatengo labda biashara unayofanya kusiwepo na mwenyeji anayefanya hiyo biashara pia.
 
aliesema shilabela kadanganya shilabela ni ka mtaa kenye pilika pilika nyingi kwa geita mambo ya kishamba shilabela hapo uongo na kuhusu magogo napo ni uongo maana ule ni mtaa mpya na wakishua haswa huwezi kukuta hivyo vituko
 
We magogo unaijua ya juzi tu mimi nimekaa pale 2021 waganga walikuwa wengi kuzidi wakazi.Mitaa ambayo wamejenga Royal kuna sehemu kabla ya kufika kule inaitwa Igembesabo ni waganga watupu sema baada ya watu kuanza ujenzi kwa kasi naona waganga kidogo kidogo wanafunga vilinge vyao
 
aliesema shilabela kadanganya shilabela ni ka mtaa kenye pilika pilika nyingi kwa geita mambo ya kishamba shilabela hapo uongo na kuhusu magogo napo ni uongo maana ule ni mtaa mpya na wakishua haswa huwezi kukuta hivyo vituko
Unapajua 14 Kambarage wewe? Shilabela barabarani hapo wewe ndio unaongelea ingia ndani ndani huko uone.
 
Umeandika uongo mwingi sana labda utaje ulikuwa kanda ya ziwa mwaka 1980.

Sasa upigwe mwano wewe umelala tu ndani unaona ni sawa?
Faini itakuhusu tu!
Msilazimishe kila mtu ambaye sio wa kwenu kufuata mila zenu za kishamba watu wamekuja na mishe zao nyie mnawaletea upuuzi wenu wa huko unafikiri kila mtu mshirikina kama nyie
 
Ila haya mambo sijui ya nzengo mimi nilishaonaga uzushi tu nimeishi miaka mi nne ila sijawahi kushiriki hizo mambo zao.

Nikipitaga mtaa naonaga wenyeji wananikata jicho kali kweli lakini mimi sinaga muda na mtu maana hamna anaenisaidia kwa chochote.
 
Hii bado ipo huko Geita karibu maeneo yote ya mkoa huo
 
Uko sahihi kabisa, huo mkoa una mambo mengi ya kushangaza
 
Ha ha uko sahihi misa /ibada za kihaya zina vibe yake na ndo zilizozoeleka, kwa asiye muhaya lazima apate ugumu kuelewa
 
Mi nshawahi changishwa mchango wa ujenzi wa kisima, niligoma kwa kuwaambia wananzengo kuwa mi ni mlipa kodi hawakunielewa hadi mtendaji wa kata akaingilia kati kusuluhisha.kuishi usukumani ni kipengele
 
Hawajawahi sungu sungu kukuburuza kwenda kutemya? Hapo ndio maajabu na watu wanakula mboko vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…